\v 4 Ndani yake kulikuwa uzima, na huo uzima ulikuwa nuru ya wanadamu wote.
\v 5 Nuru yang'aa gizani, wala giza haikuishinda.
\p
\v 6 Palikuwa na mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.
\v 7 Alikuja kama shahidi kushuhudia kuhusu ile nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye.
\v 8 Yohana hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie kuhusu ile nuru.
\v 9 Huyo iliye nuru ya kweli na ambaye huwapa wanadamu wote nuru alikuwa yuaja duniani.
\p
\v 10 Alikuwa katika dunia, na dunia iliumbwa kupitia yeye, ilhali dunia haikumjua.
\v 11 Alikuja kwa watu wake, na watu wake hawakumpokea.
\v 12 Bali kwa wale wote waliompokea, walioamini katika jina lake, aliwapa kibali cha kuwa wana wa Mungu.
\v 13 Hawa walizaliwa, sio kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu mwenyewe.
\p
\v 14 Neno alifanyika mwili na akaishi miongoni mwetu. Tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa yule aliyekuja kutoka kwa Baba, akiwa amejaa neema na kweli.
\p
\v 15 Yohana alishuhudia kumhusu, na akapaza sauti akisema, “Huyu ndiye niliye sema habari zake; ‘Ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa amekuwako kabla yangu.’
\v 16 Kwa kuwa kutoka katika utimilifu wake, sisi sote tumepokea neema baada ya neema.
\v 17 Kwa kuwa sheria ililetwa kupitia Musa. Neema na kweli vilikuja kupitia Yesu Kristo.
\v 18 Hamna mwanadamu yeyote aliyewahi kumwona Mungu wakati wowote. Mungu mwana pekee, aliye katika upande wa Baba, amemfanya yeye ajulikane.”
\p
\v 19 Na huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Makuhani na Walawi waliotumwa kwake na Wayahudi kumwuliza, “Wewe ni nani?”
\v 20 Alikiri na hakukana, bali aliungama, “Mimi sio Kristo.”
\v 21 Hivyo wakamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni nani sasa? Wewe ni Eliya?” Akasema, “Mimi siye.” Wakasema, “Wewe ni nabii?” Akajibu, “Hapana.”
\v 22 Kisha wakamwambia, “Wewe ni nani, ili kwamba tuwape jibu waliotutuma? Wajishuhudiaje wewe mwenyewe?”
\v 23 Akasema, “Mimi ni sauti yake aliaye nyikani; ‘Inyosheni njia ya Bwana,’ kama nabii Isaya alivyosema.”
\p
\v 24 Basi kulikuwa na watu wametumwa pale kutoka kwa Mafarisayo. Wakamuuliza na kusema,
\v 25 “Kwa nini unabatiza basi kama wewe sio Kristo wala Eliya wala nabii?”
\v 26 Yohana aliwajibu akisema, “Ninabatiza kwa maji. Hata hivyo, miongoni mwenu anasimama mtu msiyemtambua.
\v 27 Huyu ndiye ajaye baada yangu. Mimi sistahili kulegeza kamba za viatu vyake.”
\v 29 Siku iliyofuata Yohana alimwona Yesu akija kwake akasema, “Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu!
\v 30 Huyu ndiye niliyesema habari zake nikisema, ‘Yeye ajaye nyuma yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.’
\v 31 Sikumtambua yeye, lakini ilifanyika hivyo ili kwamba afunuliwe katika Israeli, ndipo nikaja nikibatiza kwa maji.”
\p
\v 32 Yohana alishuhudia, “Niliona Roho akishuka kutoka mbinguni mfano wa njiwa, na ilibaki juu yake.
\v 33 Mimi sikumtambua lakini yeye aliyenituma ili nibatize kwa maji aliniambia, ‘Yule ambaye utaona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.’
\v 34 Nimeona na nimeshuhudia kwamba huyu ni Mwana wa Mungu.”
