Sura hii inaeleza kwamba Yesu alikuja kwa Wayahudi kwa sababu Mungu alikuwa akitimiza sehemu yake ya agano lake na Abrahamu. Petero alifikiri kwamba Wayahudi ndio waliokuwa na hatia ya kumuua Yesu.
Warumi ndio waliomuua Yesu, lakini walimuua kwa sababu Wayahudi walimkamata, wakamleta kwa Warumi, wakawaambia wamuue. Kwa sababu hii, Petero alifikiri kwamba hao ndio waliokuwa na hatia ya kumuua Yesu. Lakini anawaeleza yakwamba hao ndio wa kwanza ambao Mwenyezi Mungu ametuma wafuasi wa Yesu kuwakaribisha watubu (Luka 3:26). (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/repent]])