\v 7 Ni sawa kwangu kujisikia hivi juu yenu ninyi nyote kwa sababu nimewaweka moyoni mwangu. Maana ninyi mmekuwa washirika wenza katika neema, katika kifungo changu na katika utetezi na uthibitishaji wangu wa injili.
\v 8 Mungu ni shahidi wangu, jinsi nilivyo na shauku juu yenu nyote katika undani wa pendo la Kristo Yesu.
\p
\v 9 Na ninaomba kwamba: upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote.
\v 10 Ninaomba kwa ajili ya hili ili muwe na uwezo wa kupima na kuchagua mambo yaliyo bora sana. Pia ninawaombea ili muwe safi pasipokuwa na hatia yoyote katika siku ya Kristo.
\v 18 Kwa hiyo Sijali, aidha njia ikiwa ni kwa hila au kwa kweli, Kristo anatangazwa, na katika hili ninafurahia! Ndiyo, nitafurahia.
\p
\v 19 Kwa kuwa ninajua ya kuwa hili litaleta kufunguliwa kwangu. Jambo hili litatokea kwa sababu ya maombi yenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo.
\v 20 Kulingana na matarajio yangu ya uhakika na kweli ni kwamba, sitaona aibu. Badala yake, kwa ujasiri wote, kama ambavyo siku zote na sasa, natarajia kuwa Kristo atainuliwa katika mwili wangu, ikiwa katika uzima au katika kifo.
\v 25 Kwa kuwa nina uhakika juu ya hili, ninajua nitabaki na kuendelea kuwa pamoja nanyi nyote, kwa ajili ya maendeleo na furaha ya imani yenu.
\v 26 Na hii italeta furaha yenu kubwa katika Kristo Yesu, kwa sababu yangu itaongezeka, kwa sababu ya uwepo wangu tena pamoja nanyi.
\p
\v 27 Mnatakiwa kuishi maisha yenu katika mwenendo mzuri uipasayo injili ya Kristo. Fanyeni hivyo ili nikija kuwaona au nisipokuja, nisikie kuwa mmesimama imara katika roho moja. Natamani kusikia kuwa mna roho moja, mkiishindania imani ya injili kwa pamoja.
\v 28 Na msitishwe na kitu chochote kinachofanywa na maadui zenu. Hii kwao ni ishara ya uharibifu. Bali kwenu ni ishara ya wokovu kutoka kwa Mungu.
\v 29 Kwa maana ninyi mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, bali na kuteswa pia katika Yeye.
\v 30 Kwa maana mna mgogoro uleule kama mliouona kwangu na mnasikia kwamba ninao hata sasa.
\v 12 Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikieni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka.
\v 13 Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu, ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye.
\p
\v 14 Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano.
\v 15 Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu.
\v 16 Shikeni sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure.
\p
\v 17 Lakini hata kama ninamiminwa kama sadaka juu ya dhabidhu na huduma ya imani yenu, ninafurahi, na ninafurahi pamoja nanyi nyote.
\v 25 Lakini nafikiri ni muhimu kumrejesha kwenu Epafradito. Yeye ni ndugu yangu na mtenda kazi mwenzangu na askari mwenzangu, mjumbe na mtumishi wenu kwa ajili ya mahitaji yangu.
\v 26 Kwa sababu alikuwa na hofu na alitamani kuwa pamoja nanyi nyote, kwa kuwa mlisikia kwamba alikuwa mgonjwa.
\v 27 Maana hakika alikuwa mgonjwa sana kiasi cha kufa. Lakini Mungu alimhurumia, na wema huo haukuwa juu yake tu, lakini pia ulikuwa juu yangu, ili kwamba nisiwe na huzuni juu ya huzuni.
\v 28 Kwa hiyo ninamrejesha kwenu haraka iwezekanavyo, Ili kwamba mtakapomwona tena mpate kufurahi na mimi nitakuwa nimeondolewa wasi wasi.
\v 29 Mkaribisheni Epafradito katika Bwana kwa furaha zote. Waheshimuni watu kama yeye.
\v 30 Kwa kuwa ilikuwa kwa ajili ya kazi ya Kristo kwamba alikaribia kufa. Alihatarisha maisha yake ili kuniokoa mimi na akafanya kile ambacho hamkuweza kufanya katika kunihudumia mimi kwani mko mbali nami.
\v 1 Hatimaye, ndugu zangu furahini katika Bwana. Sioni usumbufu kuwaandikia tena maneno yaleyale. Haya mambo yatawapa usalama.
\p
\v 2 Jihadharini na mbwa. Jihadharini na watenda kazi wabaya. Jihadharini na wale wajikatao miili yao.
