sw_ulb/42-MRK.usfm

948 lines
78 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id MRK
\ide UTF-8
\h Marko
\toc1 Marko
\toc2 Marko
\toc3 mrk
\mt Marko
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Huu ndio mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
\v 2 Kama ilivyoandikwa na nabii Isaya, “Tazama, ninamtuma mjumbe wangu mbele yako, mmoja atakayetayarisha njia yako.
\q
\v 3 Sauti ya mtu aliaye nyikani, “Ikamilisheni njia ya Bwana; zinyosheni njia zake.”
\p
\v 4 Yohana alikuja, akibatiza nyikani na kuhubiri ubatizo wa toba iletayo msamaha wa dhambi.
\v 5 Nchi yote ya Yudea na watu wote wa Yerusalemu walikwenda kwake. Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yordani, wakiungama dhambi zao.
\v 6 Yohana alikuwa anavaa vazi la singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake, na alikuwa anakula nzige na asali ya porini.
\v 7 Alihubiri na kusema, “Yupo mmoja anakuja baada yangu mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, na sina hadhi hata ya kuinama chini na kufungua kamba za viatu vyake.
\v 8 Mimi niliwabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu.”
\p
\v 9 Ilitokea katika siku hizo kwamba Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, na alibatizwa na Yohana katika mto Yordani.
\v 10 Naye Yesu alipoinuka kutoka kwenye maji, aliona mbingu zimefunguka wazi na Roho akishuka juu yake kama mfano wa njiwa.
\v 11 Na sauti ilitoka mbinguni, “Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe.”
\v 12 Kisha mara moja Roho akamwongoza kwenda nyikani.
\v 13 Alikuwako nyikani siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu na malaika walimhudumia.
\p
\v 14 Sasa baada ya Yohana kukamatwa, Yesu alikuja Galilaya akitangaza injili ya Mungu,
\v 15 akisema, “Muda umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuamini katika injili.”
\p
\v 16 Na alipokuwa anapita kando ya bahari ya Galilaya, alimwona Simoni na Andrea ndugu wa Simoni wakitupa nyavu zao katika bahari, kwa kuwa walikuwa wavuvi.
\v 17 Yesu aliwaambia, “Njooni, nifuateni, na nitawafanya wavuvi wa watu.”
\v 18 Na mara moja waliacha nyavu na wakamfuata.
\v 19 Wakati Yesu alipotembea umbali kidogo, alimwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; walikuwa kwenye mtumbwi wakitengeneza nyavu.
\v 20 Mara aliwaita na wao walimwacha baba yao Zebedayo ndani ya mtumbwi na watumishi waliokodiwa, wakamfuata.
\p
\v 21 Na walipofika Kaperinaumu, siku ya Sabato, Yesu aliingia kwenye sinagogi na kufundisha.
\v 22 Walilishangaa mafundisho yake, kwa vile alikuwa akiwafundisha kama mtu ambaye ana mamlaka na siyo kama waandishi.
\v 23 Wakati huo huo kulikuwa na mtu katika sinagogi lao aliyekuwa na roho mchafu, na alipiga kelele,
\v 24 akisema, “Tuna nini cha kufanya na wewe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani. Wewe ni Mtakatifu wa Mungu!”
\p
\v 25 Yesu alimkemea pepo na kusema, “Nyamaza na utoke ndani yake!”
\v 26 Na roho mchafu alimwangusha chini na akatoka kwake akilia kwa sauti ya juu.
\p
\v 27 Na watu wote walishangaa, hivyo wakaulizana kila mmoja, “Hii ni nini Ni mafundisho mapya yenye mamlaka? Hata huamuru pepo wachafu nao wanamtii!”
\v 28 Na habari kuhusu yeye mara moja zikasambaa kila mahali ndani ya mkoa wote wa Galilaya.
\p
\v 29 Na mara moja baada ya kutoka nje ya sinagogi, waliingia nyumbani mwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana.
\v 30 Mama mkwe wa Simoni alikuwa amelala mgonjwa wa homa, na mara moja walimwambia Yesu habari zake.
\v 31 Hivyo alikuja, alimshika kwa mkono, na kumwinua juu; homa ikaondoka kwake, na akaanza kuwahudumia.
\p
\v 32 Jioni hiyo wakati jua limekwisha zama, walimletea kwake wote waliokuwa wagonjwa, na waliopagawa na mapepo.
\v 33 Mji wote walikusanyika pamoja nje ya mlango.
\v 34 Aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa wa magonjwa mbalimbali na kutoa mapepo mengi, bali hakuruhusu mapepo kuongea kwa sababu walimjua.
\p
\v 35 Aliamka asubuhi na mapema, wakati kulikuwa bado giza; aliondoka na kwenda mahali pa faragha na aliomba huko.
\v 36 Simoni na wote waliokuwa pamoja naye walimtafuta.
\v 37 Walimpata na wakamwambia, “Kila mmoja anakutafuta”
\p
\v 38 Aliwaambia, “Tunapaswa kwenda mahali pengine, nje katika miji inayozunguka, ili niweze kuhubiri huko pia. Ndiyo sababu nilikuja hapa.”
\v 39 Alikwenda akipita Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kukemea mapepo.
\p
\v 40 Mwenye ukoma mmoja alikuja kwake. Alikuwa akimwomba; alipiga magoti na alimwambia, “Kama unataka, waweza kunifanya niwe safi.”
\p
\v 41 Yesu alimwonea huruma, alinyosha mkono wake na kumgusa, akimwambia, “Ninataka, uwe msafi.”
\v 42 Mara moja ukoma ukamtoka, na alifanywa kuwa msafi.
\v 43 Yesu akamwonya vikali na akamwambia aende mara moja,
\v 44 Alimwambia, “Hakikisha hausemi neno kwa yeyote, lakini nenda, ujionyeshe kwa kuhani, na utoe dhabihu kwa ajili ya utakaso ambayo Musa aliagiza, kama ushuhuda kwao.”
\v 45 Lakini alikwenda na kuanza kumwambia kila mmoja na kueneza neno zaidi hata Yesu hakuweza tena kuingia mjini kwa uhuru. Hivyo alikaa mahali pa faragha na watu walikuja kwake kutoka kila mahali.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Yesu aliporudi Kapernaumu baada ya siku chache walisikia kwamba yupo nyumbani.
\v 2 Watu wengi sana walikusanyika pale na haikuwepo nafasi tena, hata ile ya mlangoni, na Yesu alisema neno kwao.
\v 3 Kisha baadhi ya watu walikuja kwake waliomleta mtu aliyekuwa amepooza; watu wanne walikuwa wamembeba.
\v 4 Wakati waliposhindwa kumpitisha kwa sababu ya umati wa watu, waliondoa paa juu mahali pale alipokuwa Yesu. Na walipokuwa wamekwishatoboa tundu, walishusha kitanda ambacho mtu aliyepooza alikuwa amelala.
\v 5 Alipoiona imani yao, Yesu alimwambia mtu aliyepooza, “mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.”
\p
\v 6 Lakini baadhi ya waandishi wale waliokuwa wamekaa pale walijihoji mioyoni mwao,
\v 7 “Mtu huyu anawezaje kusema hivi? Anakufuru! Nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”
\p
\v 8 Mara Yesu alijua rohoni mwake walichokuwa wakifikiri miongoni mwao wenyewe. Aliwaambia, “Kwa nini mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
\v 9 Lipi ni jepesi zaidi kusema kwa mtu aliyepooza, Dhambi zako zimesamehewa au kusema Simama, chukua kitanda chakomkeka wako, na utembee?
\v 10 Lakini ili wapate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi katika dunia, alimwambia yule aliyepooza,
\v 11 “Inuka, chukua mkeka wako, na uende nyumbani kwako.”
\p
\v 12 Alisimama na mara moja akachukua mkeka wake, na alienda nje ya nyumba mbele ya kila mtu, hivyo wote wakashangaa na wakampa Mungu utukufu, nakusema “Kamwe, hatujawahi kuona jambo kama hili.”
\p
\v 13 Alienda tena kando ya ziwa, na umati wote wa watu walikuja kwake, na akawafundisha.
\v 14 Alipokuwa akipita alimwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi kwenye sehemu ya kukusanyia kodi na akamwambia, “Nifuate.” Alisimama na kumfuata.
\p
\v 15 Na wakati Yesu alipokuwa akipata chakula katika nyumba ya Lawi, wakusanya kodi wengi na watu wenye dhambi walikuwa wakila na Yesu na wanafunzi wake, kwa kuwa walikuwa wengi nao walimfuata.
\v 16 Wakati waandishi, ambao walikuwa Mafarisayo, walipoona kwamba Yesu alikuwa akila na watu wenye dhambi na wakusanya kodi, waliwaambia wanafunzi wake, “Kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?”
\p
\v 17 Wakati Yesu aliposikia hivi aliwaambia, “Watu walio na afya katika mwili hawamhitaji tabibu; ni watu wagonjwa pekee ndio wanamhitaji. Sikuja kuwaita watu wenye haki, lakini watu wenye dhambi.”
\p
\v 18 Wanafunzi wa Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Na baadhi ya watu walikuja kwake na kumwambia, “Kwa nini wanafunzi wa Yohana na mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
\p
\v 19 Yesu aliwaambia, “Je waliohudhuria harusi wanaweza kufunga wakati bwana harusi bado akiwa pamoja nao? Kwa vyovyote bwana harusi akiwa bado yuko pamoja nao hawawezi kufunga.”
\v 20 Lakini siku zitakuja wakati bwana harusi atakapoondolewa kwao, na katika siku hizo wao watafunga.
\p
\v 21 Hakuna mtu ashonaye kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu, vinginevyo kiraka kitararuka kutoka katika hilo, kipya kitararuka kutoka katika kikuukuu, nayo itachanika zaidi.
\v 22 Hakuna mtu atiaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu, vinginevyo divai itavipasua viriba na vyote viwili divai na viriba vitapotea. Badala yake, weka divai mpya katika viriba vipya.”
\p
\v 23 Katika siku ya Sabato Yesu alipita kwenye baadhi ya mashamba, na wanafunzi wake walianza kuchukua baadhi ya masuke ya ngano.
\v 24 Na Mafarisayo walimwambia, “Tazama, kwa nini wanafanya kitu ambacho ni kinyume cha sheria katika siku ya Sabato?”
\p
\v 25 Aliwaambia, “Hamkusoma kile alichofanya Daudi alipokuwa katika uhitaji na njaa—yeye pamoja na watu waliokuwa pamoja naye?
\v 26 Jinsi alivyoenda katika nyumba ya Mungu wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu na akala mkate uliowekwa mbele—ambao ilikuwa kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kula isipokuwa makuhani— tu. Na aliwapa hata baadhi ya wale waliokuwa pamoja naye?”
\v 27 Yesu alisema, “Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, siyo mwanadamu kwa ajili ya Sabato.
\v 28 Kwa hiyo, Mwana wa Adamu ni Bwana, wa Sabato.”
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Tena Yesu aliingia ndani ya sinagogi na palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza.
\v 2 Baadhi ya watu walikuwa wakimfuatilia kwa ukaribu kuona kama atamponya siku ya Sabato ili wamshitaki.
\v 3 Yesu alimwambia mtu mwenye mkono uliopooza, “Inuka simama katikati ya umati huu.”
\v 4 Kisha akawaambia wale watu, “Je ni halali kutenda tendo jema siku ya Sabato au kutenda yasiyo haki; kuokoa maisha, au kuua?” Lakini hawakujibu walibaki kimya.
\v 5 Akawatazama kwa hasira, akihuzunika kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, na akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha na Yesu akamponya mkono wake.
