sw_gen_text_reg/22/01.txt

1 line
556 B
Plaintext

\v 1 Ikawa kwamba baada ya mambo hayo Mungu akampima Abraham. Akamwambia, "Abraham!" Abraham akasema, "Mimi hapa." \v 2 Kisha Mungu akasema, "Mchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, na uende katika nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa mahali pale juu ya moja ya milima hiyo, ambayo nitakwambia." \v 3 Kwa hiyo Abraham akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukuwa vijana wake wawili, pamoja na Isaka mwanawe. Akakata kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akapanga safari kwenda mahali ambapo Mungu alimwambia.