sw_ulb/13-1CH.usfm

1599 lines
112 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id 1CH
\ide UTF-8
\h 1 Mambo Ya Nyakati
\toc1 1 Mambo Ya Nyakati
\toc2 1 Mambo Ya Nyakati
\toc3 1ch
\mt 1 Mambo Ya Nyakati
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Adamu, Sethi, Enoshi,
\v 2 Kenani, Mahalaleli, Yaredi,
\v 3 Henoko, Methusela, Lameki.
\v 4 Wana wa Nuhu walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi.
\q
\v 5 Wana wa Yafethi walikuwa ni Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki, na Tirasi.
\q2
\v 6 Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama.
\q2
\v 7 Wana wa Yavani walikuwa ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
\q
\v 8 Wana wa Hamu walikuwa ni Kushi, Misri, Putu, na Kanaani.
\q
\v 9 Wana wa Kushi walikuwa ni Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa ni Sheba na Dedani.
\q
\v 10 Kushi akawa baba wa Nimrodi, aliyekuwa shujaa wa Kwanza katika dunia.
\q
\v 11 Misri akawa babu wa Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
\v 12 Wapathrusi, Wakasluhi (Wafilisti walipotoka), na Wakaftori.
\q
\v 13 Kanaani akawa baba wa Sidoni, mwanae wa kwanza, na wa Hethi.
\v 14 Pia akawa babu wa Myebusi, Mwamori, Mgirgashi,
\v 15 Mhivi, Mwarki, Msini,
\v 16 Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi.
\q
\v 17 Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri, na Mesheki
\q
\v 18 Arfaksadi akawa baba wa Sala, na Sala akawa baba wa Eberi.
\q2
\v 19 Eberi alikuwa na wana wawili wa kiume. Jina la wa kwanza lilikuwa Pelegi, kwa kuwa katika siku zake dunia ilikuwa imegawanyika. Jina la kaka yake lilikuwa Yoktani.
\q2
\v 20 Yoktani akawa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
\v 21 Hadoramu, Uzali, Dikla,
\v 22 Obali, Abimaeli, Sheba,
\v 23 Ofiri, Havila, na Yobabu; wote hawa walikuwa uzao wa Yoktani.
\q
\v 24 Shemu, Arfaksadi, Shela,
\v 25 Eberi, Pelegi, Reu,
\v 26 Serugi, Nahori, Tera,
\v 27 Abramu, aliye kuwa Ibrahimu.
\q
\v 28 Wana wa Ibrahimu walikuwa Isaka na Ishmaeli.
\q
\v 29 Hawa ndio wanao: mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli alikuwa ni Nebayothi, kisha Kedari, Abdeeli, Mibsamu,
\v 30 Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
\v 31 Yeturi, Nafishi, na Kedem. Hawa ndio wana wa Ishamaeli.
\q
\v 32 Wana wa Ketura, suria wa Ibrahimu, walikuwa Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
\q2
\v 33 Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Wote hawa walikuwa uzaowa Ketura.
\q
\v 34 Ibrahimu akawa baba wa Isaka. Wana wa Isaka walikuwa Esau na Israeli.
\q
\v 35 Wana wa Esau walikuwa ni Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu, na Kora.
\q2
\v 36 Wana wa Elifazi walikuwa ni Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna, na Amaleki.
\q2
\v 37 Wana wa Reueli walikuwa ni Nahathi, Zera, Shama, na Miza.
\q
\v 38 Wana wa Seiri walikuwa ni Lotani, Shobali, Sebioni, Ana, Dishoni, Eseri, na Dishani.
\q2
\v 39 Wana wa Lotani walikuwa ni Hori na Hemamu, na Timna alikuwa dada yake Lotani.
\q2
\v 40 Wana wa Shobali walikuwa ni Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu. Wana wa Sebeoni walikuwa ni Aya na Ana.
\q2
\v 41 Mwana wa Ana alikuwa ni Dishoni. Wana wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
\q2
\v 42 Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani walikuwa Usi na Arani.
\p
\v 43 Hawa ndio wafalme walio tawala katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kuwatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori; na jina la mji wake ulikuwa Dinhaba.
\q
\v 44 Bela alipo kufa, Yohabu mwana wa Zera wa Bosra akatawala badala yake.
\q
\v 45 Yohabu alipo kufa, Hushamu wa nchi ya Watemani akatawala badala yake.
\q
\v 46 Hushamu alipo kufa, Hadadi mwana wa Bedadi, aliye washinda Wamidiani katika uwanja wa Moabu, akatawa badala yake. Jina la mji wake ulikuwa Avithi.
\q
\v 47 Hadadi alipo kufa, Samla wa Masreka akatawala badala yake.
\q
\v 48 Samla alipo kufa, Shauli wa Rehobothi Hanahari akatawala badala yake.
\q
\v 49 Shauli alipo kufa, Baal-Hanani mwana wa Akbori akatawala badala yake.
\q
\v 50 Baal-Hanani mwana wa Akbori alipo kufa, Hadari akatawala badala yake. Jina la mji wake ni Pau. Jina la mke wake lilikuwa ni Mehetabeli binti wa Matredi binti wa Mezahabu.
\v 51 Hadadi akafa. Waku wa Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi,
\v 52 Oholibama, Ela, Pinoni,
\v 53 Kenazi, Temani, Mibsari,
\v 54 Magdieli, na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Hawa ndio wana wa Israeli: Reubeni, Simioni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuloni,
\v 2 Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi, na Asheri.
\q
\v 3 Wana wa Yuda walikuwa Eri, Onani, na Shela, ambao walizaliwa na binti wa Shua, Wakanaani. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa muovu katika macho ya Yahweh, na Yahweh akamuua
\v 4 Tamari, binti-mkwe wake, alimzalia Peresi na Zera. Yuda alikuwa na wana wa kiume wa tano.
\q
\v 5 Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli.
\q
\v 6 Wana wa Zera walikuwa Zimri, Ethani, Hemani, Kalikoli na Darda, wote kwa jumla ni watano.
\q2
\v 7 Mwana wa Karmi alikuwa ni Akani, aliye leta taabu katika Israeli alipo iba kile kilicho hifadhiwa kwa ajili ya Mungu.
\q2
\v 8 Mwana wa Ethani alikuwa Azaria.
\q
\v 9 Wana wa Hezroni walikuwa ni Yerameeli, Ramu, na Kalebu.
\q2
\v 10 Ramu akawa baba wa Aminadabu, na Aminadabu akawa baba wa Nashoni, kiongozi miongoni wa uzao wa Yuda.
\q2
\v 11 Nashoni akawa baba wa Salmoni, na Salmon akawa baba wa Boazi.
\v 12 Boazi akawa baba wa Obedi, na Obedi akawa baba wa Yese.
\q2
\v 13 Yese akawa baba wa mzaliwa wake wa kwanza Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Shimia.
\v 14 Nethaneli wa nne, Radai wa tano.
\v 15 Ozemu wa sita, na Daudi wa saba.
\q2
\v 16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa Abishai, Yoabu, na Asaheli, jumla watatu.
\v 17 Abigali akamzaa Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli.
\q
\v 18 Kalebu mwana wa Hesroni akawa baba wa watoto wa Azubu mkewe, na Yeriothi. Wanawe walikuwa Yesheri, Shobabu, na Ardoni.
\v 19 Azuba akafa, na Kalebu akamuoa Efrathi, aliye mzalia Huri.
\v 20 Huri akawa baba wa Uri, na Uri akawa baba wa Besaleli.
\q
\v 21 Baadae Hesroni (alipo kuwa na miaka sitini) akamuoa binti wa Makiri, baba wa Gileadi. Akamzalia Segubu.
\v 22 Segubu akawa baba wa Yairi, aliye miliki miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
\q
\v 23 Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi na Kenathi, pamoja na miji sitini iliyo zunguka. Hawa wakazi wote walikuwa ni uzao wa Makiri, baba wa Gileadi.
\q
\v 24 Baada ya kifo cha Hesroni, Kalebu akalala na Efrata, mke wa baba yake Hesroni. Akamzalia Ashuri, baba wa Tekoa.
\q
\v 25 Wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa ni Ramu mzaliwa wa kwanza, Buna, Oreni, Ozemu, na Ahiya.
\v 26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, jina lake lilikuwa Atara. Yeye alikuwa mama wa Onamu.
\q
\v 27 Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini, na Ekeri.
\q
\v 28 Wana wa Onamu walikuwa ni Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa ni Nadabu na Abishuri.
\q2
\v 29 Jina la mke wa Abishuri lilikuwa Abihaili, na akamzalia Abani na Molidi.
\q2
\v 30 Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa pasipo watoto.
\v 31 Mwana wa Apaimu alikuwa Ishi. Mwana wa Ishi alikuwa Sheshani. Mwana wa Sheshani alikuwa Alai.
\v 32 Wana wa Yada, kaka yake Shamai, walikuwa Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa pasipo mtoto.
\q
\v 33 Wana wa Yonathani walikuwa Pelethi na Zaza. Hawa ndio uzao wa Yerameeli.
\q
\v 34 Sasa Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, bali wa kike pekee. Sheshani alikuwa na mtumishi, wa Kimisri, ambaye jina lake lilikuwa Yariha.
\v 35 Sheshani alimkabidhi binti yake kwa Yariha mtumishi wake kama mke wake. Akamzalia Atai.
\q
\v 36 Atai akawa baba wa Nathani, na Nathani akawa baba wa Zabadi.
\q
\v 37 Zabadi akawa baba wa Efalali, na Efalal akawa baba wa Obedi.
\q
\v 38 Obedi akawa baba wa Yehu, na Yehu akawa baba wa Azaria.
\q
\v 39 Azaria akawa baba wa Helesi, na Helesi akawa baba wa Eleasa.
\q
\v 40 Eleasa akawa baba wa Sismai, na Sismai akawa baba wa Shalumu.
\q
\v 41 Shalumu akawa baba wa Yekamia, na Yekamia akawa baba wa Elishama.
\q
\v 42 Wana wa Kalebu, kaka yake Yerameeli, walikuwa ni Mesha mzaliwa wake wa kwanza, aliye kuwa baba wa Zifu. Mwanae wa pili, Maresha, allikuwa baba wa Hebroni.
\v 43 Wana wa Hebroni walikuwa Kora, Tapua, Rekemu, na Shema.
\v 44 Shema akawa baba wa Rahamu, baba wa Yorkeamu. Rekemu akawa baba wa Shamai.
\q
\v 45 Mwana wa Shamai alikuwa Maoni, na Maoni alikuwa baba wa Bethsuri.
\q
\v 46 Efa, suria wa Kalebu, alimzaa Harani, Mosa, na Gazezi. Harani akawa baba wa Gazezi.
\q
\v 47 Wana wa Yadai walikuwa Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa, na Shaafa.
\q
\v 48 Maaka, suria wa Kalebu, alimza Sheberi na Tirhana.
\v 49 Pia akamza Shaafu baba wa Madmana, Sheva baba wa Makbena na baba wa Gibea. Binti wa Kalebu alikuwa Aksa. Hawa walikuwa uzao wa Kalebu.
\q
\v 50 Hawa walikuwa wana wa Huri, mzaliwa wake wa kwanza kwa Efratha: Shobali baba wa Kiriath-Yearimu.
\v 51 Salma babake Bethlehemu, na Harefu babake Beth- Gaderi.
\q
\v 52 Shobali baba wa Kiriath Yearimu alikuwa na uzao: Haroe, nusu ya Wamenuthite,
\v 53 na ukoo wa Kiriath-Yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi, na Wamishrai. Wasorathi na Waeshtaoli walitoka huku.
\q
\v 54 Ukoo wa Salma ulikuwa kama ufatao: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, na nusu ya Wamanahathi Wazori,
\v 55 na ukoo wa waandishi walioishi Yabesi: Watirathi, Washimeathi, na Wasukathi. Hawa walikuwa Wakeni walio toka kwa Hamathi, baba wa nyumba ya Warekabu.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Sasa hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa kwake huko Hebroni: mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu kutoka Yezreeli; wa pili alikuwa Danieli, kwa Abigaili kutoka Karmeli;
\v 2 watatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa ni Maaka, binti wa Talmai mfalme wa Geshuri. Wanne alikuwa ni Adoniya mwana wa Hagithi;
\v 3 watano alikuwa ni Shefatia kwa Abitali, wasita alikuwa ni Ithraeamu kwa Egla mkewe.
\q
\v 4 Hawa sita walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni, alipo tawala miaka saba na miezi sita. Kisha akatawala miaka thelathini na mitatu huko Yerusalemu.
\v 5 Hawa wana wa nne, kwa Bathishiba binti wa Amieli, walizaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, na Sulemani.
\q
\v 6 Wana tisa wengine wa Daudi walikuwa ni: Ibhari, Elishua, Elipeleti,
\v 7 Noga, Nefegi, Yafia,
\v 8 Elishama, Eliada na Elifeleti.
\q
\v 9 Hawa walikuwa wana wa Daudi, pasipo kuwehesababu wana wa masuria wake. Tamari alikuwa dada yao.
\q
\v 10 Mwana wa Sulemani alikuwa ni Rehoboamu. Mwana wa Rehoboamu alikuwa Abiya. Mwana wa Abiya alikuwa Asa. Mwana wa Asa alikuwa Yehoshafati.
\q
\v 11 Mwana wa Yehoshafati alikuwa Yoramu. Mwana wa Yehoramu alikuwa Ahazia. Mwana wa Ahazia alikuwa Yoashi.
\q
\v 12 Mwana wa Yoashi alikuwa Amazia. Mwana wa Amazia alikuwa Azaria. Mwana wa Azaria alikuwa Yothamu.
\q
\v 13 Mwana wa Yothamu alikuwa Ahazi. Mwana wa Ahazi alikuwa Hezekia. Mwana wa Hezekia alikuwa Manase.
\q
\v 14 Mwana wa Manase alikuwa Amoni. Mwana wa Amoni alikuwa Yosia.
\q
\v 15 Wana wa Yosia aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza ni Yohana, wapili Yehoyakimu, mwanae watatu Sedekia, na mwanae wanne Shalumu.
\q
\v 16 Wana wa Yehoyakimu walikuwa Yehoyakini na Sedekia.
\q
\v 17 Wana wa Yehoyakini, mateka, walikuwa Shealtieli,
\v 18 Malkiramu, Pedaya, Shenezari, Yekamia, Hoshama, na Nedabia.
\q
\v 19 Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa Meshulamu na Hanania; Shelomithi alikuwa dada yao.
\v 20 Wanawe wengine watano walikuwa Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia, na Yushabu Hesedi.
\q
\v 21 Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Mwanawe alikuwa Refaya, na uzao wake zaidi walikuwa ni Arnani, Obadia, na Shekania.
\q
\v 22 Wana wa Shekania walikuwa Shemaya na wanawe: Hatushi, Igali, Baria, Nearia, na Shafati.
\q
\v 23 Wana watatu wa Nearia walikuwa Elioenai, Hizekia, na Azrikamu.
\q
\v 24 Wana saba wa Elioenai walikuwa Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohana, Delaya, na Anani.
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 Uzao wa Yuda ulikuwa Peresi, Hesroni, Karmi, Huri, na Shobali.
\q
\v 2 Reaya, mwana wa Shobali alikuwa baba waYahathi. Yahathi alikuwa baba wa Ahumai na Lahadi. Hawa walikuwawa koo za Wasorathi.
\q
\v 3 Hawa walikuwa wana wa Etamu: Yezreeli, Ishma, na Idbashi. Dada yao alikuwa Haselelponi.
\v 4 Penueli alikuwa mwanzilish wa Gedori. Ezeri alikuwa mwanzilishi wa Husha. Hawa walikuwa uzao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na muanzilishi wa Bethelehemu.
\q
\v 5 Ashuri baba wa Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.
\q
\v 6 Naara alimzalia Ahuzamu, Heferi, Temeni na Ahashtari. Hawa walikua wana wa Naara.
\q
\v 7 Wana wa Hela walikua Serethi, Sohari, Ethnani,
\v 8 na Kozi, aliyekua baba wa Anubu na Hasobeba, na koo zilizotoka kwa Aharheli mwana wa Harumu.
\p
\v 9 Yabesi aliheshimika zaidi ya kaka zake. Mama yake alimuita Yabesi. Alisema, “Kwa sababu nimemzaa katika uchungu
\v 10 Yabesi akamuita Mungu wa Israeli na kusema, “Laiti ungenibanibariki kweli, upanue eneo langu, na mkono wako ukuwe jpamoja nami. Ukifanya hivi utaniepusha na madhara, ili kwamba niwe huru na huzuni!” Kwa hivyo Mungu akamjalia maombi yake.
\q
\v 11 Kelubu kaka wa Shuha akawa baba wa Mehiri, aliyekuwa baba wa Eshtoni.
\v 12 Eshtoni akawa baba wa Beth-Rafa, Pasea, na Tehina, ambaye alianzisha mji wa Iri Nahashi. Hawa ni wanaume walioishi Reka.
\q
\v 13 Wana wa Kenazi walikua Othinieli na Seraia. Wana wa Othinieli walikuwa Hathathi na Meonothai.
\v 14 Meonothai akawa baba wa Ofara, na Seraia akawa baba wa Yohabu, mwanzilishi wa Ge Harashimu, ambao watu wake walikua wahunzi.
\v 15 Wana wa Kalebu mwana wa Yefune walikua Iru, Ela na Namu. Mwana wa Ela alikua Kenazi.
\q
\v 16 Wana wa Yehaleli walikua Zifi, Zifa, Tiriya, na Azareli.
\q
\v 17 Wana wa Ezra walikua Yetheri, Meredi, Eferi, na Yaloni.
\v 18 Mke wake Meredi wa Kimisri alishika mimba na kuwazaa Miriamu, Shamai, na Ishiba, aliyekua baba wa Eshitemoa. Hawa walikua wana wa Bithia, binti wa Farao, ambaye Meredi alimuoa. Mke wa Kiyahudi wa Meredi alimzaa Yeredi ambaye alikua baba wa Gedore; Heberi, aliyekua baba wa Soko; na Yekuthieli aliyekua baba wa Zanoa.
\q
\v 19 Kati ya wana wawili wa mke wa Hodia, dadake Nahamu, mmoja wao akawa baba wa Keila Mgarimi. Mwingine alikua Eshitemoa Mmakathi
\q
\v 20 Wana wa Shimoni walikua Amnoni, Rina, Beni Hanani, na Tiloni. Uzao wa Ishi walikua Zohethi na Beni-Zohethi.
\q
\v 21 Uzao wa Shela mwana wa Yuda, ulikua ni Eri baba wa Leka, Laada baba wa Maresha na koo za wafanyakazi wa kushona kule Beth Ashbea,
\v 22 Yoakimu, wanaume wa Kozeba, na Yoashi na Sarafi, aliyekuwa na mamlaka huko Moabu na Yashubi Lehemu. Maelezo haya yametoka kwenye nakala za zamani.)
