sw_ulb/29-JOL.usfm

157 lines
10 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id JOL
\ide UTF-8
\h Joeli
\toc1 Joeli
\toc2 Joeli
\toc3 jol
\mt Joeli
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Neno la Bwana lililomjia Yoeli mwana wa Pethueli.
\q1
\v 2 Sikieni haya, ninyi wazee, tegeni masikio, ninyi wenyeji wote wa nchi. Je! Jambo kama hili limetokea katika siku zenu, au hata katika siku za baba zenu?
\q1
\v 3 Waambieni watoto habari hii, na watoto wenu wawaambie watoto wao, na watoto kuwaambia wao kizazi kingine.
\q1
\v 4 Yale yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige wakubwa; yale yaliyosazwa na nzige, panzi wameyala; na yaliyosazwa na panzi yameliwa na madumadu
\q1
\v 5 Amkeni, enyi walevi, lieni! Omboleza, ninyi nyote mnywao divai, kwa sababu divai nzuri imekatwa kutoka kwenu.
\q1
\v 6 Kwa maana taifa limekuja juu ya nchi yangu, lenye nguvu, lisilo na hesabu; Meno yake ni meno ya simba, Na ng'ambo za simba mkali.
\q1
\v 7 Ameharibu mzabibu wangu, ameharibu mtini wangu; Ameivua na kuitupa mbali; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
\q1
\v 8 Omboleza kama bikira aliyevaa magunia kwa kifo cha mumewe mdogo.
\q1
\v 9 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimekatiliwa mbali na nyumba ya Bwana. Makuhani, watumishi wa Bwana, huomboleza.
\q1
\v 10 Shamba limeharibika, na nchi inaomboleza; Kwa maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, na mafuta yamepungua.
\q1
\v 11 Oneni aibu, enyi wakulima, pigeni yowe, enyi watunza mzabibu, kwa ajili ya ngano na shayiri. Kwa sababu mavuno ya shambani yameharibika.
\q1
\v 12 Mzabibu umekauka na mitini umenyauka; miti ya mkomamanga, pia mitende, na miti ya epo - miti yote ya shambani imenyauka. Hakika furaha imekauka kwa kwa wanadamu.
\q1
\v 13 Jifungeni viuno, mkaomboleze, enyi makuhani! Pigeni yowe, enyi watumishi wa madhabahu. Njoni, mlale usiku wote mlale katika magunia, enyi watumishi wa Mungu wangu. Maana sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimezuiliwa nyumbani mwa Mungu wenu.
\q1
\v 14 Takaseni saumu, iteni kusanyiko takatifu. Wakusanyeni wazee na wenyeji wote wa nchi wafike nyumbani kwa Bwana Mungu wenu, mkamlilie Bwana.
\q1
\v 15 Ole kwa siku Kwa maana siku ya Bwana imekaribia. Nayo itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.
\q1
\v 16 Je, chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu, na furaha na kicheko kutoka nyumbani mwa Mungu wetu?
\q1
\v 17 Mbegu zinaoza chini ya udongo wake, ghala zimekuwa ukiwa, na mabanda yamevunjika, kwa maana nafaka imekauka.
\q1
\v 18 Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya Ng'ombe wanateseka kwa sababu hawana malisho. Pia, makundi ya kondoo yanateseka.
\q1
\v 19 Bwana, nakulilia wewe. Kwa maana moto umekula malisho ya jangwani, na moto umeteketeza miti yote ya mashamba.
\q1
\v 20 Hata wanyama wa kondeni wanakulilia, kwa maana mito ya maji imekauka, na moto umeteketeza malisho ya jangwani.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Piga tarumbeta katika Sayuni, na piga kelele juu ya mlima wangu mtakatifu! Wakazi wote wa nchi watetemeke kwa hofu; maana siku ya Bwana inakuja; Hakika iko karibu.
\q1
\v 2 Ni siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza nene. Kama asubuhi inayoenea kwenye milima, jeshi kubwa na la nguvu linakaribia. Hakujawahi kuwako jeshi kama hilo, na hakutakuwa tena, hata baada ya vizazi vingi.
\q1
\v 3 Moto unakula mbele yako, na nyuma yao miali ya moto inawaka. Nayo nchi hiyo ni kama bustani ya Edeni mbele yao, lakini nyuma yao kuna jangwa tupu Hakika hakuna chochote kitakachowaepuka
\q1
\v 4 Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; Na kama farasi wepesi, ndivyo wanavyokimbiaa.
