\v 1 Sasa nchi yote ilikuwa inatumia lugha moja na ilikua na usemi mmoja. \v 2 Ikawa waliposafiri upande wa mashariki, wakaona eneo tambarare katika nchi ya Shinari na wakakaa pale.