sw_gen_text_reg/24/39.txt

1 line
454 B
Plaintext

\v 39 Nikamwambia bwana wangu, pengine mwanamke huyo asikubali kufuatana nami.' \v 40 Lakini akaniambia, Yahwe, ambaye ninakwenda mbele yake, atatuma malaika wake pamoja nawe na atakufanikisha njia yako, kwamba utapata mke kwa ajili ya mwangu kutoka miongoni mwa ndugu zangu na kutoka katika ukoo wa baba yangu. \v 41 Lakini utakuwa huru katika kiapo changu ikiwa utafika kwa ndugu zangu na wasikuruhusu kuja naye. Ndipo utakuwa huru katika kiapo changu.