sw_gen_text_reg/47/20.txt

1 line
436 B
Plaintext

\v 20 Hivyo Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri. Kwani kila Mmisri akauza shamba lake, kwa sababu njaa ilikuwa kali sana. Kwa njia hii, nchi ikawa mali ya Farao. \v 21 Na watu, akawafanya kuwa watumwa kutoka mpaka mmoja wa Misri hata mkapa mwingine. \v 22 Ilikuwa ni nchi ya makuhani pekee ambayo Yusufu hakuinunua, kwa maana makuhani walikuwa wakipewa posho. Walikula katika sehemu aliyowapa Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.