sw_gen_text_reg/07/08.txt

1 line
287 B
Plaintext

\v 8 Wanyama ambao ni safi na wanyama ambao si safi, ndege, na kila kitambaacho juu ya ardhi, \v 9 wawili wawili mume na mke wakaja kwa Nuhu na wakaingia katika safina, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza Nuhu. \v 10 Ikawa kwamba baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya nchi.