sw_ulb/35-HAB.usfm

125 lines
7.8 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id HAB
\ide UTF-8
\h Habakuki
\toc1 Habakuki
\toc2 Habakuki
\toc3 hab
\mt Habakuki
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Ujumbe ambao habakuki nabii aliona.
\q1
\v 2 “Yahwe, kwa muda gani nitalilia msaada, na hutasikia? Nakulilia wewe kwasababu ya, vurugu! lakini hutaokoa.
\q1
\v 3 Kwa nini unanifanya nione maovu na kuangalia matendo mabaya? Uharibifu na vurugu viko mbele yangu; kuna mapambano, na ushindani unainuka.
\q1
\v 4 Kwa hivyo sheria ni dhaifu, na haki haidumu kwa wakati wowote. Kwa kuwa waovu wanawazunguka wenye haki; kwa hivyo haki iliyobadilishwa inatoweka.”
\q1
\v 5 “Angalia mataifa na uwachunguze; ukastajaabu na ushangae! Kwa maana hakika niko karibu kufanya jambo katika siku zako ambalo hutaamini utakapoambiwa.
\q1
\v 6 Kwa maana angalia! Nakaribia kuwainua Wakaldayo _taifa katili na lenye haraka _wanapita katika upana wa nchi kuteka makao yasiyo yao.
\q1
\v 7 Wanatisha na kuogofya; hukumu yao na ukuu wao hutoka kwao wenyewe.
\q1
\v 8 Farasi wao pia wanambio sana kuliko chui, wakali kuliko mbwa mwitu wa jioni. Farasi wao huwaseta, na wapanda farasi wao huja kutoka mbali _ wanapaa kama tai anayewahi kula.
\q1
\v 9 Wote huja kwa vurugu; makundi yao yanakwenda kama upepo wa jangwani, na wanakusanya mateka kama mchanga.
\q1
\v 10 Wanawadhihaki wafalme, na watawala ni dhihaka kwao. Huicheka kila ngome, maana huibomoa kama udongo na kuukamata.
\q1
\v 11 Ndipo kama upepo atapita; ataendelea kupita _watu wenye hatia, ambao nguvu zao ni mungu wao.”
\q1
\v 12 “Wewe si wa tangu milele, Yahwe Mungu wangu, uliye Mtakatifu wangu? Hatutakufa. Yahwe aliwatenga kwa ajili ya hukumu, nawe, Mwamba, umewaimarisha kwa ajili ya kusahihisha.
\q1
\v 13 Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu, wala huwezi kuangalia maovu kwa fadhila; kwa nini basi umeangalia kwa upendeleo ambao wanasaliti? Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu wanawameza wenye haki kuliko wao wenyewe?
\q1
\v 14 Unawafanya watu kama samaki baharini, kama viumbe vitambaavyo bila mtawala.
\q1
\v 15 Huwaleta wote kwa ndoana; anawakokota watu kutoka kwenye nyavu za samaki na kuwakusanya kwenye wavu wao; kwa hiyo anashangilia na kufurahi.
\q1
\v 16 Kwa hiyo anatoa sadaka kwa wavu wake na kuchoma ubani kwa juya lake, kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe, nachakula chake ni aina tajiri zaidi.
\q1
\v 17 Kwa hiyo ataendelea kumwaga wavu wake, na kuendelea kuyachinja mataifa bila huruma?”
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Nitasimama kwenye nguzo ya ulinzi na kujiweka juu ya mnara, na nitazame nione atakaloniambia na nione vile nitakavyotoka katika lalamiko langu.
\p
\v 2 Yahwe alinijibu na alisema, “Rekodi maono haya, na uandike dhahiri juu ya kibao ili kwamba anayesoma anaweza kusoma.
\q1
\v 3 Sababu maono haya bado ni kwa wakati ulioamriwa na yatashuhudia na hayatakosea. Ingawa yanakawia, yasubiri. Sababu kwa hakika itatimia na haitachelewa.
\q1
\v 4 Tazama! Yule ambaye hamu zake si haki ndani yake ni mwenye majivuno. Lakini mwenye haki ataishi kwa imani.
\q1
\v 5 Kwa kweli, kama vile mvinyo ni mdanganyifu, hata hivyo mtu mwenye kiburi hakai nyumbani. Amefanya koo lake lipanuke kama kuzimu; na kama kifo, hatosheki. Ameyakusanya pamoja mataifa, na kujiwekea watu wote kwake.
\q1
\v 6 Hawatachukua hawa wote methali na dhihaka, mafumbo kumhusu, wakisema, wake yule aongezaye visivyo vya kwake! Ni kwa muda gani utaongeza uzito wa dhamana uliyochukua?
\q1
\v 7 Je hao wanaokuuma hawatainuka ghafla na hao wanaokutisha kuamka? Utakuwa mwathirika kwa ajili yao.
\q1
\v 8 Kwa sababu umeteka nyara watu wengi, mabaki yote ya watu yatakuteka nyarawewe. Sababu umemwaga damu ya binadamu na umeitendeanchi udhalimu, miji, na wote wanaokaa ndani yake.
\q1
\v 9 Ole kwa yule anayepata mapato maovu kwa ajili ya nyumba yake, hivyo apate kukiweka kiota chake juu ili apate kujiepusha na mkono wa uovu.
