|
\v 1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (aliyeitwa pia Edom). \v 2 Esau akachukua wakeze kutoka kwa Wakanaani. Hawa walikuwa wake zake: Ada binti Eloni Mhiti; Oholibama binti Ana, mjukuu wa Zibeoni Mhivi; na \v 3 Basemathi, binti Ishmaeli, dada wa Nebayothi. |