# Taarifa ya jumla: Bwana anazungumza. # Efraimu alipozungumza Hosea ametumia neno Efraimu kumaanisha ufalme mzima wa kaskazini, japokuwa lilikuwa jina la moja ya makabila kumi na mbili. # kulikuwa na tetemeko "kulikuwa na tetemeko kati ya watu" # Alijikuza katika Israeli "kujikuza" ni kujifanya wa muhimu. # lakini akawa na hatia kwa sababu ya ibada ya Baali, naye akafa Watu wa Efraimu walipoanza kuabudu Baali wakawa dhaifu na adui zao wakawashinda. # Sasa wanafanya dhambi zaidi na zaidi. Hawa ni watu wa kabila la Efraimu na taifa zima la Israeli. # Watu hawa watoao dhabihu na kumbusu ndama Sehemu ya kuabudu sanamu ni kwa kuibusu sanamu ambayo ni sanamu ya ndama.