sw_gen_text_reg/31/26.txt

1 line
329 B
Plaintext

\v 26 Labani akamwambia Yakobo, "Umefanya nini, kwamba umewachukua binti zangu kama mateka wa vita? \v 27 Kwa nini umekimbia kwa siri na kunihadaa kwa kutokuniambia? Ningekuruhusu uondoke kwa sherehe na kwa nyimbo, kwa matari na vinubi. \v 28 Haukuniacha niwabusu wajukuu wangu na binti zangu kwa kuwaaga. Basi umefanya upumbavu.