sw_gen_text_reg/22/07.txt

1 line
353 B
Plaintext

\v 7 Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, "Baba yangu," naye akasema, " Ndiyo mwanangu." Akasema, "Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?" \v 8 Abraham akasema, "Mungu mwenyewe atatupatia mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mwanangu." Kwa hiyo wakaendelea, wote wawili pamoja.