\q1
\v 10 Umebuni aibu kwa nyumba yako kwa kukatilia mbali watu wengi, na umefanya dhambi dhidi ya maisha yako mwenyewe
\q1
\v 11 Sababu mawe yatapasa sauti kutoka ukutani, na pao la mbao litawajibu,
\q1
\v 12 Ole wake yule ajengaye mji kwa damu, na anayeimarisha mji kwa uovu.
\q1
\v 13 Haikutoka kwa Bwana wa majeshi kwamba watu wafanye kazi kwa ajili ya moto na mataifa yanajichosha yenyewe bure?
\q1
\v 14 Bado nchi itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana kama maji yaifunikavyo bahari.
\q1
\v 15 Ole wake yule anayelazimisha majirani wake kulewa _unaonyesha hasira yako na kuwafanya walewe ili uweze kutazama uchi wao.
\q1
\v 16 Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako! Kunywa, na utafichua govi lako ambalo halijatahiriwa! Kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.
\q1
\v 17 Udhalimu uliotendewa Lebanoni utakufunikiza na uharibifu wa wanyama utakuogopesha. Sababu umemwaga damu ya mtu na umei tendea nchi udhalimu, miji, na wote wanaokaa humo.
\q1
\v 18 Ni faida gani iliyoko kwa sanamu ya kuchongwa? Sababu yule aliyeichonga hiyo! Au kinyago cha kuyeyuka, mwalimu wa uongo? Sababu aliyetengeneza hutumaini kile ametengeneza anapozifanya sanamu zisizo na faida
\q1
\v 19 Ole kwa yule auambiaye ubao, Amka! Au kwa jiwe lisilo na uhai, Inuka! Vitu hivi vinafundisha? Angalia, hiki juu kimefunikwa kwa dhahabu na fedha, lakini ndani yake hakina pumzi kabisa.
\q1
\v 20 Lakini Bwana yumo katika hekalu lake takatifu! Nchi yote iwe kimya mbele zake.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Maombi ya Habakuki nabii:
\v 2 Yahwe, nimesikia habari zako, na mimi naogopa. Yahwe, fufua kazi yako katikati ya nyakati hizi; katikati ya miaka hii fanya ijulikane; kumbuka kuwa na rehema katika ghadhabu yako.
\q1
\v 3 Mungu alikuja kutoka Temani, na yule Mtakatifu kutoka Parani. Sela Utukufu wake umezifunika mbingu, na dunia ilikuwa imejaa sifa zake.
\q1
\v 4 Na mng'ao wake kama mwanga, mionzi miwili ilimulika kutoka mkononi mwake; ambapo uweza wake ulifichwa.
\q1
\v 5 Ugonjwa wa kufisha ulitangulia mbele yake, na tauni ilitoka miguuni pake.
\q1
\v 6 Yeye alisimama na akaipima nchi; aliangalia na akayatikisa mataifa. Hata milima ya milele ikatawanyika, na vilima vya kale vikainama. Njia yake ni ya kale.
\q1
\v 7 Niliona hema za Wakushi katika mateso, na vitambaa vya hema za nchi ya Midiani vinatetemeka
\q1
\v 8 Yahwe alikasirikia pale mitoni? Ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya mito, au hasira yako dhidi ya bahari, unapopanda juu ya farasina magari yako ya ushindi
\q1
\v 9 Umeleta upinde wako bila mfuniko; unaweka mishale kwenye upinde wako! Sela Uliigawa nchi na mito.
\q1
\v 10 Milima ilikuona wewe na kugeuka kwa uchungu. Gharika ya maji ikapita juu yao; vilindi vikapaza sauti. Vikainua juu mikono yake
\q1
\v 11 Jua na mwezi vilisimama imara juu mahali pake katika mwanga wa mishale yako ilipopaa, kwa mwanga wa mkuki wako umeremetao
\q1
\v 12 Umetembea juu ya nchi kwa hasira. Katika ghadhabu umewapura mataifa.
\q1
\v 13 Ulikwenda nje kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajil ya wokovu wa mteule wako. Wewe huponda kichwa cha nyumba ya mwovu kuweka wazi kutoka kwa msingi mpaka kwa shingo. Sela
\q1
\v 14 Umekichoma kichwa cha mashujaa wake kwa mishale yake mwenyewe sababu walikuja kama mawimbi kututawanya wivu wao ulikuwa kama mtu anayemwangamiza maskini mafichoni.
\q1
\v 15 Umekanyaga juu ya bahari kwa farasi wako, na kuyarundika maji makuu.
\q1
\v 16 Nilisikia, viungo vyangu ndani vilitetemeka! Midomo yangu ilitetemeka kwa sauti ile. Uozo unakuja katika mifupa yangu, na chini yangu natetemeka nikisubiri kwa kimya siku ya dhiki iwajilie watu waliotushambulia
\q1
\v 17 Ingawa mtini hautachanua na hakuna mazao kutoka kwa mizabibu; ingawaje matunda wa mti wa mzaituni inakatisha tamaa na mashamba hayatoi chakula; iwapo kundi la mifugo limekatwa kutoka kwa kibanda na hakuna ng'ombe katika zizi, hiki ndicho nitakacho kifanya.
\q1
\v 18 Bado, nitafurahia katika Bwana. Nitashangilia kwa sababu ya Mungu wa wokovu wangu.
\q1
\v 19 Bwana Yahwe ni nguvu yangu na huifanya miguu yangu kama ya kulungu. Ananifanya niende mbele mahali pangu pa juu. - Kwa mwelekezi wa muziki, kwa vyombo vyangu vya nyuzi.