\v 3 Kwa kuwa sisi ndiyo tohara. Sisi ndiyo huwa tumwabudu Mungu kwa msaada wa Roho. Tujivuniao katika Kristo Yesu, na ambao hatuna ujasiri katika mwili.
\v 4 Hata hivyo, kama kungekuwa na mtu wa kuutumainia mwili huu, mimi ningeweza kufanya hivyo zaidi.
\v 5 Kwani nilitahiriwa siku ya nane, nilizaliwa katika kabila la Waisraeli. Ni wa kabila la Benjamini. Ni Mwebrania wa waebrani. Katika kuitimiza haki ya sheria ya Musa, nilikuwa, Farisayo.
\v 8 Kwa kweli, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kutokana na ubora wa kumjua wa Kristo Yesu Bwana wangu. Kwa ajili yake nimeaacha mambo yote, nayahesabu kama takataka ili nimpate Kristo
\v 9 na nionekane ndani yake. Sina haki yangu binafisi kutoka katika sheria, bali ninayo haki ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, itokayo kwa Mungu, yenye msingi katika imani.
\v 10 Kwa hivyo sasa nataka kumfahamu yeye na nguvu ya ufufuo wake na ushirika wa mateso yake. Nataka kubadilishwa na Kristo katika mfano wa kifo chake,
\v 12 Siyo kweli kwamba tayari nimeyapata mambo hayo, au kwamba nimekuwa mkamilifu katika hayo. Bali najitahidi ili niweze kupata kile nilichopatikana na Kristo Yesu.
\v 13 Ndugu zangu, sidhani kwamba nimekwisha kupata mambo haya. Bali nafanya jambo moja: nasahau ya nyuma nayatazamia ya mbele.
\v 15 Sote tulio ukulia wokovu, tunapaswa kuwaza namna hii. Na ikiwa mwingine atafikiri kwa namna iliyotofauti kuhusu jambo lo lote, Mungu pia atalifunua hilo kwenu.
\v 16 Hata hivyo, hatua tuliyo ifikia na tuenende katika mtindo huo.
\p
\v 17 Ndugu zangu, niigeni mimi. Waangalieni kwa makini wale wanaoenenda kwa mfano ulio wa jinsi yetu.
\v 18 Wengi wanaoishi ni ni wale ambao mara nyingi nimewaambieni, na sasa nawaambia kwa machozi wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
\v 19 Mwisho wao ni uharibifu Kwa kuwa Mungu wao ni tumbo, na kiburi chao kiko katika aibu yao. Wanafikiria mambo ya kidunia.
\v 20 Bali uraia wetu uko mbinguni, ambako tunamtarajia mwokozi wetu Yesu Kristo.
\v 3 Kwa kweli, niwasihi pia ninyi watenda kazi wenzangu, muwasaidie hawa wanawake kwa kuwa walitumika pamoja na mimi katika kueneza injili ya Bwana tukiwa na Kelementi pamoja na watumishi wengine wa Bwana, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
\v 4 Furahini katika Bwana siku zote, tena nitasema, furahini.
\v 5 Upole wenu na ujulikane kwa watu wote. Bwana yuko karibu.
\v 6 Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali na kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.
\v 7 Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaada wa Kristo Yesu.
\p
\v 8 Hatimaye, ndugu zangu; yatakafarini sana mambo yote yenye ukweli, heshima, haki, usafi, upendo, na yale yenye taarifa njema, yenye busara, pamoja na yale yanayohitaji kusifiwa.
\v 10 Ninayo furaha kubwa sana juu yenu katika Bwana kwa kuwa ninyi mmeonyesha tena nia ya kujihusisha kwenu juu ya mahitaji yangu. Kwa kweli, hapo awali mlitamani kunijali kwa mahitaji yangu japo hamkupata fursa ya kunisaidia.
\v 11 Sisemi hivyo ili kujipatia kitu kwa ajili ya mahitaji yangu. Kwani nimejifunza kuridhika katika hali zote.
\v 12 Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhitaji.
\v 14 Hata hivyo, mlifanya vyema kushiriki nami katika dhiki zangu.
\p
\v 15 Ninyi Wafilipi mnafahamu kwamba mwanzo wa injili nilipoondoka Makedonia, hakuna Kanisa lililoniwezesha katika mambo yanayohusu utoaji na kupokea isipokuwa ninyi pekee yenu.
\v 16 Hata nilipokuwa Thesalonike, ninyi mlinitumia msaada zaidi ya mara moja kwa ajili ya mahitaji yangu.
\v 18 Nimepokea vitu vyote, na sasa nimejazwa na vitu vingi. Nimepokea vitu vyenu kutoka kwa Epafradito. Ni vitu vizuri vyenye kunukia mithiri ya manukato, vyenye kukubalika ambavyo vyote ni sadaka inayompendeza Mungu.
\v 19 Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo.