# Maelezo ya jumla Danieli anaendelea kumwomba Mungu juu ya watu wa Israeli. # Tumetenda dhambi na tumefanya yaliyo mabaya Virai hivi viwili vinaelezea wazo moja katika njia mbili ili kutia mkazo. # Tumeenenda kwa uovu na tumeasi Virai hivi viwili vinaelezea wazo moja katika njia mbili ili kutia mkazo. # amri na maagizo yako Maneno haya "amri na maagizo" yana maana moja na yanarejelea sheria zote kwa ujumla. # Hatujawasikiliza watumishi wako Mahali hapa "hatujawasikiliza" ina maana kwamba hawakuutii ujumbe wao. # kwa jina lako Neno "jina" linarejea mamlaka ya Mungu. "kuzungumza kwa mamlaka" # watu wote wa nchi Mahali hapa neno "nchi" linairejelea Israeli. "watu wa Israeli."