sw_gen_text_reg/24/28.txt

1 line
500 B
Plaintext

\v 28 Kisha yule msichana akakimbia na kwenda kuwaeleza watu wa nyumba ya mama yake juu ya mambo yote haya. \v 29 Na sasa Rebeka alikuwa na kaka yake, jina lake aliitwa Labani. Labani akakimbia kwa yule mtu aliye kuwa nje barabarani karibu na kisima. \v 30 Akisha kuona hereni ya puani pamoja na zile bangili kwenye mikono ya dada yake, na kusikia maneno ya Rebeka dada yake, "Hivi ndivyo yule mtu alicho niambia," alikwenda kwa yule mtu, na, Tazama, alikuwa amesimama karibu na ngamia pale kisimani.