sw_gen_text_reg/35/16.txt

1 line
552 B
Plaintext

\v 16 Wakaendelea na safari kutoka Betheli. Walipokuwa kitambo kabla ya kufika Efrathi, Raheli akashikwa na uchungu. \v 17 Akawa na utungu mzito. Alipokuwa katika utungu mzito zaidi, mkunga akamwambia, "Usiogope, kwani sasa utapata mtoto mwingine wa kiume." \v 18 Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho akamwita jina lake Benoni, lakini baba yake akamwita jina lake Benjamini. \v 19 Raheli akafa na kuzikwa katika njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). \v 20 Yakobo akaweka nguzo katika kaburi lake. Ndiyo alama ya kaburi la Raheli hata leo.