\p
\v 35 Tena siku iliyofuata Yohana alikuwa amesimama pamoja na wanafunzi wake wawili,
\v 36 walimwona Yesu akitembea na Yohana akasema, “Tazama, Mwana kondoo wa Mungu!”
\v 37 Wanafunzi wawili wakamsikia Yohana akisema haya wakamfuata Yesu.
\v 38 Hapo Yesu aligeuka na kuwaona wanafunzi wale wakimfuata, na akawauliza, “Mnataka nini?” Wakajibu, “Rabbi, (maana yake ‘mwalimu,’ unaishi wapi?”
\v 39 Akawaambia, “Njooni muone.” Kisha walikwenda na kuona mahali alipokuwa akiishi. Walikaa pamoja naye siku hiyo, kwa kuwa ilikuwa yapata kama saa kumi hivi.
\p
\v 40 Mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana akiongea na kisha kumfuata Yesu alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro.
\v 41 Akamwona ndugu yake Simoni na akamwambia, “Tumempata Masihi” (ambayo inatafsiriwa Kristo).
\v 42 Akamleta kwa Yesu. Yesu akamtazama na akasema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana, utaitwa Kefa,” (maana yake ‘Petro’).
\p
\v 43 Siku iliyofuata wakati Yesu alipotaka kuondoka kwenda Galilaya, alimpata Filipo na akamwambia, “Nifuate mimi.”
\v 44 Filipo alikuwa ni mwenyeji wa Bethsaida, mji wa Andrea na Petro.
\v 45 Filipo alimpata Nathanaeli na kumwambia, “Tumempata yule ambaye Musa aliandika habari zake katika sheria na Manabii. Yesu mwana wa Yusufu, kutoka Nazareti.”
\v 46 Nathanaeli akamwambia, “Je kitu chema chaweza kutokea Nazareti?” Filipo akamwambia, Njoo na uone.”
\v 47 Yesu akamwona Nathanaeli akija kwake na akasema, “Tazama, Mwisraeli kweli kweli asiye na udanganyifu ndani yake!”
\v 48 Nathanaeli akamwambia, “Wanifahamuje mimi?” Yesu akajibu na akamwambia, “Kabla Filipo hajakuita ulipokuwa chini ya mtini, nilikuona.”
\v 49 Nathanaeli akajibu, “Rabi wewe u Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”
\v 50 Yesu akajibu akamwambia, “Kwa sababu nilikuambia ‘Nilikuona chini ya mtini,’ je waamini? Utaona matendo makubwa kuliko haya.”
\v 51 Yesu akasema, “Amini, amini nawambieni. Mtaziona mbingu zikifunguka, na kuwaona malaika wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”
\v 3 Wakati walipoishiwa na divai, mama yake Yesu akamwambia, “Hawana divai.”
\v 4 Yesu akajibu, “Mwanamke kwa nini wanijia mimi? Muda wangu mimi bado haujatimia.”
\v 5 Mama yake akawambia watumishi, “Chochote atakachowambia fanyeni.”
\v 6 Basi kulikuwa na mitungi sita ya mawe pale iliyowekwa kwa ajili ya kunawa katika sikukuu za Wayahudi, kila moja lilikuwa na ujazo wa nzio mbili tatu.
\v 7 Yesu akawaambia, “Ijazeni maji mitungi ya mawe.” Wakajaza hadi juu.
\v 8 Kisha akawambia wale watumishi, “Chukueni kiasi sasa na mpeleke kwa muhudumu mkuu wa meza.” Wakafanya kama walivyoagizwa.
\v 9 Mhudumu mkuu aliyaonja yale maji yaliyokuwa yamebadilika na kuwa divai, ila hakujua yalikotoka (lakini watumishi waliochota maji walijua yalikotoka). Kisha akamwita bwana harusi na
\v 10 kumwambia, “Kila mmoja huanza kuwahudumia watu divai nzuri na wakiishalewa huwapa divai isiyo nzuri. Lakini wewe umeitunza divai nzuri hadi sasa”
\v 11 Ishara hii ya Kana ya Galilaya, ilikuwa ndiyo mwanzo wa ishara za miujiza aliyoifanya Yesu, akifunua utukufu wake, hivyo wanafunzi wake wakamwamini.”
\v 15 Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote waliokuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao.
\v 16 Kwa wauzaji wa njiwa akawambia, “Toeni vitu hivi mbali na mahali hapa. Acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa soko.”
\v 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa ilikuwa imeandikwa, ‘Wivu wa nyumba yako utanila.’
\p
\v 18 Wakuu wa Kiyahudi wakajibu, wakamwambia, “Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?”
\v 19 Yesu akawajibu, “Libomoeni hekalu hili nami nitalijenga baada ya siku tatu.”
\v 20 Kisha wakuu wa Wayahudi wakasema, “Ilichukua miaka arobaini na sita kujenga hekalu hili nawe unasema utalijenga kwa siku tatu?”
\v 21 Ingawa, yeye aliongea hekalu akimaanisha mwili wake.
\v 22 Hivyo baadaye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka kuwa alisema hivyo, wakaamini maandiko na kauli hii ambayo Yesu alikuwa amekwisha kuisema.
\v 1 Basi palikuwa na Farisayo mmoja jina lake Nikodemo, na kiongazi wa Kiyahudi.
\v 2 Alimjia Yesu usiku na kumwambia, “Rabi, twajua wewe ni mwalimu atokaye kwa Mungu, maana hamna mtu yeyote awezaye kufanya ishara hizi uzifanyazo asipokuwa Mungu yu pamoja naye.”
\v 3 Yesu akamjibu, “Amini, amini, mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.”
\v 4 Nikodemo akasema,” Mtu anawezaje kuzaliwa akiwa mzee? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili na kuzaliwa, je anaweza?”
\v 5 Yesu akajibu, “Amini, amini mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
\v 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, kwamba akamtoa mwanae wa pekee, ili kwamba mtu yeyote amwaminiye asiangamie bali awe na uzima wa milele.
\v 17 Kwa sababu Mungu hakumtuma mwanae duniani ili auhukumu ulimwengu, bali kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye.
\v 18 Amwaminiye Yeye hatahukumiwa. Yeye asiyemwamini tayari ashahukumiwa kwa sababu hajaliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
\v 19 Hii ndiyo sababu ya hukumu, ya kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini wanadamu wakapenda giza zaidi ya nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu.
\v 20 Kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru wala haji nuruni ili matendo yake yasije yakawekwa wazi.
\v 21 Lakini, yeye atendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane kwamba yametendwa kwa utiifu kwa Mungu.
\p
\v 22 Baada ya haya, Yesu pamoja na wanafunzi walienda katika nchi ya Yudea. Huko alitumia muda pamoja nao na alikuwa akibatiza.
\p
\v 23 Sasa Yohana pia alikuwa akibatiza huko Ainea karibu na Salim maana kulikuwa na maji mengi pale. Watu walikuwa wakija kwake na kubatizwa,
\v 25 Kisha palitokea mabishano kati ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi kuhusu shughuli za utakaso.
\v 26 Wakaenda kwa Yohana wakamwambia, “Rabi, yeye uliyekuwa naye ng'ambo ya mto Yorodani, yeye uliyeshuhudia habari zake, tazama, anabatiza na wote wanaenda wanamfuata.”
\v 27 Yohana akajibu “Mtu hawezi kupokea kitu chochote isipokuwa kama amepewa kutoka mbinguni.
\v 28 Ninyi wenyewe mwashuhudia kuwa nilisema kuwa, ‘Mimi sio Kristo,’ badala yake nilisema, ‘Nimetumwa mbele yake.’
