sw_gen_text_reg/29/15.txt

1 line
425 B
Plaintext

\v 15 Kisha Labani akamwambia Yakobo, "Je unitumikie bure kwa kuwa wewe ni ndugu yangu? Niambie, ujira wako utakuwaje? \v 16 Basi Labani alikuwa na binti wawili. Jina la mkubwa lilikuwa ni Lea, na jina la mdogo lilikuwa Raheli. \v 17 Macho ya Lea yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo na mwonekano. \v 18 Yakobo alimpenda Raheli, hivyo akasema, "Nitakutumikia miaka saba kwa ajili ya Raheli, binti yako mdogo."