\v 6 Mafarisayo wakaenda nje wakafanya njama pamoja na Maherodi dhidi yake ili kumuua.
\p
\v 7 Kisha Yesu, pamoja na wanafunzi wake, walienda baharini, na umati mkubwa wa watu uliwafuata ukitokea Galilaya na Uyahudi
\v 8 na kutoka Yerusalemu na Idumaya na mbele ya Yordani na jirani ya Tiro na Sidoni, umati mkubwa, uliposikia kila kitu alichokuwa anakifanya, walikuja kwake.
\v 9 Na aliwaambia wanafunzi wake kuandaa mtumbwi mdogo kwa ajili yake kwa sababu ya umati, ili kwamba wasije wakamsonga.
\v 10 Kwa kuwa aliwaponya wengi, kila mtu aliyekuwa na mateso alikuwa na shauku ya kumfikia ili amguse apone.
\v 11 Popote roho wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia, na walisema, “Wewe ni Mwana wa Mungu.”
\v 12 Aliwakemea kwa msisitizo wasimfanye akajulikana.
\p
\v 13 Alipanda juu ya mlima, na akawaita aliowataka, na wakamwendea.
\v 14 Akawachagua kumi na wawili (aliowaita mitume), ili kwamba wawe pamoja naye na akawatuma kuhubiri,
\v 15 na kuwapa mamlaka ya kutoa mapepo.
\v 16 Na akawachagua kumi na wawili: Simoni, aliyempa jina la Petro,
\v 17 Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, aliyepewa jina la Bonagesi, hao ni, wana wa ngurumo,
\v 18 na Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
\v 19 na Yuda Iskariote, ambaye atamsaliti.
\p
\v 20 Kisha alienda nyumbani, na umati wa watu wakimfuata kwa pamoja, tena, hata wasiweze kula hata mkate.
\v 21 Familia yake waliposikia habari hiyo, walienda kumkamata, kwani walisema, “Amerukwa na akili.”
\p
\v 22 Waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli,” na, “KwaNi mtawala wa mapepo na anatoa mapepo.”
\p
\v 23 Yesu aliwaita kwake na kusema nao kwa mifano, “Jinsi gani Shetani aweza kumtoa Shetani?
\v 24 Kama ufalme ukigawanyika wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama.
\v 25 Kama nyumba ikigawanyika yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
\v 26 Kama Shetani atainuka kinyume chake mwenyewe na kugawanyika, hawezi kusimama, na atakuwa amefika mwisho wake.
\v 27 Lakini hakuna hata mmoja awezaye kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuiba vitu vyake bila kumfunga kwanza, na kisha kukusanya vilivyomo nyumbani.
\v 28 Kweli nawambieni, dhambi zote za wana wa watu zitasamehewa, pamoja na kufuru ambazo wanatamka,
\v 29 lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, bali ana hatia ya dhambi ya milele.”
\p
\v 30 Yesu alilisema hili kwa sababu walikuwa wakisema, “Ana roho mchafu.”
\p
\v 31 Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakatuma mtu, kumwita.
\v 32 Na umati wa watu uliokuwa umekaa umeketi karibu naye wakamwambia, “mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe.”
\p
\v 33 Aliwajibu, “Ni nani mama yangu na ndugu zangu?”
\v 34 Aliwatazama waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, “Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu!
\v 35 Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu.”
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 Tena alianza kufundisha kando ya bahari, na umati mkubwa ulikusanyika ukamzunguka. Akaingia ndani ya mtumbwi baharini, na kuketi ndani ya mtumbwi. Umati wote ulikuwa pembeni mwa bahari ufukweni.
\v 2 Na akawafundisha mambo mengi kwa mafumbo, na akawaambia katika mafundisho yake.
\v 3 “Sikilizeni, mpanzi alienda kupanda mbegu.
\v 4 Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani, na ndege wakaja wakazila.
\v 5 Mbegu zingine zilianguka kwenye mwamba, ambako hapakuwa na udongo mwingi. Maramoja zikaibuka, kwa sababu haikua na udongo ya kutosha.
\v 6 Lakini jua lilipochomoza, mimea zilinyauka, kwa sababu hayakua na mizizi, zilikauka.
\v 7 Mbegu ziingine zilianguka katikati ya miiba. Miiba ilikua na ikazisonga, na hazikuzaa matunda yoyote.
\v 8 Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na zikazaa matunda wakati zikikua na kuongezeka na kuzaa mara thelathini zaidi, sitini, na pia mara mia moja.”
\v 9 Na akasema, “Yeyote mwenye masikio ya kusikia, na asikie!”
\p
\v 10 Yesu alipokuwa peke yake, wale waliokuwa karibu naye na wale kumi na wawili walimuuliza kuhusu mafumbo.
\v 11 Akawaambia, “Kwenu ninyi Mungu amewafunulia siri za ufalme wake. Lakini kwa walio nje kila kitu ni kwa mafumbo,
\q
\v 12 ili wakitazama, ndiyo watazame, lakini wasione, na wakisikia, ndiyo watasikia, lakini wasielewe, ama sivyo wakageuka na Mungu atawasamehe.”
\p
\v 13 Yesu akawaambia, “Je hamuelewi mfumbo huu? Sasa mtawezaje kuelewa mifano mingine?”
\v 14 Mpanzi alipanda neno.
\v 15 Hawa ndio wale walio kando ya njia, mahali neno lilipopandwa. Walipolisikia, maramoja Shetani akaja na kulichukua neno ambalo lilipandwa ndani yao.
\v 16 Na baadhi ni mbegu zilizopandwa juu ya mwamba; ambao, wanapolisikia neno wanalipokea mara moja kwa furaha.
\v 17 Lakini hawana mizizi yoyote ndani yao, lakini huvumilia kwa muda. Baadaye wakati dhiki na mateso yanapokuja kwa sababu ya neno, mara moja huacha imani.
\v 18 Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba. Wale ambao hulisikia neno,
\v 19 lakini masumbuko ya dunia na udanganyifu wa mali na tamaa za mambo mengine huja na kulisonga neno, na haina tija.
\v 20 Wale ambao walipandwa kwa udongo mzuri ni wale wanaoskia neno, kulipokea na huzaa matunda, thelathini, sitini, na mara mia moja zaidi.
\p
\v 21 Yesu akawaambia, “Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu au chini ya kitanda? Huileta ndani na kuiweka juu ya kinara.
\v 22 Kwa kuwa hakuna chochote kilichojificha ambacho hakitajulikana, na hakuna siri ambayo haitakua wazi.
\v 23 Yule aliye na masikio ya kusikia, na asikie!”
\p
\v 24 Akawaambia, “Muwe makini kwa kile mnachosikia, kwa kuwa kipimo mtatumia ndicho mtakachopimiwa, na zaidi yataongezwa kwenu.
\v 25 Kwa sababu yeye aliye nacho, ataongezewa zaidi, na yule asiye nacho, kwake kitachukuliwa hata kile alicho nacho.”
\p
\v 26 Akasema, “Ufalme wa Mungu ni kama mtu aliyepanda mbegu katika udongo.
\v 27 Anayelala usiku na kuamka asubuhi, na kukuta mbegu zimechipuka na kukua, ingawa hajui zilivyo chipuka.
\v 28 Aridhi huzaa nafaka yenyewe: kwanza majani, halafu maua, halafu nafaka iliyo komaa.
\v 29 Wakati mazao yameiva, yeye hutuma mara moja hupeleka mundu kwa maana mavuno yamefika.”
\p
\v 30 Na tena akasema, “ni nini tunaweza kulinganisha na ufalme wa Mungu, au ni mfumbo mgani tunaweza tumia kuieleza?
\v 31 Ni kama mbegu ya haradali, ambayo, inapopandwa, ni ndogo zaidi kuliko mbegu zote duniani.
\v 32 Hata, wakati imepandwa, hukua kubwa zaidi ya mimea yote ya bustani, na huunda matawi makubwa, kwahivyo ndege wa angani wanaweza kutengeneza viota kwa kivuli chake.”
\p
\v 33 Mafumbo mengi kama hii, yesu alinena nao neno, kwa kadri walivyoweza kuelewa,
\v 34 na hakusema nao bila mafumbo. Lakini alipokuwa peke yake, aliwaelewesha wanafunzi wake.
\p
\v 35 Siku hiyo, wakati wa jioni ulipofika, akawaambia, “Twendeni ng'ambo ile ingine.”
\v 36 Hivyo wakauacha umati wa watu, wakamchukua Yesu, vile alivyokua, ndani ya mtumbwi. Kulikua na mitumbwi mingine yaliyoambatana naye.
\v 37 Dhoruba ya upepo mkali ikatokea, na mawimbi yalikuwa yakiingia ndani ya mashua hata mashua karibu kujaa maji.
\v 38 Lakini Yesu mwenyewe alikuwa numa ya meli, amelala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamuamsha wakamwambia, “Mwalimu, hujali kwamba tuko karibu kuangamia?”
\p
\v 39 Akaamka, akaukemea ule upepo, na akaiambia bahari, “Amani! Tulia” Ule upepo ukakoma, na kukawa na utulivu mkubwa.
\v 40 Akasema nao, “Mbona mnaogopa? Bado hamna Imani?”
\p
\v 41 Walijawa na hofu kubwa ndani yao na wakaambiana, “Huyu ni nani, hata upepo na bahari vinamtii?”
\c 5
\cl Sura 5
\p
\v 1 Walikuja mpaka ng'ambo ya bahari, katika mkoa wa Gerasi.
\v 2 Wakati Yesu alipokua akitoka kwa mtumbwi, mwanaume mwenye pepochafu alikuja kwake kutoka makaburini.
\v 3 Mtu huyu aliishi makaburini. Hakuna aliyeweza kumzuia kamwe, hata kwa kumfunga minyororo.
\v 4 Alikuwa amefungwa mara kadhaa kwa pingu na minyororo. Alikata minyororo na pingu zake zikavunjika. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu za kumshinda.
\v 5 Usiku na mchana akiwa makaburini na milimani, alilia na kujikata mwenyewe kwa mawe makali.
\v 6 Alipomwona Yesu kwa umbali, alimkimbilia na kuinama mbele yake.
\v 7 Akalia kwa sauti kubwa, “Nina shughuli gani na wewe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye Juu? Nakuomba kwa jina la Mungu mwenyewe, usinitese.”
\v 8 Kwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe roho mchafu.”
\p
\v 9 Yesu akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Naye alimjibu, “Jina langu ni Jeshi, kwa kuwa tuko wengi.”
\v 10 Alimsihi tena na tena asiwapeleke nje ya mkoa.
\v 11 Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe walikua wakilisha mlimani,
\v 12 nao walimsihi, wakisema, “Utupeleke ndani ya nguruwe; tuingie ndani yao.”
\v 13 Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu walimtoka na kuingia ndani ya nguruwe, nao nguruwe walikimbia chini ya kilima mwinuko mpaka baharini, na angalau nguruwe elfu mbili walizama baharini.
\p
\v 14 Na wale waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia nakwenda kutoa taarifa ya yaliyotendeka katika mji na mashambani, na watu wengi walitoka kwenda kuona kilichotokea.
\v 15 Walikuja kwa Yesu na kumuona mtu aliyepagawa na pepo, aliyekuwa amepagawa na Jeshi la mapepo, amekaa hapo, amevishwa na katika akili yake sawa na wakaogopa.
\v 16 Wale waliokuwa wameshudia kilichotendeka kwa mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo waliwaambia kilichotokea kwa undani, na pia kuhusu nguruwe.
