sw_ulb/37-HAG.usfm

64 lines
5.9 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id HAG
\ide UTF-8
\h Hagai
\toc1 Hagai
\toc2 Hagai
\toc3 hag
\mt Hagai
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Katika mwaka wa pili wa mfalme Dario, katika mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kupitia kwa nabii Hagai kwenda kwa gavana wa Yuda, Zerubabeli mwana wa Shealitieli, na kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki, kusema,
\p
\v 2 Bwana wa Majeshi asema: “Hawa watu husema, si wakati wetu kuja au kujenga nyumba ya Jehova.”
\p
\v 3 Tena neno la Bwana lilikuja kwa mkono wa nabii Hagai kusema,
\v 4 “Je ni wakati kwenu wenyewe kuishi katika nyumba zilizokamilika, na wakati nyumba hii inaharibika?
\v 5 Kwa hivyo sasa Bwana wa Majeshi asema hivi: zitafakarini njia zenu!
\v 6 Mmepanda mbegu nyingi, lakini mkaleta mavuno kidogo; mnakula lakini hamshibi, mnakunywa lakini hamutosheki na vinywaji. Mnavaa nguo lakini hampati joto wenyewe, na mtu wa mshahara hupata pesa na kuziweka kwenye mfuko uliotoboka!
\p
\v 7 Bwana wa Majeshi asema haya:
\v 8 Zitafakarini njia zenu! Pandeni milimani, mkalete mbao, na mjenge nyumba yangu; ndipo nitaifurahia na nitatukuzwa! Asema Bwana.
\v 9 Mmetazamia kupata vingi, lakini tazama! Mmeleta nyumbani vichache, kwa kuwa nilivipeperusha mbali! Kwa nini?- Hivi ndivyo asemavyo Bwana wa Majeshi! Kwa sababu nyumba yangu inakaa kwenye uharibifu, lakini kila mtu yuko radhi kwenye nyumba yake.
\v 10 Kwa sababu ya hii mbingu zimeshikiliwa zisitoe umande kwako, na ardhi imeshikilia mazao yake.
\v 11 Nimeagiza ukame juu ya ardhi na juu ya milima, juu ya nafaka na juu ya divai mpya, juu ya mafuta na juu ya mavuno ya ardhi, juu ya watu na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono yenu.
\p
\v 12 Kisha Zerubabeli mwana wa Shealitieli, na kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehozadaki, pamoja na mabaki ya watu, wakatii sauti ya Bwana Mungu wao, na maneno ya nabii Hagai, kwa sababu Bwana Mungu wao alikuwa amemtuma na watu wakaogopa uso wa Bwana.
\p
\v 13 Ndipo Hagai, mjumbe wa Bwana, akaongea ujumbe wa Bwana kwa watu na kusema, “Niko pamoja nanyi!- Hivi ndivyo asema Bwana!”
\v 14 Bwana alitibua roho ya mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli mwana wa Shealitieli, na roho ya kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki, na roho ya masalia ya watu, kwa kiasi kwamba wakaenda kufanya kazi katika nyumba ya Bwana Mungu wa Majeshi, Mungu wao.
\v 15 Katika siku ya ishirini na Mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Katika Mwezi wa saba siku ya ishirini na moja ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kupitia kwa nabii Hagai, na kusema,
\v 2 “Ongea na mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli mwana wa Shealitieli, na kwa kuhani mkuu Yehozadaki; na kwa masalia ya watu. Sema,
\v 3 Ni nani aliyebaki kati yenu aliyeuona utukufu wa nyumba hii iliyokuwa ya kwanza? Na mnaionaje kwa sasa? Je sio kama si chochote machoni penu?
\v 4 Sasa, muwe hodari, Zerubabeli -hivi ndivyo asema Bwana - na uwe hodari, kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki; muwe hodari, enyi watu wa nchi! - Hivi ndivyo asema Bwana - na mfanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi! Hivi ndivyo asema Bwana wa Majeshi.
