\v 4 Pia wasisikilize hadithi na orodha za nasaba zisizo na mwisho. Haya husababisha mabishano zaidi kuliko kuwasaidia kuendeleza mpango wa Mungu wa imani.
\v 5 Basi lengo la agizo hili ni upendo utokao katika moyo safi, katika dhamiri nzuri na katika imani ya kweli.
\v 6 Baadhi ya watu wamelikosa lengo wakayaacha mafundisho haya na kugeukia mazungumzo ya kipumbavu.
\v 7 Wanataka kuwa waalimu wa sheria, lakini hawafahamu wanachosema au wanachosisitiza.
\p
\v 8 Lakini tunajua kwamba sheria ni njema kama mtu ataitumia kwa usahihi.
\v 9 Tunajua kuwa, sheria haikutungwa kwa ajili ya mtu mwenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, watu wasio wataua na wenye dhambi, na ambao hawana Mungu na waovu. Imetungwa kwa ajili ya wauao baba na mama zao, kwa ajili ya wauaji wa watu,
\v 10 kwa ajili ya waasherati, kwa ajili ya watu wazinzi, kwa ajili ya wale wanaoteka watu na kuwafanya watumwa, kwa ajili ya waongo, kwa ajili ya mashahidi wa uongo, na yeyote aliye kinyume na maelekezo ya uaminifu.
\v 11 Maelekezo haya yanatokana na injili yenye utukufu wa Mungu mwenye kubarikiwa ambayo kwayo nimeaminiwa.
\p
\v 12 Ninamshukuru Yesu Kristo Bwana wetu. Alinitia nguvu, kwa kuwa alinihesabu mimi kuwa mwaminifu, na akaniweka katika huduma.
\v 13 Nilikuwa mtu wa kukufuru, mtesaji na mtu wa vurugu. Lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda kwa ujinga kwa kutoamini.
\v 15 Ujumbe huu ni wa kuaminika na unastahili kupokelewa na wote, ya kuwa Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi, ambao mimi ni mbaya zaidi ya wote.
\v 16 Lakini kwa sababu hii mimi nilipata rehema ili kwamba ndani yangu mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo Yesu adhihirishe uvumilivu usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wote watakaomwamini na wapate uzima wa milele.
\v 18 Ninaliweka agizo hili mbele yako Timotheo, mtoto wangu. Nafanya hivi kulingana na unabii uliotolewa hapo kwanza kukuhusu wewe, ili kwamba uhusike katika vita vyema.
\v 19 Fanya hivyo ili kwamba uwe na imani na dhamiri njema. Baadhi ya watu wameyakataa haya wakaangamiza imani.
\v 20 Kama vile Himeneyo na Alekizanda, ambao nimempa shetani ili wafundishwe wasikufuru.
\v 5 Kwa kuwa kuna Mungu mmoja, na kuna mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu ambaye ni Kristo Yesu.
\v 6 Alijitoa mwenyewe kama fidia kwa wote, kama ushuhuda kwa wakati muafaka.
\v 7 Kwa sababu hii, mimi mwenyewe nilifanywa kuwa mjumbe wa injili na mtume. (Nasema kweli. Sisemi uongo). Mimi ni mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.
\p
\v 8 Kwa hiyo, nataka wanaume kila mahali waombe na kuinua mikono mitakatifu bila ghadhabu na mashaka.
\v 9 Vivyo hivyo, nataka wanawake wajivike mavazi yanayokubalika, kwa heshima na kujizuia. Wasiwe na nywele zilizosukwa, au dhahabu, au Lulu, au mavazi ya gharama kubwa.
\v 1 Usemi huu ni wakuaminika: Kama mtu anatamani kuwa Msimamizi, anatamani kazi njema.
\v 2 Kwa hiyo msimamizi ni lazima asiwe na lawama. Ni lazima awe mume wa mke mmoja. Ni lazima awe na kiasi, busara, mwenye utaratibu, mkarimu. Ni lazima awe na uwezo wa kufundisha.
\v 15 Lakini ikiwa nitachelewa, ninaandika ili upate kujua namna ya kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambalo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msaada wa kweli.
\v 16 Na haipingiki kwamba kweli ya Uungu uliyofunuliwa ni mkuu: “Alionekana katika mwili, akathibitishwa na Roho, akaonekana na malaika, akatangazwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa na ulimwengu, na akachukuliwa juu katika utukufu.”
\v 1 Sasa Roho anasema waziwazi kwamba katika nyakati zijazo baadhi ya watu wataiacha imani na kuwa makini kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya kipepo yatakayofundishwa
\v 6 Kama utayaweka mambo haya mbele ya ndugu, utakuwa mtumishi mzuri wa Yesu Kristo. Kwa sababu umestawishwa kwa maneno ya imani na kwa mafundisho mazuri ambayo umeyafuata.
\v 7 Lakini zikatae hadithi za kidunia ambazo zinapendwa na wanawake wazee. Badala yake, jifunze mwenyewe katika utaua.
