sw_ulb/22-SNG.usfm

258 lines
17 KiB
Plaintext

\id SNG
\ide UTF-8
\h Wimbo Wa Sulemani
\toc1 Wimbo Wa Sulemani
\toc2 Wimbo Wa Sulemani
\toc3 sng
\mt Wimbo Wa Sulemani
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Wimbo ulio Bora, ambao ni wa Sulemani. Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake
\q1
\v 2 O, laiti angenibusu na mabasu ya mdomo wake, kwa kuwa upendo wake ni bora kuliko mvinyo.
\q1
\v 3 Mafuta yako ya upako yana manukato mazuri; jina lako ni kama marashi yaeleayo, hivyo wanawake wadogo wanakupenda.
\q1
\v 4 Nichukuwe kwako, na tutakimbia. Mwanamke akizungumza mwenyewe Mfalme amenipeleka vyumbani mwake. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake; nina furahi kuhusu wewe; acha ni shereheke upendo wako; ni bora kuliko mvinyo. Ni halisi kwa wanawake wengine kupenda. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
\q1
\v 5 Mimi ni mweusi lakini ni mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, mzuri kama mapazia ya Sulemani.
\q1
\v 6 Usinishangae kwa sababu ni mweusi, kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mama yangu walikuwa na hasira juu yangu; walinifanya mtunzaji wa mashamba ya mizabibu, lakini shamba langu la mizabibu sijalitunza. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake.
\q1
\v 7 Niambie, wewe ambaye moyo wangu wakupenda, wapi unalishia mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye hakangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu
\q1
\v 8 Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji.
\q1
\v 9 Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wa kike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao.
\q1
\v 10 Mashavu yako ni mazuri kwa mapambo, shingo yako na mikufu ya madini.
\q1
\v 11 Nitakufanyia mapambo ya dhahabu yaliochanganywa na fedha. Mwanamke akiongea mwenyewe.
\q1
\v 12 Wakati mfalme akiwa amelala kitandani mwake, marashi yangu yakasambaza harufu.
\q1
\v 13 Mpenzi wangu kwangu ni kama mkebe wa marashi unaolala usiku kati ya maziwa yangu.
\q2
\v 14 Mpenzi wangu kwangu ni kama kifurushi cha maua ya hena katika mashamba ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi wake anazungumza naye.
\q1
\v 15 Sikiliza, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; ona, wewe ni mzuri; macho yako ni kama ya hua. Mwanamke anazungumza na mpenzi wake.
\q1
\v 16 Sikiliza, wewe ni mtanashati, mpenzi wangu, jinsi gani ulivyo mtanashati.
\q1
\v 17 Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Mimi ni ua katika tambarare, nyinyoro katika bonde. Mwanaume akizungumza naye
\q1
\v 2 Kama nyinyoro miongoni mwa mimba, ndivyo wewe, mpenzi wangu, miongoni mwa mabinti wengine wote. Mwanamke akizungumza mwenyewe
\q1
\v 3 Kama mti wa mpera ulivyo miongoni mwa miti ya misituni, ndivyo mpenzi wangu alivyo miongoni mwa wanaume. Nina kaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana, na tunda lake ni tamu kwa ladha yangu.
\q1
\v 4 Amenileta kwenye ukumbi wa maakuli, na bendera yake juu yangu ilikuwa upendo. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake.
\q1
\v 5 Nihuishe kwa keki za mizabibu na kuniburudisha kwa mapera, kwa kuwa nimedhohofika na mapenzi. Mwanamke akizungumza mwenyewe
\q1
\v 6 Mkono wake wa kushuto upo chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
\q1
\v 7 Ninawataka muape, mabinti wa Yerusalemu, kwa swala na paa wa porini, kwamba hamtaamsha au kuchochea mapenzi yetu hadi yatakapoisha yenyewe. Mwanamke akizungumza mwenyewe.
\q1
\v 8 Sauti ya mpenzi wangu hiyo! O, huyu yuwaja, akiruka ruka juu ya milima, akiruka vilimani.
\q1
\v 9 Mpenzi wangu ni kama swala au mtoto mdogo wa paa; angalia, amesimama nyuma ya ukuta wetu, akishangaa kupitia dirishani, akichungulia wavuni.
\q1
\v 10 Mpenzi wangu alizungumza na mimi na kusema, “Amka, mpenzi wangu; Mzuri wangu, twende pamoja nami.
\q1
\v 11 Angalia, baridi imepita; mvua imeisha na kutoweka.
\q1
\v 12 Maua yametokeza juu ya nchi; wakati wa kupunguza matawi na kuimba kwa ndege umekuja, na sauti za hua zimesikika nchini kwetu.
\q1
\v 13 Mti wa tini umepevusha tini zake za kijani, na mizabibu imechanua; yatoa marashi yake. Inuka, mpenzi wangu, mzuri wangu, na uje nami.
\q1
\v 14 Hua wangu, katika miamba ya mawe, katika miamba ya siri ya mipasuko ya milima, acha nione uso wako. Acha nisikie sauti yako, kwa kuwa sauti ni tamu, na uso wako ni mzuri.” Mwanamke akiongea mwenyewe.
\q1
\v 15 Wakamate mbweha kwa ajili yetu, mbweha wadogo wanao haribu mashamba ya mizabibu, kwa kuwa shamba letu la mizabibu limechanua.
\q1
\v 16 Mpenzi wangu ni wangu, na mimi ni wake; anakula penye nyinyoro kwa raha. Mwanamke anaongea na mpenzi wake
\q1
\v 17 Enenda zako, mpenzi wangu, kabla pepo za jioni hazija vuma na vivuli kutoweka. Nenda zako; kuwa kama ayala au mtoto mdogo wa paa katika milima ya mawe mengi.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Usiku katika kitanda changu nilikuwa na shauku ya yeye nimpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.
\q1
\v 2 Nilisema binafsi, “Nitainuka na kwenda kupitia mji, kupitia mitaa na sokoni; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.” Nilimtafuta, lakini sikumpata.
\q1
\v 3 Walinzi walinipata walipokuwa doria katika mji. Nikawauliza, “Mmemuona wa moyo wangu yule nimpendaye?”
\q1
\v 4 Ni baada ya muda mfupi nilipokuwa nimewapita nikampata wa moyo nimpendaye. Nilimshika na sikumuacha hadi nilipomleta nyumbani mwa mama yangu, katika chumba cha yeye aliyenichukua mimba. Mwanamke akiongea na wanawake wengine.
\q1
\v 5 Ninataka muape, mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kwa ayala na paa wa porini, kuwa hamtachochea wala kuwasha mapenzi yetu hadi yatakapoisha yenyewe. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\q1
\v 6 Nini hiyo inayo toka nyikani kama nguzo za moshi, umefukizwa manemane na ubani, pamoja na unga wote wa manukato unaouzwa na wafanya biashara?
\q1
\v 7 Angalia, nikitanda cha Sulemani; mashujaa sitini wamekizunguka, wakuu wa vita wa Israeli
\q1
\v 8 Wao ni wazoefu wa upanga na wanaujuzi wa vita. Kila mwanaume ana upanga wake pembeni yake, akijizatiti na maasi ya usiku.
\q1
\v 9 Mfalme Sulemani akajijengea kiti cha kifalme cha kubebwa na mbao za Lebanoni.
\q1
\v 10 Nguzo zake zilijengwa kwa fedha; nyuma kuliwekwa dhahabu, na kiti kwa kitambaa cha zambarau. Ndani mwake kulipambwa na upendo na mabinti wa wanaume wa Yerusalemu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa Yerusalemu
\q1
\v 11 Nenda nje, mabinti wa wanaume wa Sayuni, na mtazame mfalme Sulemani, akivikwa taji ambalo mamaye alimvika siku ya arusi yake, katika siku ya furaha ya maisha yake.
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 O, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; wewe ni mzuri. Macho yako ni ya hua nyuma ya kilemba chako cha uso. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka Mlima Gileadi.
\q1
\v 2 Meno yako ni kama kondoo walionyolewa, wakitoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja ana pacha, na hamna hata mmoja miongoni mwao aliyefiwa.
\q1
\v 3 Mdomo wako ni kama uzi mwekendu; mdomo wako wapendeza. Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kilemba chako cha uso.
\q1
\v 4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi ukiwa umejengwa kwa mistari ya mawe, na ngao elfu moja ikining'nia juu yake, ngao zote za wanajeshi.
\q1
\v 5 Maziwa yako mawili ni kama swala wawili, mapacha wa ayala, wakila miongoni mwa nyinyoro.
\q1
\v 6 Kabla jioni ifike na vivuli vitoweke, nitaenda kwenye mlima wa manemane na vilima vya ubani.
\q1
\v 7 Wewe ni mzuri kwa kila namna, mpenzi wangu na hakuna lawama ndani yako.
\q1
\v 8 Njoo nami kutoka Lebanoni, bibi harusi wangu. Njoo nami kutoka Lebanoni; njoo kutoka juu ya kilele cha Amana, kutoka juu ya vilele vya Seneri na Herimoni, kutoka shimoni mwa simba, Kutoka mashimo ya milima ya chui.
\q1
\v 9 Umeuiba moyo wangu, dada yangu, bibi harusi wangu; umeuiba moyo wangu, kwa mtazamo wako tu mmoja kwangu, ukiwa na mkufu wako mmoja wa shingo yako.
\q1
\v 10 Jinsi gani upendo wako ulivyo mzuri, dada yangu, bibi arusi wangu! Jinsi gani zaidi upendo wako ulivyo bora kuliko mvinyo, na harufu ya marashi yako kuliko manukato yeyote.
\q1
\v 11 Midomo yako, bibi harusi wangu, yatiririka asali; asali na maziwa viko chini ya ulimi wako; harufu ya mavazi yako ni kama marashi ya Lebanoni.
\q1
\v 12 Dada yangu, bibi harusi wangu ni bustani ilio fungwa, bustani iliyo fungwa, chemchemi iliyowekewa muhuri.
\q1
\v 13 Matawi yako ni kichaka cha miti ya komamanga yenye matunda tofauti, na ya mimea ya hina na nardo,
\q2
\v 14 Nardo na Zafarani, mchai na mdalasini pamoja na aina zote za uvumba, manemane na udi na aina bora za manukato.
\q1
\v 15 Wewe ni bustani ya chemchemi, kisima cha maji safi, mifereji inayoshuka kutoka Lebanoni. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
\q1
\v 16 Amka, upepo wa kaskazini; njoo, upepo wa kusini; vuma katika bustani yangu ili manukato yake yatoe marashi. Mpenzi wangu na aje katika bustani yake na kula matunda ya chaguo lake.
\c 5
\cl Sura 5
\p
\v 1 Nimekuja katika bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; Nimekusanya udi wangu na manukato yangu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; Nimekunywa mvinyo wangu pamoja na maziwa yangu. Marafiki wanazungumza na wapenzi Kuleni, marafiki; kunyweni na mlewe na mapenzi. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\q1
\v 2 Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu ulikuwa macho katika ndoto. Sauti ya mpenzi wangu yabisha na kusema, “Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, hua wangu, usiye na dosari, kwa kuwa kichwa changu kimelowa na matone, nywele zangu kwa unyevu wa usiku.”
\q1
\v 3 “Nimevua joho langu; je, azima nilivae tena? Nimeosha miguu yangu; je, lazima niichafue tena?”
\q1
\v 4 Mpenzi wangu kwa mkono wake kupitia kwenye kitasa cha mlango akanigusa, na moyo wangu ukawa umewaka kwa ajili yake.
\q1
\v 5 Nimeamka kumfungulia mlango mpenzi wangu; mikono yangu ikawa yamiminika na manemane, vidole vyangu na unyevu wa manemane, katika komeo la mlango.
\q1
\v 6 Nimemfungulia mlango mpenzi wangu, lakini mpenzi wangu alikuwa aligeuka na kuondoka. Moyo wangu ukadidimia aliponena; nikakosa tumaini. Nikamtafuta, lakini sikumpata; nikamuita, lakini hakunijibu.
\q1
\v 7 Walinzi waliokuwa wakizunguka mjini walinipata mimi; walinipiga chini na kunijeruhi; askari katika ukuta walichukua nguo yangu ya juu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa mji
\q1
\v 8 Ninawataka muape, mabinti wa Yerusalemu, kwamba mkimuona mpenzi wangu, ni kitu gani mtamjulisha? Mwambie nimenyong'onyea sababu ya upendo wangu kwake. Wanawake wa mji wakizungumza na mwanamke mdogo
\q1
\v 9 Mpenzi wako ana ubora gani kuliko mwanaume mwengine, wewe uliye mzuri miongoni mwa wanawake? Kwanini mpenzi wako bora kuliko mpenzi mwengine, hadi utuulize tuweke nadhiri kama hii? Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa mji
\q1
\v 10 Mpenzi wangu amenawiri na anang'aa, Kati ya wanaume elfu kumi.
\q1
\v 11 Kichwa chake ni dhahabu safi; nywele zake ni laini na nyeusi kama kunguru.
\q1
\v 12 Macho yake ni kama ya hua pembezoni mwa vijito vya maji, yameoshwa na maziwa, yameundwa kama mikufu.
\q1
\v 13 Mashavu yake ni kama vitanda vya manukato, vinavyotoa harufu ya marashi. Midomo yake ni nyinyoro, inayotiririka manemane.
\q1
\v 14 Mikono yake ni ya mianzi ya dhahabu iliyo zungushiwa mikufu; tumbo lake ni pembe lililofunikwa yakuti ya samawati.
\q1
\v 15 Miguu yake ni nguzo za marimari, iliyowekwa juu ya dhahabu safi; muonekano wake ni kama Lebanoni, mizuri kama mierezi.
\q1
\v 16 Mdomo wake ni mtamu kuliko; ni mzuri sana wa kupendeza. Huyu ni mpenzi wangu, na huyu ni rafiki yangu, mabinti wa Yerusalemu.
\c 6
\cl Sura 6
\p
\v 1 Mpenzi wako ameenda wapi, aliye mzuri miongoni mwa wanawake? Kwa uelekeo gani mpenzi wako ameenda, ili tumtafute nawe? Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\q1
\v 2 Mpenzi wangu ameenda katika bustani yake, kwenye vitanda vya manukato, kwenda kula katika bustani na kukusanya nyinyoro.
\q1
\v 3 Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; hula miongoni mwa nyinyoro kwa raha. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
\q1
\v 4 Wewe ni mzuri kama Tirza, mpenzi wangu, wapendeza kama Yerusalemu, wahamasisha kwa utusho kama jeshi lenye bendera mbele.
\q1
\v 5 Geuza macho yako mbali na mimi, kwa kuwa yananizidi ukali. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka miteremko ya Mlima Gileadi.
\q1
\v 6 Meno yako ni kama kundi la kondoo likishuka kutoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja anapacha, na hamna ata mmoja kati yao aliyefiwa.
\q1
\v 7 Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kilemba chako cha uso. Mpenzi wa mwanamke akizungumza peke yake
\q1
\v 8 Kuna malikia sitini, masuria themanini, na wanawake wachanga bila idadi.
\q1
\v 9 Hua wangu, wangu asiye na dosari, ni yeye pekee; ni binti pekee wa mama yake; ndiye kipenzi cha mwanamke aliye mzaa. Mabinti wa wenzengu wamemuona na kumuita mbarikiwa; wanawake-malikia na masuria walimuona pia, na wakamsifia: Kile walicho sema wanawake-malikia na masuria
\q1
\v 10 “Ni nani huyo anaye jitokeza kama kukicha, mzuri kama mwezi, anayeng'aa kama jua, uamasisha-kwa utisho kama bendera ya jeshi?” Mpenzi wa mwanamke akizungumza mwenyewe
\q1
\v 11 Nilienda kwenye kichaka cha miti ya milozi kuona mimea midogo ikikua bondeni, kuona kama mizabibu ilikuwa imechipua, na kama mikomamanga imestawi.
\q1
\v 12 Sikujua ni lini nafsi yangu ilinikalisha juu ya gari la farasi la mfalme wangu waungwana. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye.
\q1
\v 13 Geuka nyuma, geuka nyuma, wewe mwanamke mshunami; geuka nyuma, geuka nyuma ili niweze kukutizama kwa mshangao! Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake Kwanini wanishangaa, mwanamke mkamilifu, kana kwamba nina cheza katikati ya mistari miwili ya wachezaji?
\c 7
\cl Sura 7
\p
\v 1 Jinsi gani miguu yako ilivyo yaonekana mizuri kwenye viatu, binti wa mfalme! Mapaja yako ni kama mikufu, kama kazi ya mjenzi.
\q1
\v 2 Kitovu chako ni kama duara la bakuli; kamwe kisikose mchanganyiko wa mvinyo. Tumbo lako ni kama ngano iliyoumuka na kuzungushiwa nyinyoro.
\q1
\v 3 Maziwa yako mawili ni kama watoto wawili wa ayala, mapacha wa ayala.
\q1
\v 4 Shingo lako ni kama mnara wa pembe; macho yako ni kama maziwa ya Heshiboni kwenye lango la Bathi Rabimu. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni ambao watazama kuelekea Damasko.
\q1
\v 5 Kichwa chako ni kama Karmeli; nywele kichwani mwako ni za zambarau nyeusi. Mfalme amestaajabishwa na vifundo vyake vya nywele.
\q1
\v 6 Jinsi gani ulivyo mzuri na wakupendeza, mpenzi, na mazuri yako.
\q1
\v 7 Urefu wako ni wa kama mti wa mtende, na maziwa yako kama vifungu vya matunda.
\q1
\v 8 Nilisema, “Ninataka kuupanda huo mti wa mtende; nitashika matawi yake.” Maziwa yako nayawe kama vifungu vya mizabibu, na harufu ya pua yako iwe kama mapera.
\q2
\v 9 Mdomo wako na uwe kama mvinyo bora, ukishuka taratibu kwa mpenzi wangu, ukiteleza kwenye midomo yetu na meno. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\q1
\v 10 Mimi ni wa mpenzi wangu, na ananitamani.
\q1
\v 11 Njoo, mpenzi wangu, twende nje ya mji; tulale usiku kwenye vijiji.
\q1
\v 12 Tuamke mapema twende kwenye mashamba ya mizabibu; tuone kama mizabibu imeweka machipukizi, kama maua yake yamechanua, na kama mikomamanga imetoa mau. Pale nitakupa penzi langu.
\q1
\v 13 Mitunguja ya toa harufu yake; katika mlango wa tunapoishi kuna kila aina ya matunda, mpya na ya kale, niliyokuhifadhia, mpenzi wangu.
\c 8
\cl Sura 8
\p
\v 1 Ninatamani ungekua kama kaka yangu, aliyenyonya ziwa la mama yangu. Ila kila nilipokutana nawe nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau.
\q1
\v 2 Ningekuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu, yeye aliyenifundisha. Ningekupa mvinyo uliochachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\q1
\v 3 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akiongea na wanawake wengine
\q1
\v 4 Ninataka muape; mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamsha au kuchochea mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Wanawake wa Yerusalemu wakizungumza.
\q1
\v 5 Ni nani huyu ambaye anakuja kutoka nyikani, akimuegemea mpenzi wake? Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake nimekuamsha chini ya mti wa mpera; pale mama yako alichukua mimba; pale alikuzaa, alijifungua wewe.
\q1
\v 6 Niweke kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote.
\q1
\v 7 Maji yaliyozuka hayawezi kuzimisha upendo, wala mafuriko hayawezi kuuondoa. Mwanaume akitoa mali zake zote kwa ajili ya upendo, ukarimu wake utadharauliwa. Kaka zake mwanamke mdogo wakizungumza wenyewe
\q1
\v 8 Tuna dada mdogo, na matiti yake bado hayajakua. Tutamfanyia nini dada yetu siku hatakayoahidiwa kuolewa?
\q1
\v 9 Kama yeye ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha. Kama yeye ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
\q1
\v 10 Nilikuwa ukuta, lakini matiti yangu sasa ni kama nguzo imara; hivyo nimekomaa machoni pake mleta amani. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\q1
\v 11 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali Hamoni. Aliwakodishia wao ambao wangelitunza. Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake.
\q1
\v 12 Shamba langu la mzabibu ni langu hasa, li mbele yangu; shekeli elfu moja ni za kwako, Sulemani mpenzi, na shekeli mia mbili ni za wale wanaotunza matunda yake. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye.
\q1
\v 13 Wewe unayeishi katika bustani, marafiki zangu wanasikiliza sauti yako; acha na mimi niwezekuisikia pia. Mwanamke mdogo akiongea na mpenzi wake
\q1
\v 14 Harakisha, mpenzi wangu, na uwe kama paa au mtoto wa paa kwenye milima ya manukato.