sw_gen_text_reg/50/10.txt

1 line
403 B
Plaintext

\v 10 Hata walipokuja katika sakafu ya kupuria ya Atadi upande mwingine wa Yordani, wakaomboleza kwa majonzi ya huzuni kubwa. Yusufu akafanya maombolezo ya siku saba kwa ajili ya babaye pale. \v 11 Wenyeji wa nchi, Wakanaani, walipoona maombolezo katika sakafu ya Atadi, wakasema, "Hili ni tukio la kuhuzunisha sana kwa Wamisri." Ndiyo maana eneo hilo likaitwa Abeli Mizraimu, lililoko mbele ya Yordani.