\v 17 Nao walianza kumsihi Yesu aondoke katika mkoa wao.
\p
\v 18 Alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, yule aliyekuwa amepagawa na mapepo alimsihi kwamba aende pamoja naye.
\p
\v 19 Lakini Yesu hakumruhusu, lakini akamwambia, “Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako na uwaambie alichokufanyia Bwana, na huruma aliyokuonyesha.”
\v 20 Hivyo alienda na kuanza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake katika maeneo yote ya Dekapoli, na kila mtu alistaajabu.
\p
\v 21 Na wakati Yesu alipovuka tena upande mwingine ndani ya mtumbwi, umati mkubwa ulikusanyika karibu naye, alipokuwa kando ya bahari.
\v 22 Mmoja wa viongozi wa sinagogi aliyeitwa Yairo alikuja, na alipomwona, alianguka miguuni pake.
\v 23 Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, “Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili aweze kupata afya na kuishi.”
\v 24 Hivyo alienda pamoja naye, na umati mkubwa watu ulimfuata nao walisonga karibu wakimzunguka.
\p
\v 25 Kulikuwa na mwanamke kati yao ambaye damu yake ilikuwa inamtoka kwa miaka kumi na miwili.
\v 26 Aliteseka vya kutosha chini ya matabibu wengi na alitumia kila kitu alichokuwa nacho, lakini badala kuendelea vizuri hali yake iliendelea kuwa mbaya.
\v 27 Aliposikia habari kuhusu Yesu, alikuja nyuma yake katikati ya umati na akagusa vazi lake.
\v 28 Kwa kuwa alisema, “Kama nitayagusa mavazi yake, nitapona.”
\v 29 Alipomgusa, kutokwa damu kulikoma, na alijisikia katika mwili wake kwamba ameponywa kutoka mateso yake.
\p
\v 30 Na ghafla Yesu aligundua ndani yake mwenyewe kwamba nguvu zimemtoka. Akageuka katika ya umati ya watu na kuuliza, “Ni nani aliyeligusa vazi langu?”
\p
\v 31 Wanafunzi wake walimwambia, “Unaona umati huu umekusonga nawe wauliza, Ni nani aliyenigusa?’”
\v 32 Lakini Yesu alitazama pande zote kuona ambaye aliye mgusa.
\p
\v 33 Mwanamke huyo, akijua kilichomtendekea, aliogopa na kutetemeka. Alikuja na alianguka chini mbele yake na kumwambia ukweli wote.
\v 34 Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa amani na uponywe kutoka kwenye mateso yako.”
\p
\v 35 Yesu alipokuwa akizungumza, baadhi ya watu walikuja kutoka kwa kiongozi wa Sinagogi, wakisema, “Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua mwalimu?”
\p
\v 36 Lakini Yesu aliposikia ambacho walikisema, alimwambia kiongozi wa Sinagogi, “Usiogope. Amini tu.”
\v 37 Hakumruhusu yeyote kuongozana naye, isipokuwa Petro, Yakobo, na Yohana, ndugu yake Yakobo.
\v 38 Walikuja nyumbani kwa kiongozi wa Sinagogi naye aliona vurugu; za kulia kwingi na kuomboleza kwa nguvu.
\v 39 Alipoingia nyumbani, aliwaambia, “Kwa nini mnahuzunika na kwa nini mnalia? Mtoto hajafa bali amelala.”
\v 40 Walianza kumkejeli. Lakini aliwatoa wote nje na kumchukua baba ya mtoto na mama na wale waliokuwa naye, na akaingia mahali alipokuwa mtoto.
\v 41 Aliuchukua mkono wa mtoto na kumwambia, “Talitha koum!” ambayo ni kusema, “Binti mdogo, nakuambia, amka.”
\v 42 Ghafla mtoto akaamka na kutembea (kwa kuwa alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Na ghafla walishikwa na mshangao mkubwa.
\v 43 Aliwaamuru kwa ukali kwamba mtu yeyote asijue kuhusu hili. Kisha akawaambia wampe binti chakula.
\c 6
\cl Sura 6
\p
\v 1 Na akaondoka hapo na kwenda mjini kwao Nazareti, na wanafunzi wake wakamfuata.
\v 2 Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika Sinagogi. Watu wengi walimsikiliza na wakashangazwa. Wakasema, “Amepata wapi mafundisho haya?” “Ni hekima ya namna gani hii aliyo ipata?” “Huyu Yesu anatendaje miujiza hii kwa mikono yake?”
\v 3 “Je huyu si yule mtoto wa seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao ambao ni Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si tunaishi nao hapa pamoja nasi?” Watu wa nazareti hawakufurahishwa na mafundisho ya Yesu.
\p
\v 4 Yesu akawaambia, “Nabii hapati heshima, katika mji wake hata kwa ndugu zake wa nyumbani mwake.”
\p
\v 5 Hakuweza kutenda miujiza, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache akawaponya.
\v 6 Alishangazwa sana kwa sababu ya kutokuamini kwao. Kisha alivitembelea vijiji vya jirani akifundisha.
\p
\v 7 Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili. Aliwapa mamlaka juu ya pepo wachafu,
\v 8 na kuwaamuru wasichukue chochote wanapokwenda isipokuwa fimbo tu. Wasichukue chakula, wala mkoba, wala fedha kibindoni;
\v 9 lakini wavae viatu, na siyo kanzu mbili.
\v 10 Na akawaambia, “Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka.
\v 11 Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao.”
\v 12 Nao wakaenda wakiwaambia watu watubu na kuacha dhambi zao.
\v 13 Wanafunzi walipo kwenda waliyafukuza mapepo wengi, na waliwapaka mafuta wagonjwa na wakaponywa.
\p
\v 14 Mfalme Herode aliposikia kuhusu, habari za Yesu jinsi anavyo ponya na kufukuza mapepo, na kutambulika kwa watu. Baadhi ya watu walisema, “Itakuwa Yohana mbatizaji amefufuka na kwa sababu hiyo, hii nguvu ya miujiza inafanya kazi ndani yake.”
\v 15 Baadhi watu wakasema, “Huyu ni Eliya,” Ambaye Mungu aliahidi kwamba atarudi, wengine wakasema, “Huyu ni nabii, kama mmoja wa wale manabii wa zamani.”
\p
\v 16 Lakini Herode aliposikia haya akasema, “Yohana, niliye agiza askari wamkate kichwa amefufuka.”
\p
\v 17 Maana Herode mwenyewe alituma askari Yohana akamatwe na alimfunga gerezani kwa sababu ya Herodia (mke wa kaka yake ambaye ni Filipo) kwa sababu Herode alikuwa amemuoa.
\v 18 Kwa maana Yohana alimwambia Herode, “Si halali kumuoa mke wa kaka yako.”
\v 19 Lakini Herodia alianza kumchukia na alikuwa akitaka kumuuaYohana, lakini hakuweza, Hivyo alitafuta njia ya kumuua
\v 20 maana Herode alimwogopa Yohana; alijua kwamba ni mwenye haki mtu mtakatifu, na alimwacha salama. Na alipoendelea kumsikiliza Yohana alihuzunika sana, lakini alifurahia mazungumzo yake kuyasikiliza.
\p
\v 21 Hata ulipofika wakati mwafaka ikawa imekaribia siku ya kuzaliwa Herode akawaandalia maofisa wake sherehe, na makamanda, na viongozi wa Galilaya.
\v 22 Ndipo binti yake Herodia akaingia na kucheza mbele yao, akamfurahisha mfalme Herode na wageni walioketi wakati wa chakula cha jioni. Ndipo mfalme akamwambia binti, “Niombe chochote unachotaka nami nitakupa.”
\v 23 Akamwekea kiapo na kusema, chochote utakachoniomba, nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu ninao miliki.”
\p
\v 24 Binti akatoka nje ya chumba cha sherehe akamuuliza mama yake, “Niombe nini?” Mama Akasema omba, “Kichwa cha Yohana Mbatizaji.”
\p
\v 25 Kwa haraka sana akaingia kwa mfalme akaanza kusema, “Nataka unipatie juu ya sahani, kichwa cha Yohana Mbatizaji.”
\v 26 Mfalme alisikitishwa sana na ombi la binti, lakini kwa sababu ya kiapo chake na kwa ajili ya wageni, hakuweza kumkatalia ombi lake.
\v 27 Hivyo, mfalme akatuma askari kati ya walinzi wake na kuwaagiza kwenda kumletea binti kichwa cha Yohana. Mlinzi alikwenda kumkata kichwa Yohana akiwa kifungoni.
\v 28 Akakileta kichwa chake kwenye sahani na kumpatia binti, na binti akampa mama yake.
\v 29 Na wanafunzi wa Yohana waliposikia hayo, walikwenda kuuchukua mwili wake wakaenda kuuzika kaburini.
\p
\v 30 Na mitume, waliporudi kutoka kuhubiri walikusanyika pamoja mbele ya Yesu, wakamweleza yote waliyofanya na waliyoyafundisha.
\v 31 Naye akawaambia, “Njooni ninyi wanafunzi wangu mahali pa faragha na tupumzike kwa muda.” Watu wengi walikuwa wanakuja kwa mitume na kuondoka, hata hawakupata muda wa kula chakula.
\v 32 Hivyo wakapanda mashua wakaenda mahali pa faragha pasipokuwa na watu.
\v 33 Lakini watu waliwaona Yesu na wanafunzi wake wakiondoka na wengi wakawatambua, kwa pamoja walikimbia kwa kupitia njia ya miguu kutoka miji yote, nao wakafika pwani kabla yao.
\v 34 Yesu na wanafunzi wake Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi.
\p
\v 35 Muda uliendelea sana ilikuwa ni jioni, wanafunzi wakamjia wakamwambia, “Hapa ni mahali pa faragha hakuna makazi ya watu, na muda umeendelea sana.
\v 36 Uwaage watu waende miji ya jirani na vijiji ili wakajinunulie chakula.”
\p
\v 37 Lakini akawajibu akisema, “Wapeni ninyi chakula.” Wakamwambia, “Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa wale?”
\p
\v 38 Akawauliza,” Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Walipotazama wakamwambia, “Mikate mitano na samaki wawili.”
\v 39 Akawaamuru watu waketi katika makundi makundi, juu ya majani mabichi.
\v 40 Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini.
\v 41 Kisha akachukua mikate mitano na samaki wawili, na kutazama mbinguni, akamshukuru, Mungu, kisha akawapa wanafunzi waweke, ili wawape makutano. Wakaiweka mbele ya umati. Na kisha aligawa samaki wawili na kuwapa watu wote.
\v 42 Watu wote walikula hadi wakatosheka.
\v 43 Walikusanya vipande vya mikate iliyobaki, Vikajaa vikapu kumi na viwili, na pia vipande vya samaki.
\v 44 Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate. Na samaki. Lakini wanawake na watoto hawakuhesabiwa.
\p
\v 45 Kisha akawaambia wanafunzi wake, wapande kwenye mashua waende sehemu nyingine, hadi Bethsaida, wakati Yeye akiwaaga makutano.
\v 46 Watu walipokwisha kuondoka, Yesu akaenda mlimani kuomba.
\v 47 Ilipofika jioni, na mashua yao ilikuwa katikati ya bahari, naye Yesu alikuwa peke yake pwani.
\v 48 Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita.
\v 49 Lakini walipomwona Yesu anatembea juu ya maji, wakaingiwa na wasiwasi wakidhani ni mzimu wakapiga kelele.
\v 50 Kwa sababu walimwona wakajawa na hofu. Mara Yesu akasema nao akawaambia, “Muwe na ujasiri! Ni mimi! Msiwe na hofu.”
