sw_ulb/30-AMO.usfm

310 lines
22 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id AMO
\ide UTF-8
\h Amosi
\toc1 Amosi
\toc2 Amosi
\toc3 amo
\mt Amosi
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Haya ni mambo yanayoihusu Israeli ambayo Amosi, mmoja wa wachungaji katika Tekoa, aliyapokea katika ufunuo. Alipokea haya mambo katika siku za Uzia mfalme wa Yuda, na pia katika siku za Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli, miaka miwili kabla ya tetemeko la aridhi.
\p
\v 2 Alisema, “Yahwe atanguruma kutoka Sayuni; atainua sauti yake kutoka Yerusalemu. Malisho ya wachungaji yanaomboleza; Na kilele cha Karmeli kitanyauka.
\p
\v 3 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya chuma.
\q1
\v 4 Lakini nitapeleka moto kwenye nyumba ya Hazaeli, utakaoteketeza majumba ya Ben-Hadadi.
\q1
\v 5 Nitalivunja komeo la Dameski na kuwakatilia mbali wakaaji katika bonde la Aveni, na pia yule mtu ashikaye fimbo ya kifalme katika Beth-Edeni. Na watu wa shamu watakwenda utumwani hata Kiri,” asema Yahwe.
\p
\v 6 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Gaza, hata manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu waliwachukua mateka watu wote, kuwaweka juu ya mkono wa Edomu.
\q1
\v 7 Lakini nitatuma moto kwenye kuta za Gaza, na kuziteketeza majumba yake zake.
\q1
\v 8 Nami nitamkatilia mbali ya mwenyeji katika Ashdodi na mtu ashikaye fimbo ya kifalme kutoka Ashkeloni. Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni, na mabaki ya Wafilisti wataangamia,” asema Bwana Yahwe.
\p
\v 9 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Tiro, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu waliwapelekea watu wote kwa Edomu, na wamevunja agano lao la undugu.
\q1
\v 10 Nitapeleka moto kwenye kuta za Tiro, nao utaziteketeza ngome zake.”
\p
\v 11 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, “Kwa makosa matatu za Edomu, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu alimfuatilia ndugu yake kwa upanga na kutupilia mbali huruma zote. Hasira yake ikaendelea kuwa kali, na ghadhabu yake ikabaki milele.
\q1
\v 12 Nitapeleka moto juu ya Temani, na utaziteketeza nyumba za kifalme za Bozra.”
\p
\v 13 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, “Kwa makosa matatu za watu wa Amoni, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake, kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili waweze kupanua mipaka yao.
\q1
\v 14 Nitawasha moto katika kuta za Raba, nao utaziteketeza nyumba za kifalme, pamoja na kupiga kelele katika siku ya vita, pamoja na dhoruba katika siku ya kimbunga.
\q1
\v 15 Mfalme wao ataenda utumwani, yeye na maafisa wake pamoja,” asema Yahwe.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Moabu, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu amechoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hadi kuwa chokaa.
\q1
\v 2 Nitatuma moto juu ya Moabu, na utaangamiza majumba ya Keriothi. Moabu atakufa katika ghasia, pamoja na kelele na sauti ya tarumbeta.
\q1
\v 3 Nami nitamkatilia mbali mwamuzi kati yake, na nitawaua wakuu wake wote pamoja na yeye,” asema Yahwe.
\p
\v 4 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Yuda, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu wameikataa sheria ya Yahwe na hawakuzishika amri zake. Uongo wao umewapotosha, ambao baba zao pia waliufuata.
\q1
\v 5 Nitatuma moto juu ya Yuda, na utaimeza majumba ya Yerusalemu.”
\p
\v 6 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Israeli, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu wamewauza wasio na hatia kwa fedha na maskini kwa jozi moja ya viatu.
\q1
\v 7 Nao hupeperusha mavumbi ya nchi yaliyo kichwani mwa maskini, na kuipotosha njia ya wanyenyekevu. Mtu na baba yake wanalala na msichana mmoja na hivyo kulitia unajisi jina langu takatifu.
