sw_gen_text_reg/47/29.txt

1 line
472 B
Plaintext

\v 29 Wakati wa kufa kwake Yakobo ulipokaribia, alimwita Yusufu mwanaye na kumwambia, "Ikiwa nimepata kibali mbele zako, weka mkono wako chini ya paja langu, na unitendee kwa uaminifu na kweli. Tafadhari usinizike Misri. \v 30 Nitakapolala na baba zangu, utanitoa Misri na kunizika katika eneo la kuzikia la baba zangu." Yusufu akasema, "Nitafanya kama ulivyosema." \v 31 Israeli akasema, "Niapie," na Yusufu akamwapia. Kisha Israeli akainama chini mbele ya kitanda chake.