\v 51 Akaingia ndani ya mashua, na upepo ukaacha kuvuma, nao wakamshangaa sana.
\v 52 Hivyo hawakuwa wameelewa maana ya ile mikate. Maana akili zao zilikuwa zimeshindwa kuelewa.
\p
\v 53 Nao walipovuka ng'ambo, walifika nchi ya Genesareti mashua ikatia nanga.
\v 54 Walipotoka nje ya mashua, watu wakamtambua, Yesu na wanafunzi wake.
\v 55 Wakakimbia kutangaza katika mkoa mzima na wakaanza kuwaleta watu wagonjwa kwa machela, kila waliposikia amekuja.
\v 56 Popote alipoingia katika vijiji, au mjini, au katika nchi, watu waliwaweka wagonjwa mahali pa soko, na watu wakamwomba awaruhusu wagonjwa kugusa pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa waliponywa.
\c 7
\cl Sura 7
\p
\v 1 Mafarisayo na baadhi ya waandishi ambao walikuwa wametokea Yerusalemu walikusanyika. Wakimzunguka Yesu.
\v 2 Na mafarisayo wandishi waliona kuwa baadhi ya wanafunzi wake walikula mkate kwa mikono najisi, hiyo haijaoshwa.
\v 3 (Kwa sababu Mafarisayo na Wayahudi wote hawali mpaka wameosha mikono yao vizuri; wanashikilia utamaduni wa wazee.
\v 4 Mafarisayo wanaporudi kutoka mahali pa soko, hawali mpaka wameoga kwanza. Na kuna sheria zingine ambazo wanazifuata kabisa, ikiwa ni pamoja na kuosha vikombe, masufuria, vyombo vya shaba, na hata viti vinavyotumika wakati wa chakula.)
\p
\v 5 Mafarisayo na waandishi walimuuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wako hawatii na kufuata utamaduni wa wazee wetu, wanakula chakula pasipo kunawa mikono?”
\p
\v 6 Lakini yeye aliwaambia, “Isaya alitabiri vizuri kuhusu ninyi mafarisayo na wandishi wanafiki, aliandika, Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali na mimi.
\q
\v 7 Wananifanyia ibaada zisizo na maana, wakifundisha sheria za wanadamu kama mapokeo yao.
\p
\v 8 Mmeiacha sheria ya Mungu na kushikilia kwa tamaduni za wazee wenu.”
\v 9 Yesu kawaambia, “Mmezikataa amri za Mungu kwa kwamba mtunze tamaduni zenu!
\v 10 Kwa kuwa Musa alisema, mheshimu baba yako na mama yako, na Yeye aamtukanaye baba yake au mama yake hakika atakufa.
\v 11 Lakini mnasema, kama mtu akisema kitu cha kumwahidi baba yake au mama, cha “Msaada wowote ambao mngepokea kutoka kwangu ni hazina ya Hekalu,”’ (hiyo ni kusema kwamba, nimeutoa kwa Mungu)
\v 12 hivyo haumruhusu mtoto kufanya jambo lolote kwa ajili ya baba au mama yake.
\v 13 Mnazifanya amri za Mungu kuwa bure kwa kuleta tamaduni zenu. Mnafanya mengi ya jinsi hiyo yanayofanana.”
\p
\v 14 Yesu aliwaita makutano tena na kuwaambia, “Mnisikilize mimi, ninyi nyote, na mpate kunielewa.
\v 15 Hakuna chakula chochote kitokacho nje ya mtu ambacho chaweza kumchafua mtu kiingiapo ndani yake. Bali ni kile asemacho mtu ndicho kimchafuacho.
\v 16 “Kama mtu yeyote ana masikio ya kusikia na asikie jambo hili, na aelewe.”
\p
\v 17 Yesu alipowaacha umati wa watu kuingia nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza kuhusu mfano huo.
\v 18 Yesu akasema, “Na ninyi pia bado hamjaelewa? Hamuoni kwamba chakula chochote kimuingiacho mtu hakiwezi kumchafua,
\v 19 kwa sababu hakiwezi kwenda kwenye moyo wake, lakini kinaingia katika tumbo lake na kisha kinapita kwenda chooni.” Kwa maelezo haya Yesu alivifanya vyakula vyote kuwa safi.
\v 20 Yesu alisema, “kile ambacho kinamtoka mtu ndani ndicho kimchafuacho.
\v 21 Kwa kuwa hutoka ndani ya mtu, ndani ya moyo, hutoka mawazo maovu, usherati, wizi, mauaji,
\v 22 uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, kashfa, majivuno, ujinga.
\v 23 Maovu haya yote yanatoka ndani, na ndiyo yale yamchafuayo mtu.”
\p
\v 24 Yesu aliamka kutoka pale alipokuwa ameketi na kuondoka kwenda katika mkoa wa Tiro na Sidoni. Aliingia ndani na hakutaka mtu yeyote ajue kuwa alikuwa hapo, lakini haikuwezekana kumficha.
\v 25 Lakini ghafla mwanamke alikuja kwa Yesu, ambaye mtoto wake mdogo alikuwa na roho mchafu, alisikia habari zake, akaja, na kupiga magoti miguuni pake Yesu.
\v 26 Mwanamke huyo alikuwa Myunani, wa kabila la Kifoenike. Alimsihi yesu amfukuze pepo atoke kwa binti yake.
\v 27 Yesu akamwambia mwanamke, “Waache watoto walishwe kwanza, chakula, kwa kuwa sio sawa kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”
\p
\v 28 Lakini yule mwanamke akamjibu na kusema, “Ndiyo Bwana, hata mbwa chini ya meza hula mabaki ya chakula cha watoto.”
\p
\v 29 Yesu akamwambia, “Kwa kuwa unaamini hivi, uko huru kwenda. Pepo amemtoka binti yako.”
\v 30 Mwanamke alirudi nyumbani kwake na akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo alikuwa amemtoka.
\p
\v 31 Yesu alitoka tena nje ya mkoa wa Tiro na kupitia Sidoni kuelekea Bahari ya Galilaya mpaka kanda ya Dekapoli.
\v 32 Na wakamletea mtu aliyekuwa kiziwi na alikuwa hawezi kuzungumza vizuri, walimsihi Yesu aweke mikono juu yake.
\v 33 Yesu alimtoa mtu huyu nje ya kusanyiko kwa siri, na akaweka vidole vyake kwenye masikio yake, na baada ya kutema mate, aligusa ulimi wakewa yule mtu.
\v 34 Yesu alitazama juu mbinguni, akahema na kumwambia, “Efatha,” hiyo ni kusema “funguka!”
\v 35 Na muda ule ule masikio yakafunguka, na kilichokuwa kimezuia ulimi kiliharibiwa na akaweza kuongea vizuri.
\p
\v 36 Na aliwaamuru wasimwambie mtu yeyote. Lakini kadri alivyowaamuru, ndivyo walivyotangaza habari hizo kwa wingi.
\v 37 Hakika walishangazwa, na kusema, “Amefanya kila kitu vizuri. Hata amewafanya viziwi kusikia na mabubu kuongea.”
\c 8
\cl Sura 8
\p
\v 1 Katika siku hizo, kulikuwa tena na umati mkubwa, na hawakuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake na akawaambia,
\v 2 Ninauhurumia umati huu, kwa sababu wameendelea kuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula.
\v 3 Nikiwaaga warudi majumbani mwao bila kula wanaweza wakazimia njiani kwa njaa. Na baadhi yao wametoka mbali sana.”
\p
\v 4 Wanafunzi wake wakamjibu, “Tutaweza kupata wapi mikate ya kutosha katika sehemu kama hii isiyo na watu ili kuwashibisha watu hawa?”
\p
\v 5 Akawauliza, “mna mikate mingapi?” Wakasema, “Saba.”
\p
\v 6 Akauamuru umati ukae chini. Akachukua mikate saba, akamshukuru Mungu, na kuivunja. Akawapa wanafunzi wake waiweke mbele yao, nao wakaiweka mbele ya umati.
\v 7 Pia walikuwa na samaki wadogo wachache, na baada ya kushukuru, aliwaamuru wanafunzi wake wawagawie hivi pia.
\v 8 Walikula na wakatosheka. Na walikusanya vipande vilivyo baki, vikapu vikubwa saba.
\v 9 Kulikuwa na watu kama elfu nne. Kisha aliwaacha waende.
\v 10 Mara akapanda mashua pamoja na wanafunzi wake, na wakaenda katika ukanda wa Dalmanutha.
\p
\v 11 Kisha Mafarisayo wakatoka na kuanza kubishana naye. Walitaka awape ishara kutoka mbinguni, ili kumjaribu.
\v 12 Akahuzunika moyoni mwake akasema, “Kwa nini kizazi hiki kinatafuta ishara? Nawaambia ninyi kweli, hakuna ishara itakayotolewa kwa kizazi hiki.”
\v 13 Kisha akawaacha, akaingia ndani ya mashua tena, akaondoka kuelekea upande mwingine.
\v 14 Wakati huo wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu ndani ya mashua.
\v 15 Yesu akawaonya akisema, “Muwe macho na mjilinde dhidi ya chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.
\p
\v 16 Wanafunzi walikuwa wakibishana wao kwa wao juu ya kutokuwa na mikate
\p
\v 17 Yesu alipotambua hayo, akawauliza, “Mbona mnabishana kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamuoni au hamuelewi? Mna mioyo migumu?
\v 18 Mna macho, hamuoni? Mna masikio, hamsikii? Hamkumbuki?
\v 19 Nilipoimega mikate mitano kwa watu elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate?” Wakamjibu, “kumi na mbili.”
\p
\v 20 “Na nilipoimega mikate saba kati ya watu elfu nne, mlichukua vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate?” Wakasema, “Saba.”
\v 21 Akawaambia, “Bado hamuelewi?”
\p
\v 22 Wakafika Bethsaida. Watu pale wakamleta kipofu mmoja kwa Yesu na kumsihi Yesu amguse.
\v 23 Yesu akamshika mkono yule kipofu, na kumwongoza nje ya kijiji. Alipomtemea mate machoni na kumwekea mikono, alimuuliza, “Unaona chochote?”
\p
\v 24 Alitazama juu na kusema, “Naona watu wanaonekana kama miti inatembea.”
\v 25 Kisha akaweka tena mikono juu ya macho yake, na mtu yule akafungua macho yake, uwezo wake wa kuona ukarejea, naye aliona vitu vyote waziwazi.
\p
\v 26 Yesu akamwachilia aende nyumbani kwake na akamwambia, “Usiingie kijijini.”
\p
\v 27 Yesu aliondoka na wanafunzi wake kwenda vijiji vya Kaisaria ya Filipi. Wakiwa njiani aliwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasema mimi ni nani?”
\v 28 Wakamjibu wakasema, “Yohana mbatizaji. Wengine wanasema, Eliya na wengine, Mmoja wa Manabii.”
\p
\v 29 Akawauliza, “Lakini ninyi mnasema mimi ni nani?” Petro akamwambia, “Wewe ni Kristo.”
\p
\v 30 Yesu akawaonya wasimwabie mtu yeyote kumuhusu Yeye.
\p
\v 31 Na akaanza kuwafundisha ya kuwa Mwana wa Adamu lazima ateseke kwa mambo mengi, na atakataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na atauawa, na baada ya siku tatu atafufuka.
\v 32 Aliongea ujumbe huo waziwazi. Kisha Petro akamchukua pembeni kando na akaanza kumkemea.