\q1
\v 8 Nao hulala chini karibu na kila madhabahu kwenye nguo zilizowekwa dhamana, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya wale ambao walitozwa faini.
\q1
\v 9 Bado nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi; alikuwa na nguvu kama mialoni. Kisha nikaharibu matunda yake juu na mizizi yake chini.
\q1
\v 10 Pia, niliwapandisha kutoka nchi ya Misri na kuwaongoza miaka arobaini nyikani ili mmiliki nchi ya Wamori.
\q1
\v 11 Nimewainua manabii kutoka miongoni mwa watoto wenu wawe Wanadhiri kutoka vijana wenu. Je sio hivyo, watu wa Israeli? -Hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\q1
\v 12 Lakini mmewashawishi Wanadhiri kunywa mvinyo na kuwaamuru manabii wasifanye unabii.
\q1
\v 13 Tazama, nitawakanyaga kama mkokoteni uliojaa miganda inayoweza kumkanyaga mtu.
\q1
\v 14 Mtu akimbiaye hatapata kimbilio; mwenye nguvu hataongeza nguvu zake mwenyewe; wala shujaa kujiokoa mwenyewe.
\q1
\v 15 Apindaye upinde hatasimama; mkimbiaji sana hatakimbia; mwendesha farasi hatajiokoa mwenyewe.
\q1
\v 16 Hata wapiganaji shujaa watakimbia uchi katika siku hiyo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.”
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Sikieni neno la Yahwe aliloongea juu yenu, enyi wana wa Israeli, juu ya familia nzima ambayo niliwatoa kutoka nchi ya Misri, nikisema,
\q1
\v 2 “Nimewachagua ninyi tu kutoka familia zote za dunia. Kwa hiyo nitawaadhibu kwa dhambi zenu zote.”
\q1
\v 3 Je wawili wanaweza kutembea pamoja isipokuwa wamekubaliana?
\q1
\v 4 Je, simba huunguruma msituni wakati hakuna mawindo? Je, mwana simba ataunguruma kutoka pangoni mwake kama hajakamata kitu?
\q1
\v 5 Je, ndege ataanguka kwenye mtego ardhini wakati hakuna chambo kimewekwa kwa ajili yake? Je, mtego utafyatuka juu ardhini wakati hakuna kitu cha kukamata?
\q1
\v 6 Je, tarumbeta itapigwa mjini na watu wasitetemeke? Je, janga laweza kuja mjini bila kuletwa na Yahwe?
\q1
\v 7 Hakika Bwana Yahwe hatafanya kitu isipokuwa awafunulie mpango watumishi wake manabii.
\q1
\v 8 Simba ameshaunguruma! Nani hataogopa? Bwana Yahwe amekwisha ongea; nani asiyeweza kutabiri?
\q1
\v 9 Tangazeni hii katika majumba ya Ashidodi, na katika majumba ya nchi ya Misri; mkaseme, “Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria; tazama machafuko makubwa kati yake, na waliokandamizwa ndani yake.
\q1
\v 10 Kwa kuwa hawajui jinsi ya kufanya haki -asema Yahwe - hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.”
\p
\v 11 Kwa hiyo, hivi ndivyo Yahwe asemavyo, “Adui ataizunguka nchi pande zote. Ataziondoa nguvu zako kutoka kwako, na majumba yako yatatekwa nyara.”
\p
\v 12 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo,” Kama mchungaji aokoavyo katika kinywa cha simba miguu miwili tu au kipande cha sikio, ndivyo wana wa Israeli watakavyookolewa wale waishio katika Samaria, penye pembe ya kitanda. Kwenye ukingo wa kochi.”
\p
\v 13 Sikieni na kushuhudia juu ya nyumba ya Yakobo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi,
\q1
\v 14 “Kwa kuwa katika siku ambayo nimeadhibu dhambi za Israeli, pia nitaziadhibu madhabahu za Betheli. Pembe za madhabahu zitakatwa na kuanguka chini.
\q1
\v 15 Nitaiharibu nyumba ya wakati baridi pamoja na nyumba ya wakati wa hari. Nyumba za pembe zitaangamia, na nyumba kubwa zitakuwa na mwisho,” - hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 Lisikilizeni neno hili, ninyi ng'ombe wa Bashani, ninyi mliomo katika mlima wa Samaria, ninyi mnaowakandamiza maskini, ninyi mnaowaponda wahitaji, ninyi mnaowaambia waume zenu, “Leteni divai tunywe.”
\q1
\v 2 Bwana Yahwe ameapa kwa utakatifu wake, “Tazama, siku zitakuja kwenu atakapowaondoa kwa ndoana, na wazao wenu kwa ndoana.
\q1
\v 3 Mtatoka kupitia mahali palipo bomolewa kwenye kuta za mji, kila mwanamke moja kwa moja mbele yake, nanyi mtatupwa katika Harmoni” -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.
\q1
\v 4 “Nendeni Betheli na mtende uovu, hata Gilgali mkaongeza dhambi, leteni dhabihu zenu kila asubuhi, na zaka zenu kila baada ya siku tatu.
\q1
\v 5 Toeni dhabihu za shukurani ya kitu kilichotiwa chachue; mkatangaze sadaka mtoazo kwa hiari; na kuzihubiri habari zake kwa kuwa hii ndiyo iwapendezayo, ninyi watu wa Israeli -hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
\q1
\v 6 Niliwapeni usafi wa meno katika miji yenu yote, na kupungukiwa na mkate katika sehemu zenu zote. Lakini hamkunirudia mimi -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\q1
\v 7 Pia nikaizuia mvua ilipokuwa imebaki miezi mitatu kabla ya mavuno. Nikaifanya inyeshe juu ya mji mmoja na kuifanya isinyeshe katika mji mwingine. Kipande kimoja cha nchi ilinyesha, lakini kipande kingine cha nchi ambapo haikunyesha palikuwa pakavu.
\q1
\v 8 Basi miji miwili mitatu ikatangatanga kwenda kwenda mji mwingine ili kunywa maji, lakini hawakutosheka. Bado hamkunirudia mimi -asema Yahwe.
\q1
\v 9 Nimewapiga kwa maradhi yanayosababisha kuvu. Wingi wa bustani na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu, na mizaituni yenu, na nzige iliwala. Bado hamkunirudia mimi, hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\q1
\v 10 Nami nalituma kati yenu tauni kama tauni ya Misri. Nimewaua vijana wenu kwa upanga, farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa kambi zenu nakuiingiza katika mianzi y pua zenu. Bado hamkunirudia mimi -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.
\q1
\v 11 Naliwaangamiza baadhi yenu, kama wakati Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora. Mlikuwa kama kijinga kilichonyakuliwa kutoka kwenye moto. Bado hamkunirudia mimi- asema Yahwe.
\q1
\v 12 Kwa hiyo nitafanya jambo baya kwako, Israeli; na kwa sababu nitafanya jambo baya kwako, jiandae kukutana na Mungu, Israeli!
\q1
\v 13 Kwa kuwa, tazama, yeye atengenezaye milima pia ndiye aumbaye upepo, humfunulia mawazo yake mwanadamu, hufanya asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahala pa juu ya dunia. Yahwe, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.”
\c 5
\cl Sura 5
\p
\v 1 Sikilizeni hili neno ambalo nisemalo kama maombelezo juu yenu, nyumba ya Israeli.
\q1
\v 2 Bikira wa Israeli ameanguka; hatainuka tena; ameachwa katika ardhi yake, hakuna mtu wa kumwinua.
\p
\v 3 Kwa kuwa hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Mji ule utokao nje kwa elfu watabaki watu mia, na mji utokao nje kwa mia watabaki watu kumi kwa nyumba ya Israeli.”
\p
\v 4 Kwa kuwa hivi ndivyo Yahwe asemavyo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni na mtaishi!
\q1
\v 5 Bali msitafute Betheli; wala msiiingie Gilgali; wala msisafiri kwenda Berisheba. Kwa kuwa Gilgali hakika itachukuliwa mateka, na Betheli itakua ubatili.