\q1
\v 5 Kwa kelele kama magari ya vita huruka juu ya vilele vya milima, Kama sauti ya mwali wa moto utekekezao mabua makavu, Kama jeshi la nguvu lililo tayari kwa vita.
\q1
\v 6 Mbele yao watu wanahangaika katika uchungu na nyuso zao zimegeuka kua nyeupe kwa hofu.
\q1
\v 7 Wanakimbia kama wapiganaji wenye nguvu; wanapanda kuta kama askari; wanasonga, kila mmoja kwa hatua, na hawavunji safu zao.
\q1
\v 8 Wala hakuna mmoja anayemsukuma mwingine kando; wanasonga, kila mmoja katika safu yake; hujifanyizia njia kwa nguvu kati ya silaha wala hawaachi kuifuata njia yao.
\q1
\v 9 Wanakimbilia jiji, wanakimbia kwenye ukuta, wanapanda ndani ya nyumba, na hupita kupitia madirisha kama wezi.
\q1
\v 10 Nchi hutikisika mbele yao, mbingu hutetemeka, jua na mwezi hutiwa giza, na nyota zinaacha kuangaza.
\q1
\v 11 Bwana huinua sauti yake mbele ya jeshi lake; maana wapiganaji wake ni wengi sana; kwa maana wao ni wenye nguvu, wale wanaofanya amri zake. Kwa maana siku ya Bwana ni kubwa na ya kutisha sana. Nani anayeweza kuiistahimili?
\p
\v 12 “Lakini hata sasa,” asema Bwana, “Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza.”
\q1
\v 13 Basi rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, Mruienina Mungu wenu. Kwa maana ni mwenye neema, amejaa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema; na Yeye hughairi kufanya ubaya.
\q1
\v 14 Nani anajuaye kwamba atageuka na kughairi, na kuacha baraka nyuma yake, sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji kwa Bwana, Mungu wenu?
\q1
\v 15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Tkaseni saumu, iteni kusanyiko takatifu.
\q1
\v 16 Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto na wanyonyao; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, na bibi arusi katika hema yake.
\q1
\v 17 Basi makuhani, watumishi wa Bwana, na waliae kati ya patakatifu na madhabahu; na waseme “uwaachilie watu wako, Ee Bwana, wala usiutoe urithi wako upate aibu, ili mataifa watawale juu yao. Kwa nini waseme kusema kati ya mataifa, “Yuko wapi Mungu wao?” Ndipo Bwana atakuwa na wivu kwa ajili yanchi yake, na kuwahurumia watu wake.
\q1
\v 18 Ndipo Bwana atakuwa na wivu kwa ajili ya nchi yake, na kuwahurumia watu wake.
\p
\v 19 Bwana atajibu na kuwaambia watu wake, Tazamani, nitawaletea nafaka, divai, na mafuta, nanyi mtashimba kwa vitu hivyo; ala sitawafanya kuwa aibu kati ya mataifa.
\q1
\v 20 Lakini jeshi lilotoka kazkazini nitaliondolea mbali nanyi nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa, uso wake ukielekea bahari ya mashariki, na mgongo wake kuelekea bahari ya magharibi; Uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda kwa sababu amefanya mambo ya kuchukiza sana.
\q2
\v 21 Ee nchi, usiogope, shangilieni na kufurahi, kwa kuwa Bwana amefanya mambo makuu.
\q1
\v 22 Msiogope enyi wanyama wa porini, kwa kuwa malisho yajangwani yanachipukana mti unazaa matunda yake, na mMtini na mzabibu hutoa nguvu zake.
\q1
\v 23 Furahini basi, enyi watu wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu. Kwa maana amewapa ninyi mvua ya masika kwa uaminifu, naye atawanyeshea mvu, mvua ya masika, na mvua ya vuli katika mwezi wa kwanza.
\q1
\v 24 Sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai mpya na mafuta.
\q1
\v 25 “Nimi nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, Parare, na madumadu, na tunutu, - jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
\q1
\v 26 Mtakula chakula tele na kushiba, na kulitukuza jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawataaibishwa kamwe.
\q1
\v 27 Nanyi mtajua ya kwamba mimi niko kati ya Israeli, na kwamba mimi ni Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine. Watu wangu hawataaibishwa kamwe.
\q1
\v 28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili, na wana wenu na binti zenu watatabiri. Wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.
\q1
\v 29 Tena juu ya watumishi wangu na wajakazi wangu nitamimina Roho yangu siku zile.
\q1
\v 30 Nami nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani; damu, moto na nguzo za moshi.
\q1
\v 31 Jua litageuzwa kuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla haijaja ile siku ya Bwana iliyo kuu na ya kutisha.
\q1
\v 32 Na itakuwa kwamba kila mtu anayeliitia jina la Bwana ataokolewa. Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na Yerusalemu kutakuwapo wokovu, kama Bwana alivyosema; Miongoni mwa mabaki ambao Bwana atawaita.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Tazama, katika siku hizo na wakati huo, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu,
\q1
\v 2 Nami nitakusanya mataifa yote, na kuwaleta mpaka bonde la Yehoshafati. Nami nitawahukumu huko, kwa sababu ya watu wangu, na urithi wangu Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kwa sababu wamegawanya nchi yangu.
\q1
\v 3 Wamewapigia kura watu wangu, wametoa mtoto wa kiume kama malipo ya kahaba, na kumuuza msichana kwa divai ili wapate kunywa.
\p
\v 4 Hakika, mna nini nami, enyi Tiro, Sidoni na mikoa yote ya Wafilisti? Je! Mtanirudishia malipo? Hata kama mtanilipa, mara moja nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
\v 5 Kwa maana mmechukua fedha yangu na dhahabu yangu, nanyi mkavichukua hazina zangu za thamani na kuzileta katika hekalu zenu.
\v 6 Mmewauza watu wa Yuda na wenyenji wa Yerusalemu kwa Wayunani, ili kuwaondoa mbali na maeneo yao.
\p
\v 7 Tazama, nitawaamsha, watoke mahali ambako mliwauza, na nitawarudishia malipo juu ya vichwa vyenu wenyewe.
\v 8 Nitawauza wana wenu na binti zenu, kwa mkono wa watu wa Yuda. Wao watawauza Sheba, kwa taifa mbali. Kwa maana Bwana amesema.
\q1
\v 9 Tangazeni haya kati ya mataifa, Jitayarisheni wenyewe kwa ajili ya vita, waamsheni mashujaa, waacheni wakaribie, mashujaa wote wa vita wapande juu.
\q1
\v 10 Yafueni majembe yenu kuwa panga na visu vyenu vya kuchongea kuwa mikuki. Basi wadhaifu waseme, Nina nguvu.
\q1
\v 11 Haraka na mje, mataifa yote ya karibu, jikusanyeni pamoja huko. Ee Bwana, washushe mashujaa wako.
\q1
\v 12 Naam, mataifa yajihimize yenyewe kuja hadi bonde la Yehoshafati. Kwa maana nitaketi huko kuhukumu mataifa yote ya jirani.
\q1
\v 13 Wekamundu, kwa maana mavuno yameiva. Njoo, mponde zabibu, kwa ajiri shinikizo limejaa. Mashinikizo yanafurika, kwa sababu uovu wao ni mkubwa sana.
\q1
\v 14 Umati wa watu, makutano katika bonde la uamuzi! Kwa maana siku ya Bwana i karibu katika bonde la hukumu.
\q1
\v 15 Jua na mwezi vitatiwa giza, nyota zitapunguza mwanga wake.
\q1
\v 16 Bwana naye ataunguruma kutoka Sayuni, na atatoa sautiyake toka Yerusalemu. Mbingu na nchi zitatikisika; Bali BWANA atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.
\q1
\v 17 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, ninayekaa katika Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Ndipo Yerusalemu utakuwa mtakatifu, na hakuna mgeni atakayepita tena ndani yake kamwe.
\q1
\v 18 Na itakuwa Katika siku hiyo ya kwamba milima itadondosha divai mpya, vilima vitatiririka maziwa, na vijito vya Yuda vitafurika maji, na chemchemi itatoka katika nyumba ya BWANA na kumwagilia maji bonde la Shitimu.
\q1
\v 19 Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya udhalimu juu ya watu wa Yuda, kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.
\q1
\v 20 Bali Yuda atakaa milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi.
\q1
\v 21 Maana nitawaondolea hatia ya umwagaji wa damu, ambao sikuwaondolea kuwa na hatia; kwa maana Bwana anakaa katika Sayuni.