\v 33 Lakini Yesu aligeuka na kuwatazama wanafunzi wake na kisha akamkemea Petro na kusema, “Nenda nyuma yangu, Shetani! Huyawazi mambo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
\p
\v 34 Kisha akauita umati na wanafunzi wake pamoja, na kuwaambia, “mtu yeyote akitaka kunifuata, ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, na anifuate.
\v 35 Kwa kuwa yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, atayaokoa.
\v 36 Inamfaidia nini mtu, kuupata ulimwengu wote, na kisha kuyapoteza maisha yake?
\v 37 Mtu anaweza kutoa nini badala ya maisha yake?
\v 38 Yeyote anayenionea haya mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
\c 9
\cl Sura 9
\p
\v 1 Akawaambia, “Amini nawaambia, wako baadhi yenu wasimamao hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”
\p
\v 2 Na baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana pamoja naye juu ya mlima, peke yao. Kisha akageuka sura mbele yao.
\v 3 Mavazi yake yakang'aa sana, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angeweza kuyang'arisha.
\v 4 Kisha Eliya pamoja na Musa walitokea mbele yao, na walikuwa wakiongea na Yesu.
\v 5 Petro alijibu akamwambia Yesu, “Mwalimu, ni vyema sisi kuwa hapa, na tujenge vibanda vitatu, kimoja kwa ajili yako, kimoja kwa ajili Musa na kingine kwa ajili ya Eliya.”
\v 6 (Kwa maana hakujua la kusema, maana waliogopa sana.)
\p
\v 7 Wingu likaja na kuwafunika. Kisha sauti ikatoka katika lile wingu,” Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikieni yeye.”
\v 8 Ghafla, walipotazama huku na huko, hawakumuona tena mtu yeyote pamoja nao, isipokuwa Yesu tu.
\p
\v 9 Walipokuwa wanateremka kutoka mlimani, akawaamuru wasimwambie mtu yeyote yale yote waliyoyaona, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu.
\v 10 Kwa hiyo wakaweka jambo hilo ndani ya mioyo yao wenyewe, lakini walijadiliana wao kwa wao ni nini maana yake “kufufuka kutoka kwa wafu”
\p
\v 11 Walimwuliza Yesu, “Kwa nini waandishi husema lazima Eliya aje kwanza?”
\p
\v 12 Akawaambia, “Eliya anakuja kwanza kurejesha mambo yote, Kwa nini basi imeandikwa kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi kudharauliwa?
\v 13 Lakini nawaambia ya kwamba Eliya amekwisha kuja, na wakamfanyia walivyotaka, kama ilivyoandikwa juu yake.”
\p
\v 14 Na walipofika kwa wanafunzi, waliona kundi kubwa limewazunguka na waandishi walikuwa wanabishana nao.
\v 15 Na mara walipomwona Yesu, kundi lote lilishangaa na kumkimbilia kumsalimia.
\v 16 Aliwauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao juu ya nini?”
\p
\v 17 Mtu katika umati alimjibu, “Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako; ana roho chafu inayomfanya asiweze kuongea,
\v 18 Humkamata na kumwangusha chini, naye anatoa povu mdomoni na kusaga meno na kuwa mgumu. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo, lakini hawakuweza.
\p
\v 19 Akawajibu, “Kizazi kisichoamini, nitakaa nanyi hadi lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kwangu.”
\v 20 Wakamleta yule mvulana kwake. Roho mchafu alipomwona Yesu, ghafla ilimtia katika kutetemeka. Mvulana alianguka chini na kutoa povu mdomoni.
\v 21 Yesu alimwuliza baba yake, “Amekuwa katika hali hii kwa muda gani?” Baba alisema, “Tangu utoto.
\v 22 Mara nyingine humwangusha katika moto au kwenye maji, na kujaribu kumwangamiza. Kama unaweza kufanya chochote tuhurumie na utusaidie.”
\p
\v 23 Yesu alimwambia, “Kama unaweza? Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye.”
\p
\v 24 Ghafla baba wa mtoto alilia na kusema, “Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu.”
\p
\v 25 Wakati Yesu alipoona kundi linakimbilia kwao, alimkemea roho mchafu na kusema, “wewe roho bubu na kiziwi, nakuamuru toka kwake, usimwiiingie tena.”
\p
\v 26 Akalia na kumhangaisha mvulana kwa nguvu nakisha akamtoka. Mvulana alionekana kama amekufa, Ndipo wengi wakasema, “Amekufa,”
\v 27 Lakini Yesu alimchukua kwa mkono akamwinua, na mvulana akasimama.
\p
\v 28 Wakati Yesu alipoingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza kwa faragha, “Kwa nini hatukuweza kuitoa?”
\p
\v 29 Akawaambia, “Aina hii haitoki isipokuwa kwa maombi.”
\p
\v 30 Wakatoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo,
\v 31 kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, “Mwana wa Adamu atapeanwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokufa, baada ya siku tatu atafufuka tena.”
\v 32 Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumuuliza.
\p
\v 33 Ndipo walifika Kapernaumu. Baada ya kuingia ndani ya nyumba akawauliza, “Mlikuwa mnajadili nini njiani”?
\v 34 Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi.
\v 35 Alipoketi chini akawaita kumi na wawili pamoja, na akawambia, “Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.”
\v 36 Akamchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake na akawambia,
\v 37 “Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.”
\p
\v 38 Yohana akamwambia, “Mwalimu, tulimwona mtu anatoa pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu hatufuati.”
\p
\v 39 Lakini Yesu akasema, “Msimzuie, kwa kuwa hakuna atakayefanya kazi kubwa kwa jina langu na ndipo kisha baadaye aseme neno baya lolote juu yangu.
\v 40 Yeyote asiyekuwa kinyume nasi yuko upande wetu.
\v 41 Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa jina langu wewe ni wa Kristo, Amin nawaambia, hatapoteza thawabu yake.
\p
\v 42 Yeyote anayewakosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio mimi kujikwaa, ingekuwa vyema kwake kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini.
\v 43 Kama mkono wako ukikukosesha ukate. Ni heri kuingia katika uzima bila mkono kuliko kuingia kuzimu ukiwa na mikono yote, katika moto “usiozimika.”
\v 44 “Mahali ambapo funza hawafi na moto usiozimika.” \f + \ft haumo katika nakala za kale. \f*
\v 45 Kama mguu wako ukikukosesha, ukate. Ni vyema kwako kuingia uzimani ukiwa kilema, kuliko kutupwa kuzimu na miguu miwili.
\v 46 [“Mahali ambapo funza hawafi na moto usioweza kuzimika.”]
\v 47 Kama jicho lako likikukosesha ling'oe. Ni vyema kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa kuzimu.
\v 48 Mahali ambapo funza wao hawafi, na moto usiozimika.
\p
\v 49 Kwa maana kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.
\v 50 Chumvi ni nzuri, lakini kama chumvi ikipoteza ladha yake, unawezaje kuifanya iwe chumvi tena? Muwe na chumvi ninyi kwa ninyi na muwe na Amani kila mmoja na mwingine.”
\c 10
\cl Sura 10
\p
\v 1 Yesu akaondoka eneo hilo na akaenda katika mkoa wa Yudea na eneo ng'ambo ya Mto Yorodani, na makutano walimfuata tena. Aliwafundisha tena, kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya.
\v 2 Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, “Ni halali kwa bwana kumpa talaka mkewe?”
\p
\v 3 Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuru nini?”
\p
\v 4 Wakasema, “Musa aliruhusu kuandika cheti cha talaka na kisha kumwacha mkewe.”
\p
\v 5 “Ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu ndiyo maana aliwaandikia sheria hii,” Yesu aliwaambia.
\v 6 “Lakini kutoka mwanzo wa uumbaji, Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke.
\v 7 Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake,
\v 8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; Kwa kuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
\v 9 Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
\p
\v 10 Walipokuwa ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza tena kuhusu hili.
\v 11 Akawaambia, “Yeyote anayemtaliki mke wake na kuoa mke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake.
\v 12 Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi.”
\p
\v 13 Kisha walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.
\v 14 Lakini Yesu alipotambua hilo, alikasirika na akawaambia, “Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni wa walio kama
\v 15 Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
\v 16 Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.
\p
\v 17 Na alipoanza safari yake mtu mmoja alimkimbilia na akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niweze kurithi uzima wa milele?”
\p
\v 18 Na Yesu akasema, “Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema, isipokuwa Mungu peke yake.
\v 19 Unazijua amri: Usiue, usizini, usiibe, usishuhudieusitoe ushhidi wa uongo, usidanganyeusilaghai, mheshimu baba na mama yako.’”
\p
\v 20 Mtu yule akasema, “Mwalimu, haya yote nimeyatii tangu nikiwa kijana.”
\p
\v 21 Yesu alimwangalia na kumpenda. Akawambia, “Unapungukiwa kitu kimoja. Unapaswa kuuza vyote ulivyo navyo na uwape masikini, na utakuwa na hazina mbinguni. NdipoKisha uje unifuate.”
\v 22 Lakini alikata tamaa kwa sababu ya maelezo haya; aliondokakauli hii alionekana mwenye huzuni na akaenda zake akiwa mwenyena huzuni, kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.
\v 23 Yesu akatazama pande zote na kuwaambia wanafunzi wake, “Ni vigumu jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!
\v 24 Wanafunzi walishangazwa kwa maneno haya. Lakini Yesu akawaambia tena, “Watoto, ni vigumu jinsi gani kuingia katika ufalme wa Mungu!
\v 25 Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano, kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”
\p
\v 26 Walishangazwa sana na wakasemezana, “Hivyo nani ataokoka”
\p
\v 27 Yesu akawaangalia na kusema, “Kwa binadamu haiwezekani, lakini sio kwa Mungu. Kwa kuwa katika Mungu yote yanawezekana.”
\p
\v 28 “Petro akaanza kuzungumza naye, “Angalia tumeacha vyote na tumekufuata.”
\p
\v 29 Yesu akasema, “Ukweli nawaambia ninyi, hakuna aliyeacha nyumba, au kaka, au dada, au mama, au baba, au watoto, au ardhi, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,
\v 30 ambaye hatapokea mara mia zaidi ya sasa hapa duniani katika zama hizi: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, na ardhi, kwa pamoja na mateso, na ulimwengu ujao, uzima wa milele.
\v 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
\p
\v 32 Walipokuwa njiani, kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa amewatangulia mbele yao. Wanafunzi walishangaa, na wale waliokuwa wanafuata nyuma waliogopa. Ndipo Yesu akawatoa akawachukua pembeni tena wale kumi na wawili na akaanza kuwaeleza ambacho kitamtokea kwake hivi karibuni:
\v 33 “Tazama, tunakwenda mpaka Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atafikishwa kwa makuhani wakuu na waandishi. Watamhukumu afe na watamtoa kwa watu wa Mataifa.
\v 34 Watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga fimbo watamchapa mijeledi, na watamwua. Lakini baada ya siku tatu atafufuka.”
\p
\v 35 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walikuja kwake na kusema, “Mwalimu, tunakuhitaji tunataka utufanyie chochote tukuombacho.”
\p
\v 36 Aliwaambia, “Mnataka niwatendee nini?”
\p
\v 37 Wakasema, “Turuhusu tukae nawe katika utukufu wako, mmoja katika mkono wako wa kuume na mwingine mkono wako wa kushoto.”
\p
\v 38 Lakini Yesu aliwajibu, “Hamjui mnachoomba. Mnaweza kukinywea kikombe ambacho nitakiyweanitakinywea au kustahimili ubatizo ambao nitabatizwa?”