\q1
\v 6 Mtafuteni Yahwe nanyi mtaishi, asinje akawaka kama moto kwenye nyumba ya Yusufu. Nao utateketeza, na hakutakuwa na mtu hata mmoja kuuzima katika Betheli-
\q1
\v 7 Ninyi manaogeuza haki kuwa uchungu na kuiangusha haki chini!”
\q1
\v 8 Alizifanya Kilimia na Orioni; Hugeuza uvuli wa mauti kuwa asubuhi; na kuufanya mchana kuwa giza kama usiku; na huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi. Yahwe ndilo jina lake!
\q1
\v 9 Huwanyeshea wenye nguvu uharibifu wa ghafla hata uharibifu uje juu ya ngome.
\q1
\v 10 Wanamchukia yyeye akemeaye langoni, nao humchukia yeye anenaye kwa unyofu.
\q1
\v 11 Basi kwa kuwa mnamkanyaga maskini, na kumtoza ngano - injapokuwa mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, hamtaishi kwenye nyumba hizo. Mmependezwa na mashamba ya mizabibu, lakini hamtakunywa divai yake.
\q1
\v 12 Kwa kuwa najua ni jinsi gani mlivyo na makosa mengi na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa- ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji kwenye langoni wasipate haki yao.
\q1
\v 13 Kwa hiyo kila mtu mwenye busara atanyamaza kimya kwenye wakati kama huo, kwa kuwa ni wakati wa uovu.
\q1
\v 14 Tafuteni mazuri na sio mabaya, ili kwamba mpate kuishi. Hivyo Yahwe, Mungu wa majeshi, atakuwa na ninyi, kama msemavyo.
\q1
\v 15 Chukieni mabaya, yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni. Huenda Yahwe, Mungu wa majeshi, atawafadhili mabaki ya Yusufu.
\p
\v 16 Kwa hiyo, hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi, Bwana, “Kutakuwa na maombolezo kwenye njia kuu zote, na watasema kwenye mitaa yote, Ole! Ole! Watawaita wakulima kuomboleza na waombolezao stadi waomboleze.
\q1
\v 17 Katika mashamba yote ya mizabibu kutakuwa na kilio, kwa kuwa nitapita katikati yako,” asema Yahwe.
\q1
\v 18 Ole wenu ninyi mnaoitamani siku ya Yahwe! Kwa nini mnaitamani? Itakuwa giza na sio nuru,
\q1
\v 19 kama wakati mtu anamkimbia simba na kukutana na dubu, au aliingia katika nyumba na kuweka mkono wake kwenye ukuta na kung'atwa na nyoka.
\q1
\v 20 Je, siku ya Yahwe sia giza, wala si nuru? Je, si giza sana, na hakuna mwangaza ndani yake?
\q1
\v 21 “Nazichukia, nazidharau sikukuu zenu, wala siyapendezwi na makusanyiko yenu matakatifu.
\q1
\v 22 Hata kama mnanitolea sadaka ya kuteketeza na sadaka za unga, sitazipokea, wala kuzitazama sadaka za amani na za wanyama walionona.
\q1
\v 23 Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaisikia sauti za vinanda vyenu.
\q1
\v 24 Badala yake, acheni hukumu itelwmke kama maji, na haki kama maji makuu.
\q1
\v 25 Je, mmeniletea dhabihu na sadaka za kuteketeza jangwani kwa mda wa miaka arobaini, enyi nyumba ya israeli?
\q1
\v 26 Tena mlimchukua li Sikuthi kama mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya miungu yenu, mliyojifanyia wenyewe.
\q1
\v 27 Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni nje ya Dameski,” asema Yahwe, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.
\c 6
\cl Sura 6
\p
\v 1 Ole wenu ninyi mnaostarehe katika Sayuni, mnaotumainia mlima wa Samaria, watu mashuhuri katika taifa kuu, ambao nyumba ya Israeli huwaendea!