\v 29 Bibi arusi ni wa bwana arusi. Sasa rafiki wa bwana arusi, asimamaye na kusikiliza hufurahia sana kwa sababu ya sauti ya bwana arusi. Hii sasa ni furaha yangu iliyotimilika.
\v 31 Yeye atokaye juu, yu juu ya yote. Yeye aliye wa ulimwengu anatoka ulimwenguni na huongea mambo ya ki ulimwengu. Yeye atokaye mbinguni yuko juu ya yote.
\v 32 Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna apokeaye ushuhuda wake.
\v 9 Yule mwanamke Msamaria akamwambia, “Inakuaje wewe Myahudi, kuniomba mimi mwanamke Msamaria, kitu cha kunywa?” Kwa sababu Wayahudi hawatangamani na Wasamaria.
\v 10 Yesu akamjibu, “Kama ungelijua karama ya Mungu, na yule anayekuambia ‘Nipe maji,’ ungelimwomba, na angelikupa maji ya uzima.”
\v 11 Mwanamke akajibu, “Bwana hauna ndoo ya kuchotea, na kisima ni kirefu. Utayapata wapi Maji ya Uzima?
\v 12 Je wewe ni mkuu, kuliko baba yetu Yakobo, ambaye alitupa kisima hiki, na yeye mwenyewe na watoto wake pamoja na mifugo yake wakanywa maji ya kisima hiki?”
\v 13 Yesu akajibu, “Yeyote anywae maji haya atapata kiu tena,
\v 14 lakini yeye atakaye kunywa maji nitakayompa hatapata kiu tena. Badala yake maji nitakayompa yatakuwa chemchemi inayobubujika hata uzima milele.”
\v 15 Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, nayaomba maji hayo ili nisipate kiu, na nisihangaike kuja hapa kuchota maji.”
\p
\v 16 Yesu akamwambia, “Nenda kamwite mumeo, kisha urudi.”
\v 18 kwa maana ushakuwa na wanaume watano, na hata ambaye unaye sasa sio mume wako. Ambalo umelisema kweli!”
\p
\v 19 Mwanamke akamwambia, “Bwana naona yakuwa wewe ni nabii.
\v 20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu. Lakini ninyi mwasema ya kuwa Yerusalemu ndiyo sehemu ambayo watu wanapaswa kuabudu.”
\v 21 Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu wala Yerusalemu.
\v 22 Ninyi watu mwaabudu kile msichokijua, lakini sisi twaabudu tunachokijua, kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.
\v 23 Hata hivyo, wakati waja, na sasa upo hapa, wakati waabuduo kweli watamwabudu Baba katika Roho na kweli, kwa sababu Baba anawatafuta watu wa namna hiyo kuwa watu wake wanao mwabudu.
\v 24 Mungu ni Roho, na wale wanaomwabudu wanapaswa kumwabudu kwa Roho na kweli.”
\v 25 Mwanamke akamwambia, “Ninajua kuwa Masihi anakuja, (aitwaye Kristo). Huyo atakapokuja atatwelezea mambo yote.”
\v 26 Yesu akamwambia, “Mimi unayesema nami ndiye.”
\p
\v 27 Wakati huo huo wanafunzi wake wakarudi. Nao walishangaa kwa nini alikuwa akizungumza na mwanamke, lakini hakuna aliyethubutu kumuuliza, “Unataka nini?” au “Kwa nini unazungumza naye?”
\p
\v 28 Hivyo mwanamke akauacha mtungi wake wa maji na akaenda mjini na akawaambia watu,
\v 29 “Njooni mwone mtu aliyeniambia mambo yangu yote niliyoyatenda, je yawezekana akawa ndiye Kristo?”
\v 30 Wakatoka mjini wakaja kwa Yesu.
\p
\v 31 Wakati huohuo, wanafunzi wake walimsihi wakisema, “Rabi kula chakula.”
\v 32 Lakini yeye aliwambia, “Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.”
\v 33 Wanafunzi wakaambiana, hakuna aliyemletea kitu chochote kula. Je walileta?”