\p
\v 39 Wakamwambia, “Tunaweza” Yesu akawaambia, “Kikombe nitakachokinywea, mtakinywea. Na ubatizo ambao kwao nimebatizwa, mtaustahimili.
\v 40 Lakini atakayekaa mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto sio mimi wa kutoa, lakini ni kwa wale ambao kwao imekwisha andaliwa.”
\p
\v 41 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, wakaanza kuwakasirikia sana Yakobo na Yohana.
\v 42 Yesu akawaita kwake na kusema, “Mnajua kuwa wale wanaodhaniwa hao wanaochukuliwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala na maofisa wao mashuhuri hutekeleza mamlaka juu yao.”
\v 43 Lakini haipaswi kuwa hivi kati yenu. Yeyote atakaye kuwa mkubwa kati yenu lazima awatumikie,
\v 44 na yeyote atakaye kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumwa wa wote.
\v 45 Kwa kuwa Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kuyatoa maisha yakekutoa uhai wake kuwa fidia kwaya wengi.”
\p
\v 46 Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara.
\v 47 Aliposikia kuwa ni Yesu Mnazareti, alianzaakaanza kupiga kelele na kusema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
\v 48 Wengi walimkemea yule kipofu, wakimwambia anyamaze. Lakini alilia kwa sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”
\p
\v 49 Yesu alisimama na kuamuru aitwe. Walimwita yule kipofu, wakisema, “Kuwa shujaa! Inuka! Yesu anakuita.”
\v 50 Akalitupa pembeni koti lake, akaruka juu, na kuja kwa Yesu.
\p
\v 51 Yesu akamjibu na kusema, “Unataka nikufanyie nini?” Yule mwanaume kipofu akamjibu, “Mwalimu, ninataka kuona.”
\p
\v 52 Yesu akamwambia, “Nenda. Imani yako imekuponya.” Hapo hapo macho yake yakaona mara akaweza kuona tena; na akamfuata Yesu barabarani.
\c 11
\cl Sura 11
\p
\v 1 Sasa walipokuwa wakifika Yerusalemu, walikuwa karibu na Bethfage na Bethania, kwenye Mlima wa Mizeituni, Yesu akawatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake
\v 2 na akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mkabala wenu. Mara mtakapoingia humo, mtamkuta mwanapunda ambaye hajapandwa. Mfungueni na mmlete kwangu.
\v 3 Na kama yeyote akiwaambia, Kwa nini mnafanya hivi? mnapaswa kusema, Bwana anamhitaji na mara atamrudisha hapa.’”
\p
\v 4 Wakaenda, wakamkuta mwana-punda amefungwa nje mlangoni nje ya njia kuu nao wakamfungua.
\v 5 Na baadhi ya watu waliokuwa wamesimama pale wakawaambia, “Mnafanya nini, kumfungua mwana-punda huyo?”
\v 6 Wakawaambia kama Yesu alivyowaambia, na watu wakawaacha waende.
\p
\v 7 Wakamleta mwana-punda kwa Yesu na wakatandika nguo zao, naye akaketi.
\v 8 Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakatandaza matawi waliyoyakata mashambani.
\v 9 Wale waliotangulia mbele yake na wale waliomfuata walipiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana.
\v 10 Umebarikiwa ufalme ujao wa baba yetu Daudi! Hosana juu mbinguni”
\p
\v 11 Kisha Yesu kaingia Yerusalemu, akaingia hekaluni akatazama kila kitu. Sasa, wakati ulikuwa umeenda, alitoka kwenda Bethania pamoja nao kumi na wawili.
\p
\v 12 Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, aliona njaa.
\v 13 Na akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili aone kama angeweza kupata matunda juu yake, alipofika akakuta majani tu, kwa kuwa haikuwa majira ya tini.
\v 14 Akauambia, “Hakuna yeyote atakayekula tunda kutoka kwako tena.” Na wanafunzi wake wakasikia.
\p
\v 15 Wakafika Yerusalemu, naye akaingia hekaluni na kuanza kuwatoa nje wauzaji na wanunuzi ndani ya hekalu. Akazipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.
\v 16 Hakumruhusu yeyote kubeba chochote hekaluni kilichoweza kuuzwa.
\v 17 Akawafundisha na kusema, “Je haikuandikwa, nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Lakini mmeifanya pango la wanyang'anyi.”
\v 18 Makuhani wakuu na waandishi walisikia alivyokuwa amesema, nao walitafuta njia ya kumwangamiza. Hata hivyo walimwogopa kwa sababu umati ulishangazwa na mafundisho yake.
\v 19 Na jioni ilipofika, waliondoka mjini.
\p
\v 20 Walipokuwa wakitembea asubuhi, waliuona mti wa mtini umekauka mpaka kwenye mizizi yake.
\v 21 Petro akakumbuka na kusema, “Rabi! Tazama, mti wa mtini ulioulaani umekauka.”
\p
\v 22 Yesu akawajibu, “Muwe na imani katika Mungu.
\v 23 Amini nawaambia kwamba kila auambiaye mlima huu, Ondoka, na ukajitupe mwenyewe baharini, na kama hana mashaka moyoni mwake lakini anaamini kwamba alichokisema kitatokea, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya.
\v 24 Kwa hiyo ninawaambia: yoyote myaombayo, aminini kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.
\v 25 Msimamapo na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.
\v 26 [“Lakini msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatasamehe dhambi zenu.”]
\p
\v 27 Wakarudi Yerusalemu tena. Na Yesu alipokuwa akitembea hekaluni, makuhani wakuu, waandishi na wazee walikuja kwake.
\v 28 Na wakamwambia, “Kwa mamlaka gani unafanya mambo haya?” Na ni nani aliyekupa mamlaka kuyafanya haya?”
\p
\v 29 Yesu akawaambia, “Nitawauliza swali moja. Niambieni na mimi nitawaambia kwa mamlaka gani ninayafanya mambo haya.
\v 30 Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au ulitoka kwa wanadamu? Nijibuni.”
\p
\v 31 Wakajadiliana miongoni mwao na kushindana na kusema, “Kama tukisema, Kutoka mbinguni, atasema, Kwa nini basi hamkumwamini?
\v 32 Lakini kama tukisema, Kutoka kwa wanadamu,...” Waliwaogopa watu, kwa kuwa wote walishawishika kwamba Yohana alikuwa Nabii.
\v 33 Ndipo walimjibu Yesu na kusema, “Hatujui.” Ndipo Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nayafanya mambo haya.
\c 12
\cl Sura 12
\p
\v 1 Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mafumbo. Akasema, “Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la shinikizo la divai. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali.
\v 2 Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu.
\v 3 Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote.
\v 4 Tena akatuma kwao mtumishi mwingine, na wakamjeruhi kichwani na kumtendea aibu.
\v 5 Bado akamtuma mwingine, na huyu wakamwua. Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo, wakiwapiga wengine na kuwaua wengine.
\v 6 Alikuwa bado na mtu mmoja zaidi wa kutuma, mwana mpendwa. Naye akawa wa mwisho aliyetumwa kwao. Akisema, “Watamheshimu mwanangu.”
\v 7 Lakini wale wakulima wa mizabibu wakaambiana “Huyu ndiye mrithi. Njooni, tumuue yeye, na urithi utakuwa wetu.”
\v 8 Walimvamia, wakamuua na kumtupa nje ya shamba la mizabibu.
\v 9 Kwa hiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wa mizabibu na atalikabidhi shamba la mizabibu kwa wengine.
\v 10 Hamjapata kusoma andiko hili? “Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe la pembeni.
\v 11 Hili lilitoka kwa Bwana, na ni la ajabu machoni petu.”
\p
\v 12 Baada ya haya, viongozi wa kiyahudi walitafuta njia ya kumkamata Yesu, kwani walifahamu yakuwa alinena mfano huo juu yao. Lakini waliogopa umati wa watu. Hivyo walimwacha na wakaenda zao.
\p
\v 13 Kisha wakawatuma baadhi ya mafarisayo na maherodia kwake ili kumtega kwa maneno.
\v 14 Walipofika, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua wewe ni wa kweli na huyumbishwi na mtu yeyote, kwa kuwa huna upendeleo. Unafundisha njia ya Mungu katika ukweli. Je! Ni haki kulipa kodi kwa Kaisari au la? Je! Twaweza kulipa au la?
\p
\v 15 Lakini Yesu alijua unafiki wao na kuwaambia, “Kwa nini mnanijaribu? Nipeni dinari niweze kuitazama.”
\v 16 Wakaleta moja kwa Yesu. Akawaambia, “Je! Ni sura na maandishi ya nani yaliyo hapa? Wakasema, “Ya Kaisari.”
\p
\v 17 Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vya Kaisari na Mungu vitu vya Mungu.” Wakamstaajabia.
\p
\v 18 Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema,
\v 19 “Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.
\v 20 Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto.
\v 21 Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika. Hawakuacha watoto.
\v 22 Na wote saba hawakuacha watoto! Mwishowe na mwanamke pia akafa.
\v 23 Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwa maana ndugu wote saba walikuwa wamemwoa.”
\p
\v 24 Yesu aliwaambia, “Je! Hii sio sababu yenu kukosea, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?”
\v 25 Maana watakapofufuka kutoka kwa wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali ni kama malaika mbinguni.
\v 26 Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamjasoma katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema naye na kumwambia, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?
\v 27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Mmekosea kabisa.”
\p
\v 28 Mmoja wa waandishi akaja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, “Je! Ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi kuliko zote?”
\p
\v 29 Yesu alimjibu, “Iliyo ya muhimu ni hii, “Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja.
\v 30 Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.
\v 31 Amri ya pili ni hii, Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Hakuna amri nyingine kuu zaidi ya hizi.”
\p
\v 32 Mwandishi akasema, “Vema, Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake.
\v 33 Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe, ni zaidi ya sadaka zote za kuteketezwa na dhabihu.”
\p
\v 34 Wakati Yesu alipoona ametoa jibu la busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu.” Baada ya hapo hakuna hata mmoja aliye thubutu kumwuliza Yesu maswali yoyote.
\p
\v 35 Na Yesu alipokuwa akifundisha hekaluni, alisema, “Je! Imekuwaje waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi?
\v 36 Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.
\v 37 Daudi mwenyewe humwita Bwana Je! Kristo anaweza kuwa mwana wa Daudi kwa jinsi gani?” Na kusanyiko kuu la watu walimsikiliza kwa furaha.
\p
\v 38 Katika mafundisho yake Yesu akasema, “Jihadharini na waandishi, wanaotamani kutembea na kanzu ndefu na kusalimiwa kwenye masoko
\v 39 na kuketi kwenye viti vya wakuu katika. Masinagogi na mahali pa heshima shereheni.
\v 40 Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu.”
\p
\v 41 Kisha Yesu akaketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa.
\v 42 Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia sarafu mbili za thamani ya senti moja.
\v 43 Akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, “Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane maskini ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka.
\v 44 Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake.” Na kuketi kwenye viti vya wakuu katika masinagogi na mahali pa heshima shereheni.
\c 13
\cl Sura 13
\p
\v 1 Yesu alipokuwa akitembea kutoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwuliza, “Mwalimu, tazama mawe haya na majengo yakushangaza!”,
\v 2 Yesu akamwambia, “Unaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalo salia juu ya jingine ambalo halitaangushwa chini.”
\p
\v 3 Na alipokuwa amekaa juu ya Mlima wa Mizeituni kinyume na hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamwuliza kwa siri,
\v 4 “Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Ni nini dalili ya mambo haya kutokea?”
\p
\v 5 Yesu akaanza kuwaambia, “jihadharini mtu asiwapotoshe.
\v 6 Wengi watakuja kwa jina langu wakisema, Mimi ndiye, na watawapotosha wengi.
