sw_gen_text_reg/16/05.txt

1 line
431 B
Plaintext

\v 5 Kisha Sarai akamwambia Abram, "Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe." \v 6 Lakini Abram akamwambia Sarai, "Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake." Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka.