sw_ulb/14-2CH.usfm

1245 lines
142 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id 2CH
\ide UTF-8
\h 2 Mambo Ya Nyakati
\toc1 2 Mambo Ya Nyakati
\toc2 2 Mambo Ya Nyakati
\toc3 2ch
\mt 2 Mambo Ya Nyakati
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Sulemani mwana wa Daudi, aliimarishwa katika utawala wake, na Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye na alimpa nguvu nyingi sana.
\p
\v 2 Sulemani akasema kwa Israleli wote, na maakida wa maelfu na wa mamia, na kwa waamuzi, na kwa kila mfalme kiongozi katika Israeli yote, wakuu wa kaya.
\v 3 Hivyo Sulemani na kusanyiko lote wakaenda pamoja naye sehemu ya juu iliyokuwa Gibeoni, maana ndipo palikuwepo hema ya kukutania ya Mungu, ambayo Musa mtumishi wa Yahwe, alikuwa ameitengeneza jangwani.
\v 4 Lakini Daudi alikuwa ameleta pale sanduku la Mungu kutoka Kiriath yeriam hadi sehemu ambayo alikuwa ametayarisha, maana alikuwa ameliandalia hema huko Yerusalemu.
\v 5 Zaidi ya hayo, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli mwana wa uri mwana wa Huri ilikuwepo huko kabla ya mbele ya madhabahu ya Yahwe; Sulemani na kusanyiko wakaenda ilikokuwa.
\v 6 Sulemani akaenda huko kwenye madhabahu ya shaba mbele za Yahwe, ambayo ilikuwepo mahali pa hema ya kukutania, na akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
\p
\v 7 Mungu akamtokea Sulemani usiku huo na akasema kwake, “Omba! Nikupe nini?”
\p
\v 8 Sulemani akasema kwa Mungu, “Umeonyesha agano la uaminifu mkuu kwa Daudi baba yangu, na umenifanya mfalme katika nafasi yaye.
\v 9 Sasa, Yahwe Mungu, ahadi yako kwa Daudi baba yangu itimie, maana umenifanya mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya dunia.
\v 10 Sasa nipe hekima na maarifa, ili niweze kuwaongoza watu hawa, maana ni nani anayeweza kuwaamua watu wako, ambao ni wengi sana kwa idadi?”
\p
\v 11 Mungu akasema kwa Sulemani, “Kwa kuwa hili lilikuwa kwenye moyo wako, na kwa kuwa hujaomba mali, utajiri, au heshima, wala maisha ya wale wanaokuchukia, wala maisha marefu kwa jili yako binafsi, lakini umeomba hekima na maarifa kwa ajili yako, ili uwatawale watu wangu, ambao juu yao nimekufanya mfalme, na hivi ndivyo nitafanya.
\v 12 Sasa nitakupa hekima na maarifa, pia nitakupa mali na utajiri, na heshima, kuliko wafalme wote waliokuwepo kabla yako walivyokuwa, na baada yako hakuna yeyote atakayekuwa navyo.”
\v 13 Kwa hiyo Sulemani akaenda Yerusalemu kutoka sehemu ya juu iliyokuwepo Gibeoni, kutoka mbele ya hema ya kukutania; akatawala juu ya Israeli.
\p
\v 14 Sulemani akakusanya magari na wanaume waendesha farasi, naye alikuwa na magari 1,400 na waendesha farasi kumi na mbili elfu ambao aliwaweka katika miji ya magari, pamoja naye, mfalme katika Yerusalemu.
\v 15 Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini.
\v 16 Sulemani katika uagizaji wa farasi kutoka Misiri, wafanya biashara wake walinunua farasi kutoka Misiri kwa bei stahiki.
\v 17 Waliagiza gari kutoka Misiri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150. Pia walinunua kutoka kwa wafalme wa Wahiti na wafalme wa Washamu.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Sasa Sulemani akaamuru kulijenga nyumba kwa jina la Yahwe na nyumba kwa ajili ya ikulu ya ufalme wake.
\v 2 Sulemeni akateua wanaume elfu sabini wabebe mizigo, na wanaume elfu themanini wa kukata mbao katika mlima, na wanaume 3,600 kwa ajili ya kusimamia.
\p
\v 3 Sulemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, ukisema, “Kama ulivyofanya na Daudi baba yangu, ulivyomtumia magogo ya mierezi ili ajenge nyumba ya kuishi, fanya hivyo hivyo na mimi.
\pi
\v 4 Tazama, niko karibu kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe Mungu wangu, kuiweka wakifu kwake, kwa ajili ya kumtolea sadaka za kuteketezwa zenye viungo vitamu mbele zake, kwa ajili ya mkate wa uwepo, na kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa asubuhi na jioni, katika siku za Sabato na za mwezi mpya, na katika sikukuu zilizoteuliwa kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu. Hii itakuwa milele, kwa Israeli.
\v 5 Nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa sana, maana Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.
\v 6 Lakini ni nani anayeweza kumjengea Mungu nyumba, kama dunia yote na hata mbingu yenyewe haviwezi kumtosha? Mimi ni nani hata nimjengee nyumba, isipokuwa kufukiza sadaka mbele zake?
\pi
\v 7 Kwa hiyo nitumie mtu mwenye ujuzi wa kazi katika kazi ya dhahabu, fedha, shaba, na chuma, na ya dhambarau, na nyekundu, na sufu ya samawati, mtu anayejua kutengeza aina zote za mapambo ya mbao. Atakuwa na watu wenye ustadi waliopamoja nami katika Yuda na Yerusalemu, ambao Daudi baba yangu aliwaweka.
\pi
\v 8 Nitumieni pia mierezi, miberoshi, na miti ya msandali kutoka Lebanoni, maana najua ya kuwa watumishi wako wanajua jinsi ya kukata mbao katika Lebanoni. Angalia, watumishi wangu watakuwa na watumishi wako,
\v 9 ili kwamba watayarishe mbao nyingi kwa ajili yangu, maana nyumba ninayotaka kuijenga itakuwa kubwa na ya ajabu.
\v 10 Angalia, nitawapa watumishi wako, watu watakaozikata mbao, kori ishirini elfu za ngano ya aridhini, kori ishirini elfu za shayiri, bathi ishirini elfu za mvinyo, na bathi ishirini elfu za mafuta.” \f + \ft Maandishi ya kale yanasema: “kori ishirini elfu za ngano kama chakula.” \f*
\p
\v 11 Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akajibu kwa maandishi, ambayo alimtumia Sulemani: “Kwa kuwa Yahwe anawapenda watu wake, amekufanya kuwa mfalme juu yao.”
\v 12 Zaidi ya hayo, Hiramu akasema, “Abarikiwe Yahwe, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia, amempa Daudi mwana mwenye hekima, mwenye karama ya busara na uelewa, ambaye atajenga nyumba kwa aajili ya Yahwe, na nyumba kwa ajili ya ufalme wake.
\v 13 Sasa nimemtuma mtu mwenye ujuzi, mwenye karama ya uelewa, Hiramu, mtaalamu wangu.
\v 14 Ni mwana wa mwanamke wa binti za Dani. Baba yake alikuwa mtu kutoka Tiro. Ana ujuzi katika kazi za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe, na katika mbao, na katika dhambarau, samawati, na sufu yenkundu, na kitani safi. Pia ana ujuzi katika kutengeneza michoro ya aina yoyote na katika kubuni kitu chochote. Apatiwe nafasi miongoni mwa watumishi wako wenye ujuzi, na pamoja na wale wa bwana wangu, Daudi, baba yako.
\pi
\v 15 Sasa, ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, ambayo bwana wangu alisema, na apeleke sasa vitu hivi kwa watumishi wake.
\v 16 Tutakata mbao kutoka Lebanoni, mbao nyingi kadri unavyohitaji. Tutazileta kwako kama mitumbwi kupitia bahari kwenda Yafa, na utazibeba hadi Yerusalemu.”
\p
\v 17 Sulemani akawahesabu watu wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli, kwa kutumia njia ya Daudi, baba yake, aliyoitumia kuwahesabu. Waliwakuta kuwa 153,600.
\v 18 Miongoni mwao aliwateua sabini elfu ili wabebe mizigo, themanini elfu kuwa wakataji wa mbao katika milima, na 3,600 kuwa wasimamizi wa kuwasimamia watu wafanye kazi.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Kisha Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, ambako Yahwe alimtokea Daudi baba yake. Aliandaa sehemu ambayo Daudi aliikusudia, katika sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi.
\v 2 Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili, katika mwaka wa nne wa utawala wake.
\p
\v 3 Sasa hivi ndinyo vipimo vya ule msingi ambao Sulemani alijenga kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Akitumia mtindo wa vipimo vya zamani, urefu ulikuwa mikono sitini, na upana ulikuwa mikono ishirini.
\v 4 Urefu wa ukumbi mbele ya nyumba ulikuwa mikono ishirini, ukilingana na upana wa nyumba, urefu wake kwenda juu pia ulikuwa mikono ishirini, na Sulemani akaifunika sehemu ya ndani kwa dhahabu halisi.
\p
\v 5 Akalitengeneza paa la ukumbi mkuu kwa miti ya miberoshi, ambayo aliifunika kwa dhahabu halisi, na ambayo aliifunika kwa miti ya mitende na minyororo.
\v 6 Akaipamba nyumba kwa vito vya thamani; dhahabu ilikuwa dhahabu kutoka Parvaimu.
\p
\v 7 Pia akazifunika boriti zake, vizingiti, kuta, na milango kwa dhahabu; akachonga makerubi juu ya kuta zake.
\v 8 Akaijenga sehemu ya patakatifu pa patakatifu. Urefu wake ulilingana na upana wa nyumba, mikono ishirini, na upana wake pia ulikuwa mikono ishirini. Aliifunika kwa dhahabu halisi, thamani yake ilikuwa talanta mia sita.
\v 9 Uzito wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Alizifunika sehemu za juu kwa dhahabu.
\p
\v 10 Akachonga makerubi wawili kwa ajili ya sehemu zapatakatifu pa patakatifu, wahunzi wakayafunika kwa dhahabu. \f + \ft Maandishi ya kale yanasema: makerubi wawili waliochongwa kwenye mbao. \f*
\v 11 Mabawa ya makerubi yalikuwa na urefu wa mikono ishirini yote kwa pamoja; bawa la kerubi mmoja lilikuwa na urefu wa mikono mitano, lilifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa jingine lilikuwa na urefu wa mikono mitano pia.
\v 12 Bawa la kerubi mwingine lilikuwa mikono mitano, likifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa lake jingine lilikuwa mikono mitano pia, likigusana na bawa la kerubi wa kwanza.
\p
\v 13 Mabawa ya makerubi hawa yalienea jumla ya mikono ishirini. Makerubi yalisimama kwa miguu yake, na nyuso zao zikiuelekea ukumbi mkuu.
\p
\v 14 Akatengeneza pazia la samawati, dhambarau, na sufu nyekundu, na kitani safi, na akachora makerubi juu yake.
\v 15 SulemaniPia akatengeneza nguzo mbili, kila moja ikiwa na urefu wa mikono thelathini na tano kwenda juu, kwa maana mbele ya nyumba; taji ambazo zilikuwa juu ya nguzo zilikuwa na urefu wa mikono mitano kwenda juu.
\v 16 Akatengeneza minyororo kwa ajili ya nguzo na akaiweka juu yake, pia akatengeneza makomamanga mia moja na akayaunganisha kwenye minyororo.
\v 17 Akazisimamisha nguzo mbele ya hekalu, mkono wa kulia, na nyingine mkono wa kushoto; akaiita nguzo ya kulia Yakini, na nguzo ya kushoto akaiita Boazi.
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 Vilevile akatengeneza madhabahu ya shaba; urefu wake ulikuwa mikono ishirini, na upana wake ulikuwa mikono ishirini.
\v 2 Pia akatengeneza bahari ya mduara ya chuma cha kuyeyushwa, mikono kumi kutoka ukingo hadi ukingo. Urefu wake kwenda juu ulikuwa mikono mitano, na bahari ilikuwa na mzunguko wa mikono thelatinini.
\v 3 Chini ya kingo kuzunguka bahari kulikuwapo ng'ombe dume, kumi kila mkono,
\p
\v 4 Bahari ilisimama juu ya ng'ombe wa kulima kumi na wawili, watatu wakiangalia kaskazini, watatu wakiangalia magharibi, na watatu wakiangalia kusini, na watatu wakiangalia mashariki. Bahari iliwekwa juu yao, na robo ya sehemu zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
\v 5 Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi. Bahari ilikuwa na mabafu elfu tatu ya maji.
\p
\v 6 Pia akatengeneza birika kumi kwa ajili ya kuoshea vitu; tano akaziweka mkono wa kulia, na tano akaziweka kushoto; vifaa vilivyotumika katika kufanyia sadaka za kuteketezwa zilipaswa kuoshwa ndani ya hizo birika. Bahari, vilevile ilikuwa kwa ajili ya makuhan kuoga humo.
\p
\v 7 Akatengeza vinara vya taa kumi vya dhahabu ambavyo vilitengenezwa kutokana na maelekezo ya jinsi vilivyopaswa kuwa; akaviweka hekaluni, vitanao mkno wa kulia, na vitano mkono wa kushoto.
\p
\v 8 Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Akatengeneza birika mia moja za dhahabu.
\p
\v 9 Zaidi ya hayo akatengeneza mahakama ya makuhani na mahakama kuu, na milangu kwa ajili ya mahakama, akaifunika milango yake kwa shaba.
\v 10 Akaiweka bahari upande wa kulia wa nyumba, masharika, ikielekea upande wa kusini.
\p
\v 11 Huramu akayatengeza masufuria, majembe, na mabakuli ya kunyunyizia. Hivyo Huramu akamaliza kazi aliyofanya kwa ajili ya mfalme Sulemani katika nyumba ya Mungu:
\v 12 zile nguzo mbili, taji mfano wa upinde zilizo kuwa juu ya zile nguzo mbili, na nyavu mbili za mapambo zilizofunika zile taji mbili mfano wa upinde zilizokuwa juu ya zile nguzo.
\q
\v 13 Alikuwa ametengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu za mapambo: safu mbili za makomamanga kwa kila wavu ili kufunika vimbe mbili zilizo kuwa juu ya nguzo.
\q
\v 14 Pia akavitengeneza vitako na mabirika juu ya kitako,
\q
\v 15 bahari moja na wale ng'ombe kumi na wawili chini yake,
\q
\v 16 pia masufuria, majembe, nyuma za nyama, na vyombo vingine vyote. Huramu mtaalamu akavifanya kwa ajili ya Mfalme Sulemani, kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vya shaba iliyong'arishwa.
\v 17 Mfalme alikuwa amevisubu katika uwanda wa Yordani, katika udongo wa mfinyanzi kati kati ya Sukothi na Sereda.
\v 18 Hivyo ndivyo Sulemani alivyovitengeneza vyombo vyote kwa wingi; kwa kweli, uzito wa shaba haukuweza kujulikana.
\p
\v 19 Sulemani akazitengeza samani zote ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Mungu, pia madhabahu ya dhahabu, na meza ambazo juu yake mkate wa uwepo ulipaswa kuwekwa;
\q
\v 20 vinara pamoja na taa zake, ambazo zilitengezwa ili kumulika mbele ya chumba cha ndani—hivi vilitengenezwa kwa dhahabu halisi;
\q
\v 21 na maua, taa, na makoleo, ya dhahabu, dhahabu safi.
\q
\v 22 Pia mikasi ya taa, na mabakuli, vijiko, na vikaango vya sadaka za kuteketezwa vyote vilitengenezwa kwa dhahabu safi. Kuhusu mlango wa kuingilia kwenye nyumba, milango yake ya ndani kwenye patakatifu pa patakatifu na milango ya nyumba, ambayo ni, ya hekalu, ilitengenezwa kwa dhahabu.
\c 5
\cl Sura 5
\p
\v 1 Wakati ilipomalizika kazi aliyofanya Sulemani kwa ajili ya Yahwe, Sulemani akapeleka vitu ndani, ambavyo Daudi, baba yake, aliviweka wakfu kwa kusudi hilo, pamoja na zile fedha, dhahabu, na vyombo vyote akavileta ndani ya hazina ya nyumba ya Mungu.
\p
\v 2 Kisha Sulemani akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wa makabila yote, na viongozi wa familia za watu wa Israeli, katika Yerusalemu, ili walilete sanduku la agano la Yahwe kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni.
\v 3 Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika mbele za mfalme katika sikukuu, ambayo ilikuwa katika mwezi wa saba.
\p
\v 4 Wazee wote wa Israeli wakaja, na Walawiwakalichukua sanduku.
\v 5 Wakalileta sanduku, hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote ambavyo vilikuwa ndani ya hema. Makuhani waliokuwa wa kabila la Lawi wakavileta vitu hivyo.
\v 6 Mfalme Sulemani na kusanyiko lote la Israeli wakaja pamoja, mbele ya sanduku, wakitoa sadaka za kondoo na ng'ombe ambao hawakuweza kuhesabika.
\p
\v 7 Makuhani wakalileta sanduku la angano laYahwe ndani mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, kwenye patakatifu pa patakatifu, chini ya mabawa ya makerubi.
\v 8 Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, na walilifunika sanduku na miti yake ya kulibebea.
\v 9 Miti ilikuwa mirefu sana kwamba ncha zake zilionekana kutoka ile sehemu takatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuweza kuonekana kutoka nje. Zipo hapo hadi leo.
\v 10 Hapakuwa na kitu katika sanduku isipokuwa zile meza mbili ambazo Musa aliziweka humo huko Horebu, wakati Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka nje ya Misri.
\p
\v 11 Ilikuwa makuhani walipotoka nje ya sehemu takatifu. Makuhani wote waliokuwepo wakajiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe, bila kujiamuru wenyewe kulingana na sehemu zao.
\v 12 Pia makuhani waliokuwa waimbaji, wote kwa ujumla wao, pamoja na Asafu, Hemani, Yeduthuni, na wana wao na ndugu zao, wakiwa wamevalia kitani safi na wakipiga matoazi, vinanda, na vinubi, wakasimama upande wa Mashariki wa mwisho wa madhabahu. Pamoja nao palikuwa na makuhani 120 wakipuliza tarumbeta.
\v 13 Ikawa kwamba wapuruza tarumbeta na waimbaji wakafanya mziki pamoja, wakifanya sauti moja isikike kwa ajili ya kumsifu na kumshukuru Yahwe. Walipaza sauti zao kwa tarumbeta, toazi na vyombo vingine, na wakamsifu Yahwe. Wakaimba, “Kwa maana Yeye ni mwema, kwa kuwa uaminifu wa agano lake wadumu milele.” Kisha nyumba, ile nyumba ya Yahwe, ikajawa na wingu.
\v 14 Makuhani hawakuweza kusimama ili wahudumu kwa sababu ya lile wingu, kwa maana utukufu wa Yahwe uliijaza nyumba yake.
\c 6
\cl Sura 6
\p
\v 1 Kisha Sulemani akasema, “Yahwe alisema kwamba ataishi katika giza nene,
\v 2 lakini nimekujengea makao makuu, sehemu kwa ajili yako ya kuishi milele.”
\p
\v 3 Kisha mfalme akageuka nyuma na kuwabariki kusanyiko lote la Israeli, wakati kusanyiko lote la Israeli walikuwa wamesimama
\v 4 Akasema, “Yahwe, Mungu wa Israeli, usifiwe, uliyesema na Daudi baba yangu, na ametimiza kwa mikono yake mwenyewe, akisema.
\pi
\v 5 Tangu siku nilipowaleta watu wanagu nje ya nchi ya Misiri, sikuchagua mji wowote nje ya makabila yote ya Israeli ambamo nyumba ingejengwa, ili jina langu liwe humo. Wala sikuchagua mtu yeyote kuwamfalme juu ya watu wangu Israeli.
\v 6 Aidha, nimechagua Yeruselemu, ili kwamba jina langu liwe humo, na nimemchagua Daudi kuwa juu ya watu wanangu Israeli.
\pi
\v 7 Sasa ilikuwa ndani ya moyo wa Daudi baba yangu, kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 8 Lakini Yahwe alisema kwa Daudi Baba yangu. Kwamba ilikuwa ndani ya moyo wako kujenga nyumba kwa ajili ya jina langu, ulifanya vizuri kwa hili kuliweka moyoni mwako.
\v 9 Aidha, hutaijenga ile nyumba, badala yake, mwanao, mmoja atakayetoka kwenye viuno vyako, ataijenga nyumba kwa ajili ya jina langu.
\pi
\v 10 Yahwe ameyatimiza maneno aliyokuwa amesema, kwa maana nimeiinua sehemu ya Daudi baba yangu, na nitakaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, kama alivyoahidi Yahwe. Nimeijenga nyumba kwa ajii ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 11 Nimeliweka humo sanduku, ambamo kuna agano la Yahwe, alilofanya na watu wa Israeli.”
\p
\v 12 Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Yahwe mbele za kusanyiko lote la Israeli, na akanyosha mikono yake.
\v 13 Kwa maana alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, lenye urefu wa mikono mitano, upana wa mikono mitano, urefu wake kwenda juu mikono mitatu. Alikuwa ameliweka katikati ya uwanja. Akasimama juu yake na kupiga magoti mbele ya kusanyiko la Israeli, kisha akanyosha mikono yake kuzielekea mbingu.
\v 14 Akasema, “Yahwe, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe katika mbingu, au juu ya dunia, ambaye anatunza agano na upendo imara na watumishi wako ambao hutembea mbele zako kwa moyo wao wote;
\pi
\v 15 wewe uliyemtimizia Daudi baba yangu, uliyokuwa umemwahidi. Ndiyo, ulisema kwa kinywa chako na umetimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.
\pi
\v 16 Sasa, Yahwe, Mungu wa Israeli, tunza ahadi uliyoahidi kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, uliposema, Hautashindwa kupata mtu mbele yangu wa kukaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, ikiwa tu uzao wako ni waangalifu kutembea katika sheria zangu, kama wewe ulivyotembea mbele zangu.
\v 17 Sasa, Mungu wa Israeli, ninaomba kwamba ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi itakuwa kweli.
\pi
\v 18 Lakini kweli Mungu ataishi na wanadamu juu ya dunia? Angalia, dunia yote na mbingu yenyewe haviwezi kukubeba -sembuse na hekalu hili nililojenga!
\v 19 Nakusihi yaheshimu maombi haya ya mtumishi wako na ombi lake. Yahwe Mungu wangu; sikia kilio na maombi ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako.
\v 20 Fumbua macho yako kuelekea hekalu hili usiku na mchana, sehemu ambayo uliahidi kuliweka jina lako. Nakuomba usikie maombi atakayoomba mtumishi wako kuelekea sehemu hii.
\v 21 Hivyo sikia maombi ya mtumishi na watu wako Israeli tunapoomba kuelekea sehemu hii. Ndiyo, sikia kutoka mahali unapoishi, kutoka mbinguni; na unaposikia, samehe.
\pi
\v 22 Kama mtu atamtenda dhambi jirani yake na ikampasa kuapa kiapo, na ikiwa atakuja na kuapa kiapo mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii,
\v 23 basi sikia kutoka mbinguni kutenda. Ukawahukumu watumishi wako, ukamlipizie mwovu, ili kuyaleta matendo yake juu ya kichwa chake. Ukamtangaze mwenye haki kuwa hana hatia, ili kumlipa thawabu kwa ajili ya uaminifu wake.
\pi
\v 24 Watu wako watakaposhindwa na adui kwa sababu wamekutenda dhambi, kama watageuka nyuma kwako, wakilikiri jina lako, wakisali na kuomba msamaha mbele zako hekaluni—
\v 25 basi tafadhali sikia kutoka mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Israeli; uwarudishe katika nchi uliyoitoa kwa ajili yao na baba zao.
\pi
\v 26 Wakati mbingu zimefungwa na hakuna mvua kwa sababu watu wamekutenda dhambi—ikiwa wataomba kuelekea sehemu hii, wakilikiri jina lako, na kuziacha dhambi zao utakapokuwa umewaadhibu—
\v 27 basi sikia kutoka mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na watu wako Israeli, utakapowaelekeza kwenye njia njema iwapasayo kutembea. Tuma mvua juu ya nchi yako, ambayo umewapa watu wako kama urithi.
\pi
\v 28 Kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna ugonjwa, tauni au ukungu, nzige au viwavijeshi, au kama adui wake wameyavamia malango ya mji katika nchi yao, au kwamba kuna pigo lolote au ugonjwa—
\v 29 na ikiwa sala na maombi yamefanywa na mtu au watu wako wote Israeli—kila mmoja akilijua pigo na huzuni katika moyo wake akinyosha mikono yake kuelekea hekalu hili.
\v 30 Basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi; samehe, na umlipe kila mtu kwa njia zake zote; unaujua moyo wake, kwa sababu wewe pekee unaijua mioyo ya wanadamu.
\v 31 Fanya hivyo ili kwamba wakuogope wewe, ili waweze kutembea katika njia zako siku zote ambazo wataishi katika nchi uliyowapa baba zetu.
\pi
\v 32 Kwa mgeni ambaye siyo sehemu ya watu wako Israeli, lakini ambaye- kwa sababu ya ukuu wa jina lako, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulionyoshwa- akija na kuomba kuelekea sehemu nyumba hii,
\v 33 basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi, na fanya yote ambayo mgeni atakuomba, ili kwamba watu wote wa dunia walijue jina lako na kukuogopa wewe, kama wafanyavyo watu wako Israeli, na kwamba waweze kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako.
\pi
\v 34 Ikiwa kwamba watu wako wakaenda nje kupigana dhidi ya adui zao, kwa njia yoyote ambayo unaweza kuwatuma, na ikiwa kwamba wakaomba kwako kuelekea mji huu ambao umeuchagua, na kuelekea nyumba ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako.
\v 35 Basi sikiliza maombi yao mbinguni, ombi lao, na uwasaidie.
\pi
\v 36 Kama wametenda dhambi dhidi yako—kwa kuwa hakuna asiye tenda dhambi—na ikiwa una hasira nao na kuwakabidhi kwa adui zao, ili kwamba adui wakawabeba na kuwachukua kama mateka katika nchi zao, iwe mbali au karibu.
\v 37 Kisha wakatambua kuwa wako katika nchi ambako wamewekwa utumwani, na ikiwa watatubu na kutafuta msaada kwako katika utumwa wao. Ikiwa watasema, Tumetenda kinyume na kutenda dhambi. Tumetenda kwa uovu,
\v 38 ikiwa watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa nia yao yote katika nchi ya utumwa wao, ambako walichukuliwa kama mateka, naikiwa wataomba kukabili nchi yao, uliyowapa baba zao, na kukabili mji ambao uliuchagua na kukabili nyumba ambayo niliijenga kwa ajili ya jina lako.
\v 39 Basi sika kutoka mbinguni, mahali unapoishi, sikia kuomba kwao na maombi na wayaombayo, na uwasaidie shida zao. Wasamehe watu wako, ambao wamekutenda dhambi.
\pi
\v 40 Sasa, Mungu wangu, ninakusihi, uyafungue macho yako, na masikio yako yasikie maombi yatakayofanywa katika sehemu hii.
\q1
\v 41 Sasa basi, amka, Yahwe Mungu, kwenye mahali pako pa kupumzikia, Wewe na sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Yahwe Mungu, wavikwe wokovu, na watakatifu wako wafurahi katika wema.
\q1
\v 42 Yahwe Mungu, usiugeuze nyuma uso wa masihi wako. Yakumbuke matendo yako katika agano lako la ufalme kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako.
\c 7
\cl Sura 7
\p
\v 1 Sasa Sulemani alipokuwa amemaliza kuomba, moto ukaja kutoka mbinguni na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, na utukufu wa Yahwe ukaijaza nyumba.
\v 2 Makuhani hawakuweza kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, kwa sababu utukufu wake uliijaza nyumba yake.
\v 3 Watu wote wa Israeli wakaangalia juu moto uliposhuka chini na utukufu wa Yahwe ulikuwa juu ya nyumba. Wakalala kwa nyuso zao juu ya sakafu ya mawe, wakaabudu, na kutoa shukrani kwa Yahwe. Wakasema, “Kwa maana yeye ni mwema, kwa maana agano lake la kifalme ladumu milele.”
\v 4 Kwa hiyo mfalme na watu wote wakamtolea Yahwe sadaka Yahwe.
\v 5 Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu na kondoo 120,000 na mbuzi. Kwa hiyo mfalme na watu wote wakaiweka wakfu nyumba ya Mungu.
\v 6 Makuhani wakasimama, kila mmoja akasimama mahali pake pa kuhudumu; Walawi pia pamoja na vyombo vya muziki vya Yahwe, ambavyo mfalme Daudi alivitengeza kwa ajili ya kumpa shukrani Yahwe katika nyimbo, “Kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.” Makuhani wote wakapiga matarumbeta mbele yao, na Israeli wote wakasimama.
\p
\v 7 Sulemani akaitakasa sehemu ya katikati ya kiwanja cha mfalme mbele ya nyumba ya Yahwe. Humo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba ambayo alikuwa ametengeza haikuweza kuzibeba sadaka, sadaka za nafaka, na za mafuta.
\p
\v 8 Kwa hiyo Sulemani akaitisha sikukuu wakati huo kwa siku saba, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa, kutoka Lebo Hamathi mpaka kijito cha Misiri.
\v 9 Siku ya nane wakaitisha kusanyiko la makini, kwa maana kwa siku saba walishika kuwekwa wakfu kwa ile madhabahu.
\v 10 Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba, Sulemani akawatanya watu kwenda kwenye nyumba zao kwa furaha na mioyo ya shangwe kwa sababu ya wema aliokuwaameuonyesha Yahwe kwa Daudi, Sulemani, Israeli, na watu wake.
\p
\v 11 Hivyo Sulemani akaimaliza nyumba ya Yahwe na nyumba yake mwenyewe. Kila kitu kilichokuja katika moyo wa Sulemani kwa ajili ya kukitengeneza katika nyumba ya Yahwe na katika nyumba yake mwenyewe, alikitimiza kwa mafanikio.
\v 12 Yahwe akamtokea Sulemani usiku na kusema kwake, “Nimesikia maombi yako, na nimeichagua sehemu hii kwa ajili yangu mwenyewe kama nyumba ya dhabihu.
\pi
\v 13 Kama nitazifunga mbingu ili kwamba kusiwepo mvua, au kama nitaamuru nzige waimeze nchi, au kama nitatuma magonjwa kati kati ya watu wangu,
\v 14 kisha watu wangu, ambao wameitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, kuomba, kuutafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya, nitasikia kutoka mbinguni, kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.
\v 15 Sasa macho yangu yatakuwa wazi na masikio yangu yatasikiliza maombi yanayofanywa katika sehemu hii.
\v 16 Kwa maana sasa nimeichagua na kuitakasa nyumba hii ilikwamba jina langu lipate kuwa humo milele. Masikio yangu na moyo wangu vitakuwako kila siku.
\pi
\v 17 Kwako wewe, kama utatembea mbele zangu kama baba yako Daudi alivyotembea, ukitii yote niliyokuamuru na kuzishika sheria zangu na maagizo yangu,
\v 18 basi nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyosema katika agano na Daudi baba yako, niliposema, Mzaliwa wako hatashindwa kamwe kuwa mtawala katika Israeli.
\pi
\v 19 Lakini ukigeuka, na kuzisahau sheria zangu na amri ambazo nimeweka mbele yenu, na kama utaenda kuabudu miungu wengine na kuwasujudia,
\v 20 basi nitawang'oa kutoka kwenye nchi yangu ambayo nimewapa. Nyumba hii ambayo nimeitakasa kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali kutoka mbele zangu, na nitaifanya kuwa methali na utani miongoni mwa watu wote.
\v 21 Ingawa hekalu hili zuri sana kwa sasa, kila mtu apitaye karibu yake atashangazwa na ataguna. Watauliza, Kwa nini Yahwe ameifanyia hivi nchi hii na nyumba hii.
\v 22 Wengine watajibu, Kwa sababu walimsahau Yahwe, Mungu wao, ambaye alikuwa amewatoa babu zao nje ya nchi ya Misiri, na wakashikamana na miungu wengine na kuwainamia chini na kuwaabudu. Hii ndiyo maana Yahwe ameleta majanga haya yote juu yao.”
\c 8
\cl Sura 8
\p
\v 1 Ikawa karibu ya mwisho wa miaka ishirini, kipindi ambacho Sulemani alikuwa ameijenga nyumba ya Yahwe na ya kwake mwenye,
\v 2 kwamba Sulemani akaiajenga miji ambayo Hiramu alikuwa amempa, na ndani yake akawaweka watu wa Israeli.
\v 3 Sulemani akauvamia Hamathzoba, akaushinda.
\v 4 Akaijenga Tadmori katika nyika, na miji yote ya hazina, ambayo aliijenga katika Hamathi.
\v 5 Pia akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, mijiiliyozungushiwa kwa ukuta, malango, na makomeo.
\v 6 Akaujenga Baalathi na miji yote ya hazina aliyoimiliki, na miji yote kwa ajili ya magari yake na miji kwa ajili ya wapanda farasi wake, na chochote alichotamani kujenga kwa ajili ya starehe zake katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika nchi zote zilizokuwa chini ya utawala wake.
\p
\v 7 Kuhusu watu wengine wote ambao walikuwa wamesalia wa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, Wayebusi, ambao hawakuwa wa Israeli,
\v 8 watoto wao ambao waliachwa baada yao katika nchi, ambao watu wa Israeli hawakuwaangamiza—Sulemani akawafanyisha kazi kwa nguvu, ndivyo walivyo hata leo.
\v 9 Vile vile, Sulemani hakuwafanyisha kazi kwa nguvu watu wa Israeli. Badala yake, wakawa wanajeshi wake, maakida wake, wakuu wake, na maakida wa magari ya majeshi yake na wapanda farasi wake.
\v 10 Pia hawa walikuwa wakuu wa wakuu wakisimamia wasimamizi waliokuwa wa mfalme Sulemani, walikuwa 250, waliowasimamia watu walioifanya kazi.
\p
\v 11 Sulemani akamleta binti Farao nje ya mji wa Daudi kwenye nyumba aaliyokuwa amemjengea, kwa maana alisema, “Mke wangu lazima asiishi katika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu kila linapokuja sanduku la Yahwe ni pakatifu.”
\p
\v 12 Kisha Sulemani akatoa sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe juu ya madhabahu yake ambayo alikuwa ametengeza mbele ya ukumbi.
\v 13 Akatoa sadaka kama ilivyohitaka ratiba ya kila siku; akazitoa, kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa katika amri ya Musa, katika siku za Sabato, miezi mipya, na katika siku zilizopangwa mara tatu kila mwaka: Sikukuu ya mikate isiyochachwa, sikukuu ya majuma, na sikuku ya vibanda.
\v 14 Katika kuyatunza maagizo ya baba yake Daudi, Sulemani akayapanga makundi ya makuhani kwenye kazi yao, na Walawi kwenye nafasi zao, ili kumsifu Mungu na kuhudumu mbele za makuhani, kama ilivyotakiwa katika ratiba ya kila siku. Pia akawateua walinda lango kwa zamu zao kwa kila lango, kwa maana Daudi, mtu wa Mungu, alikuwa ameagiza hivyo pia.
\v 15 Watu hawa hawakupotea kutoka kwenye amri ya mfalme kwa makuhani na Walawi kuhusu jambo lolote, au kuhusu vyumba vya hazina.
\p
\v 16 Kazi yote aliyoagizwa na Sulemani ikakamilika, kutoka siku msingi wa nyumba ya Yahwe ulipowekwa hadi ilipokamilika. Nyumba ya Yahwe ikamalizika.
\p
\v 17 Kisha Sulemani akaenda Esion geberi, na Elothi, juu ya pwani katika nchi ya Edomu.
\v 18 Hiramu akatuma meli zake kupitia watumishi wake ambao walikuwa wana maji wenye uzoefu. Wakasafiri nawatumishi wa Sulemani hadi Ofiri. Wakachukua kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambazo walimletea Sulemani.
\c 9
\cl Sura 9
\p
\v 1 Malkia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Sulemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa
\v 2 Sulemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Sulemani akamjibu maswali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Sulemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.
\p
\v 3 Malkia wa Sheba alipoiona hekima ya Sulemani na ikulu aliyokuwa amejenga,
\v 4 chakula mezani kwake, mahali pa kukaa watumishi wake, kazi ya watumishi wake na mavazi yao, pia wabebakikombe na mavazi yao, na namna alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe, hapakuwa na roho zaidi ndani yake.
\p
\v 5 Akasema kwa mfalme, “Ni kweli, taarifa nilioisikia katika nchi yangu kuhusu maneno yako na hekima yako.
\v 6 Sikuamini nilichokisikia mpaka nilipokuja hapa, na sasa macho yangu yamekiona. Sikuambiwa nusu kuhusu hekima yako na utajiri wako! Umeuzidi umaarufu niliokuwa nimesikia kuhusu wewe.
\v 7 Wamebarikiwa watu wako, na watumishi wako ambao husimama mbele yako, kwa sababu wanaisikia hekima yako. \f + \ft Baadhi ya maandiko yanasema, “Wambarikiwa wake zako,” ikidhaniwa kwamba kifungu hicho kinapaswa kusomeka kama ilivyo katika Wafalme 10:8. \f*
\v 8 Amebarikiwa Yahwe Mungu wako, ambaye amepata raha ndani yako, aliyekuweka juu ya kiti chake cha enzi, ili uwe mfalme kwa ajili ya Yahwe Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako anaipenda Israeli, ili kuwathibisha milele, amekufanya kuwa mfalme juu yao, ili ufanye hukumu na haki.
\p
\v 9 Akampa mfalme talanta 120 za dhahabu na kiasi kikubwa manukato na vitu vya thamani. Sulemani hakupewa tena kiasi kikubwa cha manukato kama hiki ambacho alipewa na malkia wa Sheba.
\p
\v 10 Watumishi wa Hiramu na mfalme Sulemani, ambaye alileta dhahabu kutoka Ofiri, miti ya msandali, na vito vya thamani.
\v 11 Kwa miti hiyo ya msandali, mfalme Sulemani akatengeneza madari ya nyumba ya Yahwe na nyumba yake, na vinubi na vinanda kwa ajili ya wanamziki. Hapajaonekana tena mbao kama hiyo katika nchi ya Yuda.
\v 12 Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotaka, chochote alichoomba, zaidi ya vile alivyoleta kwa mfalme Sulemani. Kwa hiyo akaondoka na kurudi kwenye nchi yake, yeye na watumishi wake.
\p
\v 13 Sasa uzito wa dhahabu ambayo ililetwa kwa Sulemani ndani ya mwaka mmoja ulikuwa talanta 666 za dhahabu,
\v 14 nje na dhahabu ambayo waliileta wachukuzi na wafanya biashara. Wafalme wote wa Arabuni na maliwali katika nchi pia wakamletea Sulemani dhahabu na fedha.
\p
\v 15 Mfalme Sulemani akatengeneza ngao kubwa mia mbili za dhahabu iliyofuliwa. Shekeli mia sita za dhahabu zikatumika kwa kila ngao.
\v 16 Pia akatengeneza ngao mia tatu za dhahabu iliyopigwa. Mia tatu za dhahabu zikaenda kwa kila ngao; mfalme akaziweka kwenye ikulu ya Msitu wa Lebanoni.
\p
\v 17 Kisha mfalme atengeneza kiti cha enzi kikubwa cha pembe na kufunika kwa dhahabu safi.
\v 18 Kulikuwa na ngazi sita kwenda kwenye kiti cha enzi, na sehemu ya juu ya kiticha enzi ilikuwa duara. Kulikuwa na mikono kila upande wa kiti, na simba wawili wamesimama pembeni na hiyo mikono.
\v 19 Simba kumi na wawili walisimama juu ya zile ngazi, mmoja kila upande wa ngazi sita.
\v 20 Hapakuwa na kiti cha enzi kama hicho katika ufalme wowote mwingine. Vikombe vyote vya kunywea vya Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vikombe vyote vya mfalme katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu halisi. Hakuna hata kimoja kilichokuwa cha fedha kwa sababu fedha haikuchuliwa kuwa ya thamani katika siku za Sulemani.
\v 21 Mfalme alikuwa na meli zilizosafiri baharini, pamoja na meli za Hiramu. Mara moja kwa mwaka meli zilileta dhahabu, fedha, na pembe, na manukato, na pia nyani na tausi.
\p
\v 22 Kwa hiyo Mfalme Sulemani aliwazidi utajiri na hekima wafalme wote wa dunia.
\v 23 Dunia yote waliutafuta uwepo wa Sulemani ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.
\v 24 Waliomtembelea walileta kodi, vyombo vya shaba na dhahabu, nguo, silaha, na manukato, na farasi na nyumbu, mwaka baada ya mwaka.
\p
\v 25 Sulemani alikuwa na mazizi elfu nne kwa ajili ya farasi na magari, na wapanda farasi kumi na mbili elfu, ambao waliwaweka katika miji ya magari na pamoja naye katika Yerusalemu.
\v 26 Akatawala juu ya wafalme wote kutoka mto Efrati hadi nchi ya Wafilisti, na hadi mpaka wa Misiri.
\v 27 Mfalme alikuwa na fedha katika Yerusalemu, nyingi kama mawe juu ya ardhi. Akazifanya mbao za mierezi kuwa nyingi kama miti ya mikuyu ambayo iko nyanda za chini.
\v 28 Wakaleta farasi kutoka Misri na kutoka nchi zote kwa ajili ya Sulemani.
\p
\v 29 Kwa mambo mengine kuhusu Sulemani, mwanzo na mwisho, hayajaandikwa katika Historia ya Nathani Nabii, katika unabii wa Abiya Mshinoni, na katika Maono ya Ido mwonaji wa mambo ya Yeroboamu mwana wa Nabati?
\v 30 Sulemani akatawala katika Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.
\v 31 Akalala na baba zake na watu wakamzika katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu, mwanaye, akawa mfalme katika sehemu yake.
\c 10
\cl Sura 10
\p
\v 1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa maana Israeli wote walikuwa wanakuja Shekemu kwa ajili ya kumfanya yeye mfalme.
\v 2 Ikatokea kwamba Yeroboamu mwana wa Nebati akasikia haya (kwa maana alikuwa katika Misiri, ambako alikuwa amekimbilia kutoka kwenye uwepo wa Mfalme Sulemani, lakini Yeroboamu akarudi kutoka Misiri).
\v 3 Kwa hiyo wakatuma na kumuita yeye, na Yeroboamu na Israeli wote wakaja; wakamwambia Rehoboamu na kusema,
\v 4 “Baba yako aliifanya nira yetu ngumu. Kwa hiyo sasa, ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa rahisi, na ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu, na sisi tutakutumikiawewe.”
\p
\v 5 Rehoboamu akawaambia, “Njoni kwangu tena baada ya siku tatu.” Kwa hiyo watu wakaondoka.
\p
\v 6 Mfalme Rehoboamu akaomba ushauri kwa wazee ambao walikuwa wamesimama mbele ya Sulemani baba yake wakati alipokuwa hai; akasema, Mnanishauri niwape jibu gani watu hawa?”
\p
\v 7 Wakasema kwake, Ikiwa wewe ni mwema kwa watu hawa na uwapendeze, na usema maneno mazuri kwao, basi siku zote watakuwa watumishi wako.”
\p
\v 8 Lakini Rehoboamu akapuuza ushauri wa wazee ambao walimpa, na akashauriana na wanaume vijana ambao walikuwa wa rika lake, ambao walisimama mbele yake.
\v 9 Akawaambia, “Mnanipa ushauri gani, ili kwamba niwajibu watu waliozungumza kwangu na kusema, “Ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu?”
\p
\v 10 Wanaume vijana ambao walikuwa rika la Yeroboamu wakasema kwake, wakisema, “Hivi ndivyo utakavyosema kwa watu waliokuambia kwamba baba yako Sulemani aliifanya nira yao nzito, lakini kwamba lazima uifanye nyepesi. Hivi ndivyo utakavyosema kwao, Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.
\v 11 Kwa hiyo sasa, ingawa baba yangu aliwatwika nira nzito, nitaiongeza nira yenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini nitawaadhibu kwa nge.”
\p
\v 12 Kwa hiyo Yeroboamu na watu wote wakaja kwa Rehoboamu katika siku ya tatu, kama alivyosema mfalme, “Rudini kwangu katika siku ya tatu,”
\v 13 Yeroboamu akasema kwao kwa ukatili, akiupuuza ushauri wa wazee.
\v 14 Akasema kwao akiufuata ushauri wa wanaume vijana, akisema, “Baba yangu aliifanya nira yenu nzito, lakini mimi nitaiongeza. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini mimi nitawaadhibu kwa nge.”
\v 15 Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa ilikuwa tukio lililoletwa na Mungu, kwamba Yahwe aweze kulitimiza neno lake ambalo Ahiya Mshiloni alikuwa amemwambia Yeroboamu mwana wa Nebati.
\p
\v 16 Israeli wote, walipoona kwamba mfalme hakuwasikiliza, watu wakamjibu na kusema, “Tuna sehemu gani katika Daudi? Hatuna urithi katika wana wa Yese! Kila mmoja wenu anapaswa kwenda katika hema yake, Israeli. Sasa kila mtu aone nyumba yake, Daudi.” Kwa hiyo Israeli wote wakarudi kwenye hema zao.
\p
\v 17 Lakini kwa watu wa Yuda walioishi katika miji ya Yuda, Yeroboamu akatawala juu yao.
\p
\v 18 Kisha mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, ambaye alikuwa msimamizi wa wafanya kazi, lakini watu wa Israeli walimuua kwa kumpiga mawe. Mfalme Rehoboamu akaingia haraka ndani ya gari lake kwenda Yerusalemu.
\v 19 Kwa hiyo Israeli wakawa waasi dhidi ya nyumba ya Mungu hadi leo.
\c 11
\cl Sura 11
\p
\v 1 Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akawakusanya nyumba ya Yuda na Benjamini, wanaume 180,000 waliochaguliwa ambao walikuwa wanajeshi, kwa ajili ya kupigana dhidi ya Israeli, ili kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu.
\p
\v 2 Lakini neno la Yahwe likamjia Shemaya mtu wa Mungu, likisema,
\v 3 “Sema kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na kwa Israeli katika Yuda na Benjamini,
\v 4 Yahwe anasema hivi, “Msivamie wala kufanya vita dhidi ya ndugu zako. Kila mmoja lazima arudi kwenye nyumba yake, kwa maana nimesababisha jambo hili kutokea.” Kwa hiyo wakayatii maneno ya Yahwe na kuacha kumvamia Yeroboamu.
\p
\v 5 Yeroboamu akaishi katika Yerusalemu na kujenga miji katika Yuda kwa ajili ya kujilinda.
\v 6 Akaijenga Bethlehemu, Etamu Tekoa,
\v 7 Bethsusi, Soko, Adulamu,
\v 8 Gathi, Maresha, Zifu,
\v 9 Adoraimu, Lakishi, Azeka,
\v 10 Sora, Aiyaloni, na Hebroni. Hii ni miji yenye ngome katika Yuda na Benjamini.
\v 11 Akaziimarisha ngome na kuweka maamri jeshi ndani yake, pamoja na hazina ya chakula, mafuta, na divai.
\v 12 Akaweka ngao na mikuki katika miji yote na kuifanya imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benjamini zikawa zake.
\p
\v 13 Makuhani na Walawi waliokuwa katika Israeli yote wakaenda kwake kutoka ndani ya mipaka yao.
\v 14 Kwa kuwa Walawi waliacha nchi za malisho yao na mali zao ili kuja Yuda na Yerusalemu, kwa maana
\v 15 Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewafukuza, ili kwamba wasifanye majukumu yao ya kikuhani kwa ajili ya sehemu za juu na mbuzi na sanamu za ndama alizokuwa ametengeneza.
\v 16 Watu kutoka kabila zote za Israeli wakaja nyuma yao, wale waliokuwa wameielekeza mioyo yao kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli; wakaja Yerusalemu kwa ajili ya kumtolea dhabihu Yahwe. Mungu wa baba zao.
\v 17 Kwa hiyo wakauimarisha ufalme wa Yuda na kumfanya imara Rehoboamu mwana wa Sulemani kwa miaka mitatu, na wakatembea kwa miaka mitatu katika njia ya Daudi na Sulemani.
\p
\v 18 Rehoboamu akajitwalia mke: Mahalathi, binti wa Yerimothi, mwana wa Daudi na wa Abihaili, binti wa Eliabu, mwana wa Yese.
\v 19 Akamzalia wana: Yeushi, Shemaraia, na Zahamu.
\v 20 Baada ya Mahalathi, Rehoboamu akamchukua Maaka, binti wa Absalomu; akamzalia Abiya, Atai, Ziza, na Shelomithi.
\v 21 Rehoboamu akampenda Maaka, binti Absalomu, zaidi kuliko wake zake wengine wote na masuria (alichukua wake kumi na nane na masuria sitini, na akawa baba wa wana ishirini na nane na mabinti sitini).
\p
\v 22 Rehoboamu akamteua Abiya mwana wa Maaka kuwa mkuu, kiongozi miongoni mwa ndugu zake alikuwa na wazo la kumfanya mfalme.
\v 23 Rehoboamu akatawala kwa hekima; akawatawanya wanaye katika nchi yote ya Yuda na Benjamini katika kila mji imara. Pia akawapa chakula kwa wingi na akatafuta wake wengi kwa ajili yao.
\c 12
\cl Sura 12
\p
\v 1 Ikawa kwamba, Rehoboamu alipokuwa ameimarishwa na mwenye nguvu, kwamba akaikataa sheria ya Yahwe--na Waisraeli wote pamoja naye.
\v 2 Ilitokea katika mwaka wa tano wa Mfalme Rehoboamu, kwamba, Shishaki, mfalme wa Israeli, akaja kinyume na Yerusalemu, kwa sababu watu walikuwa wameacha kuwa waaminifu kwa Yahwe.
\v 3 Akaja na magari elfu moja na mia mbili pamoja naye na wapanda farasi elfu sitini. Askari wasio hesabika wakaja pamoja naye kutoka Misri: Walubi, Wasukii, na Waethiopia.
\v 4 Akaiteka miji yenye ngome ya Yuda na akaja Yerusalemu.
\p
\v 5 Sasa Shemaya nabii akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda ambao walikuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki. Shemaya akasema kwao, “Hivi ndivyo anavyosema Yahwe: Mmenisahau, kwa hiyo pia nimewaweka katika mkono wa Shishaki.”
\p
\v 6 Kisha wakuu wa Israeli na mfalme wakajinyenyekesha na kusema, “Yahwe ni mtakatifu.”
\p
\v 7 Yahwe alipoona kuwa wamejinyenyekeza, neno la Yahwe likamjia Shemaya, likisema, “Wamejinyenyekesha. Sitawaadhibu; nitawaokoa kwa hatua fulani, na hasira yangu haitamiminwa juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki.
\v 8 Vile vile, watakuwa watumishi wake, ili kwamba wajue nini maana ya kunitumikia mimi na kuwatumikia watawala wa nchi zingine.”
\p
\v 9 Kwa hiyo Shishaki, mfalme wa Misiri akaja Yerusalemu akazichukua hazina katika nyumba ya Yahwe, na hazina katika nyumba ya mfalme. Akachukua kila kitu; pia akazichukua ngao za dhahabu alizokuwa amezitengeneza Sulemani. Mfalme
\v 10 Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba katika nafasi zake na kuzikabidhi mikononi mwa maamri jeshi wa walinzi, ambao waliilinda milango ya kuelekea kwenye nyumba ya mfalme.
\v 11 Ikawa kwamba mfalme kila alipoingia katika nyumba ya Yahwe, walinzi wakazibeba; kisha wakazirudisha katika nyumba ya ulinzi.
\p
\v 12 Rehoboamu alipojinyenyekeza mwenyewe, ghadhabu ya Yahwe ikampisha mbali, kwa hiyo hakumwangamiza kabisa; pembeni, bado kulikuwa na baadhi ya wema wa kupatikana katika Yuda.
\p
\v 13 Hivyo mfalme Rehoboamu akafanya ufalme wake imara katika Yerusalemu, na kwa hiyo akatawala. Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka arobaini na moja alipoanza kutawala, na akatawala kwa muda wa miaka kumi na saba katika Yerusalemu, mji ambao Yahwe alikuwa ameuchagua kutoka kwa makabila ya Israeli ili kwamba aliweke jina lake humo. Jina la mamake aliitwa Naama, Mwamoni.
\v 14 Akafanya yaliyokuwa maovu, kwa sababu hakuuelekeza moyo wake kumtafuta Yahwe.
\p
\v 15 Kwa mambo mengine kuhusu Rehoboamu, mwanzo na mwisho, hayajaandikwa katika maandishi ya Shemaya nabii na ya Ido mwonaji, ambayo pia yana kumbukumbu ya vizazi na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu?
\v 16 Rehoboamu akalala pamoja na baba zake na alizikwa katika mji wa Daudi; Abiya mwanawe akawa mfalme katika nafasi yake.
\c 13
\cl Sura 13
\p
\v 1 Katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yeroboamu, Abiya akaanza kutawala juu ya Yuda.
\v 2 Akatawala kwa miaka mitatu katika Yerusalemu; jina la mama yake aliitwa Maaka, binti wa Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
\v 3 Abiya akaingia vitani na jeshi la askari, wenye nguvu, hodari, 400,000 wanaume waliochaguliwa. Yeroboamu akapanga mistari ya vita dhidi yake yenye 800,000 wanaume askari waliochaguliwa, wenye nguvu, hodari.
\p
\v 4 Abiya akasimama juu ya mlima Semaraimu, uliopo katika kilima cha nchi ya Efraimu, na akasema, “Nisikilizeni, Yeroboamu na Israeli wote!
\v 5 Hamjui kwamba Yahwe, Mungu wa Israeli, alitoa sheria juu ya Israeli kwa Daudi milele, kwake na kwa wanawe kwa agano rasmi?
\v 6 Bado Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumishi wa Sulemani mwana wa Daudi, akainuka na kuasi dhidi ya bwana wake.
\v 7 Watu wabaya, washirika wa karibu, wakamkusanyikia, wakamjia kinyume Rehoboamu mwana wa Sulemani, wakati Rehoboamu alipokuwa mdogo na asiye na uzoefu na hakuweza kuwamudu.
\p
\v 8 Sasa mnasema kwamba mnaweza kuuzuia utawala wa Yahwe wenye nguvu katika mkono wa uzao wa Daudi. Ninyi ni jeshi kubwa, na pamoja nanyi kuna ndama wa dhahabu ambao Yeroboamu alitengeneza kama miungu kwa ajili yenu.
\v 9 Hamkuwafukuza nje makuhani wa Yahwe, uzao wa Haruni, na Walawi? Hamkujifanyia makuhani katika namna ya watu wa nchi zingine? Yeyote ajaye kujitakasa mwenyewe na ngo'mbe dume kijana, na kondoo dume saba anaweza kuwa kuhani wa kile ambacho siyo miungu.
\p
\v 10 Lakini kwetu, Yahwe ni Mungu wetu, na hatujamsahau. Tuna makuhani, uzao wa Haruni, wakimtumikia Yahwe, na Walawi, ambao wako katika kazi yao.
\v 11 Kila asubuhi na jioni humtolea Yahwe sadaka za kuteketezwa na uvumba mtamu. Pia hupanga mkate wa uwepo juu ya meza takatifu; pia huweka kinara cha dhahabu pamoja na taa zake, ili watoe sadaka kila jioni. Sisi huzishika sheria za Yahwe, Mungu wetu, Lakini ninyi mmemsahau.
\v 12 Ona, Mungu yuko pamoja nasi katika vichwa vyetu, na makuhani wake wako hapa na tarumbeta kwa ajili ya kutoa sauti dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane na Yahwe, Mungu wa babu zenu, kwa maana hamtafanikiwa.”
\p
\v 13 Lakini Yeroboamu akaandaa mavamizi nyuma yao; jeshi lake lilikuwa mbele ya Yuda, na wavamizi nyuma yao.
\v 14 Yuda walipoangalia nyuma, tazama, mapigano yalikuwa pote mbele na nyuma yao. Wakamlilia Yahwe kwa sauti, na makuhani wakayapuliza matarumbeta.
\v 15 Kisha wanaume wa Yuda wakapiga kelele; walipopiga kelele, ikawa kwamba Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.
\v 16 Watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda, na akawatia kwenye mkono wa Yuda.
\v 17 Abiya na jeshi lake wakawaua kwa mauaji makuu; 500,000 watu wanaume waliochaguliwa wa Israeliwakaanguka wamekufa.
\p
\v 18 Katika namna hii hii, watu wa Israeli wakatiishwa chini wakati huo, watu wa Yuda wakashinda kwa sababu walimtegemea Yahwe, Mungu wa baba zao.
\p
\v 19 Abiya akamshawishi Yeroboamu; akachukua miji kutoka kwake; Betheli pamoja na vijiji vyake, Yeshana pamoja na vijiji vyake, na Efroni pamoja na vijiji vyake.
\v 20 Yeroboamu hakupata nguvu tena katika siku za Abiya; Yahwe akampiga, na akafa.
\p
\v 21 Lakini Abiya akawa na nguvu sana; akachukua wanawake kumi na wanne kwa ajili yake na akawa baba wa wana ishirini na mbili na mabinti kumi na sita.
\p
\v 22 Matendo ya Abiya yaliyosalia, tabia yake na maneno yake yameandikwa katika kamusi ya nabii Ido.
\c 14
\cl Sura 14
\p
\v 1 Abiya akalala pamoja na baba zake, na wakamzika katika mji wa Daudi. Asa, mwanawe, akawa mfalme katika nafasi yake. Katika siku yake nchi ilikuwa tulivu miaka kumi.
\p
\v 2 Asa alifanya yaliyomema na sahihi katika macho ya Yahwe Mungu wake,
\v 3 kwa maana aliziondosha mbali madhabahu za kigeni na sehemu za juu. Akaziangusha chini nguzo za mawe na kuzikata nguzo za Maashera.
\v 4 Akawaamuru Yuda kumtafuta Yahwe, Mungu wa baba zao, na kuzishika sheria na amri.
\v 5 Pia akaziondosha mbali sehemu za juu na madhabahu za kufukiza kutoka miji yote ya Yuda. Ufalme ulikuwa na pumziko chini yake.
\v 6 Akajenga miji ya ngome katika Yuda, kwa maana nchi ilikuwa tulivu, na hakukuwa na vita katika miaka hiyo, kwa sababu Yahwe alikuwa amempa amani.
\p
\v 7 Kwa maana Asa aliwaambia Yuda, “Tuijenge miji hii na kuizungushia kuta, na minara, mageti, na makomeo; nchi bado yetu kwa sababu tumemtafuta Yahwe Mungu wetu. Tumemtafuta yeye, na ametupa amani katika kila upande.” Kwa hiyo walijenga na wakafanikiwa.
\p
\v 8 Asa alikuwa na jeshi ambalo lilibeba ngao na mikuki; kutoka Yuda alikuwa na wanaume 300,000, na kutoka Benjamini, wanaume 280,000 waliobeba ngao na kuvuta pinde.
\p
\v 9 Zera Mwethiopia akaja juu yao na jeshi la wanajeshi milioni moja na magari mia tatu; akaja Maresha.
\v 10 Kisha Asa akatoka nje kukutana naye, na wakapanga mistari ya vita ya mapigano katika bonde la Sefatha huko Maresha.
\p
\v 11 Asa akamlilia Yahwe, Mungu wake, na akasema, “Yahwe, hakuna aliye kama wewe lakini ni wewe wa kumsaidia mtu asiye na nguvu anapokutana na mengi. Tusaidie, Yahwe, Mungu wetu, kwa maana tunakutegemea wewe, na katika jina lako tumekuja kupambana na idadi hii kubwa ya adui. Yahwe, wewe ni Mungu wetu; usimuache mtu akushinde.”
\p
\v 12 Kwa hiyo Yahwe akawapiga Waethiopia mbele za Asa na Yuda; Waethiopia wakakimbia.
\v 13 Asa pamoja na wanajeshi waliokuwa pamoja naye wakawafukuza hadi Gerari. Kwa hiyo Waethiopia wengi wakajeruhiwakiasi kwamba hawakuweza kupona, kwa maana waliangamizwa kabisa mbele za Yahwe na jeshi lake. Jeshi likachukua mateka wengi sana.
\v 14 Jeshi likaviangamiza vijiji vyote jirani karibu na Garari, kwa kuwa hofu ya Yahwe ilikuwa imekuja juu ya wakaaji. Jeshi likateka vijiji vyote, na vilikuwa na hazina nyingi sana ndani yake.
\v 15 Jeshi pia likaipiga hema ya makazi ya wachungaji; wakabeba kondoo kwa wingi, ngamia vile vile, na kisha wakarudi Yerusalemu.
\c 15
\cl Sura 15
\p
\v 1 Roho wa Mungu akaja juu ya Azaria mwana wa Odedi.
\v 2 Akaenda nje kukutana na Asa na akamwambia, “Nisikilize, Asa, na Yuda wote na Benyamini: Yahwe yuko pamoja nanyi, pale mnapokuwa naye. Kama mtamtafuta, mtampata; lakini kama mtamsahau, atawasahau ninyi.
\v 3 Sasa kwa muda mrefu, Israeli hawakuwa na Mungu wa kweli, bila kuhani wa kufundisha, na bila sheria.
\v 4 Lakini katika dhiki yao wakamrudia Yahwe, Mungu wa Israeli, na wakamtafuta, wakampata.
\v 5 Katika nyakati hizo hapakuwa na amani kwake aliyesafiri kwenda mbali, wala kwake aliyesafiri kuja hapa; badala yake shida kubwa zilikuwa juu ya wenyeji wote wa wanchi.
\v 6 Waligawanyika vikundi vikundi, taifa dhidi ya taifa, na mji dhidi ya mji, kwa maana Mungu aliwapa shida za kila aina ya mateso.
\v 7 Lakini muwe hodari, na msiuache mkono wenu kuwa dhaifu, kwa maana kazi yenu itapewa thawabu.”
\p
\v 8 Asa aliposikia maneno haya, unabii wa odedi nabii, akajipa ujasiri na kuviondosha mbali vitu vya kuchukiza kutoka nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji yote aliyokuwa ameiteka kuanzia kilima cha nchi ya Efraimu, na akaijenga tena madhabahu ya Yahwe, ambayo ilikuwa mbele ya ukumbi wa nyumba ya Yahwe.
\v 9 Akawakusanya Yuda wote na Benjamini, na wale waliokaa pamoja nao—watu wa kutoka Efraimu na Manase, na kutoka Simeoni. Kwa maana walikuja kwake katika hesabu kubwa kutoka Israeli, walipoona kwamba Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye.
\p
\v 10 Kwa hiyo wakakusanyika katika Yerusalemu katika mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa.
\v 11 Katika siku hiyo walimtolea Yahwe dhabihu baadhi ya nyara ambazo walikuwa wameleta; ng'ombe wa kulima mia saba na kondoo na mbuzi elfu saba.
\v 12 Wakaingia katika agano kwa ajili ya kumtafuta Yahwe, Mungu wa babu zao, kwa moyo wao wote na roho yao yote.
\v 13 Wakakubaliana kwamba yeyote atakayepuuza kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli, atapaswa kuuawa, awe mdogo ama mkubwa, awe mwanaume ama mwanamke.
\v 14 Wakaapa kwa Yahwe kwa sauti kubwa, kwa kelele, na kwa sauti za tarumbeta na baragumu.
\v 15 Yuda wote wakakifurahia kile kiapo. Kwa maana walikuwa wameapa kwa moyo wao wote, na walimtafuta Mungu kwa nia yao yote, na walimuona. Yahwe akawapa amani pande zote.
\p
\v 16 Pia Mfalme Asa akamwondoa Maaka, asiwe malkia, kwa sababu alikuwa amefanya sanamu ya kuchukiza ya Maashera. Asa akaivunja vunja sanamu ya kuchukiza, akaiweka kwenye mavumbi akaichoma moto huko kijitoni Kidroni.
\v 17 Lakini sehemu za juu hazikuwa zimeondolewa nje ya Israeli. Vile vile, Moyo wa Asa ulijitoa kikamilifu siku zake zote.
\v 18 Akaleta kwenye nyumba ya Mungu vitu vya baba yake na vitu vyake mwenyewe vilivyokuwa vya Yahwe: vitu vya fedha na dhahabu.
\p
\v 19 Hapakuwa na vita zaidi hadi miaka thelathini na mitano ya utawala wa Asa.
\c 16
\cl Sura 16
\p
\v 1 Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Baasha, mfalme wa Israeli, akatenda kwa ukatili dhidi ya Yuda na akaujenga Rama, ili kwamba asimruhusu mtu yeyote kutoka wala kuingia katika nchi ya Asa, mfalme wa Yuda.
\p
\v 2 Kisha Asa akaitoa fedha na dhahabu nje ya vyumba vya kuhifadhia katika nyumba ya Yahwe na nje ya nyumba ya mfalme, na akaituma kwa Ben Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye aliishi Dameski. Akasema, pawe na agano kati yako na mimi, kama palivyokuwa na agano kati ya baba yangu na baba yako. Angalia, nimekutumia fedha na dhahabu.
\v 3 Livunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache.”
\p
\v 4 Ben Hadadi akamsikiliza mfalme Asa na kutuma maakida wa majeshsi dhidi ya miji ya Israeli. Wakavamia Iyoni, Dani, Abelimaimu, na miji yoye ya kuhifadhia ya Naftali.
\v 5 Ikawa kwamba Baasha aliposikia hili, akaacha kuujenga Rama, na akaistisha kazi yake.
\v 6 Kisha Asa mfalme akawachukua Yuda wote pamoja naye. Wakayabeba mawe na mbao za Rama ambazo Baasha alikuwa anajengea ule mji. Kisha Mfalme Asa alitumia vifaa hivyo vya ujenzi kwa ajili ya kuijenga Gaba na Mispa.
\p
\v 7 Wakati huo Hanani mwonaji akaenda kwa Asa, mfalme wa Yuda, na akamwambia, “Kwa sababu umemtegemea mfalme wa Aramu, na hukumtegemea Yahwe Mungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limetoroka nje ya mikono yako.
\v 8 Waethiopia na Walubi hawakuwa jesi kubwa, wenye magari mengi na wapanda farasi wengi? Na bado, kwa sababau ulimtegemea Yahwe, alikupa ushindi juu yao.
\v 9 Kwa maana macho ya Yahwe hukimbia kila mahali katika dunia yote, ili kwamba ajioneshe mwenyewe shujaa kwa niaba ya wale amabao mioyo yao ni mikamilifu kumwelekea yeye. Lakini umetenda kipumbavu katika jambo hili. Kwa maana tangu sasa na kuendelea, utakuwa na vita.” Kisha Asa akamkasirikia mwonaji, akamuweka gerezani, kwa maana alikuwa na hasira naye juu ya jambao
\v 10 hili. Wakati huo huo, aliwagandamiza baadhi ya watu
\p
\v 11 Tazma, matendo ya Asa, kutoka mwanzo hadi mwisho, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
\v 12 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipata ugonjwa kwenye miguu yake; ugonjwa wake ulikuwa mkali sana. Hata hivyo, hakutafuta msaada kutoka kwa Yahwe, lakini kutoka kwa waganga tu.
\v 13 Asa akalala pamoja na babu zake; alikufa katika mwaka wa arobaiani na moja wa utawala wake. Wakamzika katika kaburi lake, ambalo alilichimba mwenyewe katika mji wa Daudi.
\v 14 Walimlaza juu ya kitanda kilichokuwa kimewekewa manukato na aina mbali mbali ya dawa zilizotayarishwa na wale mafundi wa manukato. KIsha wakatengeneza moto kwa heshima yake.
\c 17
\cl Sura 17
\p
\v 1 Yehoshafati mwana wa Asa akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoshafati akajiimarisha dhidi ya Israeli.
\v 2 Akaweka majeshi katika miji yote Yuda yenye ngome, na akaweka magereza katika nchi ya Yuda na katika miji ya Efraimu, ambayo Asa baba yake alikuwa ameiteka.
\p
\v 3 Yahwe alikuwa pamoja na Yehoshafati kwa sababu alitembea katika njia za kwanza za baba yake Daudi, na hakuwatafuta Mabaali. \f + \ft Baadhi ya mandiko ya kale hayana “Daudi,” na baadhi ya matoleo ya kisasa yameacha hili jina “Daudi.” \f*
\v 4 Badala yake, alimtegemea Mungu wa baba yake, na alitembea katika amri zake, siyo katika tabia ya Israeli.
\v 5 Kwa hiyo Yahwe akaimarisha sheria katika mkono wake; Yuda wote wakaleta kodi kwa Yehoshafati. Alikuwa na utajiri na heshima kubwa.
\v 6 Moyo wake ulikuwa umejikita katika njia za Yahwe. Pia aliziondoa sehemu za juu na Maashera mbali na Yuda.
\p
\v 7 Katika mwaka wa tatu wa utawala wake aliwatuma wakuu wake Ben-haili, Obadia, Zekaria, Nethania, na Mikaya, ili wafundishe katika miji ya Yuda.
\v 8 Pamoja nao walikuwepo Walawi: Shemaya, Nethanieli, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, na Tob-adonia, pamoja nao walikuwepo makuhani Elishama na Yehoramu.
\v 9 Walifundisha katika Yuda, wakiwa na kitabau cha sheria ya Yahwe. Wakaenda karibu miji yote ya Yuda na kufundisha miongoni mwa watu.
\p
\v 10 Hofu ya Yahwe ikashuka juu ya falme zote za nchi, zilizouzunguka Yuda, kwa hiyo hazikufanya vita dhidi ya Yehoshafati.
\v 11 Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi, fedha kama kodi. Waarabu pia wakamletea makundi, 7,700 kondoo waume, na mbuzi 7,770.
\p
\v 12 Yehoshafati akawa na nguvu sana.
\v 13 Akajenga ngome na miji ya maghala katika Yuda. Alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda, na wanajeshsi—imara, wanaume hodari—katika Yerusalemu.
\v 14 Hapa ni rodha yao, wamepangwa kwa majina ya nyumba za baba zo: Kutoka Yuda, maakida wa maelfu; Adna yule jemedari, na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 300,000;
\q
\v 15 akifuatiwa na Yehonani jemedari, na pamoja naye wanaume 280, 00;
\q
\v 16 akifuatiwa na Amasia mwana wa Zikri, ambaye kwa hiari alijitoa kumtumikia Yahwe; na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 200,000.
\q
\v 17 Kutoka Benyamini: Eliada mtu jasiri, na pamoja naye watu 200,000 waliovaa upinde na ngao;
\q
\v 18 akifutiwa na Yehozabadi, na pamoja naye askari 180,000 waliotayari kwa vita.
\v 19 Hawa walikuwa ni wale ambao walimtumikia mfalme, miongoni mwao ambao mfalme aliwaweka katika miji ya ngome katika Yuda yote.
\c 18
\cl Sura 18
\p
\v 1 Sasa Yehoshafati alikuwa na utajiri mwingi na heshima kubwa; alifanya undugu na Ahabu mmoja wa watu wa familia yake akamuoa binti yake.
\v 2 Baada ya miaka kadhaa, akashuka chini kwa Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja kondoo na ngo'mbe wengi kwa ajili ya yake na watu waliokuwa pamoja naye. Ahabu pia akamshawishi kuivamia Ramothi-gileadi pamoja naye.
\v 3 Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwambia Yehoshafati, mfalme wa Yuda, “Utakwenda Ramothi-gileadi pamoja nami?” Yehoshafati akamjibu, “Mimi ni kama wewe, na watu wangu ni kama watu wako; tutakuwa pamoja nawe katika vita.”
\v 4 Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, Tafadhali litafute neno la Yahwe kwanza kwa ajili ya jibu lako”
\p
\v 5 Kisha mfalme wa Israeli akawakusanya manabii pamoja, wanauame mia nne, na akasema kwao, Tutaenda vitani Ramothi-gileadi, au nisiende?” Wakasema, “Vamia, kwa maana Mungu ataitia mkononi mwa mfalme.”
\p
\v 6 Lakini Yehoshafati akasema, “Hakuna nabii mwingine hapa wa Yahwe ambaye kwake tunapaswa kutafuta ushauri?”
\p
\v 7 Mfale wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Bado kuna mtu mmoja amabaye kwake lazima tuutafute ushauri wa Yahwe, Mikaya mwana wa Imla, lakini namchukia kwa sababu yeye huwa hatabiri mema kamwe kunihusu, kila mara maovu,” Lakini Yehoshafati akasema, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”
\p
\v 8 Kisha mfalme wa Israeli akamwita akida na kusema, Haraka mlete Mikaya mwana wa Imla.”
\p
\v 9 Sasa Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wamekaa kila mmoja katika kiti cha enzi, wamevalia kanzu zao, katika sehemu ya uwazi katika maingilio ya lango la Samaria, na manabii wote walikuwa wakitabiri mbele zao.
\p
\v 10 Zedekia mwana wa Kenaani akajitengenezea pembe za chuma na kusema, Yahwe anasema hivi: Kwa kutumia hizi pembe mtawasukuma Waaramu hadi waangamie.”
\v 11 Manabii wote wakatabiri kitu kile kile, wakisema, “Vamia Raamothi-gleadi na shinda. Kwa maana Yahwe ameutia kwenye mkono wa mfalme.”
\p
\v 12 Mjumbe aliyeenda kumuita Mikaya akasema kwake, akisema, “Sasa angalia, maneno ya manabii yanatangaza mambo mema kwa ajili ya mfalme kwa kinywa kimoja. Tafadhali maneno yako yawe kama maneno ya mmoja wao na sema mambo mema.”
\p
\v 13 Mikaya akajibu, “Kama Yahwe aishivyo, mimi nitasema kile ambacho Mungu anasema.”
\p
\v 14 Alipokuja kwamfalme, mfamle akamwambaia, “Mikaya, tutaenda Ramothi -gileadi kwa ajili ya vita, au la?” Mikaya akamjibu, “Vamia na utashinda! Kwa maana utakuwa na ushindi mkuu.”
\p
\v 15 Kisha mfalme akasema kwake, “Ni mara ngapi ninapaswa kukuapisha ili usiniambie kitu chochote isipokuwa kweli katika jina la Yahwe?
\p
\v 16 Kwa hiyo Mikaya akasema, “Niliwaoana Israeli wametawanyika katika mlima, kama kondoo wasio na mchungaji, na Yahwe akasema, hawa hawana mchungaji. Ebu kila mtu arudi nyumbani kwake kwa amani.”
\p
\v 17 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba asingeweza kutabiri mema juu yangu, bali majanga tu?
\p
\v 18 Kisha Mikaya akasema, “Kwa hiyo ninyi nyote mnapashwa kulisikia neno la Yahwe: Nilimuona Yahwe amekaa juu ya kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikuwa yamekaa mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto.
\v 19 Yahwe akasema, Ni nani atakayemrubuni Ahabu, mfalme wa Israeli, ili kwamba aende na kuanguka huko Ramothi-gileadi? Mmoja alisema hivi na mwingine hivi.
\p
\v 20 Kisha roho ikaja moja kwa moja na kusimama mbele ya Yahwe na kusema, Nitamrubuni. Yahwe akamwambia, Kivipi?
\p
\v 21 Roho ikajibu, “nitatoka nje na nitakuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote. Yahwe akajibu, utamrubuni, na pia utafanikiwa. Nenda sasa na fanya hivyo.
\p
\v 22 Sasa ona, Yahwe ameweka roho ya uongo katika midomo ya manabii wako hawa, na Yahwe ametangaza majanga kwa ajili yako.”
\p
\v 23 Kisha Zedekia mwana wa Kenaana, akaja, akampiga kofi mika juu ya shavu, na kusema, “Kwa njia gani Roho wa Yahwe alitoka kwangu ili aseme nawe?”
\p
\v 24 Mika akasema, Angalia, utalijua hilo katika siku hiyo, mtakapokimbia katika baadhi ya vyumba vya ndani kwa ajili ya kujificha.”
\p
\v 25 Mfalme wa Israeli akasema kwa baadhi ya watumishi, “Enyi watu mkamateni Mikaya na mmpeleke hadi Amoni, mkuu wa mji na, na kwa Yoashi, mwanangu.
\v 26 Nanyi mtamwambia, Mfalme anasema: Muweke gerezani huyu mtu na umlishe kwa mkate kidogo tu na maji kidogo tu, mpaka nitakaporudi salama.”
\p
\v 27 Kisha Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, Yahwe hajasema nami.” Kisha akaongeza, “Sikiliza haya, enyi watu wote.”
\p
\v 28 Kwa hiyo Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, mfalme wa Yuda, wakaenda juu ya Ramothi-giledi.
\v 29 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitajibadilisha mwenyewe na kwenda vitani, lakini wewe vaa mavazi yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalame wa Israeli akajibadilisha, na wakaenda vitani.
\p
\v 30 Sasa mfalme wa Aramu alikuwa amewaamuru maakida wa magari yake, akisema, Msiwavamie wanajeshi wasio wa muhimu wala wanajeshi muhimu. Badala yake, mvamieni mfalme wa Israeli pekee,”
\v 31 Ikawa kwamba maakida wa magari walipomuona Yehoshafati wakasema, “Yule ni mfalme wa Israeli.” Wakageuka kumzunguka wamvamie, lakini Yehoshafati akalia, na Yahwe akamsaidia. Mungu akawageuza nyuma kutoka kwake.
\v 32 Ikawa kwamba maakida wa magari walipoona ya kuwa hakuwa mfalme wa Israeli, wakarudi nyuma wasimfukuze.
\p
\v 33 Lakini mtu mmoja akauvuta upinde wake kwa kubahatisha na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya maungio ya mavazi yake. Kisha Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, “Geuza nyuma na nitoe nje ya mapigano, kwa maana nimejeruhiwa vibaya sana.”
\v 34 Mapigano yakazidi kuwa makali siku hiyo, na mfalme wa israeli akashikiliwa katika gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Muda jua lilipokaribia kwenda chini, akafa.
\c 19
\cl Sura 19
\p
\v 1 Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi salama nyumbani kwake Yerusalemu.
\v 2 Kisha Yehu mwana wa Hanani, mwonaji, akatoka kukutana naye na akasema kwa mfalme Yehoshafati, “Unapaswa kuwa unawasaidia waovu? Unapaswa kuwapenda wanaomchukia Yahwe? Kwa ajili ya tendo hili, ghadhabu toka kwa Yahwe iko juu yako.
\v 3 Aidha, kuna baadhi ya mema ya kuonekana ndani yako, kwamba umeziondosha Maashera nje ya nchi, na umeukaza moyo wako kumtafuta Mungu.”
\p
\v 4 Yehoshafati akaishi katika Yerusalemu; na akaenda nje tena miongoni mwa watu wa Beer- sheba hadi nchi ya kilima ya Efraimu na akawarudisha kwa Yahwe, Mungu wa baba zao.
\v 5 Akaweka waamuzi katika nchi katika miji yote ya Yuda yenye ngome, mji kwa mji.
\v 6 Akawaambia waamuzi, “Zingatieni mnachopaswa kufanya, kwa sababu hamuamui kwa ajili ya mwanadamu, bali kwa ajili ya Yahwe; yuko pamoja nanyi katika kazi ya kuamua,
\v 7 Basi sasa iacheni hofu ya Mungu iwe juu yenu. Iweni waangalifu mnapoamua, kwa maana hakuna uovu wa Yahwe Mungu wetu, wala hakuna upendeleo wala hongo.”
\p
\v 8 Vile vile, katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na baahdhi ya viongozi wa nyumba za mababu wa Israeli, kwa ajili ya kufanya hukumu kwa ajili ya Yahwe, na kwa ajili ya migogoro. Wakaishi katika Yerusalemu.
\v 9 Akawaelekeza, akisema, “Lazima mtumike kwa heshima kwa ajili ya Yahwe, kwa uaminifu, na kwa moyo wenu wote.
\v 10 Kila mgogoro wowote utakapokuja kwenu kutoka kwa ndugu zenu wanaoishi katika miji yao, iwe inahusu mauji, iwe inahusu torati na amri, lazima muwaonye, ili kwamba wasiwe na hatia mbele za Yahwe, la sivyo ghadhabu itakuja juu yenu na juu ya ndugu zenu. Mnapaswa kufanya hivyo na hamtakuwa na hatia
\p
\v 11 Ona, Amaria kuhani mkuu yuko juu yenu katika mambo yote ya Yahwe. Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa nyumba ya Yuda, ni kiongozi katika yote katika mambo yote ya mfalme. Pia, Walawi watakuwa wasimamizi wakiwatumikia ninyi. Muwe hodari na tiini maelekezo yenu, na Yahwe awe moja nao walio wema.”
\c 20
\cl Sura 20
\p
\v 1 Ikawa baada ya hayo, kwamba watu wa Moabu na Amoni, na pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja juu ya Yehoshafati ili kupigana vita. \f + \ft Maandishi, “baadhi ya Wameuni,” yanatoa masahihisho kwa ajili ya maandishi ya Kiebrania, ambayo yanasomeka, “baadhi ya Waamoni.” Inadhaniwa kwamba “Wameuni” ndilo neno la asili, na wenye kunukuu walilibadili kuwa “baadhi ya Waamoni.” Lakaini jina hili la mwisho halileti maana, kwa sababu Waamoni tayari wamekwisha tajwa katika mstari huu. Vile vile, matoleo tofauti tofauti yanajihusha na tatizo hili katika namna mbali mbali. \f*
\p
\v 2 Kisha baadhi ya watu wakaja wakamwambia Yehoshafati, wakisema, “Umati mkubwa wanakuja juu yako ng'ambo ya Bahari iliyokufa, kutoka Edomu. Ona, wako Hason- tamari,” ambayo ndiyo En-gedi. \f + \ft Badala ya “Edomu” baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasomeka, “Aramu.” \f*
\v 3 Yehoshafati akaogopa na akajipanga kumtafuta Yahwe. Akatangaza haraka katika Yuda yote.
\v 4 Yuda wakakusanyika pamoja kwa ajili ya kumtafuta Yahwe; wakaja kutoka miji yote ya Yuda kwa ajili ya kumtafauta Yahwe.
\p
\v 5 Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, kwenye nyumba ya Yahwe, mbele ya kibaraza kipya.
\v 6 Akasema, “Yahwe, Mungu wa baba zetu, hauko mbinguni? Wewe siyo mtawala juu ya falme zote za mataifa? Nguvu na uweza viko mkononi mwako, kwa hiyo hakuna anayeweza akukupinga wewe.
\v 7 Mungu wetu, hukuwafukuza nje wakaaji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, na kuitoa milele kwa ajili ya uzao wa Abrahamu?
\v 8 Wakaishi ndani yake na kujenga sehemu takatifu kwa ajili ya jina lako, wakisema,
\v 9 Ikiwa janga litakuja juu yetu —upanga, hukumu, au ugonjwa, au njaa—tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako (kwa maana jina lako limo ndani ya nyumba hii), na tutakulilia wewe katika mateso yetu, na utatusikia na kutuokoa. \f + \ft Badala ya “hukumu” baadhi ya maandiko ya zamani yanasema “mafuriko.” \f*
\pi
\v 10 Tazama sasa, hapa kuna watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri ambao hukuwaacha Israeli wawapige walipotoka nchi ya Misri; badala yake, Israeli waliwageukia mbali na hawakuwaangamiza.
\v 11 Ona jinsi wanavyotuzawadia; wanakuja kututoa nje ya nchi yako ambayo umetupa kuirithi.
\v 12 Mungu wetu, hutawahukumu? Kwa maana hatuna nguvu dhidi ya hili jeshi kubwa ambalo linakuja juu yetu. Hatujui cha kufanya, lakini macho yetu yako kwako.
\p
\v 13 Yuda wote wakasimama mbele ya Yahwe, pamoja na wadogo wao, wake, na watoto.
\p
\v 14 Kisha kati kati ya kusanyiko, roho ya Yahwe ikaja juu ya Yahazieli, mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, mwana, Mlawi, mmoja wa wana wa Asafu.
\v 15 Yahazieli akasema, “Sikilizeni, Yuda wote na ninyi wakaaji wa Yerusalemu, na Mfalme Yehoshafati. Hivi ndivyo Yahwe asemavyao kwenu, Msiogope: msivunjike moyo kwa sababu ya hili jeshi kubwa, kwa maana vita siyo yenu, bali ni ya Mungu.
\v 16 Lazima mwende chini juu yao kesho, Ona, wanakuja wakipanda kupita njia ya Sisi. Mtawakuta mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli.
\v 17 Hamtahitaji kupigana katika vita hii. Simameni katika nafasi zenu, simameni wima, na muone wokovu wa Yahwe pamoja nanyi, Yuda na Yerusalemu. Msiogope wala kukata tamaa. Tokeni nje juu yao kesho, kwa maana yuko pamoja nanyi.”
\p
\v 18 Yehoshafati akainamisha kichwa chake pamoja na uso wake chini. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakaanguka chini mbele za Yahwe, wakimwabudu yeye.
\v 19 Walawi, wale wa uzao wa Wakohathi na wa uzao wa Wakorahi, wakasimama juu kumsifu Yahwe, Mungu wa Israeli, kwa sauti kubwa sana.
\p
\v 20 Asubuhi mapema wakasimama na kwenda nje kwenye bonde la Tekoa. Walipokuwa wakienda nje, Yehoshafati akasimama na kusema, “Nisikilizeni, Yuda, na ninyi wakaaji wa Yerusalemu! Aminini katika Yahwe Mungu wenu, na mtasaidiwa. Aminini katika manabii zake, na mtafanikiwa.
\v 21 Alipokuwa ameshauriana na watu, akawachagua wale ambao wangemwimbia Yahwe na kumpa sifa kwa ajili ya utukufu wake mtakatifu, walipokuwa wakienda wakilitangulia jeshi, na kusema, “Mshukuruni Yahwe, kwa maana uaminifu wa agano lake unadumu milele.”
\p
\v 22 Walipoanza kuimba na kusifu, Yahwe akapanga wanaume katika mavamizi juu ya watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri, ambao walikuwa wanakuja dhidi ya Yuda. Walishindwa.
\v 23 Kwa maana watu wa Aamoni na Moabu walisimama kupigana na wakaaji wa Mlima Seiri, ili kuwaua kabisa na kuwangamiza. Waliapokuwa wamemaliza kuwaangamiza wakaaji wa Mlima Seiri, wote wakasaidiana kuangamizana kila mmoja.
\p
\v 24 Yuda walipokuwa katika sehemu hiyo wakiangalia jangwani, waliangalia nje juu ya jeshi. Tazama, walikuwa wamekufa, wameanguka chini; hakuna aliyekuwa amepona.
\p
\v 25 Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara kutoka kwa hao watu, walikuta miongoni mwao bidhaa nyingi, nguo, na johari za thamani, ambazo walizichukua kwa ajili yao wenyewe, nyingi kuliko uwezo wao wa kubeba. Iliwachukua siku tatu kusomba nyara hizo, zilikuwa nyingi sana. \f + \ft Badala ya “miongoni mwao,” baadhi ya maandishi ya zamani na ya kisasa yanasema, “ng'ombe.” badala ya “nguo” baadhi ya maandiko ya kale na ya kisasa yanasema, “miili iliyokufa.” \f*
\v 26 Katika siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka, huko wakamsifu Yahwe, kwa hiyo jina la sehemu hiyo hata leo ni “Bonde la Baraka.”
\p
\v 27 Kisha, wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati katika uongozi wao, kwenda tena Yerusalemu kwa furaha, kwa maana Yahwe alikuwa amewafanya wafurahie juu ya adui zao.
\v 28 Wakaja Yerusalemu na kwenye nyumba ya Yahwe kwa vinanda, vinubi matarumbeta.
\p
\v 29 Hofu ya Yahwe ikawa juu ya falme zote za mataifa waliposikia kwamba Yahwe amepigana dhidi ya adui wa Israeli.
\v 30 Kwa hiyo ufalme wa Yehoshafati ulikuwa mtiivu, kwa maana Mungu wake alimpa amani kuzunguuka pande zake zote.
\p
\v 31 Yehoshafati akatawala juu ya Yuda: Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala. Jina la mama yake aliitwa Azubahi, binti wa Shilhi.
\v 32 Akatembea katika njia za Asa, baba yake; hakugeuka popote kuziacha; akafanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe.
\v 33 Vile vile, sehemu za juu hazikuwa zimeondoshwa mbali. Watu walikuwa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa babu zao.
\p
\v 34 Kwa mambo mengine kuhusu Yehoshafati, mwanzo na mwisho, tazama, yameandikwa katika historia ya kitabu cha wafalme wa Israeli.
\p
\v 35 Baada ya hayo, Yehoshafati, mfalme wa Yuda, akapatana na Ahazia, mfalme wa Israeli, ambaye alitenda uovu mwingi.
\v 36 Akapatana naye kujenga meli za kwenda Tarshishi; Wakazijenga meli hizo huko Esion-geberi.
\v 37 Kisha Eliezeli, mwana wa Dadavahu wa Maresha, akatoa unabii juu ya Yehoshafati; akasema, “kwa sababu umepatana na Ahazia, Yahwe ameiharibu miradi yako.” Meli zilivunjika ili kwamba zisiweze kusafiri.
\c 21
\cl Sura 21
\p
\v 1 Yehoshafati akalala pamoja na babu zake na kuzikwa pamoja nao katika mji wa Daudi;
\v 2 Yehoramu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoramu alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati: Azaria, Yerieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli, na Shefatia. Wote hawa walikuwa wana wa Yehoshafati, mfalme wa Israeli.
\v 3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi kubwa ya fedha, dhahabu, na vitu vingine vya thamani, na miji yenye ngome katika Yuda, lakini kiti cha enzi alimpa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza.
\p
\v 4 Sasa Yehoramu alipokuwa ameinuka katika ufalme wa baba yake na kujiimarisha mwenyewe kama mfalme, akawaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia viongozi wengine mbali mbali wa Israeli.
\v 5 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, na akatawala kwa miaka minane katika Yerusalemu.
\v 6 Akatembea katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa maana alikuwa na binti Ahabu kama mke wake, na akafanya yaliyo maovu katika macho ya Yahwe.
\v 7 Vile vile, Yahwe hakutaka kuiangamiza nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano ambalo alikuwa amefanya na Daudi; alikuwa ameahidi kwamba siku zote angetoa uzima kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vyake.
\p
\v 8 Katika siku za Yehoramu, Edomu wakaasi wasiwe chini ya Yuda, na wakajisimamishia mfalme juu yao.
\v 9 Kisha Yeroboamu akavuka ng'ambo pamoja na maakida na magari yake yote. Ilikuwa usiku aliposimama na kupigana dhidi ya Waedomu ambao walikuwa wamemzunguka na maakida wa magari yake.
\v 10 Kwa hiyo Edomu iliasi kutoka kuwa chini ya Yuda mpaka leo. Libna piaaliasi wakati ule ule wasiwe chini yake. Kwa sababu Yehoramu alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa baba zake.
\p
\v 11 Zaidi ya hayo, Yehoramu pia alikuwa amezijenga sehemu zake za juu katika milima ya Yuda na akawafanya wakaaji wa Yuda kuishi kama makahaba, na akawaongoza Yuda katika upotevu.
\p
\v 12 Barua kutoka kwa nabii Eliya ikaja kwa Yerohamu. Ilisema, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi, babu yako, anasema: Kwa sababu hujatembea katika njia za Yehoshafafati, baba yako, wala katika njia za Asa, mfalme wa Yuda,
\v 13 bali umetembea katika njia za wafalme wa Israeli, na umewafanya Yuda na wakaaji wa Yerusalemu kuenenda kama kahaba, kama nyumba ya Ahabu walivyofanya—na kwa sababu pia umewaua ndugu zako katika familia ya baba yako kwa upanga, watu waliokuwa bora kuliko wewe mwenyewe—
\v 14 ona, Yahwe atawapiga watu wako na pigo kubwa, watoto wako, wake zako, na mali zako zote.
\v 15 Wewe mwenyewe utakuwa na ugonjwa mwingi kwa sababu ya ugonjwa katika utumbo wako, mpaka utumbo wako uanguke nje kwa sababu ya ugonjwa, siku baada ya siku.
\p
\v 16 Yahwe akaichochea roho ya Wafilisiti dhidi ya Yuda na ya Waarabu waliokuwa karibu na Waethiopia.
\v 17 Wakaivamia Yuda, wakavamia katika nyumba ya mfalme. Pia wakawachukua wanaye na wake zake. Hakuna mwana aliyebakizwa kwa ajili yake ispokuwa, Yehoshafati, mwanaye mdogo.
\p
\v 18 Baada ya haya yote, Yahwe akampiga katika utumbo wake kwa ugonjwa usiopona.
\v 19 Ikawa wakati ulipofika, katika mwisho wa miaka miwili, kwamba utumbo wake ukaaanguka nje kwa sababu ya ugonjwa wake, na kwamba akafa kwa ugonjwa mkali. Watu wake hawakutengeneza moto kwa ajili ya heshima yake kama walivyokuwa wamefanyia baba zake.
\p
\v 20 Alikuwa ameanza kutawala alipokuwa na umri wa miaka thelathini na mbili; akatawala katika Israeli kwa miaka minane, na alikufa bila kuombolezwa. Wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya kifalme.
\c 22
\cl Sura 22
\p
\v 1 Wakaaji wa Yerusalemu wakamfanya Ahazia, mwana mdogo wa Yehoramu, mfalme katika nafasi yake, kwa maana kundi la watu ambalo lilikuja na Waarabu katika ngome lilikuwa limewauwa wanaye wakubwa wote. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akawa mfalme.
\p
\v 2 Ahazia alikuwa na umri wa miaka arobaini na mbili alipoanza kutawala; alitawala kwa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Athalia; alikuwa binti Omri.
\p
\v 3 Pia Ahazia alitembea katika njia za nyumba ya Ahabu kwa maana mama yake alikuwa mshauri katika kufanya mambo maovu.
\v 4 Ahazia alifanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama nyumba ya Ahabu walivyokuwa wakifanya, kwa maana walikuwawashauri wake baada ya kifo cha baba yake, hadi kuangamia kwake.
\v 5 Pia aliufuata ushauri wao; akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, kwa ajili ya kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu, huko Ramothi-gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu.
\p
\v 6 Yoramu akarudi Yezreeli kwa ajili ya kuponywa majeraha ambayo walipata huko Rama, alipopigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akaenda chini Yezreeli ili kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.
\p
\v 7 Sasa uharibifu wa Ahazia ulikuwa umeletwa na Mungu kupitia kutembelewa na Yoramu. Alipokuwa amewasili, alienda pamoja na Yeharamu ili kumvamia Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Yahwe alikuwa amemchagua kwa ajili ya kuiangamiza nyumba ya Ahabu.
\v 8 Ikawa kwamba, Yehu alikuwa akichukua hukumu ya Mungu juu ya nyumba ya Ahabu, kwamba aliwakuta viongozi wa Yuda na wana wa ndugu zake Ahazia wakimtumikia Ahazia. Yehu akawauwa.
\v 9 Yehu akamtafuta Ahazia; Wakamkamata akiwa amejificha katika Samaria, wakamleta kwa Yehu, na wakamuua. Kisha wakamzika, kwa maana walisema, “Ni mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Yahwe kwa moyo wake wote.” Kwa hiyo nyumba ya Ahazia haikuwa na nguvu zaidi kwa ajili ya kuutawala ule ufalme.
\p
\v 10 Sasa Athalia, mama wa Ahazia, akaona kwamba mwanaye alikuwa amekufa, akainuka na kuwaua watoto wote wa kifalme katika nyumba ya Yehu.
\v 11 Lakini Yehoshaba, binti wa mfalme, akamchukua Yoashi, mwana wa Ahazia, na akamvutia mbali kutoka miongoni mwa wana wa mfalme ambao waliuawa. Akamuweka yeye na mlezi wake katika chumba cha kulala. Kwa hiyo Yehoshaba, binti wa mfalme Yehoramu, mke wa Yehoiada kuhani (kwa maana alikuwa dada yake Ahazia), akamficha asimuone Athalia, kwa hiyo Athalia hakumuua.
\v 12 Alikuwa pamoja nao, wakiwa wamejificha katika nyumba ya Mungu kwa miaka sita, Athalia alipotawala juu ya Yuda.
\c 23
\cl Sura 23
\p
\v 1 Katika mwaka wa saba, Yehoyada alionesha nguvu zake na akaingia katika agano na maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
\v 2 Wakaenda katika Yuda na kuwakusanya Walawi kutoka miji yote ya Yuda, vile vile na wakuu wa nyumba za mababu wa Israeli, na wakaja hadi Yerusalemu.
\v 3 Kusanyiko lote wakafanya aganao na mfalme katika nyumba ya Mungu. Yehoyada akawaambia, “Ona, mwana wa mfalme atatawala, kama Yahwe alivyosema kuhusu uzao wa Daudi.
\p
\v 4 Hivi ndivyo mtakavyo fanya: theluthi yenu makuhani na Walawi ambao huja kuhudumu siku ya Sabato, mtakuwa walinzi katika milango.
\v 5 Theluthi nyingine mtakuwa katika nyumba ya mfalme, na theluthi nyingine mtakuwa katika Msingi wa Lango. Watu wote watakuwa katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.
\v 6 Msimruhusu yeyote kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, isipokuwa makuhani na Walawi wanaotumika. Wanao weza kuingia kwa sababu inawahusu.
\v 7 Lakini watu wengine wote lazima mtii amri ya Yahwe. Walawi lazima wamzunguuke mfalme pande zote, kila mtu na silaha zake mkononi mwake. Yeyote atakayeingia katika nyumba, atauawa. Kaeni na mfalme aingiapo ndani na atokapo nje.”
\p
\v 8 Kwa hiyo Walawi na Yuda wote walitumika kwa kila njia kama katika namna ambayo Yehoyada kuhani aliwaamuru. Kila mmoja alichukua watu wake, wale waliotakiwa kuja ndani kuhudumu katika Sabato, na wale watakaoondoka siku ya Sabato, kwa maana
\v 9 Yehoyada, kuhani, hakuwa amezuilia mojawapo ya zamu zao. Kisha Yeliyadaya, kuhani, akaleta kwa maakida mikuki na ngao ndogo na kubwa zilizokuwa za mfalme Daudi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mungu.
\v 10 Yehoyada akawaleta wanajeshi wote, kila mtu na mkuki wake katika mkono wake, upande wa kulia wa hekalu hadi upande wa kushoto wa hekalu, pembeni mwa madhabahu na hekalu, wakimzunguka mfalme.
\p
\v 11 Kisha wakamleta nje mwana wa mfalme, wakaiweka taji juu yake, na kumpa agano la sheria. Kisha wakamfanya mfalme, na Yehoyda na wanaye wakampaka mafuta. Kisha wakasema, “Aishi maisha marefu mfalme.”
\p
\v 12 Athalia aliposikia kelele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akatoka ili awaone watu katika nyumba ya Yahwe.
\v 13 Na akaangalia, na, tazama, mfamle alikuwa amesimama karibu na nguzo yake katika lango la, kuingilia na maakida na wapuliza tarumbeta walikuwa karibu na mfame. Watu wote wa nchi walikuwa wakifurahia na kupuliza tarumbeta na waimbaji walikuwa wakipiga vyombo vya muziki na kuongoza nyimbo za kusifu. Kisha Athalia akayararua mavazi yake na kupiga kelele. “Fitina! Fitina!”
\p
\v 14 Kisha Yehoyada, kuhani, akawaleta nje maakida wa mamia waliokuwa juu ya jeshi na kusema, “Mleteni nje kati ya safu, yeyote atakayemfuata, auwawe kwa upanga.” Kwa maana kuhani alikwishasema, “Msimuue katika nyumba ya Yahwe.”
\v 15 Kwa hiyo wakafanya njia kw ajili yake, na akaenda kwenye nyumba ya mfalme kupita njia ya Lango la Farasi, na huko wakamuuwa.
\v 16 Kisha Yehoyada alifanya agano kati yake mwenyewe, watu wote, na mfalme, kwamba watakuwa watu wa Yahwe.
\v 17 Kwa hiyo watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. Wakazivunja vipande vipande madhabahu za Baali na sanamu zake, na wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu hizo.
\p
\v 18 Yehoyada akateua wakuu kwa ajili ya nyumba ya Yahwe chini ya mkono wa makuhani, ambao walikuwa Walawi, ambao Daudi alikuwa amewapanga kwenye nyumba ya Yahwe, ili wamtolee Yahwe sadaka za kuteketezwa, kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, pamoja na kushangilia na kuimba, kama alivyotoa maelekezo Daudi.
\v 19 Yehoyada akaweka walinzi katikamalango ya nyumba ya Yahwe, ili kwamba kwa namna yoyote ile asiingie mtu asiyesafi.
\p
\v 20 Yehoyada akachukua pamoja naye maakida wa mamia, watu wakubwa, watawala wa watu, na watu wote wa nchi. Akamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe; watu wakaja kwenye nyumba ya mfalme kupitia Lango la juu na kumkalisha mfalme juu ya kiti cha enzi cha ufalme. \f + \ft Baadhi ya maandiko ya kisasa yanasema, “wakamshusha chini mfalme.” \f*
\v 21 Kwa hiyo watu wote wa nchi wakafurahia, na mji wote ulikuwa kimya. Kuhusu Asa walikuwa wamemuua kwa upanga.
\c 24
\cl Sura 24
\p
\v 1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala kwa miaka arobaini katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba.
\v 2 Yoashi alifanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe siku zote za Yehoyada, yule kuhani.
\v 3 Yehoyada akajichukulia wake wawili kwa ajili yake, na akawa baba wa wana na mabinti.
\p
\v 4 Ikawa baada ya haya, kwamba Yoashi aliamua kuitengeneza nyumba ya Yahwe.
\v 5 Akawakusanya pamoja makuhani na Walawi, na kusema kwao, “Nendeni nje kila mwaka kwenye miji ya Yuda na kukusanya fedha kutoka Israeli yote kwa ajili ya kuikarabati nyumba ya Mungu wenu. Hakikisheni kwamba mnaanza haraka.” Walawi hawakufanya kitu kwanza.
\p
\v 6 Kwa hiyo mfalme akamuita Yehoyada, yule kuhani, na kumwambia, “Kwa nini hukuwaagiza Walawi kuleta kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyoagizwa na Musa mtumishi wa Yahwe na kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya amri za hema ya agano?”
\p
\v 7 Kwa maana wana wa Athalia, yule mwanamke muovu, walikuwa wameivunja nyumba ya Mungu na kuwapa Mabaali vitu vyote vitakatifu vya nyumba ya Yahwe.
\p
\v 8 Kwa hiyo mfalme aliamuru, na wakatengeneza kasha na kulileta nje kwenye lango kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 9 Kisha wakafanya tangazo katika Yuda na Yerusalemu, kwa ajili ya watu kuleta kwa Yahwe kodi aliyoiagiza Musa mtumishi wa Mungu juu ya Israeli jangwani.
\v 10 Viongozi wote na watu wote wakafurahia na wakaleta fedha na kuiweka kwenye kasha hadi walipomaliza kulijaza.
\v 11 Ikatokea kwamba kila lilipoletwa kasha kwa mikono ya Walawi kwa wakuu wa mfalme, na kila walipoona kwamba kulikuwa na fedha nyingi sana ndani yake, waandishi wa mfalme na mkuu wa kuhani mkuu walikuja, kulihamishia fedha kasha, na kulirudisha sehemu yake. Walifanya hivyo siku baada siku, wakikusanya kiasi kikubwa cha fedha.
\v 12 Mfalme na Yehoyada akawapa zile fedha wale waliofanya kazi ya kuhudumu katika nyumba ya Yahwe, Watu hawa waliwaajiri waashi na maseremala ili waijenge nyumba ya Yahwe, na pia wale waliofanya kazi katika chuma na shaba.
\p
\v 13 Kwa hiyo wafanya kaziwakafanya kazi, na kazi ya kukarabati ikasonga mbele mikononi mwao; wakaisimamisha nyumba ya Mungu katika hali yake halisi na kuiimarisha.
\v 14 Walipomaliza, wakaleta fedha zilizobaki kwa mfalme na Yehoyada. Fedha hizo zilitumika kutengenezea samani kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vyombo vya huduma na kutolea dhabihu—vijiko na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa bila kukoma katika nyumba ya Yahwe kwa siku zote za Yehoyada.
\p
\v 15 Yehoyada akazeeka na alikuwa amejaa siku, na kisha akafa; alikuwa na umri wa mika 130 alipokufa.
\v 16 Wakamzika katika mji wa Daudi miongoni mwa wafalme, kwa sababu alikuwa amefanya mema katika Israeli, kwa Mungu, na kwa ajili ya nyumba ya Mungu,
\p
\v 17 Sasa baada ya kifo cha Yehoyada, kiongozi wa Yuda akaja na kutoa heshima kwa mfalme. Kisha mfalme akawasikiliza.
\v 18 Wakaiacha nyumba ya Yahwe, Mungu wa baba zao, na kuwaabudu miungu na maashera na sanamu. Ghadhabu ya Mungu ikaja juu ya Yuda na Yerusalemu kwa sababau ya hili kosa lao.
\v 19 Bado akatuma manabii kwao ili kuwaleta tena kwake, Yahwe, manabii wakatangaza juu ya watu, lakini walipuuza kusikiliza.
\p
\v 20 Roho wa Mungu akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada, yule kuhani; Zekaria akasimama juu ya watu na kusema kwao, “Mungu anasema hivi: Kwa nini mnazivunja amri za Yahwe, ili kwamba msifanikiwe? Kwa kuwa mmemsahau Yahwe, pia amewasahau ninyi.”
\p
\v 21 Lakini wakapanga njama dhidi yake; kwa amri ya mfalme, wakampiga kwa mawe katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.
\v 22 Katika namna hii hii, Yoashi, yule mfalme, akapuuza ukarimu ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alikuwa amemfanyia.
\p
\v 23 Ikawa karibu mwisho wa mwaka, kwamba jeshi la Aramu wakaja juu yake Yoashi. Wakaja Yuda na Yerusalemu; wakawaua viongozi wote wa watu na kupeleka nyara zote kutoka kwao kwa mfalme wa Dameski.
\v 24 Jeshi la Waaramu walikuwa wamekuja na jeshi dogo, lakini Yahwe akawapa ushindi juu ya jeshi kubwa, kwa sababu Yuda alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao. Katika namna hii Waaramu wakaleta hukumu juu ya Yoashi.
\v 25 Katika muda ambao Waaramu walikuwa wameondoka, Yoashi alikuwa amejeruhiwa vikali. Watumishi wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu ya mauaji ya wana wa Yehoyada, yule kuhani. Wakamuua katika kitanda chake, na akafa; wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya wafalme.
\p
\v 26 Hawa walikuwa watu waliopanga njama dhidi yake: Zabadi mwana wa Shimeathi, Mwamoni; na Yehozabadi mwana wa Shimrithi, Mwanamke Mmoabu.
\v 27 Sasa matukio kuhusu wanaye, unabii muhimu uliokuwa umesemwa kumhusu yeye, na kujengwa tena kwa nyumba ya Mungu, ona, yameandikwa katika Kamusi ya kitabu cha wafalme. Amazia mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\c 25
\cl Sura 25
\p
\v 1 Amaza alikuwa na umri wa miaka ishirini na na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yehoadani, wa Yerusalemu.
\v 2 Alifanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, lakini siyo kwa moyo uliojitoa kikamilifu.
\v 3 Ikawa kwamba mapema utawala wake ulipokuwa umeimarika, aliwaua watumishi ambao walikuwa wamemuua baba yake, mfalme.
\v 4 Lakini hakuwaua watoto wa wale wauaji, bali alitenda kama kama ilivyo andikwa katika sheria, katika kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamuru. “Baba hatajuta kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatakufa kwa ajili ya baba zao. Badala yake, kila mtu lazima afe kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
\p
\v 5 Aidha, Amazia aliwakusanya Yuda pamoja, na akawaandikisha kwa kufuata nyumba za baba zao, chini ya maakida wa maelfu na maakida wa mamia --wote wa Yuda na wa Benjamini. Akawahesabu kuanzia wa mika ishirini na kuendelea, na akawaona wako 300,000 wanaume waliochaguliwa, wawezao kwenda vitani, walioweza kushika mkuki na ngao.
\v 6 Pia alikodi wanaume wa kupigana 100,000 kutoka Israeli kwa fedha mia moja.
\p
\v 7 Lakini mtu wa Mungu alikuja kwake na kusema, “Mfalme, usiliache jeshi la Israeli kwenda nawe, kwa maana Yahwe hayupo pamoja na Israeli -wala na mtu Yeyote wa Efraimu.
\v 8 Lakini hata kama mtaenda na mkiwa wenye ushupavu na imara katika vita, Mungu atawatupa chini mbele ya adui, kwa maana Mungu ana nguvu za kusaidia, na nguvu za kurusha chini.”
\p
\v 9 Amazia akasema kwa mtu wa Mungu, “Lakini tutafanyaje kuhusu talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Yahwe ana uwezo wa kukupa vingi zaidi kuliko hivyo.”
\p
\v 10 Kwa hiyo Amazia akalitenganisha jeshi lilokuja kwake kutoka Efraimu; akawarudisha nyumbani tena. Hivyo hasira yao iliwaka sana dhidi ya Yuda, na walirudi nyumbani kwa hasira kali.
\p
\v 11 Amazia akajipa ujasiri na kuwaongoza watu wake kwenda nje kwenye bonde la chumvi, huko akawashinda wanaume elfu kumi wa Seiri.
\v 12 Jeshi la Yuda likawachukua elfu kumi wengine wakiwa hai. Wakawapeleka juu ya mwamba na kuwarusha chini kutoka huko, hivyo wote wakavunjika vunjika katika vipande.
\p
\v 13 Lakini watu wa jeshi ambalo Amazia alilirudisha, ili kwamba wasiende naye vitani, wakauvamia mji waYuda kuanzia Somaria hadi Beth- horoni. Wakawapiga watu elfu tatu na kuwateka wengi sana.
\p
\v 14 Sasa ikawa kwamba baada ya Amazia kurudi kutoka kuwachinja Waedomu, akaileta miungu ya watu wa Seiri, na kuisimamisha iwe miungu yake. Akainama chini mbele ya hiyo miungu na kuitolea sadaka za uvumba.
\v 15 Hivyo hasira ya Yahwe ikawaka dhidi ya Amazia. Akamtuma nabii kwake, ambaye alisema, “Kwa nini umeitafuta miungu ya watu ambayo haikuwaokoa hata watu wake yenyewe dhidi ya mkono wako?”
\p
\v 16 Ikawa kwamba yule nabii alipokuwa anaongea naye, mfalme akamwambia, “Je, wewe tumekufanya kuwa mshauri wa mfalme? Acha! Kwa nini ujitakie kuuawa?” Kisha nabii akaacha na kusema, ninajua kwamba Mungu ameamua kukuangamiza kwa sababu umefanya tendo hili na hujasikiliza ushauri wangu.”
\p
\v 17 Kisha Amazia akashauriana na washauri na kutuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israel. Akisema, “Njoni, tukutane uso kwa uso katika vita.”
\p
\v 18 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi ulioko Lebanoni, ukisema, Mtoe binti yako kwa mwanangu awe mke wake; lakini akapita hayawani katika Lebanoni akatembea na kuukanyaga chini mbaruti.
\v 19 Umesema, Ona, nimeipiga Edomu, na moyo wako umekuinua juu. Jipe fahari katika ushindi wako, lakini ukae nyumbani, kwa maana ni kwa nini ujisababishie matatizo mwenyewe na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?
\p
\v 20 Lakini Amazia hakusikiliza, kwa sababu tukio hili lilikuwa limetoka kwa Mungu, ili awatie Waisraeli katika mkono wa adui zao, kwa sababu walikuwa wametafuta ushauri kutoka kwa miungu ya Edomu.
\v 21 Kwa hiyo, Yehoashsi, mfalme wa Israeli, akavamia; yeye na Amazia, mfalme wa Yuda, wakakutana uso kwa uso huko Beth -shemishi, ulioko Yuda.
\v 22 Yuda akashindwa mbele za Israeli, na kila mtu akarudi nyumbani.
\v 23 Yehoashi, mfalme wa Israeli, akamkamata Amazia mwana wa Yehoashi mwana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, huko Beth - shemeshi. Akamleta Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi kona ya Lango, umbali wa mikono mia nne.
\v 24 Akachukua dhahabu na fedha zote, vitu vyote vilivyoonekana akatika nyumba aya Mungu kwa Obedi Edomu, na vitu vya thamani katika nyumba ya mfalme, na mateka pia, na akarudi Samaria.
\p
\v 25 Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.
\v 26 Kwa mambo mengine kuhusu Amzia, mwanzo na mwisho, tazama, je, hayajaandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli?
\v 27 Sasa kutoka wakati ambao Amazia aligeukia mbali asimfuate Yahwe, walianza kupanga njamadhidi yake katika Yerusalemu. Akakimbilia Lachishi, lakini wakatuma watu nyuma yake wamfuate Lachishsi na walimuua huko.
\v 28 Wakamleta juu ya farasi na wakamzika pamoja na baba zake katika Mji wa Yuda.
\c 26
\cl Sura 26
\p
\v 1 Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia, ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake Amazia.
\v 2 Ndiye aliyeijenga tena Elathi nakuirejesha kwa Yuda. Baada ya hapo mfalme akalala pamoja na baba zake.
\p
\v 3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala. Akatawala miaka ishirini na mbili katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yekolia; alikuwa wa Yerusalemu.
\v 4 Akafanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, akiufuata mfano wa baba yake, katika kila jamabo.
\v 5 Alijitoa kumtafuta Mungu katiaka siku za Zekaria, ambaye alimpa maelekezo kwa ajili ya kumtii Mungu. Kadri alivyomtafuta Yahwe, Mungu alimfanikisha.
\p
\v 6 Uzia akaenda na kupigana dhidi ya Wafilisti. Akaubomoa ukuta wa mji wa Gathi, Yabne, na Ashdodi; akajenga miji katika nchi ya Ashdodi na miongoni mwa Wafilisti.
\v 7 Mungu akaamsaidia dhidi ya Wafilisti, dhidi ya Waarabu waliokuwa wakiishi Gur - baali, na dhidi ya Wameuni.
\v 8 Waamoni wakalipa kodi kwa Uzia, na umaarufu wake ukaenea, hata kufika maingilio ya Misiri, kwa sababu alikuwa ameanza kuwa maarufu.
\p
\v 9 Zaidi ya hayo, Uzia akajenga minara katika Yerusalemu katika kona ya Lango, kwenye Lango la Bonde, na kwenye kona ya ukuta, na akavizungushia ngome.
\v 10 Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.
\p
\v 11 Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi la wanaume wa kupigana vita ambao walienda vitani katika makundi ambayo idadi yake ilikuwa imehesabiwa na Yeieli, mwandishi. Na Maaseya, afisa, chini ya mamlaka ya Hanania, mmoja wa maamri jeshi wa mfalme.
\v 12 Jumla ya wakuu wa nyumba za mababu, watu wa kupigana vita, walikuwa 2,600.
\v 13 Chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la watu 307,500 ambao walifanya vita kwa nguvu ili kumsaidia mfalme idi ya maadui.
\v 14 Uzia akaandaa kwa ajili yao—kwa ajili ya jeshi lote — ngao, mikuki, chapeo, deraya za majini, nyuta, na mawe ya kurusha.
\v 15 Katka Yerusalemu alijenga mitambo, iliyobuniwa na watu wenye ujuzi, ili iwe juu ya minara na juu ya buruji, kwa ajili ya kurushia mishale na mawe makubwa. Umaarufu wake ukaenea hadi nchi za mbali, kwa maana alisaidiwa sana hadi alipokuwa na nguvu sana.
\p
\v 16 Lakini Uzia alipokuwa amekuwa na nguvu nyingi, moyo wake ulijiinua akatenda kwa uovu; akafanya makosa zidi ya Yahwe, Mungu wake, kwa maana alienda kwenye nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kufukiza uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
\v 17 Azaria, kuhani, akamfuata, na pamoja naye makuhani themanini wa Yahwe, ambao walikuwa watu wenye ujasiri.
\v 18 Walimzuia Uzia, mfalme, na wakasema kwake, “Siyo jukumu lako, Uzia, kumtolea Yahwe uvumba, bali ni kazi ya makuhani, wana wa Haruni, amabao wametengwa kwa ajili ya kutoa sadaka za uvumba. Toka nje ya sehemu takatifu, kwa maana huna uaminifu na hautaheshimiwa na Yahwe Mungu.”
\p
\v 19 Kisha Uzia akakasirika. Alikuwa ameshikilia chetezo mkononi kwa ajili ya kufukiza uvumba. Wakati alipowaghadhabikia makuhani, ukoma ukatokea juu ya uso wake mbele ya makuhani katika nyumba ya Yahwe, pembeni mwa madhabahu ya uvumba.
\v 20 Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamwangalia, na, tazama, alikuwa amepatwa na ukoma juu ya uso wake. Walimwondoa pale haraka. Kwa hakika, aliharakisha kwenda nje, kwa maana Yahwe alikuwa amempiga.
\p
\v 21 Uzia, mfalme, alikuwa mwenye ukoma hadi siku ya kufa kwake na aliishi katika nyumba ya kutengwa tangu alipokuwa mwenye ukoma, kwa maana alitengwa na nyumba ya Yahwe. Yothamu, mwanaye, alikuwa mkuu wa nyumba ya mfalme na aliwatawala watu wa nchi.
\p
\v 22 Mambo mengine kuhusu Uzia, mwanzo na mwisho, yako katika kile ambacho Isaya, mwana wa Amozi, nabii, aliandika.
\v 23 Kwa hiyo Uzia akalala pamoja na baba zake; walimzika pamoja na baba zake katika uwanja wa maziko wa Mfalme, kwa maana walisema, “Ni mwenye ukoma.” Yothamu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\c 27
\cl Sura 27
\p
\v 1 Yothamu alikuwa na umri wa mika ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yerusha; alikuwa binti Sadoki.
\v 2 Akafanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe, akiufuata mfano wa baba yake, Uzia, katika mambo yote. Pia alijiepusha kuingia katika hekalu la Yahwe. Lakini watu bado walikuwa wanaenda katika njia za uovu.
\p
\v 3 Akalijenga tena lango la juu la nyumba ya Yahwe, na juu ya kilima cha Ofeli akajenga sana.
\v 4 Vile vile alijenga miji katika kilima cha Yuda, na katika msitu alijenga ngome na minara.
\p
\v 5 Pia alipigana na mfalme wa watu wa Amoni na akawashinda. Katika mwaka huo huo, watu wa Amoni walimpa talanta mia moja za fedha, kori elfu kumi za ngano, kori elfu kumi za shayiri. Watu wa Amoni wakampa hivyo hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.
\p
\v 6 Kwa hiyo Yothamu akawa na nguvu sana kwa sababu alitembea imara mbele za Yahwe Mungu wake.
\p
\v 7 Kwa mambo mengine kuhusu Yothamu, vita vyake vyote, na njia zake zote, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
\v 8 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi na sita katika Yerusalemu.
\v 9 Yothamu akalala pamoja na baba zake, na wakamzika katika mji wa Daudi. Ahazi, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\c 28
\cl Sura 28
\p
\v 1 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Hakufanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi babu yake alivyokuwa amefanya.
\v 2 Badala yake, alitembea katika njia za wafalme wa Israeli; pia alitengeneza sanamu za kusubu kwa ajila ya Mabaali.
\v 3 Zaidi ya hayo, akafukiza uvumba katika bonde la Beni Hinomu na akawaweka watoto wake ndani ya moto, kwa mjibu wa desturi za uzinzi za watu ambao Yahwe aliwafukuza nje ya nchi zao mbele za watu wa Israeli.
\v 4 Akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika sehemu za juu na juu ya vilima na chini ya kila mti wenye majani mabichi.
\p
\v 5 Kwa hiyo Yahwe Mungu wa Ahazi, akamweka katika mikono ya mfalme wa Shamu. Waaramu wakamshinda na kuchukua kutoka kwake kundi kubwa la mateka, wakawapeleka Damesiki. Ahazi pia aliwekwa katika mikono ya mfalme wa Israeli ambaye alimshinda kwa mauji makuu.
\v 6 Kwa maana Peka mwana wa Remalia, aliwaua katika Yuda wanajeshi 120, 00 kwa siku moja, wote walikuwa wanaume hodari, kwa maana walikuwa wamemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao.
\v 7 Zikri, mtu mwenye nguvu kutoka Efraimu, akawaua Maaseya mwana wa mfalme, Azrikamu, mwangalizi mkuu wa ikulu, na Elkana, ambaye alikuwa karibu na mfalme.
\v 8 Jeshi la Israeli likachukua mateka kutoka kwa ndugu zao 200,000 wake, wana, na mabinti. Pia wakachukua nyara nyingi, ambazo walipeleka Samaria.
\p
\v 9 Lakini nabii wa Yahwe alikuwapo huko, jina lake aliitwa Odedi. Alikwenda nje kukutana na jeshi likiingia Samaria. Akawaambia, “Kwa sababu Yahwe, Mungu wa baba zenu, alikuwa na hasiri na Yuda, akawatia katika mikono yenu. Lakini mmewaua katika hasira inayofika juu mbinguni.
\v 10 Sasa ninyi badala ya kuwahifadhi wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu kama watumwa wenu. Lakini je hamko na hatia ya dhambi zenu dhidi ya Yahwe Mungu wenu?
\v 11 Sasa basi, nisikilizeni: warudisheni wafungwa, ambao mmewachukua wa ndugu zenu, kwa maana ghadhabu ya Yahwe iko juu yenu.”
\p
\v 12 Kisha baadhi ya viongozi wa watu wa Efraimu--Azaria mwana wa Yohanani, Berekia mwana wa Meshiremothi, na Yehizikia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai, wakasimama kinyume na wale waliorudi kutoka vitani.
\v 13 Wakasema kwao, “Lazima msiwalete wafungwa hapa, kwa kuwa mlikusudia jambo ambalo litaleta juu yetu dhambi dhidi ya Yahwe, kuongeza dhambi juu yetu na makosa yetu, kwa maana makosa yetu ni makubwa, na kuna hasira kali dhidi ya Israeli.”
\p
\v 14 Hivyo watu wenye silaha wakawaacha wafungwa na mateka mbele ya viongozi wa Israeli na kusanyiko lote
\v 15 Watu ambao walipangwa kwa majina wakanyanyuka na kuwachukua wafungwa, na kuwavika wote waliokuwa uchi miongoni mwa mateka. Wakawavika na kuwapa viatu. Wakawapa chakula wale na kunywa. Wakawahudumia majeraha yao na kuwaweka waliodhaifu juu ya punda. Wakawarudisha kwenye familia zao katika Yeriko, (Ulioitwa mji wa mitende). Kisha wakarudi Samaria.
\p
\v 16 Wakati huo Mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa wafalme waAshuru kuwaomba wamsaidie.
\v 17 Kwa maana Waedomu walikuwa wamekuja tena na kuvamia Yuda, wakachukua wafungwa.
\v 18 Wafilisti pia wakavamia miji ya nchi ya chini na ya Negebu ya Yuda. Waliichukua Beth-shemeshi, Ayaloni, Giderothi, SoKo pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake. Wakaenda kuishi katika sehemu hizo.
\v 19 Kwa kuwa Yahwe aliishusha chini Yuda kwa sababu ya Ahazi, mfalme wa Israeli; kwa maana alikuwa ametenda maovu katika Yuda na alikuwa ametenda dhambi nzito sana dhidi ya Yahwe.
\v 20 Tiglath-pileseri, mfalme wa Ashuru, akaja kwake na akampa taabu badala ya kumpa nguvu.
\v 21 Kwa kuwa Ahazi aliteka nyara nyumba ya Yahwe na nyumba ya mfalme na viongozi, kwa ajili ya kuvitoa vitu vya thamani kwa mfalme wa Ashuru. Lakini kufanya hivyo hakukumfaidisha yeye.
\p
\v 22 Mfalme Ahazi akatenda dhambi hata zaidi dhidi ya Yahwe katika muda wa mateso yake.
\v 23 Kwa maana aliwatolea dhabihu miungu wa Dameski, miungu ambao walimshinda. Akasema, “Kwa sababu miungu wa mfalme wa Aramu waliwasaidia, nitawatolea sadaka ili wanisaidie.” Lakini walikuwa watesi wake na Israeli yote.
\p
\v 24 Ahazi akazikusanya pamoja samani za nyumba ya Mungu na kuzikata vipande vipande. Akaifunga milango ya nyumba ya Yahwe na kuzitengeneza madhabahu kwa ajili yake mwenyewe katika kila kona ya Yerusalemu.
\v 25 Katika kila mji wa Yuda akafanya sehemu za juu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa kwa miungu wengine. Akamfanya Yahwe, Mungu wa babu zake, akasirike.
\p
\v 26 Sasa matendo yake yaliyobaki, na njia zake zote, mwanzo na mwisho, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
\v 27 Ahazi akalala pamoja na baba zake, na wakamzika katika mji, katika Yerusalemu, lakini hawakumleta kwenye makaburi ya wafalme wa Israeli. Hezekia, mwanaye, akawa mfamle katika nafasi yake.
\c 29
\cl Sura 29
\p
\v 1 Hezekia alianza kutawala alipokuwa na umri wa miaka ishirini na mitano; alitawala miaka ishirini na nane katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Abiya; alikuwa binti wa Zekaria.
\v 2 Alifanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi baba yake alivyofanya.
\p
\v 3 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, katika mwezi wa kwanza, Hezekia aliifungua milango ya nyumba ya Yahwe na kuikarabati.
\v 4 Akawaleta ndani makuhani na Walawi, na akawakusanya pamoja katika uwanda upande wa mashariki.
\v 5 Akawaambia, “Nisikilizeni, ninyi Walawi! Jitakaseni wenyewe, na itakaseni nyumba ya Yahwe, Mungu wa babu zenu, na uondoeni mbali uchafu kutoka kwenye sehemu takatifu.
\v 6 Kwa kuwa baba zetu walikosea na kufanya kilichokuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wetu; walimsahau, wakageuzia mbali nyuso zao kutokasehemu ambapo Yahwe anaishi, na kuigeuzia migongo yao.
\v 7 Pia waliifunga milango ya ukumbi nakuziweka nje taa; hawakufukiza uvumba au kutoa sadaka za kuteketezwa katika sehemu takatifu kwa Mungu wa Israeli.
\v 8 Kwa hiyo hasira ya Yahwe ilikuwa imeshuka juu ya Yuda na Yerusalemu, na amewafanya kuwa kitu cha wasiwasi, cha hofu, na cha kudharauliwa, kama mnavyoona kwa macho yenu.
\v 9 Hii ndiyo maana mababa zetu wameanguka kwa upanga, na wana wetu, binti zetu, na wake zetu wako katika utumwa kwa sababu ya hili.
\v 10 Sasa ni katika moyo wangu kufanya agano na Yahwe, Mungu wa Israeli, ili kwamba hasira yake kali iweze kugeukia mbali nasi.
\v 11 Wanangu, msiwe wavivu sasa, kwa kuwa Yahwe amewachagua kwa ajili ya kusimama mbele yake, kwa ajili ya kumwabudu yeye, na kwamba muwe watumishi wake na kufukiza uvumba.”
\p
\v 12 Basi Walawi wakainuka; Mahathi mwana wa Amasai, na Yoeli mwana wa Azaria, wa watu wa Kohathi; na wa watu wa Merari, Kishi mwana wa Abdi, na Azaria mwana wa Yehaleleli; na wa Wargeshoni, Yoa mwana wa Zimna, na Edeni mwana wa Yoa;
\q
\v 13 wa wana wa Elisafani, Shimri na Yeueli; wa wana wa Asafu, Zekaria na Matania;
\q
\v 14 wa wana wa Hemani, Yehueli na Shimei; na wa wana Yeduthuni, Shemaya na Uzieli.
\p
\v 15 Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa wenyewe, na wakaenda ndani, kama alivyoamuru mfalme, wakifuata maneno ya Yahwe, kwa ajili ya kuisafisha nyumba ya Yahwe.
\v 16 Makuhani wakaenda kwenye sehemu za ndani ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kuisafisha; wakaleta nje uchafu wote walioukuta ndani ya hekalu la Yahwe katika uwanja wa nyumba. Walawi wakauchukua kuubeba nje ya hadi kwenye kijito cha Kidroni.
\v 17 Sasa wakaanza utakaso katika siku ya kwanza ya mwezi. Katika siku ya nane ya mwezi wakaufikia ukumbi wa Yahwe. Kisha siku nane zaidi wakaitakasa nyumba ya Yahwe. Katika siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza wakamaliza.
\p
\v 18 Kisha wakaenda kwa Hezekia, mfalme, ndani ya ikulu na kusema, “Tumeisafisha nyumba yote ya Yahwe, madhabahu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa pamoja na vifaa vyake vyote, na meza ya mkate wa uwepo, pamoja na vifaa vyake vyote.
\v 19 Kwa hiyo tumejiandaa na tumevitakasa vitu vyote ambavyo Mfalme Ahazi aliviondoa wakati alipoenda kwa ukengeufu katika kipindi cha utawala wake, ona, viko mbele ya madhabahu ya Yahwe.”
\p
\v 20 Kisha Hezekia mfalme akaamka mapema asubuhi na kuwakusanya viongozi wa miji; akaenda kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 21 Wakaleta ng'ombe waume saba, kondoo waume saba, wanakondoo saba, mbuzi waume saba kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya mfalme, kwa ajili ya patakatifu, kwa ajili ya Yuda. Akawaamuru makuhani, wana wa Haruni, kuwatoa sadaka juu ya madhabahu ya Yahwe.
\v 22 Kwa hiyo wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu na kuinyunyiza juu ya madhabahu. Wakawachinja kondoo dume, na kunyunyiza damu juu ya madhabahu; Pia wakawachinja wanakondoo na kuinyunyiza damu juu ya madhabahu.
\v 23 Wakawaleta mbuzi kwa ajili ya sadaka ya dhambi mbele ya mfalme na kusanyiko; wakaweka mikono yao juu ya hao mbuzi.
\v 24 Makuhani wakawachinja, na wakafanya sadaka ya dhambi kwa damu yao juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote, kwa maana mfalme alikuwa ameamuru kuwa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya dhambi lazima zifanywe kwa ajili ya Israeli wote.
\p
\v 25 Hezekia akawaweka Walawi katika nyumba ya Yahwe wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, akiwapanga kwa amri ya Daaudi, Gadi, mwonaji wa mfalme, na Nathani, nabii, kwa maana amri ilitoka kwa Yahwe kupitia manabii wake.
\v 26 Walawi wakasimama na vyombo vya Daudi, na makauhani wakasimama na matarumbeta.
\p
\v 27 Hezekia akawaamuru kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Sadaka zilipoanza, wimbo wa Yahwe ukaanza pia, kwa matarumbeta, pamoja na vyombo vya Daudi, mfalme wa Israeli.
\v 28 Kusanyiko lote wakaabudu, waimbaji wakaimba, na wapiga matarumbeta wakapiga; yote hayo yakaendelea hadi sadaka za kuteketezwa zilizipokwisha.
\p
\v 29 Walipomaliza kutoa sadaka, mfalme na watu waliokuwepo pamoja naye wakainama, na kusujudu.
\v 30 Vile vile, Hezekia, mfalme, na viongozi wakawaamuru Walawi kuimba ili kumsifu Yahwe kwa maneno ya Daudi na ya Asafu, mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama chini wakasujudu.
\p
\v 31 Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe. Njoni hapa na mlete sadaka na dhabihu za shukrani katika nyumba ya Yahwe.” Kusanyiko wakaleta sadaka na dhabihu za shukrani, na wote waliokuwa na moyo wa kuhiyarika wakaleta sadaka za kuteketezwa.
\p
\v 32 Hesabu ya sadaka za kuteketezwa ambazo kusanyiko walileta ilikuwa ng'ombe sabini, kondoo waume mia moja, na wanakondo waume mia mbili. Wote hao walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe.
\v 33 Sadaka za kuwekwa wakfu zilikuwa ng'ombe mia sita na kondoo elfu tatu.
\v 34 Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuchuna sadaka zote za kuteketezwa, kwa hiyo ndugu zao, Walawi, wakawasaidia hadi kazi ilipoisha, na hadi makuhani walipoweza kujitakasa wenyewe, kwa maana Walawi walikuwa makini sana kujitakasa wenyewe kuliko makuhani.
\p
\v 35 Zaidi ya hayo, palikuwa na sadaka za kuteketezwa nyingi sana; zilitolewa pamoja na sadaka za mafuta za amani, na kulikuwa na sadaka za vinywaji kwa kila sadaka ya kuteketezwa. Kwa hiyo huduma ya nyumba ya Yahwe ikawekwa katika utaratibu.
\v 36 Hezekia akafurahia, na watu pia, kwa sababu ya kile ambacho Mungu alikuwa ameandaa kwa ajili ya watu, kwa maana kazi ilikuwa imekamilika haraka.
\c 30
\cl Sura 30
\p
\v 1 Hezekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda, na pia akawaandikia barua Efraimu naManase, kwamba waje kwenye nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu, kusherehekea Pasaka ya Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 2 Kwa maana mfalme, viongozi wake, na kusanyiko lote katika Yerusalemu walikuwa wameshauriana pamoja, wakakubaliana kusherehekea Pasaka katika mwezi wa pili.
\v 3 Hawakuweza kuisherehekea mapema kabla ya hapo, kwa sababu hapakuwa na makuhani wa kutosha waliojitakasa wenyewe, wala watu hawakuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu.
\v 4 Pendekezo hili likaonekana sahihi katika macho ya mfalme na ya kusanyiko lote.
\v 5 Kwa hiyo wakakubaliana kufanya tangazo katika Israeli yote, kuanzia Beer-sheba hadi Dani, kwamba watu lazima waje kusherehekea Pasaka ya Yahwe, Mungu wa Israeli, huko Yerusalemu. Kwa maana walikuwa hawakuwa wameisherehekea kwa hesabu kubwa ya watu, kwa mujibu wa jinsi ilivyokuwa imeandikwa.
\p
\v 6 Hivyo matarishi wakaenda na barua kutoka kwa mfalme na viongozi wake katika Israeli na Yuda yote, kwa agizo la mfalme. Wakasema, “Ninyi watu wa Israeli, rudini kwa Yahwe, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Israeli, ili kwamba aweze kuwarudia masalia wenu ninyi mlipona kutoka kwenye mkono wa wafalme wa Ashuru.
\v 7 Msiwe kama baba zenu au ndugu zenu, ambao walimuasi Yahwe, Mungu wa mababa zao, hivyo akawaweka katika kuangamia, kama mnavyoona.
\v 8 Sasa msiwe wasumbufu, kama babu zenu walivyokuwa; badala yake, jitoeni wenyewe kwa Yahwe na njooni kwenye sehemu yake takatifu, ambayo ameitakasa milele, na mwabuduni Yahwe Mungu wenu, ili kwamba uso wake wenye hasira uwageukie mbali.
\v 9 Kwa maana ikiwa mtageuka nyuma kwa Yahwe, ndugu zenu na watoto wenu watapata huruma mbele ya hao wanaowaongoza kama wafungwa, na watarudi katika nchi hii. Kwa maana Yahwe Mungu wenu, ni mkarimu na mwenye huruma, na hatawageuzia mbali uso wake, kama mtarudi kwake.”
\p
\v 10 Kwa hiyo matarishi wakapita mji kwa mji katika majimbo ya Efraimu na Manase, njia yote hadi Zabuloni, lakini watu waliwacheka na kuwazomea.
\v 11 Lakini, watu wengine wa Asheri na Manase na Zabuloni walijinyenyekesha wenyewe na wakaja Yerusalemu.
\v 12 Mkono wa Mungu pia ukaja juu ya Yuda, kuwapa moyo mmoja, ili kulikubali agizo la mfalme na viongozi kwa neno la Yahwe.
\p
\v 13 Watu wengi, kusanyiko kubwa, likakusanyika Yerusalemu kusherehekea Sikukuu ya Mikate Isiyochacha katika mwezi wa pili.
\v 14 Waliinuka na kuchukua madhabahu zilizokuwa Yerusalemu, madhabahu zote kwa ajili ya sadaka za kufukiza; wakazirusha katika kijito Kidroni.
\p
\v 15 Kisha wakamuua mwanakondoo wa Paska katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Makuhani na Walawi wakaona aibu, kwa hiyo wakajitakasa wenyewe na kuleta sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe.
\p
\v 16 Wakasimama katika sehemu zao katika makaundi yao, wakifuata maelekezo yaliyotolewa na sheria ya Musa, mtu wa Mungu. Makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi.
\v 17 Kwa maana walikuwepo wengi katikakusanyiko ambao hawakuwa wamejitakasa wenyewe. Kwa hiyo Makuhani wakamchinja mwanakondoo wa Pasaka kwa ajili ya kila mmoja ambaye hakuwa amejisafisha na hakuweza kuzitakasa sadaka zake kwa Yahwe.
\v 18 Kwa kuwa wingi wa watu, wengi wao kutoka Efraimu na Manase, Asakari na Zabuloni, hawakuwa wamejitakasa wenyewe, bado waliula mlo wa Pasaka, kinyume na maelekezo yaliyoandikwa. Kwa kuwa Hezekia alikuwa amewaombea, akisema, “Mungu Yahwe amsamehe kila mmoja
\v 19 ambaye anauelekeza moyo wake kumtafuta Mungu, Yahwe, Mungu wa baba zake, hata kama hajasafiswa kwa utakaso wa viwango vya patakatifu.”
\v 20 Kwa hiyo Yahwe akamsikiliza Hezekia na akawaponya watu.
\p
\v 21 Watu wa Israeli waliokuwepo Yerusalemu wakaitunza Sikukuu ya Mikaate Isiyochachwa na furaha kubwa kwa siku saba. Walawi na makuhani wakamsifu Yahwe siku baada ya siku, wakiimwimbia Yahwe kwa vyombo vya sauti kuu.
\p
\v 22 Hezekia akazungumza kwa kuwatia moyo Walawi wote walioielewa ibada ya Yahwe, Kwa hiyo wakala kwa kipindi cha siku saba, wakitoa sadaka za amani, na kufanya toba kwa Yahwe, Mungu wa babu zao.
\p
\v 23 Kusanyiko lote kisha likaamua kusherehekea kwa siku zingine saba, na wakafanya hivyo kwa furaha.
\v 24 Kwa kuwa Hezekia mfalme wa Yuda aliwapa kusanyiko ng'ombe dume elfu moja, na kondoo elfu saba kama sadaka; na viongozi wakawapa kusanyiko ng'ombe dume elfu moja na kondoo na mbuzi elfu kumi. Idadi kubwa ya makuhani wakajitakasa wenyewe.
\v 25 Kusanyiko lote la Yuda, pamoja na makuhani na Walawi na watu wote walikuja pamoja kutoka nchi ya Israeli na wale walioishi Yuda--wote wakafurahia.
\v 26 Hivyo kulikuwa na furaha kuu katika Yerusalemu, kwa kuwa tangu wakati wa Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, hapakuwa na kitu kama hicho katika Yerusalemu.
\v 27 Kisha makuhani, Walawi, wakainuka na kuwabariki watu. Sauti zao zilisikika na maombi yao yakaenda juu mbinguni, sehemu takatifu ambapo Mungu anaishi.
\c 31
\cl Sura 31
\p
\v 1 Sasa wakati haya yote yalipokwisha, watu wote wa Israeli waliokuwepo pale wakaenda huko kwenye mji wa Yuda na wakazivunja vipande vipande nguzo za mawe na wakazikata nchi za maashera, na wakazibomoa sehemu za juu na madhabahu katika Yuda yote na Benjamini, na katika Efraimu na Manase, hadi walipoziharibu zote. Kisha watu wote wa Israeli wakarudi, kila mtu kwenye mali zake na kwenye mji wake.
\p
\v 2 Hezekia akayapanga makundi ya makuhani na Walawi wakajipanga kwa makundi yao, kila mtu akapangwa katika kazi yake, wote makuhani na Walawi. Aliwapanga wafanye sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kutoa shukrani, na kusifu katika malango ya hekalu la Yahwe.
\v 3 Pia akawapanga katika sehemu ya mfalme kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kutoka katika mali zake, hiyo ni kwa ajili ya, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya siku za Sabato, mwezi mpya, na siku kuu zisizobadilika, kama ilivyokuwa imeandikwa katika sheria ya Yahwe.
\v 4 Vilevile, akawaamuru watu walioishi Yerusalemu kutoa fungu kwa ajili ya makuhani na Walawi, ili kwamba wawe makini katika kuitii sheria ya Yahwe.
\v 5 Mapema mara baada ya amri kutolewa, watu wa Israeli kwa ukarimu wakatoa malimbuko ya nafaka, divai mpya, mafuta. Asali, na kila kitu kutoka kwenye mavuno ya shamba. Wakaleta ndani fungu la kumi la kila kitu; ambavyo vilikuwa kiasi kikubwa sana.
\v 6 Watu wa Israeli na Yuda ambao waliishi katika mji wa Yuda pia wakaleta zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vitakatifu amabavyo vilikuwa vimewekwa wakfu kwa Yahwe Mungu wao, na wakavifunga katika marundo.
\v 7 Ilikuwa mwezi wa tatu wakati walipoanza kufunga michango yao katika marundo, na wakamaliza mwezi wa saba.
\v 8 Hezekia na viongozi walipokuja na kuyaona marundo, wakambariki Yahwe na watu wake Israeli.
\p
\v 9 Kisha Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu marundo.
\v 10 Azaria, kuhani mkuu, wa nyumba ya Zadoki, akamjibu na akasema, “Tangu watu walipoanza kuleta matoleo katika nyumba ya Yahwe, tumekula na tulikuwa navyo vya kutosha, tulibakiza vingi, kwa maana Yahwe amewabariki watu wake. Kilichokuwa kimebaki ni kiasi kikubwa hiki hapa.”
\p
\v 11 Kisha Hezekia akaagiza vyumba vya kuhifadhia viandaliwe katika nyumba ya Yahwe, na wakaviandaa.
\v 12 Kisha kwa uaminifu wakayaleta ndani matoleo, zaka, na vitu ambavyo ni vya Yahwe. Konania, Mlawi, alikuwa meneja mkuu wa hivyo vitu, na Shimei, ndu yake, alikuwa wa pili kwake.
\v 13 Yehieli, Azaria, Nahathi, Asaheli, na Yerimothi, Yazabadi, Elieli, Ismakia, Mahathi, na Benania walikuwa wasimamizi chini ya mkono wa Konania na Shimei ndu yake, kwa uteuzi wa Hezekia, mfalme, na Azaria mwangalizi mkuu wa nyumba ya Mungu.
\p
\v 14 Kore mwana wa Imna Mlawi, bawabu katika mlango wa mashariki, alikuwa juu ya sadaka za hiari za Mungu, msimamizi wa kugawa sadaka kwa Yahwe na sadaka takatifu kuliko zote.
\v 15 Chini yake walikuwepo Edeni, Miniamini, Yoshua, Shemai, Amaaria, na Shekania, katika miji ya makuhani. Wakazijaza ofisi za uaminifu, ili kutoa sadaka hizi kwa ndugu zao fungu kwa fungu, kwa wote walio muhimu na wasio muhimu.
\p
\v 16 Pia wakatoa kwa wale wanaume wenye umri wa miaka mitatu na kuendelea, amabao walikuwa wameandikwa katika kitabu cha baba zao walioiingia nyumba ya Yahwe, kwa mujibu wa ratiba ya kila siku, kuifanya kazi katika ofisi zao na zamu zao. \f + \ft Mandishi ya kale yanasema hivi: “badala ya wanaume wa umri wa miaka mitatu na kuendelea,” wanaume wa mika thelathini na kuendelea.” \f*
\v 17 Waliwaganya makuhani kwa mujibu wa kumbu kumbu za baba zao, na hivyo hivyo kwa Walawi wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kwa mujibu wa ofisi zao na zamuzao.
\v 18 Waliwajumuisha watoto wao wadogo wote, wake zao, wana wao, na binti zao, katika jamii yote, kwa maana walikuwa waaminifu katika kujitunza wenye watakatifu.
\p
\v 19 Kwa maana makuhani, uzao wa Haruni, amabao walikuwa katika mashamba ya vijiji wakimilikiwa na miji yao, au katika kila mji, palikuwa na watu walioteuliwa kwa majina kutoa mafungu kwa ajili ya wanaume miongoni mwa makuhani, na kwa wote waliokuwa wameorodheshwa katika kumbukumbu za baba zao kuwa miongoni mwa Walawi.
\p
\v 20 Hezekia alifanya haya katika Yuda yote. Akakamilisha kilichokuwa chema, haki, na uaminifu mbele za Yahwe Mungu wake.
\v 21 Katika kila jambo ambalo alianzisha katika ibada ya nyumba ya Mungu, sheria, na zile amri, kumtafuta Mungu, alikifanya kwa moyo wake wote, na alifanikiwa.
\c 32
\cl Sura 32
\p
\v 1 Baada ya mambo haya na matendo haya ya uaminifu, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja na kuingia Yuda. Alipiga kambi kwa ajili ya kuivamia miji yenye ngome, ambayo alikusudia kuiteka kwa ajili yake.
\v 2 Sedekia alipoona kwamba Senakeribu amekuja na kwamba amedhamiria kupigana dhidi ya Yerusalemu,
\v 3 aliwashirikisha viongozi wake na watu wake wenye nguvu kuyazuia maji ya chemichemi yaliyokuwa nje ya mji; waalimsaidia kufanya hivyo.
\v 4 Kwa hiyo watu wengi wakakusanyika na kuyazuia maji ya chemichemi zote na mikondo yote amabayo ilikuwa inatiririka katikati ya nchi. Wakasema, “Kwa nini mfalme wa Ashuru aje na kupata maji mengi?”
\v 5 Hezekia akijipa ujasiri na kuujenga ukuta wote uliokuwa umeangushwa chini. Akaijenga minara mirefu, na pia ukuta mwingine nje. Pia akaiimarisha Milo katika mji wa Daudi, na akafanya kiasi kikubwa cha silaha na ngao. \f + \ft Maandishi ya kale yanasema hivi: “Badala ya, “akajenga minara mirefu,” baadhi ya matoleo ya zamani na kisasa yanasema, “akajenga minara mirefu juu yake,” Hii ni juu ya ukuta. \f*
\p
\v 6 Akaweka maamri jeshi juu wa watu. Akawakusanya pamoja kwake katika sehemu pana kwenye lango la mji na akasema kwao kwa ujasiri. Akasema,
\v 7 “Muwe imara na wenye ujasiri mzuri. Msiogope wala kukata tamaa kwa sababu ya mfalme wa Ashuru na jeshi lote ambalo liko naye, kwa maana kuna mtu yuko pamoja nasi ambaye ni mkuu kuliko
\v 8 walio naye mfalme wa Ashuru. Walionaye ni jeshi la mwili tu, lakini aliye nasi ni Yahwe, Mungu wetu, kwa ajili ya kutusaidia, na kupigana vita vyetu.” Kisha watu wakajifariji wenyewe kwa maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.
\p
\v 9 Baada ya hayo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, aliwatuma watumishi wake kwenda Yerusalemu (sasa alikuwa mbele ya Lakishi, na jeshi lake lote lilikuwa pamoja naye), kwa Hezekia, mfaalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walikuwa Yerusalemu. Akasema,
\pi
\v 10 “Hivindivyo Senakeribu, mfalme wa Ashuru, anasema: Ni kitu gani mnategemea kwa ajili ya kuhimili uvamizi katika Yerusalemu?
\v 11 Je, Hezekia hawapotoshi ninyi, ili kwamba awatoe kufa kwa njaa na kiu, anapowaambia, “Yahwe Mungu wetu atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru?
\v 12 Je, siyo Hezekia yule yule ambaye amezipeleka juu sehemu zake na madhabahu zake na kuwaamuru Yuda na Yerusalemu, juu ya madhabahu moja lazima muabudu, na juu yake lazima mchome sadaka zenu?
\pi
\v 13 Je, hamjui mimi na baba zangu tulifanya nini kwa makundi ya wote wa nchi zingine? Je, miungu ya watu wa hizo nchi iliweza kwa njia yoyote kuziokoa nchi zao dhidi ya nguvu zangu?
\v 14 Miongoni mwa miungu yote ya mataifa hayo ambayo baba zangu walitekeza, je, kulikuwa na mungu yeyote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu? Itakuwaje Mungu wenu aweze kuwakoa ninyi dhidi ya nguvu zangu?
\v 15 Sasa msimruhusu Hezekia awadanganye au kuwashawishi katika njia hii. Msimwamini, kwa maana hakuna mungu wa taifa lolote au ufalme amewahi kuwaokoa watu wake nje ya mkono wangu, au nje ya mkono wa baba zangu. Sembuse na Mungu wenu kwa namna gani atawaokoa na mkono wangu?
\p
\v 16 Watumishi wa Senakeribu hata walinena mabaya zaidi juu ya Yahwe Mungu na juu ya mtumishi wake Hezekia.
\v 17 Senakeribu pia akaandika barua ili kumdhihaki Yahwe, Mungu wa Israeli, na kunena kinyume naye. Alisema, “Kama ambavyo miungu ya mataifa haikuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu, hivyo hivyo na Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu.”
\v 18 Wakawalilia kwa lugha ya Wayahudi watu wa Yerusalemu waliokuwa juu ya ukuta, ili kuwaogopesha na kuwasumbua, ili kwamba waweze kuuteka mji.
\v 19 Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu kama walivyowanenea miungu ya Dunia, ambao ni kazi ya mikono ya wanadamu tu.
\p
\v 20 Hezekia, mfalme, na Isaya mwana wa Amozi, nabii, wakaomba kwa sababu ya jambo hili na wakalia hadi mbinguni.
\v 21 Yahwe akatuma malaika, ambaye aliwaua wanaume wa kupigana vita, majemedari, na maakida wa mfalme katika kambi. Kwa hiyo Senakeribu akarudi katika nchi yake akiwa na uso wa aibu. Alipokuwa ameenda katika nyumba ya mungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua huko kwa upanga.
\p
\v 22 Katika namna hii, Yahwe akamwokoa Hezekia na wakaaji wa Yerusalemu kutoka kwenye mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na kutoka kwenye mikono ya wengine, na akawapa pumzika juu ya kila upande. \f + \ft Maandishi ya kale yanasema hivi: badala ya “akawapa pumziko juu ya kila pande,” baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasema, “akawaongoza juu ya kila pande.” \f*
\v 23 Wengi walikuwa wakileta sadaka kwa Yahwe katika Yarusalemu, na zawadi za thamani kwa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa hiyo aliinuliwa mbele za macho ya mataifa yote toka wakati huo na kuendelea.
\p
\v 24 Katika siku hizo Hezekia akaugua hadi hatua ya kufa. Akaomba kwa Yahwe, ambaye alisema kwake na kumpaishara kwamba angeponywa.
\v 25 Lakini Hezekia hakumlipa Yahwe kwa ajili ya msaada uliotolewa kwake, kwa maana moyo wake uliinuliwa juu.
\v 26 Kwa hiyo hasira ikaja juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu. Hata hivyo, baadaye Hezekia alijinyenyekesha mwenyewe kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, wote Yeye na wakaaji wa Yerusalemu, hivyo hasira ya Yahwe haikuja juu yao wakati wa siku za Hezekia.
\p
\v 27 Hezekia alikuwa na utajiri mwingi sana na heshima kubwa. Alijipatia mwenyewe vyumba vya kuhifadhia kwa ajili ya fedha, dhahabu, vito vya thamani, na kwa ajili ya manukato, na kwa ajili ya ngao na na vyombo vyote vya thamani pia.
\v 28 Pia alikuwa na nyumba za maghala kwa ajili ya mavuno ya nafaka, divai mpya, na mafuta, na malisho kwa ajili ya aina zote za wanyama.
\v 29 Pia alikuwa na makundi katika mazizi. Zaidi ya hayo, alijipatia mwenyewe miji na makundi ya na ng'ombe kwa wingi, kwa maana Mungu alikuwa amempa afya tele. \f + \ft Maandishi ya kale yanasema hivi: Badala ya “miji” baadhi ya matoleo ya kisasa yanasema “punda,” na baadhi mengine ya kisasa yanaacha neno nzima. \f*
\p
\v 30 Alikuwa ni Hezekia ambaye alisimamisha chemi chemi ya juu ya maji ya Gihoni, na aliyeileta moja kwa moja chini upande wa magharibi mwa mji wa Daudi. Hezekia alifanikiwa katika miradi yake yote.
\v 31 Hata hivyo, katika jambo la mabalozi wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuwauliza waliofahamu, kuhusu ishara za miujiza iliyokuwa imefanywa katika nchi, Mungu alimwachia mwenyewe, ili kumjaribu, na kujua yote yaliyokuwa katika moyo wake.
\p
\v 32 Kwa mambo mengine kuhusu Hezekia, pamoja na matendo yake ya uaminifu wa agano, unaweza kuona kwamba yameandikwa katika Maono ya Nabii Isaya Mwana wa Amozi, na katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
\v 33 Hezekia akalala pamoja na baba zake, na wakamzika katika mlima wa makaburi ya vizazi vya Daudi. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakamheshimu katika kifo chake. Manase mwanaye akawa mfalme katika nafasi yake.
\c 33
\cl Sura 33
\p
\v 1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu.
\v 2 Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama yalivyo mambo ya machukizo ya mataifa ambao Yahwe alikuwa amewafukuza mbele ya watu wa Israeli.
\v 3 Kwa maana alizijenga tena sehemu za juu ambazo baba yake Hezekia alikuwa amezibomoa, na akajenga madhabahu kwa ajili ya mabaali, akatengeneza sanamu za Maashera, na akaziinamia chini nyota zote za mbinguni na kuziabudu.
\v 4 Manase akajenga madhabahu za kipagani katika nyumba ya Yahwe, ingawa Yahwe alikuwa ameamuru, “Ni katikaYerusalemu ambapo jina langu litawekwa milele.”
\v 5 Alijenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika vile viwanja viwili vya nyumba ya Yahwe.
\v 6 Katika bonde la Beni Hinomu akawaweka wanawe katika moto. Akafanya misemo ya ubashiri, na uchawi, akasoma utabiri; akashauriana na wale waliozungumza na wafu na pepo. Akafanya maovu mengi katika macho ya Yahwe na alimfanya Mungu akasirike.
\p
\v 7 Ile sanamu ya Maashera aliyokuwa amefanya, akaiweka katika nyumba ya Mungu. Ni kuhusu nyumba hii ambayo Mungu alikuwa amesema kwa Daudi na Sulemani mwanaye; alikuwa amesema, “Ni katika nyumba hii na katika Yerusalemu, ambao nimeuchagua kutoka makabila yote ya Israeli, kwamba nitaliweka jina langu milele.
\v 8 Sitawaondoa tena watu wa Israeli katika nchi hii ambayo niliitoa kwa baba zao, ikiwa tu watakuwa makini katika kuyashika yote niliyowaamuru, kuzishika sheria zangu, amri zangu, na sheria zangu nilizowapa kupitia Musa.”
\v 9 Manase akawaongoza Yuda na wakaaji wa Yerusalemu hata kufanya uovu zaidi kuliko hata watu wa mataifa ambao Yahwe alikuwa amewateketeza mbele za Israeli.
\p
\v 10 Yahwe akasema kwa Manase, na kwa watu wake wote, lakini hawakumsikiliza.
\v 11 Kwa hivyo Yahwe akaleta juu yao maamri wa jeshi la Ashuru, ambao walimchukua Manase katika minyonyoro, wakamfunga kwa pingu, na wakampeleka Babeli.
\v 12 Manase alipokuwa katika dhiki, alimuomba Yahwe, Mungu wake, na akajinyenyekesha sana mbele za Mungu wa baba zake.
\v 13 Akaomba kwake; na Mungu akamsikiliza, na Mungu akasikia kuomba kwake na akamrudisha Yerusalemu, katika ufalme wake. Kisha Manase akafahamu kwamba Yahwe alikuwa Mungu.
\p
\v 14 Baada ya hayo, Manase akajenga ukuta wa nje ya mji wa Daudi, upande wa magharibi wa Gihoni, katika bonde, hadi kwenye lango la Samaki. Akauzungushia mlima wa Ofeli na akaupandisha ukuta hadi usawa mrefu sana. Akaweka maamri jeshi jasiri katika ngome zote za miji ya Yuda.
\v 15 Akaipeleka mbali miungu yote ya kigeni, akaondoa sanamu zote kwenye nyumba ya Yahwe, na madhabahu zote ambazo alikuwa amejenga juu ya mlima wa nyumba ya Yahwe na katika Yerusalemu, na kuvitupa nje ya mji.
\v 16 Akaijenga tena madhabahu ya Yahwe na juu yake akatoa sadaka za amani na sadaka za shukrani; akamwamuru Yuda amtumikie Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 17 Hata hivyo watu bado walitoa sadaka mahali pa sehemu za juu, lakini kwa Yahwe, Mungu wao peke yake
\p
\v 18 Katika mambo mengine kuhusu Manase, maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji ambao walisema kwake katika jina la Yahwe, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa miongoni mwa matendo ya wafalme wa Israeli.
\v 19 Katika matukio hayo kuna historia ya maombi yake, na jinsi Mungu alivyoguswa na maombi hayo. Pia kuna kumbu kumbu ya dhambi zake zote na makosa yake, na sehemu ambako alikuwa amejenga sehemu za juu na kuzisimamisha Maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeshamwenyewe -- na imeandikwa kuhusu hayo katika tarehe ya waonaji. \f + \ft Maandishi ya kale yanasema hivi, “tarehe ya Hozai,” ambayo ni maandishi ya kifungu asili. Lakini matoleo mengi ya kisasa yamesahihisha na kusomeka “tarehe ya waonaji. Pia, matoleo machache ya kisasa yanasema “tarehe ya waonaji.” \f*
\v 20 Kwa hiyo Manase akalala na baba zake, na wakamzika katika nyumba yake mwenyewe. Amoni, mwaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\p
\v 21 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu.
\v 22 Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama Manase, baba yake, alivyofanya. Amoni alitoa sadaka kwa sanamu zote za kuchonga ambazo alitengeneza Manase baba yake, na aliziabudu.
\v 23 Hakujinyenyekesha mbele za Yahwe, kama baba yake Manase alivyokuwa amefanya. Badala yake, Amoni alifanya makosa zaidi na zaidi.
\p
\v 24 Watumishi wake wakapanga njama dhid yake na wakamuua katika nyumba yake mwenyewe.
\v 25 Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya njama dhidi ya Mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia, mwanaye, mfalme katika nafasi yake.
\c 34
\cl Sura 34
\p
\v 1 Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; alitawala miaka thelathini na moja katika Yerusalemu.
\v 2 Alifanya yaliyo haki katika macho ya Yahwe, na alitembea katika njia za Daudi baba yake, na hakugeuka mbali iwe kulia au kushoto.
\p
\v 3 Kwa maana ndani ya miaka minane ya ya utawala wake, alipokuwa bado kijana, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi, babu yake. Katika miaka ishirini, alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kutoka sehemu za juu, vituo vya Maashera, na sanamu za kuchonga na sanamu za chuma ya kuyeyushwa.
\v 4 Watu wakazivunja madhabahu za Baali katika uwepo wake; akazibomoa nguzo za Maashera na na zile sanamu za kuchonga, na sanamu za chuma ya kuyeyushwa katika vipande hadi zikawa mavumbi. Akayasambaza mavumbi juu ya makaburi ya wale ambao walizitolea sadaka.
\v 5 Akaichoma mifupa ya makuhani wao juu ya madhabahu zao. Katika namna hii, akaisafisha Yuda na Yerusalemu.
\v 6 Alifanya hivyo hivyo katika miji ya Manase, Efraimu, na Simeoni, sehemu zote hadi Neftali, na katika maeneo yaliyoizunguka.
\v 7 Alizivunja madhabahu, akayapiga Maashera, na sanamu za kuchonga kuwa unga, na kuzisambaratisha madhabahu zote za uvumba katika nchi yote ya Israeli; kisha akarudi Yerusalemu.
\p
\v 8 Sasa katika kipindi cha miaka ishirini ya utawala wake, baada ya Yosia kuisafisha nchi na hekalu, alimtuma Shafani mwana wa Azali, Manaseya, akida wa mji, na Yoa mwana wa Yoahazi katibu, kuikarabati nyumba ya Yahwe Mungu wake.
\p
\v 9 Wakaenda kwa Hilkia, kuhani mkuu, nawakakabidhi kwake fedha ambazo zilikuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Mungu, ambazo Walawi, walinzi wa milingo, walikuwa wamekusanya kutoka Manase na Efraimu, kutoka kwa masalia wote wa Israeli, kutoka Yuda yote na Benjamini, na kutoka kwa wakaaji wa Yerusalemu.
\p
\v 10 Wakaikabidhi zile fedha kwa watu waliosimamia kazi ya hekalu ya Yahwe. Watu wale wakawalipa watendakazi waliokarabati na kulijenga tena hekalu.
\v 11 Wakawalipa maseremala na wajenzi kwa ajili ya kununua mawe ya kuchonga na mbao kwa ajili ya kuungia, na kutengeneza boriti za nyumba ambazo baadhi ya wafalme wa Yuda waliziacha zikachakaa.
\p
\v 12 Watu walifanya kazi kwa uaminifu. Wasimamizi wao Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, kutoka kwa wana wa Wakohathi. Walawi wengine, wote kati ya wale waliokuwa wana mziki wazuri sana, kwa ukaribu waliwaelekeza watendakazi.
\v 13 Walawi hawa walikuwa viongozi wa wale waliobeba vifaa vya ujenzi na watu wengine wote waliofanya kazi kwa namna yoyote ile. Pia palikuwa na Walawi ambao walikuwa makatibu, watawala na walinda lango.
\p
\v 14 Walipozileta fedha ambazo zilikuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, Hilikia yule kuhani alikipata kitabu cha sheria ya Yahwe ambacho kilikuwa kimetolewa kupitia Musa.
\v 15 Hilikia akamwambia Shafani yule mwandishi, “Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe.” Hilikia akakileta kitabu kwa Shefani.
\p
\v 16 Shefani akakipeleka kitabu kwa mfalme, na pia akatoa taarifa kwake, akisema, “Watumishi wako wanafanya kila kitu walichokabidhiwa.
\v 17 Walizitoa fedha zote ambazo zilipatikana katika nyumba ya Yahwe, na walizikabidhi katika mikono ya wasimamizi na watendakazi.”
\v 18 Shefani mwandishi akamwambia mfalme.” Hilikia kuhani amenipa kitabu.” Kisha Shefani akamsomea mfalme katika hicho kitabu.
\p
\v 19 Ikawa kwamba mfalme alipokuwa ameyasikia maneno ya sheria, aliyararua mavazi yake.
\v 20 Mfalme akamwamuru Hilikia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake, akisema,
\v 21 “Nendeni mkaulize mapenzi ya Yahwe kwa ajili yangu, na kwa wale waliobaki katika Israeli na Yuda, kwa sababu ya maneno ya kitabu ambacho kimeokotwa. Kwa maana ni kuu, ghadhabu zake Yahwe zilizomiminwa kwetu kwa sababu baba zetu hawakuyasikiliza maneno ya kitabu hiki ili kuyatii yote yaliyokuwa yameandikwa ndani yake.” \f + \ft Badala ya “ambayo yamemiminwa juu yetu,” baadhi ya matoleo yanasema, “ambayo yamemulikwa dhidi yetu.” \f*
\p
\v 22 Kwa hiyo Hilkia, na wale ambao mfalme alikuwa amewaamuru, wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tohathi mwana wa Hasra, mtunza mavazi (aliishi katika Yerusalemu katika wilaya ya pili), na walizungumza naye katika namna hii.
\p
\v 23 Akasema kwao, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema: Mwambie mtu aliyewatuma kwangu,
\v 24 Hivi ndivyo Yahwe anasema: Ona, niko karibu kuleta maafa juu ya sehemu hii na wakaaji wake, laana zote zilizoandikwa katika kitabu walichokisoma mbele ya mfalme wa Yuda.
\v 25 Kwa sababu wamenisahau na wametoa sadaka za uvumba kwa miungu mingine, ili kwamba waniweke katika hasira kwa matendo yote waliyofanya -- kwa hiyo hasira yangu itamiminwa juu ya hii sehemu, na haitazimwa. (Badala ya “ambayo yamemiminwa juu yetu,” baadhi ya matoleo yana “amabyo yamemlikwa dhid yetu.”)
\v 26 Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliyewatuma kumuuliza Yahwe alichopaswa kufanya, hivi ndivyo mtakavyosema kwake, Yahwe, Mungu wa Israeli anasema hivi: Kuhusu maneno uliyosikia,
\v 27 kwa sababu moyo wako ulipondeka, na ulijinyenyekeza mbele zangu ulipoyasikia maneno yake dhidi ya sehemu hii na wakaaji wake, na kwa sababu umejinyenyekeza mwenyewe mbele zangu, na umeyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nami pia nimekusikiliza —hili ni azimio la Yahwe
\v 28 Ona nitakukusanya kwa mababa zako. Utakusanywa katika kaburi lako kwa amani, na macho yako hayataona maafa yoyote nitakayoleta juu ya sehemu hii na wakaaji wake.” Wale watu wakarudisha ujumbe huu kwa mfalme.
\v 29 Mfalme akatuma wajumbe na kuwakusanya wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.
\v 30 Kisha mfalme akaenda kwenye nyumba ya Yahwe, na watu wote wa Yuda wakaaji wa Yerusalemu, na makuhani, Walawi, na watu wote, kuanzia wakubwa hadi wadogo. Kisha akasoma mbele zao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichokuwa kimepatikana katika nyumba ya Yahwe.
\p
\v 31 Mfalme akasimama katika sehemu yake na kufanya agano mbele za Yahwe, kutembea mbele za Yahwe, na kuzishika amri zake, taratibu zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na roho yake yote, kuyatii maneno ya agano yaliyokuwa yameandikwa katika kitabu hiki.
\p
\v 32 Aliwasababisha wote walioonekana katika Yerusalemu na Benjamini kusimama kwa agano. Wakaaji wa Yerusalemu wakatembea kwa agano la Mungu, Mungu wa baba zao.
\p
\v 33 Yosia akapeleka mbali mambo yote ya machukizo kutoka kwenye nchi iliyomilikiwa na watu wa Israeli. Akamfanya kila mtu katika Israeli amwabudu Yahwe, Mungu wao. Kwa maisha ya siku zake zote, hawakugeuka mbali kwa kutomfuata Yahwe, Mungu wa mababa zao.
\c 35
\cl Sura 35
\p
\v 1 Yosia alisherehekea Pasaka kwa ajili ya Yahwe katika Yerusalemu, na wakachinja wanakondoo katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
\v 2 Akawaweka makuhan katika nafasi zao na akawatia moyo katika huduma za nyumba ya Yahwe.
\v 3 Akasema kwa Walawi waliowafundisha Israeli wote na waliokuwa wamewekwa wakfu kwa Yahwe, “Liwekeni sanduku takatifu katika nyumba ambayo Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli aliijenga. Hamtakuwa na mzigo tena mabegani mwenu. Sasa mwabuduni Yahwe Mungu wenu, na watumikieni watu wake Israeli.
\v 4 Jikusanyeni wenyewe kwa majina ya nyumba za baba zenu na zamu zenu, mkifuata maelekezo ya Daudi, mfalme wa Israeli, na yale ya Sulemani, mwanaye.
\p
\v 5 Simameni katika sehemu takatifu, mkichukua nafasi zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababa wa ndugu zenu, uzao wa watu, na mchukue sehemu zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa Walawi.
\v 6 Chinjeni wana kondoo wa Pasaka, jitakaseni wenyewe, andaeni wana kondoo kwa ajili ya ndugu zenu, kufanya sawa sawa na neno la Yahwe ambalo lilitolewa kwa mkono wa Musa.”
\p
\v 7 Yosia akawapa watu wote wana kondoo elfu thelathini na wana mbuzi kutoka katika makundi kwa ajili ya sadaka za Pasaka kwa wote waliokuwepo, na akatoa ng'ombe dume elfu tatu; hawa walikuwa kutoka katika mali ya mfalme.
\p
\v 8 Viongozi wake wakatoa sadaka za hiari kwa watu, makuhani, na Walawi. Hilikia, Zekaria, na Yeieli, viongozi wasimamizi wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani ndama 2,600 na ng'ombe mia tatu kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.
\v 9 Pia Konania, Shemaya na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, Yeieli, na Yazabadi, mkuu wa Walawi, akawapa Walawi wana-kondoo elfu tano na fahali mia tano kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.
\p
\v 10 Kwa hiyo huduma iliandaliwa, na makuhani wakasimama katika sehemu zao, pamoja na Walawi kwa zamu zao, kwa mujibu wa agizo la mfalme.
\v 11 Wakawachinja wana kondoo wa Pasaka, na makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi, na Walawi wakawachuna wana kondoo.
\v 12 Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, ili kuzisambaza katika makundi ya nyumba za mababa wa watu, ili wamtolee Yahwe, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa. Wakafanya vile vile kwa wale ng'ombe dume.
\v 13 Wakawaoka kwa moto wanakondoo wa Pasaka wakifuata maelekezo, kuhusu sadaka takatifu, walizichemsha kwenye vyungu, masufuria na makaangoni, na haraka wakayapeleka kwa watu.
\v 14 Baadaye waliandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu makuhani, uzao wa Haruni, walikuwa wametengwa katika kazi ya kutoa sadaka za kuteketezwa na za mafuta hadi usiku ulipoingia, kwa hiyo Walawi wakaandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, wana wa Haruni.
\p
\v 15 Waimbaji, wana wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagizwa na Daudi, Asafu, Hemani, na Yeduthuni, mwonaji wa mfalme, na walinzi walikuwa katika kila lango. Hawakutakiwa kuziacha huduma zao, kwa sababu ndugu zao Walawi walifanya maandalizikwa ajili yao.
\p
\v 16 Kwa hiyo, wakati huo huduma yote ya Yahwe ilifanyika kwa ajili ya kusherehekea Pasaka na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Yahwe, Kama alivyoamuru mfalme Yosia.
\v 17 Watu wa Israeli ambao walikuwepo wakaifanya Pasaka wakati huo, na kisha Sikukuu ya Mikate isiyochachwa kwa siku saba.
\v 18 Pasaka kama hiyo haijafanyika tena katikaIsraeli tangu siku za nabii Samweli, wala hakuna mfalme yeyote miongoni mwa wafalme wa Israeli ambaye amewahi kusherekea Pasaka kama Yosia alivyofanya, pamoja na makuhani, Walawi, na watu wote wa Yuda na Israeli waliokuwepo, na wakaaji wote wa Yerusalemu.
\v 19 Pasaka hii ilitunzwa ndani ya miaka kumi na minane ya utawala wa Yosia.
\p
\v 20 Baada ya haya yote, baada ya Yosia kuliweka hekalu katika utaratibu, Neko, mfalme wa Misiri, akaenda juu kupigana dhidi ya Karkemist karibu na mto Frati, na Yosia akaenda kupigana juu yake.
\v 21 Lakini Niko akatuma wajumbe kwake, akisema, “Nikufanye nini, mfalme wa Yuda? Leo siji kinyume nawe, lakini dhidi ya nyumba ambayo nafanya vita nayo. Mungu ameniamuru kuharakisha, kwa hivyo acha kumwingilia Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.”
\p
\v 22 Hata hivyo, Yosia alipuuza kurudi nyuma. Akajibadilisha ili apigane naye. Hakusikiliza maneno ya Neko ambayo yalikuja kutoka kwenye kinywa cha Mungu; hivyo akaenda kupigana katika bonde la Megido.
\p
\v 23 Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, na mfalme akawaambia watumishi wake, “Niondoeni hapa, kwa maana nimejeruhiwa vibaya.”
\v 24 Kwa hiyo watumishi wake wakamtoa nje ya gari, na kumuweka katika gari lake la tahadhari. Wakampeleka Yerusalemu, ambako alikufa. Alizikwa katika makaburi ya baba zake. Yuda wote na Yerusalemu wakamwomboleza.
\p
\v 25 Yeremia akamwomboleza Yosia; waimbaji wote wa kiume na wa kike wakaomboleza kuhusu Yosia hata leo. Nyimbo hizi zikawa desturi katika Israeli; tazama, zimeandikwa katika nyimbo za maombolezo.
\p
\v 26 Kwa mambo mengine kuhusu Yosia, na matendo yake mema aliyoyafanya katika kuti kile kilichoandikwa katika sheria ya Yahwe—
\v 27 na matendo yake, kutoka mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
\c 36
\cl Sura 36
\p
\v 1 Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoazi mwana wa Yosia, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake katika Yerusalemu.
\p
\v 2 Yehoazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, na akatawala miezi mitatu katita Yerusalemu.
\v 3 Mfalme wa Misiri akamwondoa katika Yerusalemu, na akamlazimisha kutoa faini kwa nchi ya talanta za fedha mia moja na talanta moja ya dhahabu.
\v 4 Mfalme wa Misiri akamfanya Eliakimu, ndugu yake, mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, na akambadilisha jina lake kuwa Yehoakimu. Kisha Neko akamchukua ndugu yake Eliakimu - Yeahazi na kumpeleka Misiri.
\p
\v 5 Yehoakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.
\v 6 KishaNebukadreza, mfalme wa Babeli, akamvamia na kumfunga katika minyororo kumuongoza kwenda mbali Babeli.
\v 7 Nebukadreza pia akabeba baadhi ya vitu katika nyumba ya Yahwe kwenda Babeli, na akaviweka katika ikulu yake huko Babeli.
\p
\v 8 Kwa mambo mengine kuhusu Yehoyakimu, mambo mabaya aliyofanya, na yaliyopatikana dhidi yake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Basi Yekonia, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\p
\v 9 Yekonia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; alitawala miezi mitatu na siku kumi katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe.
\v 10 Katika kipindi cha mwisho cha mwaka, mfalme Nebukadreza akatuma watu na wakampeleka Babeli, pamoja vitu vya thamani kutoka katika nyumba ya Yahwe, na kumfanya Sedekia ndugu yake, mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.
\p
\v 11 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu machoni mwa Yahwe Mungu wake.
\v 12 Hakujinyenyekesha mwenyewe mbele za Yeremia nabii, ambaye alisema kutoka kinywani mwa Yahwe.
\v 13 Sedekia pia akaasi dhidi ya Mfalme Nebukadreza, ambaye alikuwa amemfanya aape uaminifu kwake kupitia Mungu. Lakini Sedekia aliishupaza shingo yake na kuufanya moyo wake mgumu usigeuke kwa Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 14 Vilevile, viongozi wote wa makuhani na watu hawakuwa waaminifu, na waliufuata uovu wa mataiafa. Wakainajisi nyumba ya Yahwe ambayo alikuwa ameitakasa katika Yerusalemu.
\p
\v 15 Yahwe, Mungu wa baba zao, akatuma maneno kwao tena na tena kupitia wajumbe wake, kwa sababu alikuwa na huruma juu ya watu wake na juu ya sehemu anayoishi.
\v 16 Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, wakayadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hadi hasira ya Yahwe ilipoinuka dhidi ya watu wake, hadi pasiwepo na msaada.
\v 17 Hivyo Mungu aliwapeleka juu yao mfalme wa Wakaldayo, ambaye aliwaua vijana wao kwa upanga nyumbani patakatifu, na hakuwa na huruma juu ya vijana au mabikra, watu wazee au wenye mvi. Mungu akawatoa wote mikononi mwake.
\v 18 Vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za nyumba ya Yahwe, na hazina za mfalme na watumishi wake—vyote hivi akavipeleka Babeli.
\v 19 Wakaichoma moto nyumba ya Mungu, wakauangusha chini ukuta wa Yerusalemu, wakachoma ikulu zake zote, na wakaviaribu vitu vizuri vyote ndani yake.
\p
\v 20 Mfalme akawapeleka mbali Babeli wale waliokuwa wameoka na upanga. Wakawa watumishi wake pamoja na wanawe hadi utawala wa Waajemi.
\v 21 Hili lilitokea ili kulitimiza neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia, hadi nchi itakapokuwa imefurahia mapumziko ya Sabato yake. Iliishika Sabato kwa muda mrefu hadi kukataliwa kwake, ili miaka sabini itimie katika namna hii.
\p
\v 22 Sasa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia liweze kutimizwa, Yahwe akaipa hamasa roho yaKoreshi, mfalme wa Uajemi, kwamba akafanya tangazo katika ufalme wake wote, na akaliweka pia katika maandishi. Akasema,
\p
\v 23 “Hivi ndivyo Koreshi, mfalme wa Uajemi, anasema: Yahwe, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia. Ameniagiza nijenge nyumba kwa ajili yake katika Yerusalemu, ambayo ipo Yuda. Yeyote aliye miongoni mwenu kutoka katika watu wake wote, Yahwe Mungu wenu, awe naye. Akwee kwenye ile nchi.”