\v 7 Mtakaposikia habari za vita na fununu za vita, msiogope; mambo haya lazima yatatokea, lakini mwisho bado.
\v 8 Kwa maana taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme. Patakuwa na matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali, na njaa. Hayo ni mwanzo wa utungu.
\p
\v 9 Jihadharini. Watawapeleka hadi mabarazani, na mtapigwa katika masinagogi. Mtasimamishwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao.
\v 10 Lakini injili lazima kwanza ihubiriwe kwa mataifa yote.
\v 11 Watakapo wakamata na kuwakabidhi, msiogope kuhusu kile mtakachosema. Kwa maana katika muda huo, mtapewa kile mtakachokisema; haitakuwa nyinyi mnaosema, bali Roho Mtakatifu.
\v 12 Ndugu atamsaliti ndugu auawe, baba atamsaliti mtoto wake. Watoto watainuka dhidi ya wazazi wao na kuwafanya wauwawe.
\v 13 Mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, mtu huyo ataokoka.
\p
\v 14 Mtakapoliona chukizo la uharibifu limesimama mahali ambapo halipaswi kusimama (asomaye na afahamu), ndipo walioko ndani ya Yudea wakimbilie milimani,
\v 15 naye aliyeko juu ya paa asishuke ndani ya nyumba, wala kuchukua kitu ndani yake,
\v 16 na aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.
\v 17 Lakini ole wao wanawake wenye mimba na wanyonyeshao katika siku hizo!
\v 18 Ombeni kwamba isitokee wakati wa baridi.
\v 19 Kwa maana hizo zitakua siku za dhiki kuu, ambayo, hajatokea namna yake tangu Mungu alipoumba ulimwengu, hata sasa, wala haitakuwapo tena.
\v 20 Kama Bwana asingalifupisha siku hizo, hakuna mtu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule, aliowachagua alifupisha siku hizo.
\v 21 Wakati huo kama mtu yeyote atawaambia, “Tazama, Kristo yuko hapa! au Tazama, yuko pale! msiamini.
\v 22 Kwani makristo wa uongo na manabii wa uongo watatokea na watatoa ishara na maajabu, ili kwamba, wawadanganye, yamkini hata wateule.
\v 23 Jihadharini. Nimekwisha wambia haya yote kabla ya wakati.
\p
\v 24 Lakini baada ya dhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake,
\q1
\v 25 nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu zilizoko mbinguni zitatikisika.
\v 26 Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu kubwa na utukufu.
\v 27 Ndipo atatuma malaika zake na atawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande kuu nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
\p
\v 28 Jifunzeni kutoka kwa mtini. Mara tu tawi linapoanza kuwa laini na kuchipua majani yake, mnajua majira ya kiangazi yamekaribia.
\v 29 Vivyo hivyo, mwonapo mambo hayo yakitendeka, tambueni ya kuwa yeye yu karibu na malango.
\v 30 Kweli, nawambieni, kizazi hiki hakitapita mpaka mambo haya yote yatukie.
\v 31 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
\v 32 Lakini kuhusu siku hiyo au saa, hakuna ajuaye, hata malaika mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
\v 33 Kuweni wangalifu, Kesheni, kwa sababu hamjui ni muda gani yatatokea.
\v 34 Ni kama mtu anayesafiri, anaacha nyumba yake, na kuweka watumishi wake kuwa watawala wa nyumba, kila mmoja na kazi yake, Na kumwamuru mlinzi kukaa macho.
\v 35 Kwa hiyo iweni macho! Kwani hamjui ni lini bwana wa nyumba atakaporudi nyumbani, yawezekana ni jioni, usiku wa manane, wakati jogoo atakapowika, au asubuhi.
\v 36 Kama akija ghafla, asikute umelala.
\v 37 Ninachowaambia nawaambia kila mtu: Kesheni!”
\c 14
\cl Sura 14
\p
\v 1 Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na waandishi walikuwa wakitafuta namna ya kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.
\v 2 Maana walikua wanasema, “Sio wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.”
\p
\v 3 Wakati Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, na alipokuwa akiegemea mezani, mwanamke mmoja akaja kwake akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya thamani kubwa, ambayo ni nardo safi. Akaivunja ile chupa na kumwaga ile nardo kichwani mwake.
\v 4 Lakini kulikuwa na baadhi yao waliokasirika. Wakazungumza wao kwa wao na kusema, “Ni nini sababu ya upotevu wa manukato haya?
\v 5 Manukato haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na wakapewa maskini.” Kisha wakamkemea.
\p
\v 6 Lakini Yesu akasema, “Mwacheni. Kwa nini mnamsumbua? Amefanya jambo zuri kwangu.
\v 7 Siku zote mnao maskini pamoja nanyi, na wakati wowote mnapotamani mnaweza kufanya mazuri kwao, lakini hamtakuwa nami wakati wote.
\v 8 Amefanya kile anachoweza: ameupaka mwili wangu mafuta kwa ajili ya maziko.
\v 9 Kweli nawaambia, kila mahali injili inapohubiriwa katika ulimwengu wote, kile alichofanya mwanamke huyu kitazungumzwa kwa ukumbusho wake.
\p
\v 10 Kisha Yudas Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili, alikwenda kwa makuhani wakuu ili kwamba apate kumkabidhi kwao.
\v 11 Wakati makuhani wakuu walisikia hivyo, walifurahi na wakaahidi kumpa fedha. Alianza kutafuta nafasi ya kumkabidhi kwao.
\p
\v 12 Siku ya kwanza ya mkate usiotiwa chachu, wakati walipotoa mwanakondoo wa pasaka, wanafunzi wake walimwambia, “Unataka twende wapi tukaandae ili upate kula mlo wa Pasaka?”
\p
\v 13 Akawatuma wawili wa wanafuzi wake na kuwaambia, “Nendeni mjini, na mwanamume amebeba mtungi wa maji atakutana nanyi. Mfuateni.
\v 14 Nyumba atakayoingia, mfuateni na mumwambie mwenye nyumba hiyo, Mwalimu asema, “Kiko wapi chumba cha wageni mahali nitakapokula Pasaka na wanafunzi wangu?”
\v 15 Atawaonesha chumba kikubwa cha juu kilicho na samani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi kwa ajili yetu pale.”
\v 16 Wanafunzi waliondoka wakaenda mjini. Walikuta kila kitu kama alivyokuwa amewaambia, na wakaandaa mlo wa Pasaka.
\v 17 Wakati ilipokuwa jioni, alikuja na wale Kumi na wawili.
\p
\v 18 Na walipokuwa wakiikaribia meza na kula, Yesu alisema, “Kweli nawaambia, mmoja kati yenu anayekula pamoja nami atanisaliti.”
\p
\v 19 Wote walisikitika, na mmoja baada ya mwingine walimwambia, “Hakika siyo mimi?”
\p
\v 20 Yesu alijibu na kuwaambia, “Ni mmoja wa Kumi na wawili kati yenu, mmoja ambaye sasa anachovya tonge katika bakuli pamoja nami.
\v 21 Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakwenda kama vile maandiko yasemavyo juu yake. Lakini ole wake mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu atasalitiwa! Ingekuwa vizuri zaidi kwake kama mtu yule asingezaliwa.”
\p
\v 22 Na walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akaubariki, na kuumega. Aliwapa akisema, “Chukueni. Huu ni mwili wangu.”
\v 23 Akachukua kikombe, akashukuru, na akawapatia, na wote wakakinywea.
\v 24 Akawaambia, “Hii ni damu yangu ya agano, damu imwagikayo kwa ajili ya wengi.
\v 25 Kweli nawaambia, sitakunywa tena katika zao hili la mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika ufalme wa Mungu.”
\v 26 Walipokwisha kuimba wimbo, walikwenda nje katika Mlima wa Mizeituni.
\p
\v 27 Yesu akawaaambia, “Ninyi nyote mtajitenga mbali nami, kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika.
\v 28 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia mbele yenu Galilaya.”
\p
\v 29 Petro alimwambia, “Hata kama wote watakuacha, mimi sitakuacha.”
\p
\v 30 Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, leo-naam, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu.”
\p
\v 31 Lakini Petro akasema kwa msisitizo, “ikiwa ni lazima nife nawe, sitakukana.” Wote walitoa ahadi ile ile.
\p
\v 32 Wakafika mahali paitwapo Gethsemane, na Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati nasali.”
\v 33 Akawachukua Petro, Yakobo, na Yohana pamoja naye, akaanza kuhuzunika na kutaabika sana.
\v 34 Aliwaambia, “Nafsi yangu ina huzuni sana, hata kufa. Bakini hapa na mkeshe.”
\v 35 Yesu akaenda mbele kidogo, akaanguka chini, akaomba, kama ingewezekana, kwamba saa hii ingemwepuka.
\v 36 Alisema, “Aba, Baba, Mambo yote yanawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini siyo mapenzi yangu, bali mapenzi yako.”
\v 37 Akarudi na kuwakuta wamelala, na akamwambia Petro, “Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hata saa moja?
\v 38 Kesheni na muombe kwamba msije mkaingia katika majaribu. Hakika roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”
\v 39 Akaenda tena na kuomba, na alitumia maneno yaleyale.
\v 40 Aliporudi tena, akawakuta wamelala, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito. Hawakujua nini cha kumwambia.
\v 41 Akarudi mara ya tatu na kuwaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Yatosha! Saa imefika. Tazama! Mwana wa Adamu anasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.
\v 42 Amkeni, twendeni. Tazama, yule anayenisaliti yuko karibu.”
\p
\v 43 Alipokuwa bado anaongea, Yudas, mmoja wa wale kumi na wawili, akafika, na kundi kubwa pamoja naye wenye mapanga na marungu, kutoka kwamakuhani wakuu, waandishi na wazee.
\v 44 Wakati huo msaliti wake alikuwa amewapa ishara, akisema, Yule nitakayembusu, ndiye. Mkamateni na kumpeleka chini ya ulinzi.”
\v 45 Wakati Yuda alipofika, moja kwa moja alienda kwa Yesu na kusema, “Mwalimu!” Na akambusu.
\v 46 Kisha wakamtia chini ya ulinzi na kumkamata.
\v 47 Lakini mmoja kati yao aliyesimama karibu naye akachomoa upanga wake akampiga mtumishi wa kuhani mkuu na kumkata sikio.
\p
\v 48 Yesu akawaambia, “Mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama mnyang'anyi?
\v 49 Wakati kila siku nilikuwa nanyi na nikifundisha hekaluni, hamkunikamata. Lakini hili limefanyika ili maandiko yatimie.
\p
\v 50 Na wale wote waliokuwa na Yesu walimwacha na kukimbia.
\v 51 Kijana mmoja, aliyekuwa amevaa vazi la kitani pekee alilokuwa amejizungushia, alikua anamfuata Yesu. Wale watu walipomkamata,
\v 52 aliiacha ile nguo ya kitani na kukimbia uchi.
\p
\v 53 Walimwongoza Yesu kwa kuhani mkuu. Pale walikusanyika pamoja naye wakuu wa makuhani wote, wazee, na waandishi.
\v 54 Sasa Petro akamfuata kwa mbali, kuelekea kwenye ua wa kuhani mkuu. Aliketi pamoja na maafisa, akiota moto ili kupata joto.
\v 55 Wakati huo makuhani wakuu wote na Baraza zima la wayahudi walikuwa wakitafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumwua. Lakini hawakuupata.
\v 56 Kwa kuwa watu wengi walileta ushuhuda wa uongo dhidi yake, lakini hata ushahidi wao haukufanana.