\q1
\v 2 “Vukeni hata Kalne, mkaone; na kutoka huko nendeni hadi Hamathi, mji mkuu; kisha shuka mpaka Gathi ya Wafilisti. Je! Weweni wabora kuliko falme hizi? Au je, eneo lao ni kubwa kuliko eneo lenu?”
\q1
\v 3 Ole wenu ninyi mnaoweka mbali siku ya adhabu, mnaoleta karibumakao ya jeuri.
\q1
\v 4 Ninyi mnaolala juu ya vitanda vya pembe na kujinyoosha juu ya viti vyenu. Mnaokula wana kondoo kutoka kwenye kundi na ndama kutoka kwenye zizi.
\q1
\v 5 Ninyi mnaoimba nyimbo za kijinga pamoja na sauti ya vinanda; na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi kama vile Daudi.
\q1
\v 6 Ninyi mnaokunywa divai katika mabakuli na kujipaka marahamu ilyo nzuri, lakini hawahuzuniki juu ya mateso ya Yusufu.
\q1
\v 7 Kwa hiyo sasa watachukuliwa mateka, kama wafungwa wa kwanza, na hao waketio katika karamu wataondolewa.
\p
\v 8 “Mimi Bwana Yahwe, nimeapa kwa nafsi yangu -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi, naizira fahari ya Yakobo; nachukia boma zake. Kwa hiyo nitautoa huo mji pamoja vyote vilivyomo humo.”
\p
\v 9 Kisha itakuwa, watu kumi wakikaa katika nyumba moja, watakufa.
\v 10 Na mtu wa jamaa ya wafu, pamoja na mtu atakayezichoma moto, atakapoichukua mizoga na kuitoa nje ya nyumba, atamwambia aliye ndani ya nyumba, “Je! Kuna zaidi na wewe?” Kisha mtu atasema, “Hapana” Naye atasema, nyamaza ulimi wako, kwa maana hatuthubutu kulitaja jina la Bwana.
\q1
\v 11 Tazama, Yahwe atatoa amri, na nyumba kubwa itapigwa kuwa vipande vipande, na nyumba ndogo kuwa na nyufa.
\q1
\v 12 Je, farasi watakimbia juu ya mteremko wa miamba? Je, mtu atalima huko na ng'ombe? Bado mmegeuza haki kuwa sumu na tunda la haki kuwa uchungu.
\q1
\v 13 Ninyi mnaofurahia Lo Debari, msemao, “Je! Hatukujitwalia Karnaimu kwa nguvu zetu wenyewe?”
\q1
\v 14 “Lakini tazama, nitainua juu yenu taifa, enyi nyumba ya Israeli,” hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe, Mungu wa majeshi. “Watawatesa ninyi kuanzia maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Araba.”
\c 7
\cl Sura 7
\p
\v 1 Hivi ndivyo ambavyo Bwana Yahwe alivyonionyesha. Tazama, aliumba kundi kubwa la nzige wakati wa kuchipuka kwa mmea, na, tazama, ulikuwa ni mmea wa mwisho baada ya mavuno ya mfalme.
\v 2 Wakati walipomaliza kula mbogamboga za nchi, kisha nikasema, “Bwana Yahwe, tafadhali nisamehe; Je, Yakobo ataishije? Kwa kuwa yeye ni mdogo sana.”
\p
\v 3 Yahwe akapunguza hasira kuhusu hili. “Haitatokea,” akasema.
\p
\v 4 Hivi ndivyo ambavyo Bwana Yahwe alivyonionyesha: Tazama, Bwana Yahwe aliita juu ya moto kuhukumu. Nao ukakausha sana, kilindi chini ya dunia na kutaka kuitekeza nchi, pia.
\v 5 Lakini nikasema, “Bwana Yahwe, acha tafadhali; Yakobo ataishije? Kwa kuwa yeye ni mdogo sana.”
\p
\v 6 Yahwe akagairi kuhusiana na hili, “Hili halitajitokeza pia,” asema Bwana Yahwe.