\v 23 Hawa walikuwa ni wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera na kufanya kazi kwaMfalme.
\q
\v 24 Uzao wa Simeoni ulikua Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera, na Shauli.
\q2
\v 25 Shalumu alikua mwana wa Shauli, Mibisamu alikua mwana wa Shalumu, na Mishima alikua mwana wa Mibisamu.
\q2
\v 26 Ukoo wa Mishima ulikua Hamueli mwana wake, Zakuri mjukuu wake, na Shimei kitukuu chake.
\p
\v 27 Shimei alikua na wana kumi na sita na mabinti sita. Kaka zake hawakuwa na watoto wengi, Kwa hiyo koo zao hazikuongezeka sana kwa kama watu wa Yuda walivyoongezeka.
\v 28 Waliishi Beasheba, Molada, na Hazari Shuali.
\v 29 Pia waliishi Bilha, Ezemu, Toladi,
\v 30 Bethueli, Horma, Zikilagi,
\v 31 Bethi Markabothi, Hazari Susimi, Bethi Biri, na Shaaraimu. Hii ilikua miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi.
\v 32 Vijiji vyao vitano vilikua Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani,
\v 33 pamoja na vijiji vya kando mpaka Balith Haya yalikua makazi yao, na walitunza kumbukumbu za uzao wao.
\p
\v 34 Viongozi wa ukoo walikua Meshobabu, Yamileki, Yoshahi mwana wa Amazia,
\v 35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia mwana wa Seraia mwana wa Asieli,
\v 36 Elioenai, Yaakoba, Yeshohaia, Asaia, Adieli, Yesimieli, Benaia,
\v 37 na Ziza mwana wa Shifi mwana wa Aloni mwana wa Yedaia mwana wa Shimiri mwana wa Shemaia.
\v 38 Hawa walio orodheshwa kwa majina walikua viongozi wa koo zao, na koo zao ziliongezeka sana.
\v 39 Walienda karibu na Gedori, upande wa mashariki wa bonde, kutafuta malisho ya mifugo yao.
\v 40 Walipata malisho mengi na mazuri. Nchi ilikua tambarare, tulivu na ya amani. Wahamu waliishi hapo awali.
\v 41 Hao walio orodheshwa hapo kwa majina walikuja katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda, na wakashambulia makazi ya Wahamu na Wameuni, ambao pia walikua hapo. Waliwaangamiza kabisa na kuishi hapo sababu walipata malisho kwa ajili ya mifugo yao.
\p
\v 42 Wanaume mia tano wa kabila la Simeoni walienda katika mlima Seiri, pamoja na Pelatia, Nearia, Refaia, na Uzieli, wana wa Ishi, kama kiongozi wao.
\v 43 Waliwashinda wakimbizi wa Waamaleki waliobakia, na wakaishi hapo hadi siku hii.
\c 5
\cl Sura 5
\p
\v 1 Wana wa Rubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli - sasa Rubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, lakini haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa kwa wana wa Yusufu mwana wa Israeli kwa sababu Rubeni alinajisi kochi la baba yake. Kwa hivyo hajaandikwa katika nasaba kuwa ana haki ya mzaliwa wa kwanza.
\v 2 Yuda ndiye alikuwa na nguvu kati ya ndugu zake, na kiongozi angetoka kwake. Lakini haki ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu -
\v 3 wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli alikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi.
\q
\v 4 Uzao wa Yoeli ulikuwa huu: Mwana wa Yoeli alikuwa Shemaia. Mwana wa Shemaia alikuwa Gogi. Mwana wa Gogi alikuwa Shimei.
\v 5 Mwana wa Shimei alikuwa Mika. Mwana wa Mika alikuwa Reaia. Mwana wa Reaia alikuwa Baali.
\v 6 Mwana wa Baali alikuwa Bera, ambaye Tiligathi Pileseri alimpeleka matekani kule Assiria. Bera alikuwa kiongozi katika kabila la Rubeni.
\q
\v 7 Ndugu zake kwa na koo zao, walioandikishwa katika nasaba kwa vizazi vyao: Yeieli kiongozi, Zekaria,
\v 8 na Bela mwana wa Azazi mwana wa Shema mwana wa Yoeli. Waliishi Aroeri, kwa umbali wa Nebo na Baali Meoni,
\v 9 na kuelekea mashariki hadi mwanzo wa jangwa linaloendelea hadi Mto Efarati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka katika nchi ya Gileadi.
\q
\v 10 Katika siku za Sauli, kabila la Rubeni lilishambulia Wahagiri na kuwashindaWakaishi ndani ya hema za Wahagiri katika nchi yote mashariki mwa Gileadi.
\q
\v 11 Watu wa kabila la Gadi waliishi karibu nao, katika nchi ya Basha Saleka.
\v 12 Yoeli alikuwa kiongozi wao, Shafamu alikuwa wa pili na Yanai na Shafati walikuwa wa Bashani.
\q2
\v 13 Ndugu zao, kwa koo zao, walikuwa Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Sia na Eberi - jumla saba wote.
\q2
\v 14 Hawa watu walio tajwa hapo juu ni uzao wa Abihaili, na Abihaili alikuwa mwana wa Huri. Huri alikuwa mwana wa Yaroa. Yaroa alikuwa mwana wa Gileadi. Gileadi alikuwa mwana wa Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Yeshishai. Yeshishai alikuwa mwana wa Yado. Yado alikuwa mwana wa Buzi.
\q2
\v 15 Ahi mwana wa Abidieli mwana wa Guni, alikuwa kichwa cha ukoo wao.
\q
\v 16 Waliishi Gileadi, Bashani, katika miji yake, na katika nchi zote za malisho ya Sharoni kwa umbali wa mipaka yake.
\v 17 Hawa wote waliorodheshwa katika nakaka za uzao katika siku za Yothamu mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.
\p
\v 18 Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase walikuwa na wana jeshi 44,760 walio fuzu kwa vita, walio beba ngao na upanga, na waliovuta upinde, ambao wangewezakwenda vitani.
\v 19 Waliwashambulia Wahagiri, Yeturi, Nafishi, na Nodabu.
\v 20 Walipokea msaada wa kiungu dhidi yao. Katika hili Wahagiri na wote walio kuwa nao walishindwa. Hii ni kwa sababu Waisraeli walipaza sauti katika vita, na yeye akawajibu, kwa sababu waliweka tumaini lao kwake.
\v 21 Walikamata wanya wao, pamoja na ngamia elfu hamsini, kondoo 250,000, punda elfu mbili, na wanaume 100,000.
\v 22 Kwa sababu Mungu aliwapigania, waliua maadui wengi. Waliishi katika nchi yao mpaka nyakati za kuwekwa utumwani.
\p
\v 23 Wana wa nusu ya kabila la Manase waliishi katika nchi ya Bashani kwa umbali wa Bali Hermoni na Seniri (hiyo ni, Mlima Hermoni).
\p
\v 24 Hawa walikuwa viongozi wa koo zao: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia, na Yahdieli. Walikuwa mashujaa hodari, wanaume mashuhuri, viongozi wa familia zao.
\v 25 Lakini walikuwa sio waaminifu kwa Mungu wa babu zao. Walifanya uzinzi na miungu ya watu wa hiyo nchi, ambao Mungu aliwaangamiza mbele yao.
\v 26 Mungu wa Israeli akamchochea Puli mfalme wa Assiria (ambaye pia uitwa Tiligathi Pileseri, mfalme wa Assiria). Aliwapeleka matekani Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase. Aliwaleta kwa Hala, Habori, Hara, na kwenye mto wa Gozani, ambapo wapo hadi leo.
\c 6
\cl Sura 6
\p
\v 1 Wana wa Levi walikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.
\q
\v 2 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
\q
\v 3 Wana wa Amramu walikuwa Aruni, Musa, Miriamu. Wana wa Aruni walikuwa Nadabu, Abihu, Eleazari, na Ithamari.
\q2
\v 4 Eleazari akawa baba wa Finehasi, na Finehasi akawa baba wa Abishua.
\q2
\v 5 Abishua akawa baba wa Buki, na Buki akawa baba wa Uzi.
\q2
\v 6 Uzi akawa baba wa Zerahia, na Zerahia akawa baba wa Meraioti.
\q2
\v 7 Meraioti akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
\q2
\v 8 Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Ahimazi.
\q2
\v 9 Ahimazi akawa baba wa Azaria, na Azaria akawa baba wa Yohanani.
\q2
\v 10 Yohanani akawa baba wa Azaria, aliye hudumu katika hekalu alilo lijenga Sulemani ndaniya Yerusalemu.
\q2
\v 11 Azaria akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
\q2
\v 12 Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Shalumu.
\q2
\v 13 Shalumu akawa baba wa Hilikia, na Hilikia akawa baba wa Azaria.
\q2
\v 14 Azaria akawa baba Seraia, na Seraia akawa baba wa Yehozadaki.
\v 15 Yehozadaki akaenda matekani Yahweh alipo wapeleka utumwani Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Nebukadneza.
\q
\v 16 Wana wa Levi walikuwa Gerishomu, Kohathi, na Merari.
\q2
\v 17 Wana wa Gerishomu walikuwa Libini na Shimei.
\q2
\v 18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
\q
\v 19 Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Hawa walikuwa koo za Walawi kwa familia za baba zao.
\q
\v 20 Uzao wa Gerishomu ulianza na mwanae Libini. Mwana wa Libini alikuwa Jahathi. Mwanae alikuwa Zima.
\q2
\v 21 Mwanae alikuwa Yoa. Mwanae alikuwa alikuwa Ido. Mwanae alikuwa Zera. Mwanae alikuwa Yeatherai.
\q
\v 22 Uzao wa Kohathi ulianza na mwanae Aminadabu. Mwanae alikuwa Kora. Mwanae alikuwa Asiri.
\q2
\v 23 Mwanae alikuwa Elikana. Mwanae alikuwa Ebiasa. Mwanae alikuwa Asiri.
\q2
\v 24 Mwanae alikuwa Tahathi. Mwanae alikuwa Urieli. Mwanae alikuwa uzia. Mwanae alikuwa Shauli.
\q
\v 25 Wana wa Elikana walikuwa Amasai, Ahimothi
\q2
\v 26 Elikana mwanawe, Zofai mwanae, Nahathi mwanawe,
\q2
\v 27 Eliabu mwanawe, Yehoramu mwanawe na Elikana mwanawe.
\q
\v 28 Wana wa Samwali walikuwa mzaliwa wa kwanza, Yoeli, na Abija, wa pili.
\q
\v 29 Mwana wa Merari alikuwa Mahili. Mwanae alikuwa Libini.
\q2
\v 30 Mwanae alikuwa Shimei. Mwanae alikuwa Uza. Mwanae alikuwa Shimea. Mwanae alikuwa Hagia. Mwana alikuwa Asaia.
\p
\v 31 Haya ndio majina ya wanaume ambao Daudi waliwaeka kusimamia muziki katika nyumba ya Yahweh, baada ya sanduku kuja hapo.
\v 32 Walitumika kwa kuimba mbele ya hema, hema la kukutania, mpaka Sulemani alipo jenga nyumba ya Yahweh ndani ya Yerusalemu. Walikamilisha wajibu wao kwa kadiri ya maelekezo waliopewa.
\p
\v 33 Hawa walitumika pamoja na wana wao. Katika makabila ya Wakohathi alitoka Hemani mwana muziki. Babu zake walikuwa hawa, kurudi nyuma ya wakati: Hemani alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Samweli.
\q2
\v 34 Samweli alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Yerohamu. Yerohamu alikuwa mwana wa Elieli. Elieli alikuwa mwana wa Toa.
\q2
\v 35 Toa alikuwa mwana wa Zufi. Zufi alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Mahathi. Mahathi alikuwa mwana wa Amasai. Amasai alikuwa mwana wa Elikana.
\q2
\v 36 Amasai alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Azaria. Azaria alikuwa mwana wa Zefania.
\q2
\v 37 Zefania alikuwa mwana wa Tahathi. Tahathi alikuwa mwana wa Asiri. Asiri alikuwa mwana wa Ebiasa. Ebiasa alikuwa mwana wa Kora.
\q2
\v 38 Kora alikuwa mwana wa Izhari. Izhari alikuwa mwana wa Kohathi. Kohathi alikuwa mwana wa Lawi. Lawi alikuwa mwana wa Israeli.
\q
\v 39 Mfanyakazi mwenzake Hemani alikuwa Asafu, aliye simama mkono wake wa kuume. Asafu alikuwa mwana Berekia. Berekia alikuwa mwana wa Shimea.
\q2
\v 40 Shimea alikuwa mwana Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Baaseia. Baaseia alikuwa mwana wa Malikiya.
\q2
\v 41 Malikiya alikuwa mwana wa Ethini. Ethini alikuwa mwana wa Zera. Zera alikuwa mwana wa Adaia.
\q2
\v 42 Adaia alikuwa mwana wa Ethani. Ethani alikuwa mwana wa Zima. Zima alikuwa mwana wa Shimei.
\q2
\v 43 Shimei alikuwa mwana wa Yahathi. Yahathi alikuwa mwana wa Gerishomu. Gerishomu alikuwa mwana wa Lawi.
\q
\v 44 Upande wa mkono wa kushoto wa Hemani walikuwa wafanyi kazi wa wana wa Merari. Alikuwa Ethani mwana wa Kishi. Kishi alikuwa mwana wa Abdi. Abdi alikuwa mwana wa Maluki.
\q2
\v 45 Maluki alikuwa mwana wa Hashabia. Hashabia alikuwa mwana wa Amazia. Amazia alikuwa mwana wa Hilikia.
\q2
\v 46 Hilikia alikuwa mwana wa Amzi. Amzi alikuwa mwana wa Bani. Bani alikuwa mwana wa Shemeri.
\q2
\v 47 Shemeri alikuwa mwana wa Mahili. Mahili alikuwa mwana wa Mushi. Mushi alikuwa mwana wa Merari. Merari alikuwa mwana wa Lawi.
\p
\v 48 Washirika wao, Walawi, walipewa kazi yote ya hema, nyumba ya Mungu.
\p
\v 49 Aruni na wana wake walitoa sadaka katika madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketeza; na sadaka katika madhabahu ya uvumba kwa kazi zote katika pa patakatifu. Hizi sadaka zilifanya maombezi kwa ajili ya Waisraeli, kwa kadiri ya yote ambayo Musa mtumishi wa Mungu aliwaamuru.
\q
\v 50 Uzao wa Aruni una kumbukwa kama ifuatavyo: Mwana wa Aruni alikuwa Eleazari. Mwana Eleazari alikuwa Finehasi. Mwana wa Finehasi alikuwa Abishua.
\q2
\v 51 Mwana wa Abishua alikuwa Buki. Mwana wa Buki alikuwa Uzi. Mwana wa Buki alikuwa Zerahia.
\q2
\v 52 Mwana wa Zerahia alikuwa Meraiothi. Mwana wa Meraiothi alikuwa Amaria. Mwana wa Amaria alikuwa Ahitubi.
\q2
\v 53 Mwana wa Ahitubi alikuwa Zadoki. Mwana wa Zadoki alikuwa Ahimazi.
\p
\v 54 Hizi ni sehemu ambazo wazao wa Aruni walipangiwa kuishi, wazao wa Aruni ambao walitoka katika koo za Wakohathi (maeneo ya kwanza yalikuwa yao).
\pi
\v 55 Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda na nchi ya malisho,
\v 56 lakini maeneo ya mji na vijiji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
\pi
\v 57 Kwa wazao wa Aruni waliwapa: Hebroni (mji wa makimblio), na Libina pamoja na nchi ya malisho, Yatiri, Eshitemoa pamoja na nchi ya malisho,
\v 58 Hileni pamoja na nchi ya malisho, na Debiri pamoja na nchi ya malisho.
\v 59 Na Ashani pamoja na nchi ya malisho na Bethi Shemeshi pamoja na nchi ya malisho;
\v 60 na kutoka katika kabila la Benjamini walipewa Geba pamoja na nchi ya malisho, Alemethi pamoja na nchi ya malisho, na Anothothi na nchi ya malisho. Jumla ya miji yao ilikuwa kumi na tatu.
\p
\v 61 Kwa mwengine wa Kohathi waliwapa kwa sehemu miji kumi kutoka kwa kabila la Manase.
\p
\v 62 Kwa uzao wa Gerishomu kwa koo zao tofauti walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri, Naftali, na nusu ya kabila la Manase huko Bashani.
\p
\v 63 Kwa uzao wa Merari walipewa miji kumi, kulingana na koo zao, kutoka kwa makabila ya Rubeni, Gadi, na Zebuluni.
\p
\v 64 Hivyo watu wa Israeli walitoa hii miji pamoja na nchi za malisho kwa Walawi.
\v 65 Waligawa kwa kura miji iliyo tajwa kwa majina kutoka katika kabila za wana wa Yuda, Simeoni, na Benjamini.
\p
\v 66 Kwa baadhi ya koo za Wakohathi walitoa miji kutoka kwa kabila la Efraimu.
\pi
\v 67 Waliwapa: Shekemu (mji wa makimbilio) pamoja na nchi ya malisho katika milima ya Efraimu, Gezeri na nchi ya malisho,
\v 68 Jokimeamu pamoja na nchi ya malisho, Bethi Horoni pamoja na nchi ya malisho,
\v 69 Aiyaloni pamoja na nchi ya malisho, na Gathi Rimoni pamoja na nchi ya malisho.
\pi
\v 70 Nusu ya kabila la Manase waliwapa Wakohathi: Aneri pamoja na nchi ya malisho na Bileamu pamoja na nchi ya malisho. Hizi zikawa mali za koo za Wakohathi.
\p
\v 71 Kwa uzao wa Gerishomu kutoka koo za nusu ya kabila la Manase, waliwapa: Golani huko Baashani na nchi ya malisho na Ashitarothi pamoja na nchi ya malisho.
\q2
\v 72 Kabila la Isakari liliwapa uzao wa Gerishomu: Kedeshi pamoja na nchi ya malisho, Dabera pamoja na nchi ya malisho,
\v 73 Ramothi pamoja na nchi ya malisho, na Anemu pamoja na nchi ya malisho.
\q2
\v 74 Isakari alipokea kutoka kwa kabila la Asheri: Mashali pamoja na nchi ya malisho, Abdoni pamoja na nchi ya malisho,
\v 75 Hukoki pamoja na nchi ya malisho, na Rehobu pamoja na nchi ya malisho.
\q2
\v 76 Walipokea kutoka kabila la Naftali: Kedeshi iliyo Galileya pamoja na nchi ya malisho, Hamoni pamoja na nchi ya malisho, na Kiriathaimu pamoja na nchi ya malisho.
