sw_gen_text_reg/01/11.txt

1 line
373 B
Plaintext

\v 11 Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake." Ikawa hivyo. \v 12 Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. \v 13 Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu.