sw_gen_text_reg/19/14.txt

1 line
384 B
Plaintext

\v 14 Lutu akatoka na akazungumza na wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake, akawambia, "Ondokeni upesi mahali hapa, kwa kuwa Yahwe anakaribia kuuangamiza mji." Lakini kwa wakwe zake alionekana kuwa anawatania. \v 15 Alfajiri, malaika wakamsihi Lutu, wakisema, ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili ambao wako hapa, ili kwamba usipotelee katika adhabu ya mji huu."