\v 5 Na hii ndiyo agano niliyoiweka na nyinyi mlipokuwa mukitoka Misri, na Roho wangu anadumu katikati yenu. Msiogope
\v 6 kwa kuwa Bwana wa majeshi anasema haya: “kitambo kidogo kwa mara nyingine nitatikisa mbingu na dunia, bahari na nchi kavu!
\v 7 Na nitalitikisa kila taifa, na kila taifa litaleta vitu vyao vya thamani kwangu, na nitaijaza nyumba hii na utukufu! asema Bwana wa Majeshi.
\v 8 Dhahabu na fedha ni yangu! - Hivi ndivyo asema Bwana wa majeshi.
\v 9 Utukufu wa nyumba hii utakuwa mkubwa siku zijazo kuliko utukufu wa nyumba ya kwanza, asema Bwana wa majeshi, na nitawapa amani mahali hapa! - Hivi ndivyo asema Bwana wa majeshi.”
\p
\v 10 Katika siku ya ishirini na nne mwezi wa tisa, mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Bwana lilimjia nabii Hagai na kusema,
\v 11 “Bwana wa Majeshi asema hivi: Muulizeni kuhani kuhusu sheria, na useme:
\v 12 Kama mtu atabeba nyama iliyotolewa kwa Bwana katika pindo la vazi lake, kama upindo utagusa mkate au mchuzi, mvinyo au mafuta, au chakula kingine, je chakula hicho kinafanyika kitakatifu?” Kuhani alijibu akasema, “Hapana”
\p
\v 13 Halafu Hagai akasema. “Kama mtu ni najisi kwa ajili ya kumgusa maiti na kugusa vitu hivi, vyote vinaweza kuwa najisi?” Kuhani akajibu na kusema, “Ndiyo, vitakuwa najisi.”
\p
\v 14 Kwa hiyo Hagai akajibu nakusema, “Ni pamoja na hawa watu na pamoja na taifa liliko mbele yangu! - Haya anayasema Bwana- na pia kila kitu kimekwisha kwa mkono wake: walichotoa hakikuwa kisafi kilikuwa kichafu.
\p
\v 15 Kwa hiyo sasa, tafakarini hayo kuanzia leo na kuendelea, kabla jiwe halijawekwa juu ya jiwe lingine katika hekalu la Bwana,
\v 16 Ilikuwaje basi? Kila mtu alipokuja kwenye vipimo ishirini vya nafaka, kumbe kulikuwa na vipimo kumi tu, na aliyekuja kuchota divai ya vipimo hamsini, kumbe kuliwa na vipimo ishirini tu.
\v 17 Niliwataabisha ninyi na kazi za mikono yenu kwa ukame na ukungu na mvua ya mawe lakini hamkunirudia- asema Bwana.
\p
\v 18 Tafakari siku hii ya leo na kuendelea, kutoka siku ya ishirini na nne katika mwezi wa tisa, toka siku ile msingi wa hekalu la Bwana uliwekwa. Tafakarini hilo!
\v 19 Je, bado kuna mbegu katika ghala? Mzabibu, mti wa mtini, komamanga, na mti wa mzeituni havikuzaa matunda! Lakini kutoka siku hii ya leo nitawabariki!”
\p
\v 20 Tena neno la Bwana likaja kwa mara ya pili kwa Hagai siku ya ishiri na nne katika mwezi kusema,
\v 21 “Sema na mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli umwambie, Nitatikisa mbingu na dunia.
\v 22 Kwa hiyo nitaangusha viti vya falme na kuharibu nguvu za falme za mataifa! Nitaangusha magari na wapandao; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa sababu ya upanga wa ndugu yake.
\p
\v 23 Siku hiyo'-hivi ndivyo asema Bwana wa Majeshi- Nitakuchukua wewe Zerubabeli mwana wa Shealitieli, kama mtumishi wangu! Hivi ndivyo Bwana anavyosema. “Nitakutumia kama pete ya muhuri wangu, kwa sababu mimi nimekuchagua!- asema Bwana wa Majeshi!”