sw_gen_text_reg/47/15.txt

1 line
474 B
Plaintext

\v 15 Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha, Wamisri wote wakaja kwa Yusufu wakisema, "Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?" \v 16 Yusufu akasema, "Ikiwa pesa yenu imekwisha, leteni wanyama wenu nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu." \v 17 Hivyo wakaleta wanyama wao kwa Yusufu. Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi, kondoo, mbuzi na kwa punda. Akawalisha kwa mkate kwa kubadilisha na wanyama wao mwaka ule.