sw_gen_text_reg/38/27.txt

1 line
255 B
Plaintext

\v 27 Muda wake wa kujifungua ukafika, tazama, mapacha walikuwa tumboni mwake. \v 28 Ikawa alipokuwa akijifungua mmoja akatoa mkono nje, na mkunga akachukua kitambaa cha rangi ya zambarau na kukifunga katika mkono wake na kusema, "Huyu ametoka wa kwanza."