\v 34 Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya mapenzi yake yeye aliyenituma na kutimiza kazi yake.
\v 35 Je, hamsemi, ‘Bado miezi minne na mavuno yatakuwa tayari?’ Ninawaambieni, tazameni mashamba yalivyo tayari kwa mavuno!
\v 37 Kwa kuwa msemo huu ni wa kweli, ‘Mmoja apanda na mwingine avuna.’
\v 38 Niliwatuma kuvuna ambacho hamkukihangaikia. Wengine wamefanya kazi na ninyi mmeingia katika furaha ya kazi yao.”
\p
\v 39 Wasamaria wengi katika mji ule walimwamini kwa sababu ya taarifa ya yule mwanamke aliyekuwa akishuhudia, “Aliyeniambia mambo yote niliyoyafanya.”
\v 41 Na wengi zaidi wakamwamini kwa sababu ya neno lake.
\v 42 Wakamwambia yule mwanamke, “Tunaamini sio tu kwa maneno yako, kwa sababu sisi wenyewe tumesikia, na sasa twafahamu kuwa hakika huyu ndiye mwokozi wa ulimwengu.”
\p
\v 43 Baada ya siku hizo mbili, Yesu akaondoka na kuelekea Galilaya.
\v 44 Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ametangaza kuwa nabii hana heshima katika nchi yake mwenyewe.
\v 45 Alipokuja katika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha. Walikuwa wameona mambo yote aliyoyafanya Yerusalemu kwenye sikukuu, kwa sababu na wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye sikukuu.
\v 46 Alikuja tena Kana ya Galilaya huko alikoyabadilisha maji kuwa divai. Palikuwa na ofisa ambaye mwanaye alikuwa ni mgonjwa huko Kapernaumu.
\v 47 Aliposikia kuwa Yesu alitoka Judea na kwenda Galilaya, alienda kwa Yesu na kumsihi ateremke amponye mwanawe, ambaye alikuwa karibu kufa.
\v 48 Ndipo Yesu akamwambia, “Ninyi msipoona ishara na maajabu hamwezi kuamini.
\v 49 Kiongozi akasema, “Bwana shuka chini kabla mwanangu hajafa.”
\v 50 Yesu akamwambia, “Nenda, mwanao aishi.” Yule mtu akaamini neno alilolisema Yesu na akaenda zake.
\v 51 Alipokuwa akishuka, watumishi wake walimpokea na kumwambia mwanaye alikuwa mzima.
\v 52 Hivyo akawauliza ni muda gani alipata nafuu. Wakajibu, “Jana muda wa saa saba homa ilipomwacha.”
\v 53 Ndipo baba yake akatambua kuwa ni muda ule ule Yesu aliosema, “Mwana wako ni mzima.” Hivyo yeye na familia yake wakaamini.
\v 1 Baada ya hapo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, na Yesu alipanda kwenda Yerusalemu.
\v 2 Na kule Yerusalemu palikuwa na birika kwenye mlango wa kondoo, lililokuwa likiitwa kwa lugha ya Kiaramu Bethzatha, nalo lina matao matano.
\v 3 Idadi kubwa ya wagonjwa ilikuwemo, vipofu, viwete, au waliopooza walikuwa wamelala katika matao hayo. \f + \ft Zingatia: Maneno ya mstari wa 3 hayaonekani katika nakala nzuri za kale. “Wakisubiri maji kutibuliwa.” \f* Kwa hakikia wakati fulani malaika alishuka ndani ya Bwana na kuyatibua maji.
\v 4 Hivi kwamba, yule ambaye alikuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alifanywa mzima kutokana na chochote kilichokuwa kimemshika kwa wakati huo.
\v 5 Palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane ndani ya matao.
\v 6 Yesu alipomwona amelala ndani ya matao na baada ya kutambua kuwa amelala pale kwa muda mrefu, Yesu alimwambia, “Je unataka kuwa mzima?”