\p
\v 7 Hivi ndivyo ambavyo Yahwe alivyo nionyesha: Tazama, Bwana amesimama karibu na ukuta, pamoja na uzi wa timazi kwenye mkono wake.
\v 8 Yahwe akanambia, “Amosi, unaona nini?” nikasema, “Uzi wa timazi.” Kisha Bwana akasema, “Tazama, nitaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitawapita tena.
\q1
\v 9 Mahala pa juu pa Isaka pataharibiwa, patakatifu pa Israeli pataangamia, na nitainuka juu ya nyumba ya Yeroboamu kwa upanga”
\p
\v 10 Kisha Amazia, yule kuhani wa Betheli, akatuma ujumbe kwa Yeroboamu, mfalme wa Israeli: “Amosi amefanya njama dhidi yako katikati ya nyumba ya Israeli. Nchi haiwezi kubeba maneno yote haya.
\v 11 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Amosi, Yeroboamu atakufa kwa upanga, na hakika Israeli itakwenda utumwani kutoka nchi yake.”
\p
\v 12 Amazia akamwambia Amosi, “Mwonaji, nenda, kimbia irudie nchi ya Yuda, na hapo ule mkate na kutabiri.
\v 13 Lakini usitabiri tena hapa katika Betheli, kwa kuwa ni patakatifu pa mfalme na nyumba ya kifalme.”
\p
\v 14 Kisha Amosi akamwambia Amazia, “Mimi sio nabii wala mwana wa nabii. Mimi ni mchungaji wa mifugo, na mtunza mikuyu.
\v 15 Lakini Yahwe akanichukua kutoka kuchunga mifugo na kunambia, Nenda, katabiri kwa watu wangu Israeli.
\q1
\v 16 Sasa sikia neno la Yahwe. Wewe usemaye, Usitabiri juu ya Israeli, na usiongee juu ya nyumba ya Isaka.
\p
\v 17 Kwa hiyo hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Mke wako atakuwa kahaba katika mji; wana wako waume na binti zako wataanguka kwa upanga; nchi yako itapimwa na kugawanywa; utakufia katika nchi najisi, na Israeli hakika itakwenda utumwani kutoka nchi yake.”’
\c 8
\cl Sura 8
\p
\v 1 Hiki ndicho ambacho bwana Yahwe amenionyesha. Tazama, kikapu cha matunda ya hari!
\v 2 Akasema, “Unaona nini, Amosi?” Nikasema, “Kikapu cha matunda ya hari.” Kisha Yahwe akaniambia, “Mwisho umefika kwa watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe.
\p
\v 3 Nyimbo za kwenye hekalu zitakuwa vilio. Katika siku hiyo-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe. Mizoga itakuwa mingi, katika kila sehemu wataitupa katika ukimya!”
\q1
\v 4 Sikieni haya, ninyi mnaowameza wahitaji na kuwakomesha maskini.
\p
\v 5 Wakisema, “Mwezi mpya utaondoka lini, hivyo tunaweza kuuza nafaka tena? Na Sabato, ili tufanye biashara yangano? Kuifanya efa kuwa ndogo, na shekeli kuwa kubwa, na kuipotosha mizani kwa hila.
\q1
\v 6 Hivi ndivyo ambavyo tunaweza kuuza ngano mbaya, kununua fukara kwa fedha, na masikini kwa jozi moja ya viatu.”
\p
\v 7 Yahwe ameapa kwa fahari ya Yakobo, “Hakika sitasahau kamwe kazi zao hata moja.”
\q1
\v 8 Je, nchi haitatetemeka kwa ajili ya hayo, na kuomboleza kila mtu akaaye ndani yake? Yote hayo yatainuka kama Mto Naili, nayo itataabika juu na kupwa tena, kama mto wa Misri.
\p
\v 9 “Itakuja siku ambayo -huu ndio usemi wa Bwana Yahwe- kwamba nitafanya jua litue wakati wa mchana, na nitaiweka giza dunia wakati wa mchana.
\q1
\v 10 Nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa maombolezoo. Nitaleta nguo za magunia juu ya viuno vyote, na kila kichwa kitakua na kipara. Nitayafanya kuwa kama maombolezo yamwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.
\q1
\v 11 Tazama, siku zinakuja -asema Bwana Yahwe- wakati nitakapoleta njaa katika nchi, sio njaa ya mkate, wala kiu ya maji, bali ya kuyasikia maneno ya Yahwe.
\q1
\v 12 Nao watatangatanga toka bahari hata bahari; toka upande wa kaskazini hata mashariki; wataenda mbio huko na huko, wakilitafuta neno la Yahwe, lakini hawataliona.
\p
\v 13 Katika siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kutokana na kiu.
\q1
\v 14 Wale waapao kwa dhambi ya Samaria na kusema, “kama aishivyo Mungu wako, Ee Dani, na kama iishivyo njia ya Beeri-Sheba!, wataanguka na hawatainuka tena.”
\c 9
\cl Sura 9
\p
\v 1 Nikamwona Bwana amesimama karibu na madhabahu, akasema, “Vipige vichwa vya nguzo ili kwamba misingi itikisike. Vivunje vipande vipande juu ya vichwa vyao vyote, nami nitawaua wa mwisho wao kwa upanga. Hakuna mmoja wao atakaye kimbiawala atakayeokoka.
\q1
\v 2 Hata kama watachimba kwenye Sheoli, kuna mkono wangu utawachukua. Hata kama watapanda juu kwenda mbinguni, huko nitawaleta chini.
\q1
\v 3 Hata kama watajificha juu ya Karmeli, nitawatafuta huko na kuwachukua. Hata kama watajificha kwenye vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka, na atawauma.
\q1
\v 4 Hata kama wataenda kwenye utumwa, watabanwa na maadui zao mbele yao, nitauagiza upanga huko, na utawaua. Nitaelekeza macho yangu juu yao kwa ubaya sio kwa uzuri.”
\q1
\v 5 Bwana, Mungu wa majeshi, yeye aigusaye nchi nayo ikayeyuka; na wote wakaao humo wanaomboleza; yote yatafurika kama Mto, na kupungua kama mto wa Misri.
\q1
\v 6 Yeye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi yake katika nchi. Yeye ndiye anayeyaita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa dunia, Yahwe ndilo jina lake.
\q1
\v 7 “Je, ninyi si kama wana wa Kushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli? - Hivi ndivyo Yahwe asemavyo. “Je! Sikuwapandisha Israeli kutoka nchi ya misri, Wafilisti kutoka Kaftori, na Washami kutoka Kiri?
\q1
\v 8 Tazama, macho ya Bwana Yahwe yanauelekea ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia, lakini sitaiharibu nyumba ya Yakobo kabisa, -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\q1
\v 9 Maana hakik nitaamuru, na nitaipepeta nyumba ya Israeli kati ya mataifa yote, kama vile nafaka inavyopepetwa katikaungo, walakini punje ndogo haitaanguka chini.
\q1
\v 10 Wenye dhambi wote wa watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, Msiba hautatupata wala kutukabili.
\q1
\v 11 Katika siku hiyo nitaiinua hema ya Daudi, iliyoanguka, na kutengeneza mahali palipobomoka. Nitayainua magofu yake, na kuijenga tena kama katika siku za kale,
\q1
\v 12 ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote walioitwa kwa jina langu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo-afanyaye jambo hili haya.
\p
\v 13 Tazama, siku zinakuja-hivi ndivyo Yahwe asemavyo-ambaye alimaye atamfikilia avunaye na akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu. Milima itadondosha divai tamu, na vilima vyote vitatiririka.
\q1
\v 14 Nami nitawarudisha kutoka utumwani watu wangu Israeli. Wataijenga miji iliyoharibiwa na kukaa ndani yake. Watapanda bustani za mizabibu na kunywa divai yake, nao watatengeneza bustani na kula matunda yake.
\q1
\v 15 Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang'olewa tena kutoka katika nchi niliyowapa,” asema Yahwe Mungu wako.