sw_gen_text_reg/38/24.txt

1 line
457 B
Plaintext

\v 24 Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, "Tamari mkweo amefanya ukahaba, na kwa hakika, yeye ni mjamzito." Yuda akasema, "Mleteni hapa ili achomwe." \v 25 Alipoletwa nje, alipeleka ujumbe kwa mkwewe, "Mimi ni mjamzito kwa mtu mwenye vitu hivi." Akasema, "Tambua tafadhari, mhuri huu na mshipi na fimbo ni vya nani." \v 26 Yuda akavitambua na kusema, "Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwani sikumpa Shela, mwanangu awe mme wake." Hakulala naye tena.