\q
\v 77 Wazao wengine wa Merari walipokea kutoka Kwa kabila la Zebuluni: Yokineamu, Karita na Rimono pamoja na nchi ya malisho na Tabori pamoja na nchi ya malisho;
\q2
\v 78 na kutoka kabila la Rubeni upande wa pili wa Yordani upande wa mashariki wa Yeriko, walipokuwa Bezeri katika jangwa, Yahza,
\v 79 Kedemothi pamoja na nchi ya malisho, na Mefathi pamoja na nchi ya malisho
\q2
\v 80 Walawi walipokea kutoka kabila la Gadi: Ramothi ya Gileadi pamoja na nchi ya malisho, Mahanaimu pamoja na nchi ya malisho,
\v 81 Heshiboni pamoja na nchi ya malisho, na Yazeri pamoja na nchi ya malisho.
\c 7
\cl Sura 7
\p
\v 1 Wana wanne wa Isakari walikuwa Tola, Pua, Yashubi, na Shimironi.
\q
\v 2 Wana wa Tola walikuwa Uzi, Refaia, Yerie, Yamai, Ibisami, Samueli. Walikua vichwa katika nyumba za koo zao, toka uzao wa Tola na waliorodheshwa kama mashujaa hodari miongoni mwa kizazi chao. Katika siku za Daudi walikua na idadi ya 22,600.
\q
\v 3 Mwana wa Uzi alikua Izrahia. Mwana wake walikua Michaeli, Obadia, Yoeli, na Ishia, wote watano walikua viongozi wa ukoo
\q2
\v 4 Pamoja nao walikua na jeshi la watu elfu thelathini na sita wa mapambano, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao, kwa kuwa walikuwa na wake wengi pamoja na wana wa kiume.
\q
\v 5 Ndugu zao kutoka koo zote za Isakari, walikua na mashujaa hodari themanini na saba, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
\q2
\v 6 Wana watatu wa Benjamini walikuwa Bela, Beka, na Yediaeli.
\q
\v 7 Wana watano wa Bela walikuwa Ezibono, Uzi, Uzieli, Yerimoti, na Iri. Walikua ni viongozi wa koo na mashujaa hodari. Walikuwa na idadi 22,034, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
\q2
\v 8 Wana wa Beka walikuwa Zemira, Yoashi, Elieza, Elionai, Omri, Yeremoti, Abiya, Anatoti, na Alemeti. Wote hawa walikuwa wana wake.
\q2
\v 9 Orodha ya koo zao ilikua na idadi ya 20,200 viongozi wa koo zao mashujaa hodari.
\q
\v 10 Mwana wa Yediaeli alikuwa Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa Yeushi, Benjamini, Ehudi, Kenaana, Zetani, Tarishishi, na Ahishahari.
\q
\v 11 Wote hawa waikuwa wana wa Yediaeli. Waliorodheshwa katika ukoo orodha ilikuwa 17,200 viongozi wa nyumba na mashujaa hodari waliofa kwa huduma ya kijeshi.
\q
\v 12 Shupimu na Hupimu walikuwa waza wa Iri, na Hushimu walikuwa wazao wa Aheri.
\q
\v 13 Wana wa Naftali walikuwa Yazieli, Guni, Yezeri, na Shilemu, wazao wa Bilhahi.
\q
\v 14 Wazao wa Manasse walikua Asrieli, liyekuwa uzao wake kupitia suria wake wa Kiaramia. (Pia alimzaa Makiri, baba wa Gileadi.
\q2
\v 15 Kisha Makiri alimchukua mke wake kutoka kwa Hupimu na Shupimu na jinala dada yake lilikuwa Maaka.) Jina la wa pili ilikuwa Zelofehadi, ambaye alikuwa na mabinti pekee.
\q2
\v 16 Kisha Maaka, mke wa Makiri, alimzaa mwana wa kiume na alimuita Pereshi, na jina la Kaka yake lilikua Shereshi, na wana wake walikuwa Ulamu na Rakemu.
\q2
\v 17 Mwana wa Ulami alikuwa Bedani. Hawa walikuwa uzao wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase.
\q
\v 18 Dada wa Gileadi Hamoleketi alimzaa Ishihodi, Abiezeri, na Mahila.
\q
\v 19 Wana wa Shemida walikuwa Ahiana, Shekemu, Liki, na Aniamu.
\q
\v 20 Uzao wa Efraimu ulikuwa kama ifuatavyo: Efraimu mwana wa Shutela. Shutela mwana wa Beredi. Beredi mwana wa Tahati.
\q2
\v 21 Tahati mwana wa Eleada. Eleada mwana wa Shutela. Eza na Eleadi waliuawa na wanaume wa Gati, wenyeji wa nchi, walipoenda kuiba mifugo yao.
\v 22 Efraimu baba yao aliomboleza kwa siku nyingi, na kaka zake walikuja kumfariji.
\q
\v 23 Alilala na mkewe. Akapata mimba akamzaa mwana. Efraimu akamuita Beria, kwa sababu maafa yalishakuja nyumbani mwake.
\v 24 Binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga miji juu na chini Beth Horon na Uzzen Sheerah.
\q
\v 25 Mwana wake alikuwa Rafa. Mwana wa Rafa alikuwa Reshefi. Mwana wa Reshafi alikuwa Tela. Mwana wa Tela alikuwa Tahani.
\q2
\v 26 Mwana wa Tahani alikuwa Ladani. Mwana wa Ladani alikuwa Amihudi. Mwana wa Amihudi alikuwa Elishama.
\q2
\v 27 Mwana wa Elishama alikuwa Nuni. Mwana wa Nuni alikuwa Joshua.
\p
\v 28 Mali zao na makazi yao yalikuwa Betheli na yalizungukwa na vijiji. Waliongeza upande wa mashariki hadi Naarani na upande wa magharibi hadi Gezeri na vijiji vyake, na Shekemu na vijiji vyake hadi Aya na vijiji vyake.
\q
\v 29 Katika mipaka pamoja na Manasse kulikuwa na Beti shani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake, na Dori na vijiji vyake. Katika huu mji waliishi uzao wa Josefu mwana wa Israeli.
\q
\v 30 Wana wa Asha walikuwa Imna, Ishiva, Ishivi, na Beria. Sera alikuwa dada yao.
\q
\v 31 Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malchieli, Ambaye alikuwa baba wa Birzaiti.
\q2
\v 32 Wana wa Heberi walikuwa Yafeti, Shomer, na Hotamu. Dada yao alikuwa Shua.
\q
\v 33 Wana wa Yafeti walikuwa Pasaki, Bimhali, na Ashivati. Hawa walikuwa watoto wa yafeti.
\q
\v 34 Shoma, kaka wa Yafeti alikuwa na wana hawa: Roga, Huba, na Aramu
\q
\v 35 Kaka yake Shema, Helemu, alikuwa na wana hawa: Zofa, Imna, Sheleshi na Amali.
\q2
\v 36 Wana wa Zofa walikuwa Sua, Harinefa, Shua, Beri, Imra
\v 37 Beza, Hodi, Shamma, Shilsha, Ithrani, na Beera.
\q2
\v 38 Wana wa Yeta walikuwa Yefune, Pispa, na Ara.
\q
\v 39 Wana wa Ulla walikwa Ara, Hannieli, na Rizia.
\p
\v 40 Hawa wote walikuwa uzao wa Asha. Walikuwaviongozi wa koo, wanaume mashuhuri, mashujaa hodari, na wakuu kati ya viongozi. Kulikuwa na wanaume elfu ishirini na sita walioorodheshwa waliofaa kwa utumishi ya kijeshi, kwa mujibu wa idadi iliyo orodheshwa.
\c 8
\cl Sura 8
\p
\v 1 Wana watano wa Benjamini walikuwa Bela mwana wake wa kwanza, Asibeli, Ahara,
\v 2 Noha, na Rafa.
\q
\v 3 Wana wa Bela walikuwa Adari, Gera, Abihudi,
\v 4 Abishau, Naamani, Ahoa,
\v 5 Gera, Shefufani, na Huramu.
\q2
\v 6 Hawa walikuwa uzao wa Ehudi ambao walikuwa vichwa vya koo kwa wakazi wa Geba, ambao walihimizwa kuhamia Manahati:
\v 7 Naamani, Ahijahi, na Gera. Wa mwishi, Gera, aliwaongoza katika kuhama. Alikuwa baba wa Uza na Ahihudi.
\q
\v 8 Shaharaimu akawa baba wa watoto katika ardhi ya Moabu, baada ya kuwatariki wake zake Hushimu na Baara.
\v 9 Kwa mke wake Hodeshi, Shaharaimu akawa baba wa Yobabu, Zibia, Mesha, Malkamu,
\v 10 Yeuzi, Shachia, na Mirima. Hawa walikuwa wana wake, viongozi katika koo zao.
\v 11 Alikwisha kuwa baba wa Abitubi, na Elipaali kwa Hushimu.
\q
\v 12 Wana wa Elipaali walikuwa Eba, Mishamu, na Shemedi (ambao walijenga Ono na Lodi pamoja na vijiji vilivyozunguka.)
\v 13 Pia walikuwako Beria na Shema. Walikuwa vichwa vya nyumba za baba zao wa walioishi Aijaloni, ambao waliwaondoa wakazi wa Gati.
\q2
\v 14 Beria alikuwa na wana watatu: Ahio, Shashaki, Yeremothi,
\v 15 Zebadia, Aradi, Eda,
\v 16 Mikaeli, Ishipa, na Joha
\q
\v 17 walikuwa wa na wa Beria Zebadia, Meshulamu, Hiziki, Heba,
\v 18 Ishimerai, Izilia, na Yobabu walikuwa wana wa Elipaali.
\q
\v 19 Yokimu, Zikri, Zabdi,
\v 20 Elienai, Zilletai, Elieli,
\v 21 Adaia, Beraia, na Shimrati walikuwa wana wa Shimei.
\q
\v 22 Ishipani, Eba, Elieli,
\v 23 Abdoni, Zikri, Hanani,
\v 24 Hanania, Elamu, Antothiya,
\v 25 Ifdeia, na Penueli walikuwa wana wa Shashaki.
\q
\v 26 Shamsherai, Sheharia, Athalia,
\v 27 Yaareshia, Eliya, na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
\p
\v 28 Hawa walikuwa vichwa vya koo- kwa mujibu wa kumbukumbu za koo zao walikuwa vichwa. Walikuwa wanaume wakuu walioishi Yerusalemu.
\q
\v 29 Baba wa Gibeoni, Jeieli, ambaye mke wake aliitwa Maaka, aliishi ndani ya Gibeoni.
\v 30 Mzaliwa wake wa kwanza wa kiume alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Zuri, Kishi, Baali, Nadabu
\v 31 Gedori, Ahio, na Zekari.
\q
\v 32 Mwana mwingine wa Yeieli alikuwa Mikloti, ambaye akaja kuwa baba wa Shimea. Pia wanaishi karibu na ndugu zao Yerusalemu.
\q
\v 33 Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, Malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
\q
\v 34 Mwana wa Yonathani alikuwa Meribu Baali. Meribu Baali alikuwa baba wa Mika.
\q
\v 35 Wana wa Mika walikuwa Pithoni, Meleki, Tarea, and Ahazi.
\q
\v 36 Ahazi akawa baba wa Yehoada. Yehoada alikuwa baba wa Amelethi, Azimavethi, na Zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
\q
\v 37 Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Rafa. Rafa alikuwa baba wa Eleasa. Eleasa alikuwa baba wa Azeli.
\q
\v 38 Azeli alikuwa na wana sita: Azrikamu, Bokeru, Ishimaeli, Obadia, na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Azeli.
\q
\v 39 Wana wa Esheki, kaka yake, walikuwa Ulamu mzaliwa wake wa kwanza, Yeushi wa pili, na Elifeleti wa tatu.
\q2
\v 40 Wana wa Ulamu walikuwa wanaume wa mapambano na warusha mishale wa zuri. Walikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla ya 150. Wote hawa walikuwa uzao wa Benjamini.
\c 9
\cl Sura 9
\p
\v 1 Kwa hivyo watu wote wa Israeli walinakiliwa ki uzao. Walinakiliwa katika vitabu vya kifalme vya Israeli. Yuda, walipelekwa matekani Babylon kwasababu ya dhambi zao.
\v 2 Wakwanza kurudi kuishi katika miiji yao walikuwa Waisraeli, Makuhani, Walawi, na Watumishi wa hekalu.
\p
\v 3 Baadhi ya uzao wa Yuda, Benjamin, Efraimu, na Manase waliishi Yerusalemu.
\q
\v 4 Wahamiaji walijumusha Uthai mwana wa Ammihudi mwana wa Omri mwana wa Bani, moja ya uzao wa Perezi mwana wa Yuda.
\q
\v 5 Kati ya Washilani kulikuwa na Asaia mtoto wa kwanza na wana wake.
\q
\v 6 Kati ya uzao wa Zera alikuwa Yeuli. Uzao wao ulikuwa na namba 690.
\q
\v 7 Katika uzao Benjamini walikuwa Salu mwana wa Meshulamu mwana wa hodavia mwana wa Hssenua.
\q
\v 8 Pia walikuwa Ibneia mwana wa Yerohamu; Ela mwana wa Uzzi mwana wa Mikri; na Meshullam mwana wa Shefatia mwana waReuli mwana wa Ibnija.
\q
\v 9 Ndugu zao waliandika kwenye orodha ya namba 956 ya vizazi vyao. Wanaume wote hawa walikuwa viongozi wa koo za mababu zao.
\p
\v 10 Makuhani walikuwa Yedaia, Yehoiarib, na Yokini.
\q
\v 11 Walikuwa pia Azaria mwana wa Hilkia mwana wa Meshullamu mwana wa Zadoki mwana wa Meraioti mwana wa Ahitubi, aliyekuwa na mamlaka katika nyumba ya Mungu.
\q
\v 12 Kulikuwa na Adaia mwana wa Yerohamu mwana wa Pashuri mwana wa Malkija. Pia kulikuwa na Maasai mwanawa Adieli mwana wa Yazera mwana wa Meshulamu mwana wa Meshilemiti mwana wa Imma.
\q
\v 13 Ndugu zao, ambao walikuwa viongozi katika koo za mababu zao, idadi ya 1,760. Walikuwa ni wanaume wenye uwezo sana wa kufanya kazi katika nyumba ya Mungu.
\q
\v 14 Kati ya Walawii, kulikuwa na Shemaia mwana wa Hashubu mwana wa Azrikam mwana wa Hashabia, kati ya uzao wa Merari.
\q
\v 15 Walikuwako pia Bakbakari, Hereshi, Galali, na Mattania mwana wa Mika mwana wa Zikri mwana wa Asafu.
\q
\v 16 Walikuwako pia Obadia mwana wa Shemaia mwana wa Galali mwana wa Yedutuni; na Berekia mwana wa Asa mwana wa Elkana, aliyeishikatika vijiji vya Wanetophathi.
\q
\v 17 Walinzi wa lango walikuwa Shalumu, Akubi, Talimoni, Ahimani, na uzao wao. Shalumu alikuwa kiongozi wao.
\v 18 Awali walisimama kulinda katika geti la mfalme upande wa mashariki wa kambi ya uzao wa Walawi.
\q2
\v 19 Shalumu mwana wa Kore mwana wa Ebiasafu, ambaye kama mwana wa Kora, na ndugu zake kutoka nyumba ya baba yake, Korahite, alikuwa na mamlaka kwa kazi ya huduma, Walilinda mlango wa hema, kama mababu zao walivyolinda kambi ya Yawehi, na pia walilinda lango la kuingilia.
\q
\v 20 Finehasi mwana wa Eleaza aliwaongoza kipindi cha nyuma, na Yahwehi alikuwa pamoja nae.
\q
\v 21 Zekaria mwana wa Meshelemia alikua mlinzi katika mlango wa kuingilia hekalu, “eneo la kukutania.”
\p
\v 22 Hawa wote walichaguliwa kana walinzi wa mageti ya kuingilia kwa idadi ya 212. Majina yao yaliandikwa kwenye kumbukumbu za watu katika vijiji vyao. Mtabiri aliwaweka Daudi na Samueli katika nafasi ya uaminifu.
\v 23 Kwa hivyo wao na watoto wao walilinda mageti katika nyumba ya Yaweh, hema la kuabudia.
\v 24 Walinzi wa mageti waliwekwa katika pande zote nne, upande wa mashariki, magharibi, kaskazini, na kusini.
\v 25 Kaka zao, walioishi kwenye vijiji vyao, walikuja kuwasaidia baada ya mzunguko wa siku saba.
\v 26 Lakini viongozi wanne wa walinzi, ambao walikwa walawi, walipangiwa kulinda vyumba na vyumba vya kuhifadhi katika nyumba ya Mungu.
\v 27 Walitumia usiku wao sehemu walizowekwa kuzunguka nyumba ya Mungu, kwao ilikuwa ni wajibu wao kulinda. Na walifungua geti kila asubuhi.
\p
\v 28 Baadhi yao waliwajibika katika hekalu la vifaa; walihesabu makala zilizo ingizwa ndani na zilizo tolewa nje.
\v 29 Baadhi yao pia waliwekwa kutunza vitu vitakatifu, vifaa, na vitu, kujuisha unga safi, mvinyo, mafuta, manukato, na uvumba.
\v 30 Baadhi ya wana wa makuhani walichanganya uvumba.
\v 31 Matithia, mmoja wa walawi, ambaye alikuwa mtoto wa kwanza wa Shalumu wa Wakorahi, alikuwa na wajibu wa kuandaa mikate kwa ajili ya sadaka.
\v 32 Baadhi ya kaka zao, uzao wa kohathite, waliwajibika kwa mikate ya uwepo, kuandaa kila Sabato.
\p
\v 33 Waimbaji na viongozi wa familia ya Walawi waliishi ndani ya vyumba katika mahali takatifu walipo kuwa hawafanyi kazi, kwa sababu wapiswa kufanya kazi walio pangiwa usiku na mchana.
\p
\v 34 Hawa walikuwa viongozi wa familia miongoni mwa Walawi, kama ilivyo orodheshwa katika kumbukumbu za uzao wao. Waliishi Yerusalemu.
\q
\v 35 Baba wa Gibeoni, Yeiel, ambaye mkewe aliitwa Maaka, aliishi Gibeoni.
\q
\v 36 Mtoto wake wa kwanza alikuwa Abdoni, alafu wana wake Zuri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,
\v 37 Gedori, Ahio, Zekaria, na Mikloti.
\q2
\v 38 Mikloti alikuwa baba wa Shimeamu. Pia waliishi karibu na kaka yao huko Yerusalemu.
\q
\v 39 Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
\q
\v 40 Mwana wa Jonathani alikuwa Merib baali. Merib baali alikuwa baba wa Mika.
\q
\v 41 Mwana wa Mika walikuwa pithoni, Meleki, Tahrea, na ahazi.
\q2
\v 42 Ahazi alikuwa baba wa Jara. Jara alikuwa baba wa Alemeti, Azmaveti, na zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
\v 43 Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Refaia. Refaia alikuwa baba wa Eleas. Eleasa alikuwa baba wa Azeli.
\q2
\v 44 Wana sita wa Azeli walikuwa Azrikamu, Bochera, Ishmaeli, shearia, Obdia, na Hanani. Hawa walikuwa wana wa
\c 10
\cl Sura 10
\p
\v 1 Wafilisti wakapigana dhidi ya Israeli. Kila mwanaume wa Israeli alikimbia Wafilisti na kuanguka na kufa katika Mlima Giliboa.
\v 2 Wafilisti waliwakimbiza Sauli na mwanae. Waflisti walimuua Yonathani, Abinadabu, na Malikishua, wana wake.
\v 3 Pambano lilikuwa zito kwa Sauli, na wapiga mishale wakamshambulia na kumjeruhi.
\p
\v 4 Kisha Sauli akasema kwa mbeba ngao wake, “Vuta upanga wako na unichome nao. Lasihivyo, hawa wasio tahiriwa watukuja na kunitesa.” Lakini mbeba ngao wake hakutaka, kwa kuwa aliogopa sana. Kwa hiyo Sauli akachukuwa upanga wake na kuuangukia.
\p
\v 5 Mbeba ngao alivyoona kuwa Sauli amekufa, naye akaangukia upanga wake na kufa.
\v 6 Kwaiyo Sauli akafa, na wana wake watatu, wote wa nyumba yake wakafa pamoja.
\p
\v 7 Kila mwanaume wa Israeli katika bonde alivyoona kuwa wamekimbia, na Sauli na wana wake wamekufa, walitelekeza miji yao na kukimbia. Kisha Wafilisti wakaja na kuishi humo.
\p
\v 8 Ikawa siku inayofuata, Wafilisti walipo kuja kukagua wafu, walimkuta Sauli na wana wake wameanguka katika Mlima Giliboa.
\v 9 Wakamvua nguo zote na kuchukuwa kichwa chake na ngao yake. Wakatuma wajumbe wapeleke habari Filistia yote kwa miungu yao na watu wote.
\v 10 Ngao yake wakaeka ndani ya hekalu la miungu yao, na kichwa chake waka kining'iniza katika hekalu la Dagoni.
\p
\v 11 Wakati Yabeshi Gileadi yote ilipo sikia Wafilisti waliyo mtendea Sauli,
\v 12 wanaume wote wa vita wakaenda na kuchukuwa mwili wa Sauli na hiyo ya wanae, na kuirejesha Yabeshi. Walizika mifupa yao chini ya mti huko Yabeshi na wakafunga siku saba.
\p
\v 13 Hivyo Sauli akafa kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwa Yahweh. Hakutii maelekezo ya Yahweh, lakini akauliza ushauri kwa mtu anaye ongea na wafu.
\v 14 Hakutafuta mwongozo kwa Yahweh, hivyo Yahweh akamua na kupindua ufalme kwa Daudi mwana wa Yese.
\c 11
\cl Sura 11
\p
\v 1 Kisha Waisraeli wote walikuja Hebroni kwa Daudi na kusema, “Angalia, sisi ni nyama na mifupa yako.
\v 2 Katika wakati uliopita, Sauli alipoo kuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliye ongoza jeshi la Israeli. Yahweh Mungu wako alisema kwako, utawachunga watu wangu wa Isaraeli, na utakuwa mtawala wa watu wangu wa Israeli.’”
\p
\v 3 Kwaiyo wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni, na Daudi akafanya agano nao mbele ya Yahweh. Wakampaka mafuta Daudi kuwa mfalme wa Israeli. Kwa namna hii, neno la Yahweh lilo nenwa na Samweli likawa kweli.
\p
\v 4 Daudi na Israeli yote wakaenda Yerusalemu (yani, Yebusi). Sasa Wayebusi, wakazi wa nchi, walikuwa pale.
\v 5 Wakazi wa yebusi wakamwabia Daudi, “Hautakuja humu.” Lakini Daudi alichukuwa ngome ya Sayuni, mji wa Daudi.
\p
\v 6 Daudi alikuwa amesema, “Yeyote atakaye washambulia Wayebusi akiwa wa kwanza atakuwa mkuu na komanda wa jeshi.” Kwaiyo Yoabu mwana wa Zeruia akashambulia wa kwanza, hivyo akafanywa mkuu wa jeshi.
\p
\v 7 Kisha Daudi akaanza kuishi katika ngome. Kwaiyo wakaiita mji wa Daudi.
\v 8 Akaimarisha mji kutoka Milo na hadi mpaka ukuta unao zunguka. Yoabu akaimairisha mji wote uliyo baki.
\v 9 Daudi akawa mkuu na mkuu kwa sababu Yahweh wa Majeshi alikuwa naye.
\p
\v 10 Hawa walikuwa viongozi Daudi aliyo kuwa nao, waliyo jionyesha imara katika ufalme wake, pamoja na Israeli, kumfanya mfalme, kutii neno la Yahweh kuhusu Israeli.
\v 11 Hii ni orodha ya wanajeshi shupavu wa Daudi. Yashobeami, mwana wa Mhakimoni, alikuwa mkuu wa kikosi cha thelathini. Aliwaua wanaume mia tatu na mkuki wake katika sehemu moja.
\p
\v 12 Baada ya yeye alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, Mahohi, aliyekuwa mmoja wa wanaume watatu hodari.
\v 13 Alikuwa na Daudi huko Pasidamimu, na pale Wafilisti wakakusanyika pamoja kwa mapambano, ambapo palikuwa na uwanja wa ngano na jeshi liliwakimbia Wafilisti.
\v 14 Walisimama katikati ya uwanja. Wakautetea na kuwakata Wafilisti na Yahweh akawaokoa na ushindi mkubwa.
\p
\v 15 Kisha watatu wa viongozi thelathini wakashuka chini kwenye mwamba wa Daudi, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti walieka kambi katika bonde la Refaim.
\v 16 Kwa wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu.
\v 17 Daudi alikuwa na kiu ya maji na akasema, “Laiti mtu akanipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho Bethilehemu, kisima kilicho pembeni mwa lango!”
\v 18 Hawa wanaume hodari watatu wakatoboa kupita jeshi la Wafilisti na kuchota maji kwenye kisima cha Bethilehemu, kisima pembeni mwa lango. Wakachukuwa maji na kumletea Daudi, lakini alikataa kunywa. Badala yake, akamwaga chini kwa Yahweh.
\v 19 Kisha akasema, “Iwe mbali mbele ya Mungu kwamba nifanye hivi Je ninywe damu ya wanaume hawa walio hatarisha maisha yao?” Kwa sababu waliyaweka maisha ya hatarini, Daudi akakataa kuyanywa. Haya ni matendo ya wale mashujaa
\p
\v 20 Abishai kaka wa Yoabu, alikuwa kiongozi wa wale watatu. Aliwahi kutumia mkuki wake dhidi ya watu mia tatu na kuwaua. Ametajwa pamoja na wale watatu.
\v 21 Kati ya wale watatu, yeye alipewa heshima mara mbili na akawa kiongozi wao, ijapo hakuwa mmoja wa miongoni mwao.
\p
\v 22 Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa shujaa jasiri kutoka Kabizeli, aliye fanya matendo makuu. Aliua wana wawili wakiume wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka chini ya shimo na kumuua simba wakati theluji ilikuwa ikianguka.
\v 23 Hata alimuua Mmisri, mwanaume mwenye mita mbili na theluthi moja. Mmisri alikuwa na mkuki kama gongo la mshonaji, lakini alimfuata chini na fimbo tu. Akakamata mkuki katika mkono wa Mmisri na kumuua na mkuki wake.
\v 24 Benaia mwana wa Yehoiada alifanya haya matukio, na akatajwa miongoni mwa wale wanaume hodari watatu.
\v 25 Alisifika zaidi ya wale wanajeshi thelathini kwa ujumla, lakini hakuwa pewa hadhi ya wale wanajeshi watatu hodari. Lakini Daudi alimweka juu ya walinzi wake.
\q
\v 26 Mashujaa hodari walikuwa Asaheli kaka wa Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethilehemu,
\q2
\v 27 Shamothi Mherori, Helezi Mpeloni,
\q2
\v 28 Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abieza Manathothi,
\q2
\v 29 Sibekai Mhushathite, Ilai Mahohi,
\q2
\v 30 Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathite,
\q2
\v 31 Itai mwana wa Ribai wa Gibea uzao wa Benjamini, Benaia Mpirathoni,
\q2
\v 32 Hurai wa mabonde ya Gaashi, Abieli Marbathi,
\q2
\v 33 Azmavethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,
\q2
\v 34 wana wa Hashemu Mgizoni, Yonathani mwana wa Shagee Mharari,
\q2
\v 35 Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, Elifali mwana wa Uri,
\q2
\v 36 Hefa Mmekarathi, Ahija Mpeloni,
\q2
\v 37 Hezro Mkarimeli, Naarai mwana wa Ezibai,
\q2
\v 38 Yoeli kaka wa Nathani, Mibhari mwana wa Hagiri,
\q2
\v 39 Zeleki Mamoni, Naharai Mberothi (mbeba ngao ya Yoabu mwana wa Zeruia),
\q2
\v 40 Ira Mithire, Garebu Mithire,
\q2
\v 41 Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Ahlai,
\q2
\v 42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni (kiongozi wa Wareubeni) na thelathini pamoja naye,
\q2
\v 43 Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithini,
\q2
\v 44 Uzia Mashiterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Waaroeri,
\q2
\v 45 Jediaeli mwana wa Shimri, Joha (kaka yake Mtize),
\q2
\v 46 Elieli Mmahavi, Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu, Ithima Mmoabi,
\q2
\v 47 Elieli, Obedi, na Yaasieli mmezobai.
\c 12
\cl Sura 12
\p
\v 1 Hawa walikuwa wanaume walio kuja kwa Daudi huko Zikilagi, wakati akiwa bado amefukuzwa katika uwepo wa Sauli mwana wa Kishi. Walikuwa miongoni mwa wanajeshi, wasaidizi wake katika mapambano.
\v 2 Walikuwa wana upinde na waliweza kutumia mkono wa kuume na wakushoto kurusha mawe na manati na kupiga mishale kutoka kwenye upinde. Walikuwa Wabenjamini, jamaa wa Sauli.
\p
\v 3 Kiongozi alikuwa Ahi Eza, halafu Yoashi, Wana wote wa Shemaa Mgibeathi. Kulikuwa na Yezieli na Peleti, wana wa Azimavethi. Kulikuwa pia na Beraka, Yehu Waanathothi,
\q
\v 4 Ishimaia Mgibeoni, mwanajeshi kati ya wale thelathini (na kiongozi wa wale thelathini); Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi Mgederathi
\q
\v 5 Eluzai, Yerimothi, Bealia, Shemaria, Shefatia Mharufi,
\q
\v 6 Wakorahi ni Elkana, Ishia, Azareli, Yoeza, Yashobeamu, na
\q
\v 7 Yoela na Zebadia, wana wa Yeroham wa Gedori.
\p
\v 8 Baadhi ya Wagadi walijiunga na Daudi katika ngome iliyo nyikani. Walikuwa mashujaa hodari, wanaume wa vita, tayari kwa vita, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesikama swala juu ya milima.
\q
\v 9 Kulikuwa na Eza kiongozi, Obadia wapili, Eliabu watatu,
\q
\v 10 Mishimana wanne, Yeremia watano,
\q
\v 11 Atai wasita, Elieli wasaba,
\q
\v 12 Yohanani wanane, Elizabadi watisa,
\q
\v 13 Yeremia wakumi, Makibanai wakumi na moja.
\p
\v 14 Wana wa Gadi walikuwa viongozi wa jeshi. Wamwisho aliongoza mia moja, na mkubwa aliongoza elfu moja.
\v 15 Walivuka Yordani mwezi wa kwanza, ilipofurika kingo zake, na kuwafanya wote wanaoishi katika mabonde kukimbia, kuelekea mashariki na kuelekea magharibi.
\p
\v 16 Baadhi ya wanaume wa Benjamini na Yuda walikuja kwenye ngome kwa Daudi.
\v 17 Daudi alienda nje kuwasalimu na kuwahutubia: “kama mmekuja kwa amani kunisaidia, moyo wangu utaungana nanyi Lakini kama mmekuja kunisaliti kwa maadui zangu, Mungu wa mababu zetu awaone na kuwakemea, kwa kuwa sijakosa.”
\p
\v 18 Kisha roho ikaja juu ya Amasai, ambaye alikuwa kiongozi wa wale thelathini. Amasai alisema, “Sisi ni wako, Daudi. Sisi tupo upande wako, mwana wa Yesse. Na amani iwe juu ya yeyote atakaye kusaidia. Amani na iwe wanaokusaidia, kwa kuwa Mungu wako anakusaidia.” Kisha Daudi akawapokea na kuwafanya wakuu wa watu wake.
\p
\v 19 Baadhi kutoka kwa Manase pia wakamwendea Daudi alipokuja na Wafilisti dhidi ya Sauli katika pambano. Lakini hawakuwasaidia Wafilisti kwasababu mabwana wa Wafilisti walishauriana na wakamfukuza Daudi. Walisema, “Atamwendea Bwana wake Sauli na kuhatarisha maisha yetu.”
\v 20 Alipokwenda kwa Zikilagi, wanaume wa Manase walioungana nae walikuwa Adina, Yozabadi, Yediaeli, Yozabadi, Elihu, na Zilethai, viongozi wa maelfu wa Manase.
\v 21 Walimsaidia Daudi kupigana na kikundi cha wezi, maana walikuwa wanaume wa mapambano. Baadae walikuwa wakuu katika jeshi.
\v 22 Siku hadi siku, wanaume walikuja kwa Daudi kumsaidia, mpaka wakawa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
\p
\v 23 Hii ni kumbukumbu ya wanajeshi wa vita, walio kuja kwa Daudi Hebroni, kuupindua ufalme wa Sauli kwake, ilikutimiza neno la Yahweh.
\q
\v 24 Waanume wa Yuda walio beba ngao na mkuki ni 6,800, tayari kwa vita.
\q
\v 25 Kutoka kwa Wasimeoni walikuwa 7,100 mashujaa hodari waliofunzwa vita.
\q
\v 26 Kutoka kwa Walawi kulikuwa na wanaume wa mapambano 4,600.
\q2
\v 27 Yehoiada alikuwa kiongozi wa uzao wa Aruni, na kwa yeye walikuwa 3,700.
\q2
\v 28 Pamoja na Zadok, kijana mmoja, shujaa wa vita, walikuwa viongozi ishirini na mbili kutoka ukoo wake
\q
\v 29 Kutoka kwa Benjamini, jamaa ya Sauli, walikuwa elfu tatu. Wengi wao walikuwa wameilinda nyumba ya Sauli mpaka wakati huu.
\q
\v 30 Kutoka kwa Waefraimu palikuwa na mashujaa wa vita 20,800, wanaume maarufu kwenye koo zao.
\q
\v 31 Kutoka kabila nusu la Manase palikuwa na wanaume elfu kumi na nane maarufu walio kuja kufanya Daudi mfalme.
\q
\v 32 Kutoka kwa Isakari, palikuwa na viongozi mia mbili waliokuwa na ufahamu wa nyakati na walijua kile ambacho Israeli walipaswa kufanya. Ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
\q
\v 33 Kutoka Zebuloni palikuwa na wanaume elfu hamsini wa mapambano, tayari kwa vita, na silaha zote za vita, na tayari kutoa uwaminifu usiogawanyika.
\q
\v 34 Kutoka kwa Naftali palikuwa na askari elfu moja, na pamoja nao wanaume elfu thelathini na saba wenye ngao na mikuki.
\q
\v 35 Kutoka kwa Wadani palikuwa na wanaume 28,600 wameandaliwa kwa ajili ya pambano.
\q
\v 36 Kutoka kwa Asheri palikuwa na wanaume elfu arobaini wameandaliwa kwa pambano.
\q
\v 37 Kutoka upande wa pili wa Yordani, kutoka kwa Warubeni, Wagadi, na nusu kabila la Manase, palikuwa na wanaume 120,000 wameandaliwa na silaha za kila namna kwa ajili ya pambano.
\p
\v 38 Hawa wanajeshi wote, waliandaliwa kwa pambano, walikuja Hebroni na moyo wote ili kumfanya Daudi awe mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wote waliosalia walikubali kumfanya Daudi mfalme pia.
\v 39 Walikuwa pale na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa kuwa jamaa zao waliwapa mahitaji ya kwenda nayo.
\v 40 Kwa kuongezea, wao walio kuwa karibu nao, kwa umbali wa Isakari na Zebuloni na Naftali, walileta mkate kwa punda, ngamia, nyumbu na fahali, na keki za tini, mvinyo, vishada vya zabibu kavu, divai, mafuta, ng'ombe na kondoo, kwa maana kulikwa na furaha katika Israeli.
\c 13
\cl Sura 13
\p
\v 1 Daudi akashuriana na wakuu wa jeshi la maelfu na mamia, na kila kiongozi.
\v 2 Daudi akasema kwa kusanyiko la Isaraeli, “Kama itakuwa vyema, na kama hii inatoka kwa Yahweh Mungu wetu, na tutume wajumbe kila sehemu kwa ndugu zetu walio baki maeneo yote ya Israeli, na kwa makuhani na Walawi walio kwenye miji yao. Waambiwe wakunje wajiunge nasi.
\v 3 Na tulirudishe kwetu wenyewe sanduku la Mungu wetu; kwa maana hatukutafuta mapenzi yake katika siku za utawala Sauli.”
\v 4 Kusanyiko lote liliafiki kufanya haya yote, kwa kuwa yalionekana sawa machoni pa watu wote.
\p
\v 5 Kwaiyo Daudi akakusanya Israeli yote, kutoka mto Shihori ulio Misri hadi Lebo Hamathi, kuleta sandaku la Mungu kutoka Kiriathi Yearimu.
\v 6 Daudi na Israeli yote walienda mpaka Baala, ambayo ni, Kiriathi Yearimu, ambao ni ya Yuda, kuleta sanduku la Mungu, ambalo linaitwa kwa jina la Yahweh, Yahweh, aketiye juu ya makerubi.
\p
\v 7 Kwa hiyo wakaliweka sanduku la Mungu juu ya mkokoteni mpya. Wakalilitoa nje ya nyumba ya Abinadabu. Uza na Ahio walikuwa wakiongoza mkokoteni.
