sw_gen_text_reg/37/01.txt

1 line
338 B
Plaintext

\v 1 Yakobo akaishi katika nchi aliyokaa babaye, katika nchi ya Kanaani. \v 2 Haya ndiyo matukio yaliyomhusu Yakobo. Yusufu, aliyekuwa kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akilichunga kundi pamoja na ndugu zake. Alikuwa pamoja na wana wa Bilha na pamoja na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akaleta taarifa yao mbaya kwa baba yao.