sw_gen_text_reg/29/23.txt

1 line
336 B
Plaintext

\v 23 Wakati wa jioni, Labani akamchukua Lea binti yake mkubwa na kumleta kwa Yakobo, aliyelala naye. \v 24 Labani akampa mtumishi wake wakike Zilpa kuwa mjakazi wa Lea. \v 25 Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, "Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa?