sw_ulb/65-3JN.usfm

31 lines
2.0 KiB
Plaintext

\id 3JN
\ide UTF-8
\h 3 Yohana
\toc1 3 Yohana
\toc2 3 Yohana
\toc3 3jn
\mt 3 Yohana
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Mimi Yohana Mzee, nakuandikia Gayo mpenzi, ninayempenda katika kweli.
\v 2 Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa.
\v 3 Maana nilifurahi sana wakati nilipoambiwa na waumuni waliokuja na kutoa ushuhuda juu ya kweli yako, kama vile unavyoenenda katika kweli.
\v 4 Sina furaha kubwa zaidi ya hii, kusikia kwamba watoto wangu wa kiroho wanatembea katika kweli.
\v 5 Mpendwa, unaenenda kwa uaminifu kwa Mungu unapowahudumia ndugu na wageni,
\v 6 wageni wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa. Unafanya vizuri kuwasaidia kuwasafirisha katika safari zao kwa namna ambayo inampendeza Mungu.
\p
\v 7 Kwa ajili ya Jina la Yesu, walienda bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa watu wa Mataifa.
\v 8 Hivyo, tunatakiwa kuwakaribisha watu kama hawa, ili tuwe watenda kazi tukishirikiana kwa ajili ya kutangaza kweli ya Mungu.
\p
\v 9 Nimekuandikia wewe pamoja na kusanyiko jambo fulani, lakini Diotrofe, anayependa kujifanya kuwa kiongozi miongoni mwa waumini, hakubaliani na mimi Yohana na waumini wenzangu.
\v 10 Hivyo, kama nikija nitayakumbuka matendo yake anayoyafanya, jinsi anavyosema maneno mabaya yakutushutumu kinyume nasi. Hajaridhika na matendo haya, yeye mwenyewe Diotrofe hawapokei waumini. Pia huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao waumini na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko.
\p
\v 11 Mpenzi, Gayo usiige kilicho kibaya, bali iga kilicho chema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu; na yeye atendaye mabaya hajamwamini Mungu.
\p
\v 12 Demetrio ameshuhudiwa na wote na kweli yenyewe. Sisi pia ni mashahidi, na unajua kuwa ushahuhuda wetu ni wa kweli.
\p
\v 13 Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa kalamu na wino.
\v 14 Bali ninatarajia kukuona hivi karibuni, na tutaongea nawe ana kwa ana.
\v 15 Amani iwe pamoja nawe. Marafiki nilionao hapa wanakusalimu. Pia nawasalimu marafiki kila mmoja kwa jina lake.