sw_gen_text_reg/50/18.txt

1 line
435 B
Plaintext

\v 18 Ndugu zake pia wakaenda na kuinamisha nyuso zao mbele zake. Wakasema, "Tazama, sisi ni watumishi wako." \v 19 Lakini Yusufu akawajibu, "Msiogope, Je mimi ni badala ya Mungu? \v 20 Lakini kwenu, mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, kuhifadhi maisha ya watu wengi, kama mwonavyo leo. \v 21 Hivyo basi msiogope. Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo." Kwa njia hii aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole.