# Maneno kwa Ujumla: hili ni tukio linalofuata katika simulizi,ambalo Yesu anapanda kwenda Yerusalemu na anamponya mtu.Mistari hii inatoa mambo ya nyuma kuhusu mwanzoni mwa simulizi. # Baada ya hili ina maanisha baada Yesu kumponya mwana wa afisa. ona namna ambavo unaweza kufasiri hili. # kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi "Wayahudi walikuwa wakisherehekea sikukuu" # alipanda kwenda Yerusalemu Yerusalemu iko juu ya kilima. Mabarabara ya Yerusalemu yalipanda juu na kutelemka katika vilima vidogo . Kama lugha yako ina neno tofauti kwa kupanda juu ya kilima kuliko kuliko kutembea katika tambarare unaweza kuitumia hapa. # dimbwi hili lilikuwa ni shimo chini ambalo watu walijaza maji. Wakati mwingine walilizungushia kwa vigae na mawe. # Bethzatha "Bethzatha" maana yake ni nyumba ya huruma. # matao muundo ulioezekwa angalau pasipo kuwa ukuta mwingine katika jengo. # Idadi kubwa ya watu "watu wengi"