\v 10 Kwa kuwa ni kwa sababu hii tunataabika na kufanya kazi kwa bidii sana. Kwa kuwa tunao ujasiri katika Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, lakini hasa kwa waaminio.
\v 4 Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu.
\v 5 Lakini mjane kweli kweli ni yule aliyeachwa peke yake. Naye huweka tegemeo lake kwa Mungu. Siku zote hudumu katika sala na maombi usiku na mchana.
\v 7 Na uyahubiri haya mambo ili kwamba wasiwe na lawama.
\v 8 Ila kama mtu asipowatunza ndugu zake, hususani wale walioko nyumbani mwake, ameikana imani na ni mbaya kuliko mtu asiye amini.
\p
\v 9 Basi mwanamke aandikishwe kwenye orodha kama mjane akiwa na umri usiopungua miaka sitini, na ni mke wa mume mmoja.
\v 10 Lazima awe amejulikana kwa matendo mema, ikiwa ni kwamba amewajali watoto, au ameshakuwa mkarimu kwa wageni, au ameosha miguu ya waaminio, au amewasaidia ambao wamekuwa wakiteswa, au alijitoa kwa kazi yeyote njema.
\v 11 Lakini kwa wale wajane vijana, kataa kuwaandikisha kwenye orodha ya wajane. Kwa kuwa wakiingia kwenye matamanio ya kimwili yakizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa.
\v 12 Kwa njia hii huingia kwenye hatia kwa kuwa huvunja kujitoa kwao kwa awali.
\v 13 Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema.
\v 14 Kwa hiyo mimi nataka wanawake vijana waolewe, wazae watoto, wasimamie nyumba zao, ili kutokumpa adui nafasi ya kutushitaki kwa kufanya dhambi.
\v 15 Kwa sababu baadhi yao wameshamgeukia Shetani.
\v 21 Nakuagiza kwa dhati mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu, na malaika wateule, kwamba uyatunze maagizo haya bila ubaguzi wowote, na kwamba usifanye jambo lolote kwa upendeleo.
\p
\v 22 Usimwekee mtu yeyote mikono haraka. Usishiriki dhambi ya mtu mwingine. Yakupasa kujitunza mwenyewe uwe msafi.
\v 23 Haikupasi kunywa maji pekee. Badala yake, unywe mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo na magonjwa yako ya mara kwa mara.
\v 24 Dhambi za baadhi ya watu hujulikana kwa uwazi, na huwatangulia hukumuni. Lakini baadhi ya dhambi hufuata baadaye.
\v 1 Acha wale wote walio chini ya nira kama watumwa wawachukulie mabwana zao kama wenye heshima zote. Wanatakiwa kufanya hivyo ili jina la Mungu na mafundisho yasitukanwe.
\v 2 Watumwa wenye mabwana waaminio wasiwadharau kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie zaidi. Kwa sababu mabwana wanaosaidiwa kazi zao ni waamini na wanapendwa. Fundisha na kuyatangaza mambo haya.
\v 3 Iwapo mtu fulani anafundisha kwa upotovu na hayapokei maelekezo yetu yenye kuaminika, ambayo ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo, iwapo hawalikubali fundisho liongozalo kwenye utauwa.
\v 4 Mtu huyo anajivuna na hajui chochote. Badala yake, ana vurugu na mabishano juu ya maneno. Maneno haya huzaa wivu, ugomvi, matukano, shuku mbaya,
\v 5 na vurugu za mara kwa mara kati ya watu wenye akili zilizoharibika. Wanaiacha kweli. Wanafikiri kwamba utauwa ni njia ya kuwa matajiri”
\p
\v 6 Sasa utauwa na kuridhika ni faida kubwa.
\v 7 Kwa maana hatukuja na chochote duniani. Wala hatuwezi kuchukua chochote kutoka duniani.
\v 9 Sasa hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego. Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya, na katika kitu chochote kinachowafanya watu wazame katika maangamizi na uharibifu.
\v 10 Kwa kuwa kupenda fedha ni chanzo cha aina zote za uovu. Watu ambao hutamani hiyo, wamepotoshwa mbali na imani na wamejichoma wenyewe kwa huzuni nyingi.
\v 12 Piga vita vizuri vya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba ulitoa ushuhuda mbele ya mashahidi wengi kwa kile kilicho chema.
\v 15 Mungu atadhihirisha ujio wake kwa wakati sahihi- Mungu, Mbarikiwa, nguvu pekee, Mfalme anayetawala, Bwana anayeongoza.
\v 16 Peke yake anaishi milele na akaaye katika mwanga usiokaribiwa. Hakuna mtu awezaye kumwona wala awezaye kumtazama. Kwake iwe heshima na uweza wa milele. Amina.
\p
\v 17 Waambie matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, na wasitumaini katika utajiri, ambao siyo wa uhakika. Badala yake, wanapaswa kumtumaini Mungu. Ambaye hutupatia utajiri wote wa kweli ili tufurahie.
\v 18 Waambie watende mema, watajirike katika kazi njema, wawe wakarimu, na utayari wa kutoa.