\v 57 Baadhi walisimama na kuleta ushahidi wa uongo dhidi yake; wakisema,
\v 58 “Tulimsikia akisema, Nitaliharibu hekalu hili lililotengenezwa kwa mikono, na ndani ya siku tatu nitajenga lingine lisilotengenezwa kwa mikono.’”
\v 59 Lakini hata ushahidi wao haukufanana.
\p
\v 60 Kuhani mkuu akasimama katikati yao na akamwuliza Yesu, “Je, huna jibu? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
\v 61 Lakini alikaa kimya na hakujibu chochote. Mara tena Kuhani mkuu akamhoji na kusema, “Je wewe ni Kristo, mwana wa Mungu aliye, barikiwa?”
\p
\v 62 Yesu alisema, “Mimi ndiye. Na utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa nguvu na akija na mawingu ya mbinguni.”
\p
\v 63 Kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Je, bado tunahitaji mashahidi?
\v 64 Mmesikia kufuru. Uamuzi wenu ni upi?” Na wote walimhukumu kama mmoja aliyestahili kifo.
\p
\v 65 Baadhi wakaanza kumtemea mate na kumfunika uso na kumpiga kwa ngumi zao na kumwambia, “Tabiri!” Maafisa walimchukua na kumpiga.
\p
\v 66 Huku Petro alipokuwa yuko chini uani, mtumishi mmoja wa watumishi wa kike wa kuhani mkuu akaja kwake.
\v 67 Alimwona Petro alipokuwa amesimama akiota moto, na akamtazama kwa karibu na kusema, “Nawe pia ulikuwa na Mnazareti, Yesu.”
\p
\v 68 Lakini alikanusha, akisema, “Sijui wala sielewi unachoongea!” Kisha akatoka mpaka langonii Na jogoo akawika.
\p
\v 69 Lakini mtumishi wa kike, alimwona na alianza kuwaambia tena wale ambao walikuwa wamesimama pale, “Mtu huyu ni mmoja wao!”
\p
\v 70 Lakini alikana tena. Baadaye kidogo wale waliokuwa wamesimama pale walikuwa wakimwambia Petro, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya.”
\p
\v 71 Lakini alianza kujiweka mwenyewe chini ya laana na kuapa, “Simjui huyu mtu mnayemzungumzia.”
\p
\v 72 Mara jogoo aliwika mara ya pili. Kisha Petro akakumbuka maneno ambayo Yesu aliyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Na aliangua kilio.
\c 15
\cl Sura 15
\p
\v 1 Asubuhi na mapema wakuu wa makuhani, na wazee na waandishi na baraza zima la wayahudi wakashauriana pamoja. Kisha wakamfunga Yesu na kumuongoza na wakampeleka kwa Pilato.
\v 2 Pilato akamwuliza, “wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” “Akamjibu, “Wewe umesema hivyo.”
\v 3 Wakuu wa makuhani wakaeleza mashitaka mengi juu ya Yesu.
\v 4 Pilato akamwuliza tena, “Hujibu chochote? Huoni jinsi wanavyokushtaki kwa mambo mengi?
\v 5 Lakini Yesu hakumjibu Pilato, na hiyo ilimshangaza.
\p
\v 6 Kwa kawaida wakati wa sikukuu Pilato humfungulia mfungwa mmoja, mfungwa waliyemwomba.
\v 7 Palikua na mtu aitwaye Baraba gerezani, amefungwa pamoja na waasi walioua wakati wa uasi.
\v 8 Umati ukaja kwa Pilato, na kumwomba kuwafanyia kama alivyofanya hapo awali.
\v 9 Pilato akawajibu na kusema, “Mnataka niwaachilie Mfalme wa Wayahudi?”
\v 10 Kwa kuwa alijua ni kwa sababu ya wivu wakuu wa makuhani walimkamata Yesu na kumleta kwake.
\v 11 Lakini wakuu wa makuhani walichochea umati kupiga kelele kwa sauti kwamba Baraba aachiliwe badala yake.
\v 12 Pilato akawajibu tena na kusema, “Nimfanye nini Mfalme wa Wayahudi?
\p
\v 13 Wakapiga kelele tena, “Msulibishe!”
\p
\v 14 Pilato akawaambia, “Amefanya jambo gani baya?” Lakini wakazidi kupiga kelele zaidi na zaidi “Msulibishe.”
\v 15 Pilato akitaka kuwaridhisha umati, akawafungulia Baraba. Akampiga Yesu mijeledi kisha akamtoa ili asulibiwe.
\p
\v 16 Askari walimwongoza hadi ndani ya ua (ulio makao makuu ya serikali) na wakakusanya kikosi kizima cha askari.
\v 17 Wakamvika Yesu kanzu ya rangi ya zambarau, na wakasokota taji ya miiba wakamvika.
\v 18 Wakaanza kumdhihaki na kusema, “Salam, Mfalme wa Wayahudi!”
\v 19 Walikua wakimpiga kichwani kwa fimbo ya mwanzi na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake kwa kumheshimu.
\v 20 Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua ile kanzu ya rangi ya zambarau na kumvika mavazi yake, na wakamtoa nje kwenda kumsulubisha.
\p
\v 21 Mtu fulani, Simoni Mkirene, aliyekuwa anaingia mjini kutoka shambani (baba yake Aleksanda na Rufo) na wakamlazimisha kubeba mslaba wa Yesu.
\v 22 Askari wakampeleka Yesu mahali paitwapo Goligotha (maana ya tafsiri hii ni, Sehemu ya Fuvu la kichwa).
\v 23 Wakampa mvinyo iliyochanganywa na manemane, lakini hakunywa.
\v 24 Wakamsulibisha na wakagawana mavazi yake, wakayapigia kura kuamua kipande atakachopata kila askari.
\p
\v 25 Yapata saa tatu asubuhi walipomsulibisha.
\v 26 Wakaweka juu yake ubao ulioandikwa shitaka, “Mfalme wa Wayahudi.”
\v 27 Walimsulubisha pamoja na majambazi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine kushoto kwake.
\v 28 “Na maandiko yakatimia yaliyonena kwamba alihesabiwa pamoja na waasi.
\v 29 Nao waliokuwa wakipita walimtukana, wakitikisa vichwa vyao wakisema, “Aha! Wewe utakayevunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu,
\v 30 jiokoe mwenyewe na ushuke chini toka msalabani!”
\p
\v 31 Kwa namna ile ile wakuu wa makuhani walimdhihaki wakisemezana, pamoja na waandishi na kusema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe.
\v 32 Mwache Kristo, Mfalme wa Israel, shuka chini sasa toka msalabani, ili tuweze kuona na kuamini. “Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana.
\p
\v 33 Ilipofika saa sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa tisa.
\v 34 Wakati wa saa tisa, Yesu alipiga kelele kwa sauti kubwa, “Eloi, Eloi, lama sabaktani?” ikiwa na maana “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”
\p
\v 35 Baadhi ya hao waliosimama waliposikia wakasema, “Tazama, anamwita Eliya.”
\p
\v 36 Mtu mmoja akakimbia, aweka divai ya siki katika sponji na kuiweka juu ya mti wa mwanzi, akampa ili anywe. Mtu mmoja akasema, “Ngoja tuone kama Eliya atakuja kumshusha chini.”
\v 37 Kisha Yesu akalia kwa sauti kubwa na akafa.
\v 38 Pazia la hekalu likagawanyika vipande viwili toka juu mpaka chini.
\p
\v 39 Wakati jemadari mmoja aliyekuwa amesimama akimwelekea Yesu, alipoona amekufa kwa jinsi ile, akasema, “Kweli huyu mtu alikuwa Mwana wa Mungu.”
\v 40 Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakitazama kwa mbali. Miongoni mwao alikuwepo Mariamu Magdalena, Mariamu (mama yake Yakobo mdogo wa Yose), na Salome.
\v 41 Wakati alipokuwa Galilaya walimfuata na kumtumikia. Na wanawake wengine wengi pia waliambatana naye hadi Yerusalemu.
\p
\v 42 Kulipokuwa jioni, na kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio, siku kabla ya Sabato,
\v 43 Yusufu wa Arimathaya alikuja pale. Alikuwa ni mjumbe wa Baraza anayeheshimiwa mtu anayeutarajia Ufalme wa Mungu. Kwa ujasiri akaenda kwa Pilato, na kuuomba mwili wa Yesu.
\v 44 Pilato akashangazwa kwamba Yesu tayari amekufa; akamwita yule jemedari akamwuliza kama Yesu amekufa.
\v 45 Alipopata uhakika kwa jemadari kwamba amekufa, alimruhusu Yusufu kuuchukua mwili.
\v 46 Yusufu alikuwa amenunua sanda. Akamshusha toka msalabani, akamfunga kwa sanda, na kumweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika mwamba. Kisha akalivingirisha jiwe mlangoni mwa kaburi.
\v 47 Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yose waliona sehemu alipozikwa Yesu.
\c 16
\cl Sura 16
\p
\v 1 Wakati sabato ilipokwisha, Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yakobo, na Salome, walinunua manukato mazuri, ili waweze kuja na kuupaka mafuta mwili wa Yesu.
\v 2 Asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma, walienda kwenye kaburi wakati jua lilipochomoza.
\v 3 Wakisemezana wao kwa wao, “Nani atavingirisha jiwe kwa ajili yetu ili tuingie kaburini?”
\v 4 Wakati walipotazama, waliona ya kuwa jiwe limekwisha kuvingirishwa, nalo lilikuwa kubwa sana.
\p
\v 5 Wakaingia kwenye kaburi na wakamwona kijana amevaa joho jeupe, ameketi upande wa kulia, na wakashangazwa.
\v 6 Akawaambia, “Msiogope. Mnamtafuta Yesu, Mnazareti, aliyesulibiwa. Amefufuka! Hayupo hapa. Tazama mahali pale walipokuwa wamemweka.
\v 7 Lakini nendeni, mkawaambie wanafunzi wake na Petro ya kuwa amewatangulia kuelekea Galilaya. Huko mtamwona, kama alivyokua amewaambia.”
\v 8 Wakaondoka na kukimbia kutoka kwenye kaburi; wakitetemeka na kushangaa. Hawakusema chochote kwa mtu yeyote sababu waliogopa sana.
\p
\v 9 Mapema katika siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alimtokea kwanza Mariamu Magdalena, ambaye kutoka kwake alimtoa mapepo saba.
\v 10 Aliondoka na kuwaambia wale ambao walikuwa pamoja naye, wakati walipokuwa wakiomboleza na kulia.
\v 11 Wakasikia kwamba yu hai na ameonekana naye, lakini hawakumwamini.
\v 12 Baada ya mambo haya, alionekana katika sura tofauti na wawili wao walipokuwa wakienda mashambani.
\v 13 Wakarudi na kuwaambia wanafunzi wengine waliobaki, lakini hawakuwaamini.
\v 14 Yesu baadaye akajitokeza kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wakila mezani, na akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo, kwa sababu hawakuwaamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.
\p
\v 15 Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni mwote, na kuhubiri injili kwa viumbe vyote.
\v 16 Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokolewa, na yule asiyeamini atahukumiwa.
\v 17 Ishara hizi zitaambatana na wote waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo. Watasema kwa lugha mpya.
\v 18 Watashika nyoka kwa mikono yao, na hata wakinywa kitu chochote cha kuuwa hakitawadhuru. Wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
\p
\v 19 Baada ya Bwana Yesu kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
\v 20 Wanafunzi wakaondoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akitenda kazi pamoja nao na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizoambatana nao.]