sw_gen_text_reg/47/07.txt

1 line
377 B
Plaintext

\v 7 Kisha Yusufu akamwingiza Yakobo baba yake na kumweka mbele ya Farao. Yakobo akambariki Farao. \v 8 Farao akamwambia Yakobo, "Umeishi kwa muda gani?" \v 9 Yakobo akamwambia Farao, "Miaka ya safari zangu ni mia moja na thelathini. Miaka ya maisha yangu imekuwa mifupi na ya maumivu. Siyo kama miaka ya baba zangu." \v 10 Kisha Yakobo akambariki Farao na kuondoka mbele zake.