sw_gen_text_reg/07/13.txt

1 line
387 B
Plaintext

\v 13 Katika siku iyo hiyo Nuhu pamoja na watoto wake, Shem, Ham, na Yafethi na mke wa Nuhu, na wale wake watatu wa wana wa Nuhu pamoja waliingia katika safina. \v 14 Waliingia pamoja na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho juu ya ardhi kwa jinsi yake, na kila aina ya ndege kwa jinsi yake, kila aina ya kiumbe chenye mabawa.