# damu Msemo "damu" humaanisha kimiminika chekundu kinachotoka kwenye ngozi ya mtu panapokuwa na jeraha au kovu. Damu huleta virutubisho vitoavyo uhai kwa mwili mzima wa mtu. * Damu hutoa ishara ya uhai na inapomwagwa au kutolewa nje, hutoa ishara ya kupoteza maisha, au kifo * Watu waliotoa dhabihu kwa Mungu, waliua mnyama na waliimimina damu yake juu ya madhabahu. Hili lilitoa ishara ya dhabihu ya uhai wa mnyama kulipa dhambi za mtu. * Kwa kupitia kifo chake msabani, kiishara damu ya Yesu iliwasafisha watu kutoka katika dhambi zao na hulipa ile adhabu wanayostari kwa ajili ya dhambi hizo dhambi zao * Yale maelezo "nyama na damu" humaanisha wanadamu * Yale maelezo "mwili na damu yako mwenyewe" humaanisha watu wanaohusiana kizazi MAELEZO YA UFASIRI * Msemo huu sharti ufasiriwe na msemo unaotumika kwa damu katika lugha lengwa * Yale maelezo "mwili na damu" yangeliweza kufasiriwa kama "watu" au viumbe vyenye uhai." * Kulinga na muktatha, yale maelezo "nyama na damua yangu mwenyewe "waweza kufasiriwa kama "familia yangu mwenyewe" au "jamaa yangu mwenyewe" au watu wangu mwenyewe." * Endapo kutakuwa na maelezo yoyote katika lugha lengwa yanayotumika pamoja na maana hii, yangeweza kufasiri "mwili na damu" # roho, -a kiroho Msemo roho hulenga sehemu ya watu isiyo na maumbile isiyoweza kuonekana. Mtu anapokufa, roho yake huuacha mwili wake. Pia "roho" yaweza kumaanisha tabia au hali ya kujisikia. * Ule msemo "roho" waweza kumaanisha kiumbe kisicho na mwili unaoonekana, hasa roho ovu. * Roho ya mtu ni sehemu yake inayoweza kumjua Mungu na kuamini katika Yeye. * Kwa ujumla msemo "-a kiroho" hukielezea chochote katika ulimwengu usio na maumbile * Kwenye Biblia, hasa hulenga chochote kile kinachohusiana na Mungu, moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu. * Kwa mfano, "chakula cha kiroho" huhusiana na mafundisho ya Mungu yatoayo lishe kwa roho ya mtu, "Ile "hekima ya kiroho" humaanisha ufahamu na tabia adilifu inayotokana na uweza wa Roho Mtakatifu. * Mungu ni Roho naye aliumba viumbe roho wengine wasio na miili ya kuonekana. * Malaika ni viumbe roho, pamoja na wale walioasi dhidi ya Mungu na wakawa roho waovu. * Ule msemo "roho ya" pia waweza kumaanisha "kuwa na tabia bainishi za," kama vile katika, "roho ya hekima" au "katika roho ya Eliya." * Mifano ya "roho" kama nia au hisia ungejumuisha "roho ya woga" au "roho ya wivu" MAPENDEKEZO YA UFASIRI * Kwa kutegeana na muktadha, baadhi ya njia za kufasiri "roho" zinaweza kuhusisha, "kiumbe kisicho na maumbile" au "sehemu za ndani" au "utu wa ndani." * Katika mazingira mengine, ule msemo "roho" waweza kufasiriwa kama "roho ovu" au "kiumbe roho ovu" * Wakati mwingine ule musemo "roho" umetumika kuelezea hisia ya mtu aka vile, "roho yangu ilihuzunishwa katika utu wangu wa ndani." Hii pia yaweza kufasiriwa kama, "nilijisikia kuhuzunishwa rohoni mwangu" au "nilisikia kuhuzunishwa mno." * Kile kirai roho ya" chaweza kufasiriwa kama, "mwenendo wa, au ushawishi wa," au "nia ya" au fikira" # uweza, weuzo Ule msemo "uweza" humaanisha uwezo wa kufanya mambo au kusababisha mambo yatokee, mara kwa mara kwa kutumia nguvu kubwa. "Uwezo" humaanisha watu au roho zenye uwezo wa kusababisha mambo kutokea. * Ule "uweza" wa Mungu hurejelea uwezon wa Mungu wa kufanya mambo yatokee, hasa mambo yasiyowezekana kwa watu kuyatenda. * Mungu anauweza kamili juu ya kila kitu ambacho amekiumba * ungu huwapa watu wake uwezo wa kufanya kile atakacho, ili kwamba wanapoponya watu au kutenda miujiza, wawe wanafanya hivi kwa uweza wa Mungu. MAPENDEKEZO YA UFASIRI * Kwa kutegemeana na muktadha, ule msemo "uweza" pia wawweza kufasiriwa kama "uwezo" au "nguvu" au "bidii" au "uwezo wa kutenda miujiza au kudhibiti." * Njia zinazowezekana kufasiri msemo "uweza" yaweza kuhusisha "wenye uhai walio na uwezo mkubwa" au roho zenye kutawala" au "wale wanaotawala wengine" * Yale maelezo kama vile "utuokoe kutoka katika nguvu za adui zetu" waweza kufasiriwa kama, "utuokoe kutokana na kugandamizwa na adui zetu" au "utuokoe kutoka katika kutawaliwa na adui zetu." Katika hali hii, "uweza" una maana ya kutumia nguvu za mwingine kudhibiti na kugandamiza wangine.