\v 8 Daudi na Israeli yote walikuwa wakishangilia mbele za Mungu kwa nguvu zao zote. Walikuwa wakiimba kwa vinubi, na vinanda, matari, upatu, na tarumbeta.
\p
\v 9 Walipo kuja eneo la kupepeta mazao huko Kidoni, Uza alinyoosha mkono wake ili kukamata sanduku kwa sababu ng'ombe walijikwa.
\v 10 Hasira ya Yahweh ikawaka juu ya Uza, na Yahweh akamua kwa sababu Uza alishika na mkono wake sanduku. Akafa pale mbele za Mungu.
\p
\v 11 Daudi alipatwa na hasira kwa kuwa Yahweh alimshambulia Uza. Hiyo sehemu inaitwa Perezi Uza hadi leo.
\p
\v 12 Daudi alimuogopa Mungu hiyo siku. Akasema, “Nawezaje kuleta sanduku la Mungu nyumbani mwangu?”
\v 13 Kwa hiyo Daudi hakuleta sanduku kwenye mji wa Daudi, lakini aliweka pembeni mwa nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.
\v 14 Sanduku la Mungu lilibaki nyumbani mwa Obedi Edomu kwa miezi mitatu. Kwaiyo Yahweh akabariki nyumba yake na yote aliyo miliki.
\c 14
\cl Sura 14
\p
\v 1 Kisha Hiramu mfalme wa Tire alituma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, maseremala, na wajenzi. Walijenga nyumba kwa ajili yake.
\v 2 Daudi alijua kuwa Yahweh alimfanya kuwa mfalme juu ya Waisraeli, na hivyo ufalme wake ulitukuzwa juu sana kwa ajili ya watu wa Israeli.
\p
\v 3 Ndani ya Yerusalemu, Daudi aliongeza wake, na akawa baba wa wana wengi na mabinti.
\v 4 Haya yalikuwa majina ya watoto waliozaliwa nae huko yerusalemu: Shammua, Shobabu, Nathani, Suleimani,
\v 5 Ibhari, Elishua, Elipeleti,
\v 6 Noga, Nefegi, Yafia,
\v 7 Elishama, Beliada, na Elifeleti.
\p
\v 8 Sasa wakati Wafilisti waliposikia Daudi amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Waisraeli yote, wote walitoka nje kwenda kumtafuta. Lakini Daudi alisikia kuhusu hilo naye akaenda nje kinyume nao.
\v 9 Sasa wafilisti walikuja na kufanya shambulio katika bonde la Refaimu.
\v 10 Kisha Daudi akaomba msaada kwa Mungu. Akasema, “Je niwashambulie Wafilisti? Utanipa ushindi juu yao?” Yahweh akamwambia, “Shambulia, kwa uhakika nitawakabidhi kwako.”
\p
\v 11 Kwa hivyo wakaja Baali Perazimu na akawashinda. Akasema, “Yahweh kapasua maadui zangu kwa mkono wangu kama vile mpasuko wa mafuriko ya maji.” Hivyo jina la sehemu ile likawa Baali Perazimu.
\v 12 Wafilisti walitelekeza miungu yao pale, na Daudi akatoa amri wateketezwe kwa moto.
\p
\v 13 Kisha Wafilisti wakavamia kwa mara nyingine tena.
\v 14 Hivyo Daudi akaomba msaada kwa Mungu tena. Mungu akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu ya balisamu.
\v 15 Utakaposikia sauti ya wanajeshi wanatembea kwenye upepo uvumao kutoka juu ya miti ya balisamu, kisha shambulia kwa nguvu. Fanya hivyo kwasababu Mungu atakutangulia kwenda kuwashambulia majeshi ya wafilisti.”
\v 16 Hivyo Daudi alifanya kama Mungu alivyo muamuru. Aliwashinda jeshi la Wafilisti kutoka Gibeoni mpaka Gezeri.
\p
\v 17 Kisha umaarufu wa Daudi ukaenda katika nchi zote, na Yahweh akasababisha mataifa yote kumuhofia.
\c 15
\cl Sura 15
\p
\v 1 Daudi akajingea nyumba zake katika mji wa Daudi. Akaanda sehemu kwa ajili ya sanduku la Mungu na hema lake.
\v 2 Kisha Daudi akasema, “Walawi pekee ndio watabeba sanduku la Mungu, kwa kuwa walichaguliwa na Yahweh kubeba sanduku la Yahweh, na kumtumikia milele.”
\p
\v 3 Kisha Daudi akakusanya Israeli yote Yerusalemu, kuleta sanduku la Yahweh sehemu aliyo iandaa.
\v 4 Daudi akakusanya uzao wa Aruni na Walawi pamoja.
\v 5 Kutoka uzao wa Kohathi, palikuwa na Urieli kiongozi na ndugu zake, wanaume 120.
\q
\v 6 Kutoka uzao wa Merari, palikuwa na Asaia kiongozi na ndugu zake, wanaume 220.
\q
\v 7 Kutoka uzao wa Gerishomu, palikuwa na Yoeli kiongozi na ndugu zake, wanaume 130.
\q
\v 8 Kutoka uzao wa Elizafani, palikuwa na Shemaia kiongozi na ndugu zake, wanaume 200.
\q
\v 9 Kutoka uzao wa Hebroni, palikuwa na Elieli kiongozi na ndugu zake, wanaume themanini.
\q
\v 10 Kutoka uzao wa Uzieli, palikuwa na Aminadabu kiongozi na ndugu zake, wanaume 112.
\p
\v 11 Daudi akaagiza Zadoki kuitwa na Abiathari kuhuani, na Walawi Urieli, Asaia, Yoeli, Shemaia, Elieli, na Aminadabu.
\v 12 Akasema, “Nyinyi ni viongozi wa familia za Kilawi. Jiwekeni wakfu, nyie na ndugu zenu, ilikwamba mlete sanduku la Yahweh, Mungu wa Israeli, kwenye sehemu niliyo iandaa.
\v 13 Mara ya kwanza hamkubeba. Ndio maana Yahweh Mungu wetu akawa na hasira kwetu, kwa kuwa hatuku mtafuta wala kutii amri yake.”
\p
\v 14 Hivyo makuhani na Walawi waka jiweka wakfu iliwaweze kuleta sanduku la Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 15 Hivyo Walawi wakabeba sanduku la Mungu katika mabega yao na nguzo, kama Musa alivyo amuru-kwa kufuata sheria zilizo tolewa na Yahweh.
\p
\v 16 Daudi akazungumza na viongozi wa Walawi kuwapangia ndugu zao kuwa wana muziki wenye vyombo vya muziki, vyombo vya uzi, vinubi na upatu, kwa kupiga kwa sauti na furaha wakipaza sauti zao.
\p
\v 17 Hivyo Walawi wakamchagua Hemani mwana wa Yoeli na mmoja wa kaka zake, Asafu mwana wa Berekia. Pia walimchagua ndugu wa uzao wa Merari na Ethani mwana wa Kushaia.
\v 18 Pamoja nao walikuwa ndugu wa daraja la pili: Zekarai, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaia, Maasaeia, Matithia, Elifelehu, Mikineaia, Obedi Edomu, na Yeieli, mlinzi wa lango.
\p
\v 19 Wanamuziki Hemani, Asafu, na Ethani walichaguliwa kupiga upatu wa shaba.
\v 20 Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseia, na Benaia walicheza vinanda, vilivyowekwa kwa Alamothi
\v 21 Matithia, Elifelehu, Mikineia, Obedi Edomu, Yeieli, na Azazia walitangulia kwa vinubi vilivyowekwa kwa Sheminithi.
\v 22 Kenania, kiongozi wa Walawi, aliongoza uimbaji sababu alikuwa mwalimu wa muziki.
\p
\v 23 Berekia na Elikana walikuwa walinzi wa sanduku.
\v 24 Shebania, Yoshafati, Nethanieli, Amasai, Zekaria, Benaia, na Eliezeri, makuhani, walikuwa wa kupuliza matarumbeta mbele ya sanduku la Mungu. Obedi Edomu na Yehia walikuwa walinzi wa sanduku.
\p
\v 25 Hivyo Daudi, wazee wa Israeli, na wakuu wa maelfu wakaenda kuchukua sanduku la agano la Yahweh kutoka nyumba ya Obedi Edomu kwa shangwe.
\v 26 Wakati Mungu aliwasaidia Walawi waliolichukua sanduku la agano la Yahweh, walitoa dhabihu fahali saba na kondoo waume saba
\v 27 Daudi alivishwa joho la kitani nzuri, kama vile Walawi walio beba sanduku, waimbaji, na Kenania, kiongozi wa nyimbo na waimbaji. Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
\v 28 Hivyo Israeli yote wakaleta sanduku la agano la Yahweh kwa kelele za furaha, na sauti za pembe na tarumbeta, kwa upatu, na kwa vinanda na vinubi.
\p
\v 29 Lakini sanduku la agano la Yahweh lilipoingia mji wa Daudi, Mikali binti wa Sauli, alichungulia dirishani. Akamuona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea. Kisha akamdharau moyoni mwake.
\c 16
\cl Sura 16
\p
\v 1 Wakaleta ndani Sanduku la Mungu na kuweka katikati ya hema ambalo Daudi aliandaa. Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika mbele ya Mungu.
\v 2 Daudi alipo maliza kutoa dhabiu ya kuteketeza na sadaka za ushirika, aliwabariki watu kwa jina la Yahweh.
\v 3 Alisambaza kwa kila Misraeli, mwanaume na mwanamke, kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu.
\p
\v 4 Daudi aliewapangia baadhi ya Walawi kutumika mbele ya sanduku la Yahweh, na kusheherekea, kushukuru na kumsifu Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 5 Hawa Walawi walikuwa Asafu kiongozi, wa pili kutoka kwake Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaia, Obedi Edomu, na Yeieli. Hawa walikuwa wacheze vinanda na vinubi. Asafu alikuwa apige upatu, kwa kelele.
\v 6 Benaia na Yahazieli walikuwa wakupiga tarumbeta kila mara, mbele sanduku la agano la Mungu.
\p
\v 7 Kisha katika hiyo siku Daudi akawachagua Asafu na kaka zake kuimba hii nyimbo ya shukurani kwa Yahweh.
\q1
\v 8 Mpeni shukurani Yahweh, liitieni jina lake; fahamisheni mataifa matendo yake.
\q1
\v 9 Mwiimbieni, imbeni sifa kwake; semeni matendo yake ya ajabu.
\q1
\v 10 Jisifuni katika jina lake takatifu; acha mioyo ya wanao mtafuta Yahweh ishangilie.
\q1
\v 11 Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote.
\q1
\v 12 Kumbukeni matendo aliyo ya fanya kwenu, miujiza yake na amri za kinywa chake,
\q1
\v 13 enyi uzao wa Israeli mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wateule wake.
\q1
\v 14 Yeye ni Yahweh, Mungu wetu. Amri zake zipo duniani kote.
\q1
\v 15 Tunzeni agano lake akilini mwenu milele, neno alilo liamuru kwa vizazi elfu moja.
\q1
\v 16 Anakumbuka agano alilo lifanya na Ibrahimu, na nadhiri yake kwake Isaka.
\q1
\v 17 Hili ndilo alilo lithibitisha kwa Yakobo kama amri maalumu, na kwa Israeli kama agano la milele.
\q1
\v 18 Alisema, “Nitakupa nchi ya Kanani kama sehemu ya urithi wako.”
\q1
\v 19 Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana, kuwa wageni katika nchi,
\q1
\v 20 walitangatanga kutoka taifa hadi taifa, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
\q1
\v 21 Hakumruhusu yeyote awatese; aliwahadhibu wafalme kwa ajili yao.
\q1
\v 22 Alisema, “Msiwaguse wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu.”
\q1
\v 23 Imbeni kwa Yahweh, dunia yote; tangazeni wokovu wake siku hadi siku.
\q1
\v 24 Tangazeni utukufu wake kwa mataifa, matendo yake makuu kwa mataifa yote.
\q1
\v 25 Kwa kuwa Yahweh ni mkuu na ni wakusifiwa sana, na ni wakuogopewa kuliko miungu yote.
\q1
\v 26 Kwa kuwa miungu ya mataifa ni sanamu, lakini ni Yahweh aliyeziumba mbingu.
\q1
\v 27 Fahari na ukuu zipo uweponi mwake. Nguvu na furaha zipo mahali pake.
\q1
\v 28 Mpeni sifa Yahweh, enyi koo za watu, mpeni Yahweh utukufu na nguvu;
\q1
\v 29 Mpeni Yahweh utukufu upasao jina lake. Leta sadaka na mje kwake. Muinamieni Yahweh katika fahari ya utakatifu
\q1
\v 30 Tetemeka mbele zake, dunia yote. Dunia imeimarishwa; haiwezi kutikisika.
\q1
\v 31 Mbingu nazifurahi, na dunia ishangilie; na wasema kati ya mataifa, “Yahweh anatawala.”
\q1
\v 32 Bahari na ingurume, na inayo ijaza ipige kelele kwa furaha. Mashamba yawe na furaha tele, na vyote vilivyomo ndani yake.
\q1
\v 33 Na miti iliyopo misituni ipige kelele kwa Yahweh, kwa kuwa anakuja kuhukumu dunia.
\q1
\v 34 Toeni shukurani kwa Yahweh, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake hudumu milele.
\q1
\v 35 Kisha sema, “Tuokoe, Mungu wa wokovu wetu. Tukusanye pamoja na utuokoe kutoka kwa mataifa mengine, ilikwamba tutoe shukurani kwa jina lako takatifu na tufurahi katika sifa zako.”
\q1
\v 36 Na Yahweh, Mungu wa Israeli, asifiwe kutoka milele na milele. Watu wote wakasema, “Amina” na wakamsifu Yahweh.
\v 37 Hivyo Daudi akamwacha Asafu na kaka zake pale mbele ya sanduku la Yahweh, kutumika daima mbele ya sanduku, kama kazi za kila siku zilivyo itaji. Obedi Edomu pamoja na ndugu sitini na nane walijumuishwa.
\v 38 Obedi Edomu mwana wa Yeduthuni, pamoja na Hosa, walikuwa wawe walinzi wa lango.
\p
\v 39 Zadoki kuhani na makuhani wenzake walikuwa watumike mbele ya hema la Yahweh katika mahali pa juu huko Gibeoni.
\v 40 Walikuwa watoe sadaka za kuteketeza kwa Yahweh kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketeza daima asubui na jioni, kwa mujibu wa yote yalio andikwa katika amri za Yahweh, aliyo wapa Waisraeli kama sheria.
\v 41 Hemani na Yeduthuni walikuwa nao, pamoja na walio chaguliwa kwa jina, kumpa shukurani Yahweh, kwa sababu uaminifu wa agano lake la dumu hatamilele
\v 42 Hemani na Yeduthuni walikuwa viongozi wa wao waliopiga tarumbeta, upatu, na vyombo vingine kwa muziki wa kumuabudu Mungu. Wana wa Yeduthuni walilinda lango.
\p
\v 43 Kisha watu wote walirudi nyumbani, na Daudi akarudi kuwabariki watu wa nyumbani mwake.
\c 17
\cl Sura 17
\p
\v 1 Ikawa kwamba baada ya Daudi kukaa nyumba mwake, alimwambia Nathani yule nabii, “Angalia, nina ishi katika nyumba iliyo jengwa na mierezi, lakini sanduku la agano la Yahweh lipo kwenye chini ya hema.”
\p
\v 2 Kisha Nathani akasema kwa Daudi, “Nenda, fanya yalio moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yupo nawe.”
\p
\v 3 Lakini usiku huo neno la Mungu lilimjia Nathani, nakusema,
\pi
\v 4 “Nenda umwambie Daudi mtumishi wangu, Hivi ndivyo Yahweh asemavyo: Hautanijengea nyumba ya kuishi.
\v 5 Kwa kuwa sijaishi katika nyumba toka ile siku niliyo ileta Israeli hadi leo. Badala yake, nimeishi ndani ya hema, hema la kukusanyikia, sehemu mbalimbali.
\v 6 Katika sehemu zote nilizo enda na Israeli, niliwai kusema lolote kwa viongozi wa Israeli niliyo wachagua kuwa chunga watu wangu, kwa kusema, “Kwa nini haujanijengea mimi nyumba ya mierezi?”
\pi
\v 7 “Kisha sasa, mwambie mtumishi wangu Daudi, Hili ndilo Yahweh wa majeshi anasema: Nilikuchugua kutoka malishoni, kufuata kondoo, ilikwamba uwe mtawala wa watu wangu Waisraeli.
\v 8 Nimekuwa nawe pote ulipo enda na nimewakata maadui zako wote, na na nitakufanyia jina, kama jina la wakuu wa dunia.
\v 9 Nitateua mahali pa watu wangu Israeli na nitawapanda hapo, iliwaishi sehemu yao na wasisumbuliwe tena. Watu wa ovu hawata watesa tena, kama walivyo fanya hapo awali,
\v 10 kama walivyo kuwa wakifanya toka siku zile nilipo waamuru waamuzi kuwa juu ya watu wangu Waisraeli. Kisha nitawatiisha maadui zako wote. Zaidi sana nina kwambia kwamba mimi, Yahweh, nitakujengea nyumba.
\v 11 Itakuwa siku zako zitakapotimia za wewe kwenda kwa baba zako, nitainua uzao wako baada yako, na mmoja wa uzao wako nitaimarisha ufalme wake.
\v 12 Yeye atanijengea nyumba, na nitaimarisha kiti chake cha enzi milele.
\v 13 Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwana wangu. Sitaondoa uwaminifu wa Agano langu kwake, kama nilivyo ondoa kwa Sauli, aliye tawala kabla yako.
\v 14 Nitamweka juu ya nyumba yangu na katika ufalme wangu milele, na kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele.”
\p
\v 15 Nathani akanena haya kwa Daudi na kumtaarifu, na akamwambia kuhusu maono yote.
\p
\v 16 Kisha Daudi mfalme akaenda ndani na kuketi mbele za Yahweh; akasema, “Mimi ni nani, Yahweh Mungu, na familia yangu ni nini, hadi unilete umbali huu?
\pi
\v 17 Hili lilikuwa jambo dogo machoni pako, Mungu. Umezungumzia familia ya mtumishi wako kwa muda mrefu ujao, na umenionyesha vizazi vijavyo, Yahweh Mungu.
\pi
\v 18 Nini zaidi mimi, Daudi, niseme? Umemheshimu mtumishi wako. Umempa mtumishi waki heshima ya kipekee.
\v 19 Yahweh, kwa ajili ya mtumishi wako, na kutimiza kusudi lako, umefanya hili ilikudhihirisha matendo yako yote makuu.
\pi
\v 20 Yahweh, hakuna aliye kama wewe, na hakuna Mungu zaidi yako, kama tulivyo sikia mara zote.
\v 21 Maana ni taifa gani duniani lililo kama watu wako Israeli, ambao wewe, Mungu, ulikomboa kutoka Misri kuwa watu kwa ajili yako, ili ujifanyie jina kwa matendo makuu na ya kutisha? Uliondoa mataifa mbele za watu wako, ulio wakomboa kutoka Misri.
\v 22 Ulifanya Israeli watu wako milele, na wewe, Yahweh, ukawa Mungu wao.
\pi
\v 23 Hivyo sasa, Yahweh, ile ahadi uliyo iweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake lithibitishwe milele. Fanya kama ulivyo nena.
\v 24 Jina lako na litukuzwe milele na kuwa kuu, ili watu waseme, Yahweh wa majeshi ni Mungu wa Israeli, na nyumba yangu, mimi Daudi, mtumishi wako ikiwa imeimarishwa mbele zako.
\pi
\v 25 Kwa kuwa wewe, Mungu wangu, umedhihirisha kwa mtumishi wako utamjengea nyumba. Hiyo ndio sababu, mimi mtumishi wako, nimepata ujasiri wa kuomba kwako.
\v 26 Sasa, Yahweh, wewe ni Mungu, na umefanya hii ahadi nzuri kwa mtumishi wako:
\v 27 Sasa imekupendeza kubariki nyumba ya mtumishi wako, iliiendelee milele mbele zako. Wewe, Yahweh, umeibariki, na itabarikiwa milele.”
\c 18
\cl Sura 18
\p
\v 1 Baada ya haya Daudi akawashambulia Wafilisti na kuwashinda. Alichukuwa Gathi na vijiji vyake katika utawala wa Wafilisti.
\p
\v 2 Kisha akamshinda Moabu, na Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakamlipa ushuru maalumu.
\p
\v 3 Daudi kisha akamshinda Hadadezeri, mfalme wa Zoba huko Hamathi, wakati Hadadezeri alipo kuwa akisafiri kuimarisha utawala wake kwa Mto wa Frati.
\v 4 Daudi akateka magari ya farasi elfu, wanaume wa farasi elfu saba, na wanajeshi wa miguu elfu ishirini. Daudi aliwajeruhi farasi wote wagari, lakini akahifadhi baadhi kwa ajili ya magari ya farasi mia moja.
\p
\v 5 Wakati Waaramia wa Damasko walipo kuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Zoba, Daudi aliua wanaume elfu ishirini na mbili wa Kiaramia.
\v 6 Kisha Daudi akaweka vikosi huko Aramu ya Damasko, na Waaramia wakawa watumishi wake na wakamletea ushuru maalaumu. Yahweh alimpatia Daudi ushindi popote alipoenda.
\p
\v 7 Daudi alichukua ngao za dhahabu zilizo kuwa kwa watumishi wa Hadadezeri na kuleta Yerusalemu.
\v 8 Kutoka Teba na Kuni, miji ya Hadadezeri, Daudi alichukuwa shaba nyingi sana. Ilikuwa shaba hii ambayo baadae Sulemani alifanya beseni ya shaba, iitwayo “bahari,” nguzo na vifaa vya shaba.
\p
\v 9 Wakati Toi, mfalme wa Hamathi, aliposikia kuwa Daudi ameshinda majeshi yote ya Hadadezeri mfalme wa Zoba,
\v 10 Toi akamtuma Hadoramu mwanae kwa Mfalme Daudi kumsalimia na kumbariki. Alifanya hili kwa sababu Daudi alipigana na Hadadezeri na kumshinda, na kwa sababu mara nyingi Toi alikuwa kwenye vita naHadadezeri. Toi pia alimtumia Daudi vyombo vya aina mbalimbali dhahabu, na fedha, na shaba.
\p
\v 11 Mfalme Daudi alivitenga vitu hivi kwa Yahweh, pamoja na fedha na dhahabu aliyo ibeba kutoka kwa mataifa yote: Edomu, Moabu, watu wa Amoni, Wafilisti, na Waamaleki.
\p
\v 12 Abishai mwana wa Zeruia akawaua Waedomi elfu kumi na nane katika Bonde la Chumvi.
\v 13 Alieka vikosi huko Edomu, na Waedomi wote wakawa watumishi wa Daudi. Yahweh alimpa Daudi ushindi pote alipoenda.
\p
\v 14 Daudi alitawala Israeli yote, na alitoa haki na uadilifu kwa watu wote.
\v 15 Yoabu mwana wa Zeruia alikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mtunza kumbukumbu.
\v 16 Zadoki mwana wa Ahitubi na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Shavisha alikuwa mwandishi.
\v 17 Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa kiongozi wa Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa maofisa wakuu mkononi mwa mfalme.
\c 19
\cl Sura 19
\p
\v 1 Ilikuja baadaye kwamba Nahashi, mfalme wa watu wa Amoni, akafa, na mwanae akawa mfalme baada yake.
\v 2 Daudi akasema, “Nitaonyesha ukarimu kwa Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alionyesha ukarimu kwangu.” Hivyo Daudi akatuma wajumbe kumfariji kuhusu baba yake. Watumishi wa Daudi wakaingia nchi ya Waamoni na wakaenda kwa Hanuni, ilikumfariji.
\v 3 Lakini wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Unadhani Daudi anamheshimu baba yako sababu ametuma watu kukufaraji? Watumishi wake hawaji kwako ili kuipeleleza na kuichunguza nchi ili waipindue?
\p
\v 4 Hivyo Hanuni akawakamata watumishi wa Daudi, akawanyoa, akakata nguo zao katikati kwenye matako na kuwafukuza.
\p
\v 5 Walipo eleza haya kwa Daudi, alienda kukutana nao, kwa maana watu hao waliona aibu sana. Mfalme akasema, “Bakini Yeriko hadi ndevu zenu ziote tena, kisha mrudi.”
\p
\v 6 Wakati Waamoni waliona wamekuwa uvundo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni walituma talanta elfu moja za fedha kukodisha magari ya farasi kwa Waaremei na wanaume wa farasi kutoka Naharaimu, Maka, na Zoba.
\v 7 Waliwakodishia magari ya farasi elfu thelathini na mbili pamoja na mfalme wa Maka na jeshi lake, walio kuja na kueka kambi mbele ya Medeba. Kisha Waamoni wakajikusanya pamoja kutoka miji yao, na wakaja kwa vita.
\p
\v 8 Wakati Daudi aliposikia, alimtuma Yoabu na jeshi lake lote la mashujaa.
\v 9 Watu wa Amoni walikuja na kupanga mstari kwa ajili ya pambano katika lango la mji, nao wafalme waliokuja walikuwa peke yao katika shamba.
\p
\v 10 Wakati Yoabu alipoona mistari ya pambano imemzunguka mbele na nyuma, alichagua wapiganaji bora wa Israeli na kuwapanga dhidi ya Waaremi.
\v 11 Na jeshi lingine aliliweka chini ya Abishai kaka yake, akawapanga kwa mstari ya pambano dhidi jeshi la Amoni.
\v 12 Yoabu akasema, “Kama Waaremi wananguvu kunishinda, basi wewe, Abishai, lazima uniokoe. Lakini kama jeshi la Waamoni lina nguvu kukuzidi, basi nitakuja kukuokoa.
\v 13 Kuwa hodari na tujionyeshe kuwa hodari kwa ajili ya watu wetu na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu, kwa kuwa Yahweh atafanya lililo jema machoni mwake.”
\p
\v 14 Hivyo Yoabu na askari wa jeshi lake wakasogea kwenye pambano dhidi ya Waaremi, walio lazimika kukimbia mbele ya jeshi la Waisraeli.
\v 15 Wakati jeshi la Waamoni lilipoona kuwa Waaremi wamekimbia, nao pia wakamkimbia Abishai, ye Yoabu, na wakakurudi mjini. Kisha Yoabu akarudi kutoka kwa watu wa Amoni na kurudi Yerusalemu.
\p
\v 16 Waaremi walipoona kwamba wameshindwa na Waisraeli, wakatuma wajumbe na kuwarudisha Waaremi kutoka ng'ambo ya Mto Frati, na Shofaki mkuu wajeshi la Hadadezeri.
\p
\v 17 Daudi alipo ambiwa haya, akakusanya Israeli yote, akuvuka Yordani, na kuja juu yao. Alipanga jeshi kwa ajili ya pambano dhidi ya Waaremi, na wakapigana nao.
\v 18 Waaremi waliwakimbia Waisraeli, na Daudi akaua waendesha magari ya farasi ya Waaremi elfu saba na wanajeshi wa miguu elfu arobaini. Pia alimuua Shopaki, mkuu wa jeshi.
\p
\v 19 Wafalme wote walio kuwa watumishi wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, walifanya amani na Daudi na kumtumikia. Hivyo watu wa Aramu hawakuwa tayari kuwasaidia Waamoni.
\c 20
\cl Sura 20
\p
\v 1 Ikaja kuwa wakati wa mvua, kipindi wafalme huenda vitani, Yoabu akaongaza jeshi kwenda kupambana na kuiharibu nchi ya Waamoni. Alienda na kuteka Raba. Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu alishambulia Raba na kuiharibu kabisa.
\v 2 Daudi alichukuwa taji la mfalme wao kichwani mwake, na akagundua linauzito wa talanta moja ya dhahabu, na ndani yake kulikuwa na mawe ya thamani. Taji liliwekwa kichwani mwa Daudi, na akaleta mali nyingi za mji.
\v 3 Aliwaleta watu walio kuwa ndani ya mji na kuwalazimisha wafanye kazi kwa msumeno na suluji za chuma na shoka. Daudi aliwataka watu wote wa mji kufanya kazi hii. Kisha Daudi na watu wote wakarudi Yerusalemu.
\p
\v 4 Ilikuwa baada ya haya kukawa na pambano huko Gezeri na Wafilisti. Sibekai Mhushathi akamua Sipai, mmoja wa uzao wa Refaimu, na wa Filisti wakazidiwa.
\p
\v 5 Ikawa tena katika pambano na Wafilisti huko Gobu, kwamba Elhanani mwana wa Yari Mbethilehemu akamua Lami kaka wa Goliathi Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa kama gongo la mshonaji.
\p
\v 6 Ikaja kuwa tena katika pambano lingine huko Gathi kwamba mwanaume mmoja aliye mrefu sana mwenye vidole sita kila mkono na vidole sita mguuni. Naye alikuwa pia wa uzao wa Refaimu.
\v 7 Alipo dhihaki jeshi la Israeli, Yehonadabu mwana wa Shimea, kaka wa Daudi, akamuua.
\p
\v 8 Hawa walikuwa uzao wa Refaimu wa Gathi, na waliuawa na mkono wa Daudi na mkono wa watumishi wake.
\c 21
\cl Sura 21
\p
\v 1 Adui akainuka dhidi ya Israeli na kumchochea Daudi kuhesabu Israeli.
\p
\v 2 Daudi akamwabia Yoabu na kwa wakuu wa Jeshi, “Nenda, wahesabu watu wa Israeli kutoka Beerisheba mpaka Dani na mniletee taarifa, ilinijue idadi yao.”
\p
\v 3 Yoabu akasema, “Yahweh na afanya jeshi lake mara mia zaidi ya lilivyo. Lakini bwana wangu mfalme, je! Wote hawamtumikii bwana wangu? Kwa nini bwana wangu anataka hili? Kwa nini ulete hatia kwa Israeli?”
\p
\v 4 Lakini neno la mfalme lilitimizwa juu ya Yoabu. Hivyo Yoabu akaondoka na kwenda Israeli yote. Kisha akarudi Yerusalemu.
\v 5 Yoabu akatoa taarifa ya idadi ya jumla ya wanaume wa mapambano kwa Daudi. Kulikuwa ndani ya Israeli wanaume 1,100,000 walio beba upanga. Yuda peke yake kulikuwa na wanajeshi 470,000.
\v 6 Lakini Law na Benjamini hawakuhesabiwa miongoni mwao, kwa kuwa amri ya mfalme ilichukiza Yoabu.
\p
\v 7 Mungu alikwazika na hili tendo, hivyo akashambulia Israeli.
\v 8 Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya hili. Sasa chukua hatia ya mtumishi wako, maana nimefanya upumbavu sana.”
\p
\v 9 Yahweh akamwambia Gadi, nabii wa Daudi,
\v 10 “Nenda useme kwa Daudi, “Hili ndilo Yahweh anasema: Ninakupa maamuzi matatu. Chagua moja wapo.”
\p
\v 11 Hivyo Gadi akaenda kwa Daudi na kusema, “Yahweh anasema hivi, Chagua moja ya haya:
\v 12 kati ya miaka mitatu ya ukame, miezi mitatu unakimbizwa na adui zako na kupatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa Yahweh, yani, pigo katika nchi, malaika wa Yahweh akiharibu nchi yote ya Israeli. Hivyo sasa, amua jibu gani ni mpelekee yeye aliye nituma.”
\p
\v 13 Kisha Daudi akamwambia Gadi, “Niko kwenye dhiki kubwa. Acha nianguke katika mikono ya Yahweh kuliko kuangukia mikono ya mwanadamu, sababu matendo yake ya rehema ni makubwa mno.”
\p
\v 14 Hivyo Yahweh akatuma pigo Israeli, na watu elfu sabini wakafa.
\v 15 Mungu akatuma malaika Yerusalemu kuiharibu. Alipokuwa anakaribia kuiharibu, Yahweh akatazama na kubadili nia yake kuhusu shambulio. Akasema kwa malaika wa uharibifu, “Imetosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Yahweh alikua amesimama eneo la kupeta la Orinani Myebusi.
\p
\v 16 Daudi akatazama juu na kuona malaika wa Yahweh amesimama kati ya nchi na mbingu, akiwa na upanga mkonono mwake akiuelekeza Yerusalemu. Kisha Daudi na wazee, wakiwa wamevaa magunia, wakalala chini uso ukiwa kwenye ardhi.
\p
\v 17 Daudi akamwambia Mungu, “Si ni mimi niliye amuru jeshi kuhesabiwa? Nilifanya hichi kitu kiovu. Lakini hawa kondoo, wamefanya nini? Yahweh Mungu wangu! Acha mkono wako unipige mimi na ukoo wangu, lakini usiache pigo iliendelee kubaki kwa watu wako.”
\p
\v 18 Hivyo malaika wa Yahweh akamuamuru Gadi kusema kwa Daudi, kwamba Daudi aende juu na kujenga madhabahu ya Yahweh katika eneo la kupeta la Arauna Myebusi.
\v 19 Daudi akaenda kama Gadi alivyo muelekeza cha kufanya kwa jina la Yahweh.
\p
\v 20 Wakati Orinani akipepeta ngano, aligeuka na kumuona malaika. Yeye na wanawe wanne wakajificha.
\v 21 Wakati Daudi alipo kuja kwa Orinani, Orinani akatazama na kumuona Daudi. Aliacha eneo la kupeta na akamuinamia Daudi uso wake ukiwa kwenye ardhi.
\p
\v 22 Kisha Daudi akasema kwa Orinani, “Niuzie hili eneo la kupeta, iliniweze kumjenga Yahweh madhabahu. Nitalipa gharama yote, ili pigo liondolewe kwa watu.”
\p
\v 23 Orinani wakwambia Daudi, “Chukuwa kama lako, bwana wangu mfalme. Fanya nalo linalo kupendeza. Tazama, nitakupa ng'ombe kwa sadaka ya kuteketeza, vifaa vya kupeta kwa ajili ya mbao, na ngano kwa sadaka ya mbegu; nitakupa yote wewe.”
\p
\v 24 Mfalme Daudi akamwambia Orinani, “Hapana, nina sisitiza kununua kwa bei yote. Sitachukua kilicho chako na kutoa kama sadaka ya kuteketeza kwa Yahweh kama haitanighramu chochote.”
\p
\v 25 Hivyo Daudi akalipa shekeli mia sita ya dhahabu kwa hilo eneo.
\v 26 Daudi akajenga madhabahu ya Yahweh pale na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za ushirika. Akamuita Yahweh, aliye mjibu kwa moto kutoka mbinguni kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketezwa.
\p
\v 27 Kisha Yahweh akampa agizo malaika, na malaika akarudisha upanga kwenye mfuko wake.
\v 28 Daudi alipo ona kuwa Yahweh amemjibu kwenye eneo la kupeta la Orinani Myebusi, alitoa dhabihu pale pale kwa wakati huo.
\v 29 Sasa kwa wakati huo, hema la kuabudia la Yahweh, ambalo Musa alilitengeneza nyikani, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa, zilikuwa sehemu ya juu huko Gibeoni.
\v 30 Walakini, Daudi hakuweza kwenda huko kumuliza Mungu muelekeo, kwa kuwa alikuwa anaogopa upanga wa malaika wa Yahweh.
\c 22
\cl Sura 22
\p
\v 1 Kisha Daudi akasema, “Hapo ndipo nyumba ya Yahweh Mungu itakuwepo, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa za Israeli.”
\p
\v 2 Hivyo Daudi akaagiza watumishi wake wawakusanye pamoja wageni wote wanao ishi katika nchi ya Israeli. Aliwapangia kuwa wachonga mawe, kuchonga matofali ya mawe, ilikuweza kujenga nyumba ya Mungu.
\v 3 Daudi alisambaza idadi kubwa ya chuma kwa ajili ya misumari na vitasa vya kuweka kwenye malango. Pia alitoa shaba zaidi kushinda kipimo,
\v 4 na miti ya mierezi zaidi ya kipimo. (Wasidoni na Watiria walileta magogo mengi sana ya mierezi kwa Daudi asiweze kuhesabu
\p
\v 5 Daudi akasema, “Mwanangu Sulemani ni mdogo na hana uzoefu, na nyumba itayo jengwa kwa Yahweh lazima iwe maridadi, ilikwamba iwe maarufu na ya utukufu kwa nchi zingine zote. Hivyo nitaanda ujenzi wake.” Hivyo Daudi akafanya maandalizi ya kina kabla ya mauti yake.
\p
\v 6 Kisha akamwita Sulemani mwanae na kumuamuru ajenge nyumba ya Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 7 Daudi akasema kwa Sulemani, “Mwanangu, ilikuwa dhamira yangu kujenga nyumba mwenyewe, kwa ajili ya jina la Yahweh Mungu wangu.
\v 8 Lakini Yahweh alikuja kwangu na kusema, Wewe umemwaga damu nyingi na umepigana mapambono mengi. Hautajenga nyumba kwa jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi kwenye ardhi machoni pangu.
\v 9 Walakini, utapata mwana ambaye atakuwa mtu wa amani. Nitampa kupumzika na maadui zake kwa kila upande. Kwa kuwa jina lake litaitwa Sulemani, na nitatoa amani na utulivu kwa Israeli katika siku zake.
\v 10 Ata jenga nyumba kwa jina langu. Ata kuwa mwana wangu, na nitakuwa baba yake. Nitaimarisha kiti cha ufalme wake juu ya Israeli milele.
\p
\v 11 Sasa, mwanangu, Yahweh awe nawe na kukuwezesha kufanikiwa. Uweze kujenga nyumba ya Yahweh Mungu wako, kama alivyo sema utajenga.
\v 12 Yahweh tu akupe uwelewa na ufahamu, ili utii sheria ya Yahweh Mungu wako, ata kapokuweka kiongozi juu ya Israeli.
\v 13 Kisha utafanikiwa, kama tu ukitii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli. Kuwa hodari na jasiri. Usiogope wala usikate tamaa
\p
\v 14 Sasa, ona, kwa bidii kubwa nimeandaa kwa ajili ya nyumba ya Yahweh talanta 100,000 za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na shaba na chuma katika idadi kubwa. Pia nimetoa mbao na mawe. Lazima uongeze zaidi katika haya.
\v 15 Una wafanya kazi wengi: wachonga mawe, waashi, maseremala, na mafundi stadi bila idadi wa kila aina,
\v 16 wenyeuwezo wa kufanya kazi na dhahabu, fedha, shaba, na chuma. Inuka na uanze kazi, na Yahweh awe nawe.
\p
\v 17 Daudi akawaagiza viongozi wote Waisraeli wamsaidie Sulemani mwanae, akisema,
\v 18 “Yahweh Mungu wenu yupo nanyi na amewapa amani kila pande. Amewakabidhi mikononi mwangu wenyeji wote mkoa. Mkoa umetiishwa mbele za Yahweh na watu wake.
\v 19 Sasa mtafuteni Yahweh Mungu wenu kwa moyo wenu wote na nafsi. Simameni na mjenge sehemu takatifu ya Yahweh Mungu. Kisha mwaweza kuleta sanduku la agano la Yahweh na vitu vya Mungu ndani ya nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya jina la Yahweh.
\c 23
\cl Sura 23
\p
\v 1 Daudi alipokuwa mzee na kukaribia mwisho wa maisha yake, alimfanya Sulemani mwanae mfalme juu ya Israeli.
\p
\v 2 Aliwakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, na makuhani na Walawi.
\v 3 Walawi walio kuwa miaka thelathini na zaidi walihesabiwa, na idadi yao ikawa elfu thelathini na nane.
\v 4 Kwa hawa, elfu ishirini na nne walikuwa kusimamia kazi ya nyumba ya Yahweh, na elfu sita walikuwa maaskari na waamuzi.
\v 5 Elfu nne walikuwa walinzi wa lango, na elfu nne walikuwa wamsifu Yahweh na vyombo nilivyo vitengeneza vya kusifu.” Daudi akasema.
\p
\v 6 Akawatenganisha kwenye vikundi kulingana na wana wa Lawi: Gerishoni, Kohathi, na Merari.
\v 7 Kwa koo za uzao wa Gerishoni, kulilkuwa na Ladani na Shimei.
\q
\v 8 Palikuwa na watatu wa wana wa Ladani: Yehieli kiongozi, Zethami, na Yoeli.
\q
\v 9 Palikuwa na watatu wa wana wa Shimei: Shelomothi, Hazieli, na Harani. Hawa walikuwa viongozi wa koo ya Ladani.
\q
\v 10 Palikuwa na wanne wa wana wa Shimei: Yahathi, Ziza, Yeushi, na Beria.
\q2
\v 11 Yahathi alikuwa mkubwa, Ziza wapili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi, hivyo walihesabiwa kama ukoo mmoja na kupangiwa kazi sawa.
\v 12 Palikuwa na wanne wa wana wa Kohathi: Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
\q
\v 13 Hawa walina wa Amramu: Aruni na Musa. Aruni alichaguliwa kuandaa vitu vitakatifu, yeye na uzao wake watatoa uvumba kwa Yahweh, kumtumikia na kumpa baraka kwa jina lake.
\q2
\v 14 Lakini kwa Musa mtu wa Mungu, wana wake walihesabiwa kuwa Walawi.
\q
\v 15 Wana wa Musa walikuwa Gerishomu na Eliezeri.
\q2
\v 16 Uzao wa Gerishomu ulikuwa Shebueli mkubwa.
\q2
\v 17 Uzao wa Eliezeri alikuwa Rehabia. Eliezeri hakuwa na wana wengine, lakini Rehabia alikuwa na uzao mkubwa.
\q
\v 18 Mwana wa Izihari alikuwa Shelomithi kiongonzi.
\q
\v 19 Uzao wa Hebroni ulikuwa Yeria, mkubwa, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
\q
\v 20 Wana wa Uzieli walikuwa Mika mkubwa, na Ishia wapili.
\v 21 Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Wana wa Mahili walikuwa Eleazari na Kishi.
\q2
\v 22 Eleazari alikufa bila mtoto wa kiume. Alikuwa na mabinti tu. Wana wa Kishi waliwaoa.
\q
\v 23 Wana wa Mushi watatu walikuwa Mahili, Ederi, na Yeremothi.
\p
\v 24 Hawa walikuwa uzao wa Lawi kulingana na koo zao. Walikuwa viongozi, wamehesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, kuanzia koo zilizo fanya kazi katika nyumba ya Yahweh, kutoka miaka ishirini na zaidi.
\v 25 Kwa kuwa Daudi alisema, “Yahweh, Mungu wa Israeli, amewapa pumziko watu wake. Anafanya makao yake Yerusalemu milele.
\v 26 Walawi hawatahitaji kubeba hema la kuabuadia na vifaa vyake vinavyo tumika kwenye utumishi wake.”
\v 27 Kwa maneno ya Daudi ya mwisho Walawi walihesabiwa, miaka ishirini na kuendelea.
\p
\v 28 Wajibu wao ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh. Walikuwa washughulikie nyuani, vyumbani, utakasaji wa vitu vyote vya Yahweh, na kazi zingine katika utumishi wa nyumba ya Mungu.
\v 29 Pia walishughulikia mkate wa uwepo, unga safi wa mbegu za sadaka, mikate kaki isiotiwa chachu, sadaka zilizookwa, sadaka ziliochanganywa na mafuta, na vipimo vyote vya kiasi na ukubwa wa vitu.
\v 30 Pia walisimama kila asubui kumshukuru na kumsifu Yahweh. Pia walifanya hivi jioni
\v 31 na kila wakati sadaka ya kuteketezwa ilipo tolewa kwa Yahweh, siku ya Sabato na sherehe za mwezi mpya na siku za maakuli. Idadi maalumu, iliyo tolewa kwa amri, siku zote ilibidi iwepo mbele ya Yahweh.
\p
\v 32 Walikuwa viongozi wa hema la kukutania, patakatifu, na kuwasaidia jamaa zao wa uzao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh.
\c 24
\cl Sura 24
\p
\v 1 Makundi vya kazi kulingana na uzao wa Aroni yalikuwa haya: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
\p
\v 2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao kufa. Walikuwa hawana watoto, kwa hiyo Eleazari na Ithamari walitumika kama makuhani.
\v 3 Daudi pamoja na, uzao wa Eleazari, na Zadoki wa Ithamari, waliwagawanya katika makundi ya kazi yao kama makuhani.
\v 4 Kulikuwa na wanaume viongozi zaidi kati ya uzao wa Eleazari kuliko kati ya uzao wa Ithamari, kwahiyo waligawanya uzao wa Eleazari katika makundi kumi na sita. Walifanya hivyo na viongozi wa ukoo na uzao wa Ithamari. Magawanyo haya yalikuwa nane kwa idadi, sambamba na koo zao.
\v 5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kura, kwa kuwa walikuwa waamuzi watakatifu na waamuzi wa Mungu, kutoka pande zote uzao wa Eleazari na uzao wa Ithamari.
\p
\v 6 Shemaia mwana wa Nethaneli mwandishi, Mlawi, aliandika majina yao mbele ya mfalme, muamuzi, kuhani Zadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa makuhani na familia za Walawi. Ukoo mmoja ulichaguliwa kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, na kisha uliofata utachaguliwa kutoka uzao wa Ithhamari.
\q
\v 7 Kura ya kwanza ilienda kwa Yehoiaribu, ya pili kwa Yedaia,
\q
\v 8 ya tatu kwa Harimu, ya nne kwa Seorimu,
\q
\v 9 ya tano kwa Malikija, ya sita kwa Mijamini,
\q
\v 10 ya saba kwa Hakozi, ya nane kwa Abija,
\q
\v 11 ya tisa kwa Yeshua, ya kumi kwa Shekania,
\q
\v 12 ya kumi na moja kwa Eliashibu, ya kumi na mbili kwa Yakimu,
\q
\v 13 ya kumi na tatu kwa Hupa, ya kumi na nne kwa Yesheheabu,
\q
\v 14 ya kumi na tano kwa Biliga, ya kumi na sita kwa Imma,
\q
\v 15 ya kumi na saba kwa Heziri, ya kumi na nane kwa Hapizezi,
\q
\v 16 ya kumi na tisa kwa Pethaia, ya ishirini kwa Yehezikeli,
\q
\v 17 ya ishirini na moja kwa Yakini, ya ishirini na mbili kwa Gamuli,
\q
\v 18 ya ishirini na tatu kwa Delaia, na ya ishirini na nne kwa Maazia.
\p
\v 19 Hii ilikuwa taratibu ya utumishi wao, walipo kuja kwenye nyumba ya Yahweh, wakifuata utaratibu waliopewa na Aruni babu yao, kama Yahweh, Mungu wa Israeli, alivyo waagiza.
\v 20 Hawa walikuwa Walawi waliobakia: Wana wa Amiramu, Shebueli; wana wa Shebaeli, Yedeia.
\q
\v 21 Wana wa Rehabia: wana wa Rehabia, Ishia kiongozi.
\q
\v 22 Wa Waizari, Shelomothi; mwana wa Shelomothi, Yahathi.
\q
\v 23 Wana wa Hebroni: Yeria kiongozi, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
\q
\v 24 Wana wa uzao wa Uzieli ulimjumuisha Mika. Uzao wa Mika ulimjumuisha Shamiri.
\q2
\v 25 Kaka wa Mika alikuwa Ishia. Wana wa Ishia akijumuishwa Zakaria.
\q
\v 26 Wana na Merari: Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia, Beno.
\q2
\v 27 Wana wa Merari: Yaazia, Beno, Shohamu, Zakuri, na Ibrri.
\q2
\v 28 Wana wa Mahili: eleazari, ambaye alikuwa hana wana.
\q
\v 29 Wana wa Kishi: Yerameli
\q2
\v 30 wana wa Mushi: Mahli, Eda, na Yerimothi. Walikuwa Walawi, walio orodheshwa na familia zao.
\v 31 Wanaume hawa ambao walikuwa vichwa wa kila koona kila kaka zao wadogo zao, walipiga kura katika uwepo wa Mfalme Daudi, na Zadoki na Ahimeleki, pamoja na viongozi wa familia wa makuhani na Walawi. Walirusha kura kama uzao wa Aroni walivyofanya.
\c 25
\cl Sura 25
\p
\v 1 Daudi na viongozi wa jeshi walichagua baadhi ya wana wa Asafu, Hemani, na Yeduthuni kutabiri kwa vinanda na vinubi, na kwa upatu. Hii ni orodha ya wanaume walioifanya hii kazi:
\v 2 Kutoka wana wa Asafu: Zakuri, Yosefu, Nethania, na Asharela, wana wa Asafu, chini ya mwongozo wa Asafu, ambaye alitabiri chini ya uwangalizi wa mfalme.
\v 3 Kutoka wana wa Yeduthuni: Gedalia, Zeri, Yeshaia, Shimei, Hashabia, na Matithia, sita kwa ujumla, chini ya mwongozo wa baba yao Yeduthuni, ambaye alitabiri, akipiga kinubi kwa kutoa shukurani na kumsifu Yahweh.
\q
\v 4 Kutoka wana wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yerimothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti Ezeri, Yoshibekasha, Mallothi, Hothiri, na Mahaziothi.
\v 5 Hawa wote walikuwa wana wa Hemani, nabii wa mfalme. Mungu alimpa Hemani wana kumi na nne na mabinti watatu kuinua pembe yake.
\p
\v 6 Hawa wote walikuwa chini ya mwongozo wa baba zao. Walikuwa ni waimbaji katika nyumba ya Yahweh kwa upatu, vinanda, na vyombo vya uzi, wakihudumu katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni, na Hemani walikuwa chini ya uwangalizi wa mfalme.
\v 7 Wao na kaka zao waliokuwa na ujuzi na mafundisho ya kufanya muziki kwa Yahweh walikuwa na idadi ya 288.
\v 8 Wapiga kura kwa ajili ya kazi zao, wote sawa, sawa vivyo hivyo kwa vijana na kwa wazee, kwa mwalimu na kwa mwanafunzi.
\q
\v 9 Sasa kuhusu wana wa Asafu: kura ya kwanza iliangukia katika familia ya Yusufu; ya pili iliangukia katika familia ya Gedalia, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 10 ya tatu iliangukia kwa Zakuri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 11 ya nne iliangukia kwa Izri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 12 ya tano iliangukia kwa Nethania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\q
\v 13 ya sita iliangukia kwa Bukia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 14 ya saba iliangukia kwa Yesharela, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 15 ya nane iliangukia kwa Yeshaia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 16 ya tisa iliangukia kwa Matania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\q
\v 17 ya kumi iliangukia kwa Shimei, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 18 ya kumi na moja iliangukia kwa Azareli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 19 ya kumi na mbili iliangukia kwa Hashabia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 20 ya kumi na tatu iliangukia kwa Shubaeli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\q
\v 21 ya kumi na nne iliangukia kwa Matithia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 22 ya kumi na tano iliangukia kwa Yeromothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 23 ya kumi na sita iliangukia kwa Hanania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 24 ya kumi na saba iliangukia kwa Yoshibekasha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\q
\v 25 ya kumi na nane iliangukia kwa Hanani, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 26 ya kumi na tisa iliangukia kwa Malothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 27 ya ishirini iliangukia kwa Eliatha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 28 ya ishirini na moja iliangukia kwa Hothiri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\q
\v 29 ya ishirini na mbili iliangukia kwa Gidalti, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 30 ya ishirini na tatu iliangukia kwa Mahaziothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 31 ya ishirini na nne iliangukia kwa Romamti Eza, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili.
\c 26
\cl Sura 26
\p
\v 1 Haya ndiyo makundi yawalinzi wa lango: Kutoka kwa Wakora, Meshelemia mwana wa Kore, wa uzao wa Asafu.
\q2
\v 2 Meshelemia alikuwa na wana wa kiume: Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wapili, Zebadia watatu, Yathinieli wanne,
\v 3 Elamu watano, Yehohanani wasita, Eliehoenai wasaba.
\q
\v 4 Obedi alikuwa na wana wa kiume: Shemaia wa kwanza, Yehozabadi wapili, Yoa watatu, na Sakari wanne, na Nethanieli watano,
\v 5 Amieli wasita, Isakari wasaba, Peulethai wanane, kwa kuwa Mungu alimbariki Obedi Edomu.
\q2
\v 6 Kwa Shemaia mwanaye walizawa wana walio tawala koo zao; walikuwa wanaume wenye uwezo mkuu.
\q2
\v 7 Wana wa Shemaia walikuwa Othini, Refaeli, Obedi, na Elizabadi. Jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali.
\q2
\v 8 Hawa wote walikuwa uzao wa Obedi Edomu. Wao na wanao na jamaa zao walikuwa wanaume wenye uwezo wa kufanya wajibu wao katika huduma ya hema la kuabudia. Palikuwa na sitini na mbili walio kuwa na undugu na Obedi Edomu.
\q
\v 9 Meshelemia alikuwa na wana na jamaa, wanaume wenye uwezo, jumla ya kumi na nane.
\q
\v 10 Hosa, mzao wa Merari, alikuwa na wana: Shimiri kiongozi (ijapo hakuwa mzaliwa wa kwanza, baba yake alimfanya kiongozi),
\v 11 Hilikia wapili, Tebalia watatu, Zekaria wanne. Wote wa wana wa Hosa na jamaa walikuwa kumi na tatu kwa idadi.
\p
\v 12 Haya makundi ya walinzi wa lango, sambamb a na viongozi, yalikuwa na majukumu, kama jamaa zao, kutumika katika nyumba ya Yahweh.
\v 13 Walipiga kura, wadogo kwa wakubwa, kulingana na koo zao, kwa kila lango.
\v 14 Kura ilipo pigwa kwa lango la mashariki, ilimuangukia Shelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanaye, mshauri mwenye busara, na kura yake ikatokea kwa lango la kaskazini.
\q
\v 15 Kwa Obedi Edomu alipangiwa lango la kusini, na wanawe walipangiwa nyumba za ghala.
\v 16 Shufimu na Hosa walipangiwa lango la magharibi pamoja na lango la Shalekethi, kwenye barabara ya juu. Walinzi walikuwa karibu sana.
\v 17 Kwa mashariki walikuwa Walawi sita, kaskazini wanne kwa siku moja, kusini wanne kwa siku moja, na nyumba za ghala jozi mbili.
\v 18 Kwenye nguzo upande wmagharibi wanne kulikuwa na wanne waliosimama kwenye barabara na wawili kwenye nguzo.
\p
\v 19 Haya yalikuwa makundi ya walinzi wa lango waliokuwa uzao wa Kora na Merari.
\p
\v 20 Miongoni mwa Walawi, Ahija alikuwa kiongozi wa hazina ya nyumba ya Mungu, na hazina ya vitu vya Yahweh.
\v 21 Wazao wa Ladani, walitoka kwa Gerishoni kupitia kwake na walio kuwa viongozi wa familia za Ladani Mgerishoni, walikuwa Yehieli
\v 22 na wanae Yehieli: Zethamu na Yoeli kaka yake. Walikuwa wamesimamia hazina za nyumba ya Yahweh.
\p
\v 23 Kutoka koo za Amramu, koo za Izhari, koo za Hebroni, na koo za Uzieli:
\q
\v 24 Shebueli uzao wa Gerishomu mwana wa Musa, alikuwa msimamizi wa hazina.
\v 25 Jamaa zake wa ukoo wa Eliezeri walikuwa Rehabia mwanawe, mwana wa Rehabia Yeshaia, mwana wa Yeshaia Yoramu, mwana wa Yoramu Zikiri, na mwana wa Zikiri Shelomothi.
\v 26 Shelomothi na jamaa zake walikuwa wasimamizi wa hazina zote za ghala zinazo hifadhi vitu vyote vya Yahweh, ambavyo Daudi mfalme, viongozi wa familia, wakuu wa maelfu na mamia, na wakuu wa jeshi walivyo vitenga.
\v 27 Walitenga vitu walivyo vichukuwa kwenye mapambano kwa ajili ya kutunza nyumba ya Yahweh.
\v 28 Pia walikuwa wahusika wa kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh na Samweli nabii, Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Zeruia. Kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh kilikuwa chini ya ulinzi wa shelomothi na jamaa zake.
\q
\v 29 Wa uzao wa Izhari, Kenania na wana wake walikuwa wahusika wa mambo ya ndani ya Israeli. Walikuwa maafisa na waamuzi.
\q
\v 30 Wa uzao wa Hebroni, Hashabia na kaka zake, wanaume wenye uwezo 1,700, walikuwa wahusika wa kazi ya Yahweh na kazi ya mfalme. Walikuwa upande wa mgharibi mwa Yordani.
\v 31 Kutoka uzao wa Hebroni, Yeriya alikuwa kiongozi wa koo, kulingana na orodha za familia zao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi walitathimini kumbukumbu na kugundua miongoni mwao wanaume wa uwezo mkubwa katika Yazeri ya Gileadi.
\v 32 Yerija alikuwa na ndugu 2,700, walio kuwa viongozi wenye uwezo katika familia. Daudi aliwafanya waangalizi wa makabila ya Rubeni na Gadi, na nusu kabila la Manase, kwa kila jambo linalo muhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.
\c 27
\cl Sura 27
\p
\v 1 Hii ni orodha ya familia za viongozi wa Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, pamoja na maafisa wa jeshi walio mtumikia mfalme kwa namna tofauti. Kila kikosi cha jeshi kilitumika mwenzi hadi mwezi kwa mwaka mzima. Kila kikosi kilikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 2 Juu ya kikosi kwa mwezi wa kwanzaalikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
\v 3 Alikuwa miongoni mwa uzao wa Perezi na msimamizi wa maafisa wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
\q
\v 4 Juu ya kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai, wa ukoo wa uliotoka kwa Ahoa. Mikilothi alikuwa wa pili kwa cheo. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 5 Mkuu wa jeshi wa mwezi wa tatu alikuwa Benaia mwana wa Yehoiada, kuhani na kiongozi. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\v 6 Huyu ni Benaia aliye kuwa kiongozi wa wale thelathini na juu ya wale thelathini. Amizabadi mwanae alikuwa katika kikosi chake.
\q
\v 7 Mkuu kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli kaka wa Yoabu. Zebadia mwanae akawa mkuu baada yake. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 8 Mkuu kwa mwezi wa tano alikuwa Shamihuthi, mzao wa Izra. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 9 Mkuu kwa mwezi wa sita alikuwa Ira mwana wa Ikeshi, kutoka Tekoa. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 10 Mkuu kwa mwezi wa saba alikuwa Helezi Mpeloni, kutoka watu wa Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 11 Mkuu kwa mwezi wa nane alikuwa Sibekai Mhushathi, kutoka ukoo ulitoka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 12 Mkuu kwa mwezi wa tisa alikuwa Abi Ezeri Manathothi, kutoka kwa kabila la Benjamini. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 13 Mkuu kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai kutoka mji wa Netofa, kutoka ukoo ulio toka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 14 Mkuu kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaia kutoka mji wa Pirathoni, kutoka kabila la Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\q
\v 15 Mkuu kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Helidai kutoka mji wa Netopafa, kutoka ukoo uliotoka kwa Othinieli. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\p
\v 16 Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli: Kwa kabila la Rubeni, Eliezeri mwana wa Zikri alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Simeoni, Shefatia mwana wa Maka alikuwa kiongozi.
\q
\v 17 Kwa kabila la Lawi, Hashinia mwana wa Kemueli alikuwa kiongozi, na Zadoki aliongoza uzao wa Aruni.
\q
\v 18 Kwa kabila la Yuda, Elihu, mmoja wa kaka zake Daudi, alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Isakari, Omri mwana wa Mikaeli alikuwa kiongozi.
\q
\v 19 Kwa kabila la Zebuluni, Ishimaia mwana wa Obadia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Naftali, Yeremothi mwana wa Azirieli alikuwa kiongozi.
\q
\v 20 Kwa kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Manase, Yoeli mwana wa Pedaia alikuwa kiongozi.
\q
\v 21 Kwa nusu kabila la Manase lililo Gileadi, Ido mwana wa Zekaria alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Benjamini, Yaasieli mwana wa Abneri alikuwa kiongozi.
\q
\v 22 Kwa kabila la Dani, Azareli mwana wa Yerohamu alikuwa kiongozi. Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli.
\p
\v 23 Daudi hakuwa hesabu wenye umri wa miaka ishirini au chini zaidi, kwasababu Yahweh alihaidi kuongeza Israeli kama nyota za mbinguni.
\v 24 Yoabu mwana wa Zeruia alianza kuhesabu wanaume, lakini hakumaliza. Gadhabu iliangukia Israeli kwa hili. Hii idadi haikuandikwa kwenye nyakati za mfalme Daudi.
\q
\v 25 Azimavethi mwana wa Adieli alikuwa mhusika wa hazina za mfalme. Yonathani mwana wa Uzia alikuwa juu ya nyumba za ghala katika mashamba, kwenye miji, na vijijini, na kwenye minara iliyo imarishwa.
\v 26 Ezri mwana wa Kelubi alikuwa juu ya mashamba, hao walio lima ardhi.
\v 27 Shimei kutoka Rama alikuwa juu ya mashamba ya mizabibu, na Zabdi Mshefamu alikuwa juu ya zabibu na pishi za mvinyo.
\q
\v 28 Mwangalizi wa miti mizeituni na miti ya mikuyu iliyo kuwa bondeni alikuwa Baali Hanani kutoka Gederi, na juu ya nyumba za ghala za mafuta alikuwa Yoashi.
\v 29 Juu ya mifugo iliyo kuwa inalishwa huko Sharoni alikuwa Shitrai kutoka Sharoni, na juu ya mifugo iliyo kuwa mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai.
\q
\v 30 Msimamizi wa ngamia alikuwa Obili Mishimaeli, na juu ya punda wakike alikuwa Yehideia kutoka Meronothi. Juu ya mifugo alikuwa Yazizi Mhagri.
\v 31 Hawa maafisa wote walikuwa wasimamizi wa mali za Mfalme Daudi.
\q
\v 32 Yonathani, mjomba wake Daudi alikuwa mshauri, sababu alikuwa na busara na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakimoni aliwajali wana wa mfalme.
\v 33 Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme, na Hushai kutoka watu wa Mwarki aliyekuwa rafiki yake mfalme.
\v 34 Nafasi ya Ahithofeli ilichukuliwa na Yehoiada mwana wa Benaia, na Abiathari. Yoabu alikuwa mkuu wa jeshi la mfalme.
\c 28
\cl Sura 28
\p
\v 1 Daudi akakusanya maafisa wote wa Israeli Yerusalemu: maafisa wa makabila, maafisa wa vitengo walio mtumikia mfalme katika kazi walizo pangiwa, wakuu wa maelfu na mamia, wasimamizi wa mali zote za mfalme na wanawe, na maafisa na wanaume wa mapambano, ukijumuisha wale wenye ujuzi sana.
\p
\v 2 Kisha Daudi mfalme akainuka kwa miguu yake na kusema, “Sikilizeni mimi, kaka zangu na watu wangu. Ilikuwa dhumuni langu kujenga hekalu kwa ajili ya sanduku la agano la Yahweh; stuli ya miguu kwa ajili ya Mungu wetu, na nimefanya maandalizi kuijenga.
\v 3 Lakini Mungu akaniambia, Hautajenga hekalu kwa ajili ya jina la langu, kwasababu wewe ni mwanaume wa vita na umemwaga damu.
\p
\v 4 Bado Yahweh, Mungu wa Israeli, alinichagua kutoka katika familia ya baba yangu kuwa mfalme wa Israeli milele. Amechagua kabila la Yuda kama kiongozi. Katika kabila la Yuda, na nyumba ya baba yangu, kutoka kwa wana wa baba yangu, amenichagua kuwa mfalme wa Israeli.
\v 5 Kutoka kwa wana wengi ambao Yahweh amenipa, amemchagua Sulemani, mwanangu, kuketi katika kiti cha enzi cha ufalme wa Yahweh, juu ya Israeli.
\v 6 Aliniambia, Sulemani mwanae atanijengea nyumba yangu na nyuani mwangu, kwa kuwa nimemchagua kuwa mwana wangu, nami nitakuwa baba yake.
\v 7 Nitaimarisha ufalme wake, akidumu kutii sheria na amri zangu, kama ulivyo siku ya leo.
\p
\v 8 Kisha sasa, katika macho ya Waisraeli wote, hili kusanyiko la yahweh, na katika uwepo wa Mungu wetu, nyinyi nyote lazima mshike na kufanya amri zote za Yahweh Mungu wenu. Fanyeni hivi ili mmiliki nchi hii nzuri na kuiacha kama urithi kwa uzao wenu baada yenu milele.
\p
\v 9 Kwako wewe, Sulemani mwanangu, mtii Mungu wa baba yako, mtumikie kwa moyo wako wote na roho ya utayari. Fanya hivi kwa sababu yahweh anachunguza mioyo yote na kufahamu amasa ya kila wazo la mtu. Ukimtafuta, ataonekana nawe, lakini ukimtelekeza, atakukataa milele.
\v 10 Elewa kuwa Yahweh amekuchagua kulijenga hekalu hili kama patakatifu pake. Uwe hodari na uifanye.”
\p
\v 11 Kisha Daudi akamkabidhi Sulemani mwanae mipango ya ukumbi wa hekalu, majengo ya hekalu, vyumba vya hifadhi, vyumba vya juu, vyumba vya ndani, na chumba chenye kifuniko cha upatanisho.
\v 12 Alimpatia mipango aliyo chora ya nyuani kwa ajili ya nyumba ya Yahweh, vyumba vyote vilivyo zunguka, vyumba vya hifadhi katika nyumba ya Mungu, na hazina za vitu vya Yahweh.
\v 13 Alimpatia masharti kwa vitengo vya makuhani na Walawi, kwa majukumu walio pangiwa kwa utumishi wa nyumba ya Yahweh, na kwa vyombo vyote vinavyo tumika katika nyumba ya Yahweh.
\v 14 Aliamua uzito wa vifaa vyote vya dhahabu kwa kila huduma, uzito wa vifaa vya fedha kwa kila huduma,
\v 15 uzito wa dhahabu wa vifaa vyote vya dhahabu, kuwavinara vya taa na taa za dhahabu, uzito wa dhahabu kwa kila kinara cha taa, uzito wa fedha kwa kila kinara cha fedha, kulingana na matumizi ya kila kinara cha taakatika huduma.
\v 16 Alitoa uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza za mkate wa uwepo, kwa kila meza, na uzito wa fedha kwa meza za fedha.
\v 17 Alitoa uzito wa dhahabu safi kwa uma za nyama, beseni, na vikombe. Alitoa uzito kwa kila bakuli ya dhahabu, na uzito kwa kila bakuli ya fedha.
\v 18 Alitoa uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya uvumba, na za dhahabu kwa muundo wa gari, makerubi waliye tanda mabawa yao na kufunika sanduku la agano la Yahweh.
\p
\v 19 Daudi akasema, “Nimeweka haya katika maandishi kama Yahweh alivyonielekeza na kunipa kuelewa kuhusu mchoro.”
\p
\v 20 Daudi akasema kwa Sulemani mwanae, “Kuwa hodari na mjasiri. Fanya kazi. Usiogope au kufadhai, kwa kuwa Yahweh Mungu, Mungu wangu, yupo nawe. Hatakuacha wala kukutelekeza mpaka kazi ya huduma ya hekalu la Yahweh imekamilika.
\v 21 Ona, hivi ni vitengo vya makuhani na Walawi kwa huduma katika hekalu la Mungu. Watakuwa nawe, pamoja na wanaume walio tayari na wenye ujuzi, kukusaidia katika kazi na kutenda huduma. Maafisa na watu wote wako tayari kufuata amri zako.”
\c 29
\cl Sura 29
\p
\v 1 Mfalme Daudi akasema kwa kusanyiko lote, “Sulemani mwanangu, ambaye mwenyewe Mungu amemchagua, bado ni mdogo na hana uzoefu, na jukumu ni kubwa. Maana hekalu sio kwa ajili ya watu bali la Mungu.
\v 2 Hivyo nimefanya kwa ubora wangu kutoa kwa ajili ya hekalu la Mungu. Nina toa dhahabu kwa vitu vitakavyotengenezwa na dhahabu, fedha kwa vitu vitu vitakavyotengenezwa na fedha, shaba kwa vitu vitakavyotengenezwa na shaba, nishati kwa vitu vitakavyotengenezwa na nishati, na mbao kwa vitu vitakavyotengenezwa na mbao. Pia nina toa mawe ya shohamu, mawe ya kupangwa, mawe ya upambaji wandani ya rangi mbali mbali - kila haina ya mawe ya thamani - na marimari kwa wingi.
\v 3 Sasa, kwa sababu ya mapenzi yangu kwa nyumba ya Mungu, ninatoa hazina yangu binafsi ya dhahabu na fedha. Ninafanya hivi kwa nyongeza kwa yote niliyofanya katika hekalu takatifu:
\v 4 talanta za dhahabu elfu tatu kutoka Ofiri, na talanta elfu saba za fedha zilizotakasika, ili kufunika kuta za majengo.
\v 5 Ninachangia dhahabu kwa vitu vya kutengenezwa na dhahabu, na fedha kwa vitu vya kutengenezwa na fedha, na vitu vya kazi zote zinazotakiwa kufanywa na mafundi. Nani mwingine anataka kuchangia kwa Yahweh leo na kujitoa kwake?”
\p
\v 6 Kisha sadaka za hiari zilitolewa na viongozi wa mababu wa familia zao, viongozi wa makabila ya Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, na waamuzi walio juu ya kazi ya mfalme.
\v 7 Walitoa kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu talanta elfu tano na darkoni elfu kumi za dhahabu, talanta elfu kumi za fedha, talanta elfu kumi na nane za shaba, na talanta za chuma 100,000.
\v 8 Hao walio na mawe ya thamani waliyatoa katika Hazina ya nyumba Yahweh, chini ya usimamizi wa Yehieli, mzao wa Gerishoni.
\v 9 Watu walifurahi kwa ajili ya hizi sadaka za hiari, kwa sababu walitoa kwa moyo wao wote kwa Yahweh. Mfalme Daudi pia alifurahi sana.
\p
\v 10 Daudi alimbariki Yahweh mbele ya kusanyiko lote. Alisema, “Na uabudiwe, Yahweh, Mungu wa Israeli babu wetu, milele na milele.
\q1
\v 11 Kwako, Yahweh, kuna ukuu, nguvu, utukufu, ushindi, na enzi. Kwa kuwa yote yalio mbinguni na duniani ni yako. Kwako ni ufalme, Yahweh, na umetukuzwa kama mtawala juu ya vyote.
\q1
\v 12 Utajiri na heshima hutoka kwako, na unatawala juu ya watu wote. Mkononi mwako kuna nguvu na uwezo. Unao uweza na nguvu ya kuwafanya watu kuwa mkuu na kumpa uweza yeyote.
\q1
\v 13 Kisha sasa, Mungu wetu, tunakushukuru na kusifu jina lako tukufu.
\p
\v 14 Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuwe na uwezo wa kutoa vitu hivi kwa hiari hivi? Hakika kila kitu kimetoka kwako, na tumerundisha kilicho chako
\q1
\v 15 Kwa maana sisi tu wageni na wapanganji mbele yako, kama babu zetu wote walivyokuwa. Siku zetu katika dunia ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kubaki duniani.
\q1
\v 16 Yahweh Mungu wetu, utajiri huu wote tulio kusanya ili kujenga hekalu kwa kuheshimu jina lako - watoka kwako na ni wako.
\q1
\v 17 Nijua pia, Mungu wangu, ya kuwa wewe wauchunguza moyo na kuufurahia unyofu. Kwangu mimi, kwa unyofu wa moyo wangu nimetoa kwa hiari vitu hivi vyote, na sasa natazama kwa furaha watu wako waliopo hapa wakitoa zawadi kwa hiari kwako.
\q1
\v 18 Yahweh, Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Israeli - mababu zetu - hifadhi hili katika fikra za watu wako. Elekeza mioyo yao kwako.
\q1
\v 19 Mjalie Sulemani mwanangu moyo mkamilifu ili azishike amri zako, na amri zako za maagano, na sheria zako, na atekeleze mipango hii yote ya kuijenga jumba hili ya kifalme niliyoiandaa.”
\p
\v 20 Daudi akasema kwa kusanyiko lote, “Sasa mbariki Yahweh Mungu wenu.” Kusanyiko lote likambariki Yahweh, Munug wa mababu zao, wakainamisha vichwa vyao na kumuabudu Yahweh na kusujudu mbele za mfalme.
\p
\v 21 Kwa siku iliyo fuata, wakatoa dhabiu kwa Yahweh na kumtolea sadaka ya kuteketeza. Walitoa sadaka ya fahali elfu moja, kondoo dume elfu moja, na wana-kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji na dhabihu tele kwa Israeli yote.
\v 22 Siku ile, walikula na kunywa mbele za Yahweh kwa furaha kubwa. Walimfanya Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme mara ya pili, na kum mafuta kwa mamlaka ya Yahweh kuwa mtawala. Pia walimpaka mafuta Zadoki kuwa kuhani.
\v 23 Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha Yahweh kama mfalme mahali pa Daudi baba yake. Alifanikiwa, na Israeli yote ikamtii.
\v 24 Viongozi wote, wanajeshi, na wana wa Mfalme Daudi wakatoa utii kwa Mfalme Sulemani.
\p
\v 25 Yahweh alimheshimu sana Sulemani na akampa ukuu wa kifalme kuliko mfalme yeyote aliyetangulia kabla yake Israeli.
\p
\v 26 Daudi mwana wa Yese alitawala juu ya Israeli yote.
\v 27 Daudi alikuwa mfalme wa Israeli kwa miaka arobaini. Alitawala kwa miaka saba Hebroni na miaka thelathini na tatu Yerusalemu.
\v 28 Alikufa katika uzee mwema, baada ya kufurahia maisha marefu, mali na heshima. Sulemani mwanawe alitawala baada yake.
\p
\v 29 Mafanikio ya mfalme Daudi yameandikwa katika historia ya Samweli nabii, katika historia ya Nathani nabii, na katika historia ya Gadi nabii.
\v 30 Yaliyo andikwa hapo ni matendo ya utawala wake, nguvu zake na matukio yaliyompata yeye, israelI, na falme zote za nchi nyingine.