sw_gen_text_reg/35/01.txt

1 line
467 B
Plaintext

\v 1 Mungu akamwambia Yakobo, "Inuka, panda kwenda Betheli, na ukae pale. Unijengee madhabahu pale, niliyekutokea pale ulipomkimbia Esau kaka yako." \v 2 Kisha Yakobo akawambia nyumba yake na wote aliokuwa nao, "Wekeni mbali miungu yote ya kigeni iliyo kati yenu, jitakaseni wenyewe, na kubadili mavazi yenu. \v 3 Kisha tuondoke na kwenda Betheli. Nitajenga pale madhabahu kwa Mungu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, naye amekuwa pamoja nami kila nilikokwenda.