\v 4 Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituchagua sisi ambao tunaamini katika Kristo. Alituchagua sisi ili tuweze kuwa watakatifu na tusiolaumika mbele yake.
\v 5 Katika pendo Mungu alituchagua mwanzo kwa kututwaa kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Alifanya hivi kwa sababu alipendezwa kufanya kile alichotamani.
\v 11 Katika Kristo tulikuwa tumechaguliwa na kukusudiwa kabla ya wakati. Hii ilikuwa ni kutokana na mpango wa anayefanya vitu vyote kwa kusudi la mapenzi yake.
\v 13 Ilikuwa kwa njia ya Kristo kwamba mlisikia neno la kweli, injili ya wokovu wenu kwa njia ya Kristo. Ilikuwa katika yeye pia kwamba mmeamini na kutiwa mhuri na Roho Mtakatifu aliye ahidiwa.
\v 15 Kwa sababu hii, tangu wakati niliposikia kuhusu imani yenu ndani ya Bwana Yesu na kuhusu pendo lenu kwa wale wote ambao wametengwa kwa ajili yake.
\v 18 Ninaomba kwamba macho yenu ya moyoni yatiwe nuru kwa ninyi kujua ni upi ujasiri wa kuitwa kwenu. Naomba kwamba mjue utajiri wa utukufu wa urithi wake miongoni mwa wale waliotengwa kwa ajili yake.
\v 19 Naomba kwamba ujue ukuu uzidio wa nguvu yake ndani yetu ambao tunaamini. Huu ukuu ni kutokana na kufanya kazi katika nguvu zake.
\v 20 Hii ni nguvu iliyofanya kazi ndani ya Kristo wakati Mungu alipomfufua kutoka kwa wafu na kumketisha katika mkono wake wa kuume katika mahali pa mbingu.
\v 21 Alimketisha Kristo juu mbali na utawala, mamlaka, nguvu, enzi, na kila jina litajwalo. Alimketisha Yesu si tu kwa wakati huu lakini kwa wakati ujao pia.
\v 1 Kama vile mlivyo kuwa mmekufa katika makosa na dhambi zenu.
\v 2 Ilikuwa katika hali kwamba kwanza mlienenda kulingana na nyakati za ulimwengu huu. Mlikuwa mkienenda kwa kufuata mtawala wa mamlaka ya anga. Hii ndiyo roho yake yule afanyaye kazi katika wana wa kuasi.
\v 3 Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa miongoni mwa hawa wasioamini. Tulikuwa tukitenda kwa tamaa mbaya za miili yetu. Tulikuwa tukifanya mapenzi ya mwili na ufahamu wetu. Tulikuwa kwa asili wana wa ghadhabu kama wengine.
\p
\v 4 Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi.
\v 5 Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba tumeokolewa.
\v 6 Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu.
\v 7 Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu.
\v 10 Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.
\v 11 Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili. Mnaitwa “msio na tohara” kwa kile kinachoitwa tohara ya mwili inayofanywa kwa mikono ya binadamu.
\v 12 Kwa wakati huo mlikuwa mmetengwa na Kristo. Mlikuwa wageni kwa watu wa Israel. Mlikuwa wageni kwa agano la ahadi. Hamkuwa na uhakika wa wakati ujao. Mlikuwa bila Mungu katika ulimwengiu.
\v 13 Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu mmeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.
\p
\v 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu. Alifanya wawili kuwa mmoja. Kwa mwili wake aliuharibu ukuta wa utengano ambao ulikuwa umetutenganisha, huo uadui.
\v 15 Kwamba alikomesha sheria ya amri na kanuni ili kwamba aumbe mtu mmoja mpya ndani yake. Akafanya amani.
\v 19 Hivyo basi, ninyi watu wa mataifa si wasafiri na wageni tena. Bali ni wenyeji pamoja na wale watakatifu kwa ajili ya Mungu na wajumbe katika nyumba ya Mungu.
\v 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Kristo Yesu mwenyewe alikuwa jiwe kuu la pembeni.
\v 21 Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana.
\v 22 Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho Mtakatifu.
\v 6 Ukweli huu uliofichika ni kwamba watu wa Mataifa ni washiriki wenzetu na wajumbe wenzetu wa mwili. Niwashiriki pamoja na ahadi ya Kristo Yesu kupitia injili.
\v 8 Mungu alitoa zawadi hii kwangu, japo kuwa mimi ni mtu mdogo wa wote kuliko wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu. Zawadi hii ni kwamba inanipasa kuwatangazia mataifa injili yenye utajiri usiochunguzika wa Kristo.
\v 9 Inanipasa kuwa tangazia watu wote juu ya nini ni mpango wa Mungu wa siri. Huu ni mpango ambao ulikuwa umefichwa kwa miaka mingi iliyopita, na Mungu ambaye aliviumba vitu vyote.
\v 10 Hii ilikuwa kwamba, kupitia Kanisa, watawala na mamlaka katika sehemu za mbingu wapate kujua pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu.
\v 12 Kwa kuwa katika Kristo tuna ujasiri na uwezo wa kuingia kwa ujasiri kwa sababu ya imani yetu kwake.
\v 13 Kwa hiyo nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu. Haya ni utukufu wenu.
\p
\v 14 Kwa sababu hii napiga magoti kwa Baba.
\v 15 Ambaye kwake yeye kila familia mbinguni na juu ya nchi imeitwa jina.
\v 16 Ninaomba kwamba apate kuwaneemesha, kutokana na utajiri wa utukufu wake, awafanye imara kwa nguvu kupitia Roho wake, ambaye yu ndani yenu.
\v 17 Ninaomba kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani.
\v 18 Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Muwe katika pendo lake ili muweze kuelewa, pamoja na wote waaminio, jinsi upana, na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo.
\v 13 Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo.
\v 14 Hii ni ili kwamba tusiwe tena kama watoto, tusirushwerushwe huku na huko. Ili kwamba tusichukuliwe na kila aina ya upepo wa fundisho, kwa hila za watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka.
\v 15 Badala yake, tutaongea ukweli katika upendo na kukua zaidi katika njia zote ndani yake ambaye ndiye kichwa, Kristo.
\v 16 Kristo ameunganisha, kwa pamoja, mwili wote wa waumini. Umeungamanishwa pamoja na kila kiungo ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe katika upendo.
\v 28 Yeyote aibaye lazima asiibe tena. Badala yake ni lazima afanye kazi. Afanye kazi yenye manufaa kwa mikono yake, ili kwamba aweze kumhudumia mtu aliye na hitaji.
\v 29 Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza.
\v 2 Mtembee katika pendo, vilevile kama Kristo alivyotupenda sisi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Yeye alikuwa sadaka na dhabihu, kuwa harufu nzuri ya kumfurahisha Mungu.
\v 3 Zinaa na uchafu wowote na tamaa mbaya visitajwe kati yenu, kama inavyotakiwa kwa waaminio,
\v 4 wala machukizo yasitajwe kwenu na mazungumzo ya kipumbavu, au mizaha ya udhalilishaji, ambayo siyo sawa, badala yake iwepo shukrani.
\v 5 Mnaweza kuwa na uhakika ya kwamba kuna zinaa, uchafu, wala atamaniye, huyo ni mwabudu sanamu, hana urithi wowote katika ufalme wa Kristo na Mungu.
\v 6 Mtu yeyote asikudanganye kwa maneno matupu, kwa sababu ya mambo haya ya hasira ya Mungu inakuja juu ya wana wasiotii.
\v 25 Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake.
\v 26 Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno.
\v 27 Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala mawaa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa.
\v 28 Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe.
\v 29 Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huulisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa.
\v 1 Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.
\v 2 “Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),
\v 3 “ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu duniani.”
\p
\v 4 Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
\p
\v 5 Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. Muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo.
\v 6 Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu,
\v 7 watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu,
\v 9 Na Mabwana fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu. Msiwatishe mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni. Mkijua kuwa hakuna upendeleo ndani yake.
\p
\v 10 Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.
\v 11 Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba muweze kuzipinga hila za shetani.
\v 12 Kwa kuwa vita vyetu si vya damu na nyama, bali ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala wa ulimwengu wa uovu na giza, dhidi ya pepo katika ulimwengu wa roho.
\v 13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kusimama imara dhidi ya uovu katika kipindi hiki kiovu. Baada ya kumaliza kila kitu, mtasimama imara.
\v 14 Hatimaye simameni imara, Mkiwa mmefunga ukweli kiunoni, na kuvaa ya haki kifuani.
\v 15 Fanyeni hivi mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu wa kutangaza injili ya amani.
\v 16 Katika kila hali mkichukua ngao ya imani, ambayo itakuwezesha kuizima mishale yenye moto ya yule mwovu.
\v 17 Vaeni kofia ya wokovu na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu.
\v 18 Pamoja na maombi na sala. Ombeni kwa Roho kila wakati. Kwa mtazamo huu iweni waangalifu kila wakati kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waamini wote.
\v 19 Ombeni kwa ajili yangu, ili nipewe ujumbe ninapofungua mdomo wangu. Ombeni kwamba nieleweshe kwa ujasiri kweli iliyofichika ihusuyo injili.
\v 20 Ni kwa ajili ya injili mimi ni balozi niliyefungwa minyororo, ili kwamba ndani mwao niseme kwa ujasiri kama ninavyopaswa kusema.
\p
\v 21 Lakini ninyi pia mjue mambo yangu na jinsi ninavyoendelea, Tikiko ndugu yangu kipenzi na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawajulisha kila kitu.