\v 7 Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana sina mtu, wa kuniweka katika birika wakati maji yanapotibuliwa. Wakati ninapokuja kuingia mtu mwingine hunitangulia.”
\v 8 Yesu akamwambia, “Inuka na uchukue godoro lako na uende.”
\v 18 Kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kumtafuta ili wamuue sio tu kwa sababu ya kuivunja Sabato, bali kwa kumwita Mungu Baba yake, akijifanya kuwa sawa na Mungu.
\v 19 Yesu akawajibu, “Amini, amini, Mwana hawezi kufanya kitu chochote isipokuwa kile ambacho amemwona Baba yake anakifanya, kwa kuwa chochote Baba akifanyacho ndicho na Mwana atakachofanya.
\v 20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, na amwonyesha kila kitu anachokifanya na atamwonyesha mambo makubwa kuliko haya ili kwamba mzidi kushangaa.”
\v 21 Kwa kuwa kama vile ambavyo Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, halikadhalika Mwana pia humpa uzima yeyote apendaye.
\v 22 Kwa kuwa Baba hamhukumu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote
\v 23 ili kwamba wote wamuheshimu Mwana kama vile Mwana anavyomuheshimu Baba. Yeye asiyemuheshimu Mwana hamuheshimu Baba aliyemtuma.
\v 24 Amini, amini, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Badala yake, amepita kutoka mautini na kuingia uzimani.
\v 28 Msishangazwe na hili, kwa kuwa wakati unakuja ambao wafu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake
\v 29 nao watatoka nje: waliotenda mema kwa ufufuo wa uzima, na walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
\v 30 Siwezi kufanya kitu chochote kutoka kwangu mwenyewe. Kama nisikiavyo, ndivyo ninavyo hukumu na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
\p
\v 31 Kama nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingelikuwa wa kweli.
\v 32 Kuna mwingine anayenishuhudia na ninajua kwa hakika ushuhuda anaonishuhudia ni wa kweli.
\v 33 Mlituma watu kwa Yohana naye ameishuhudia kweli.
\v 34 Hatahivyo, ushuhuda ninaoupokea hautoki kwa mwanadamu. Ninayasema haya ili kwamba mweze kuokolewa.
\v 36 Bali ushuhuda nilionao ni mkuu kuliko ule wa Yohana, kwa kuwa kazi ambazo Baba amenipa kuzikamilisha, hizo kazi nizifanyazo zashuhudia kuwa Baba amenituma.
\v 37 Baba aliyenituma yeye mwenyewe ameshuhudia kuhusu mimi. Hamjawahi kusikia sauti yake wala kuona umbo lake wakati wowote.
\v 38 Hamna neno lake linalokaa ndani yenu kwa kuwa hamumwamini yeye aliyetumwa.
\v 39 Mnayachunguza maandiko mkidhani ndani yake mna uzima wa milele, na hayo maandiko yanashuhudia habari zangu na
\v 40 wala hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima wa milele.
\v 7 Filipo akamjibu, “Hata mikate ya thamani ya dinari mia mbili isingelitosha hata kila mmoja kupata hata kipande kidogo.”
\v 8 Andrea, mmoja wa wanafunzi wake ndugu yake Simoni Petro akamwambia
\v 9 Yesu, “Kuna mvulana hapa ana mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hii yafaa nini kwa watu wengi namna hii?”
\v 10 Yesu akawaambia, “Waketisheni watu chini” (kulikuwa na nyasi nyingi mahali pale). Hivyo wanaume wapata elfu tano wakakaa chini.
\v 11 Kisha Yesu akachukua ile mikate mitano akashukuru akawagawia wale waliokuwa wamekaa. Vivyo hivyo akawagawia samaki kwa kadiri ya vile wavyohitaji.
\v 12 Watu waliposhiba, aliwambia wanafunzi wake, “Vikusanyeni vipande vya mabaki, vilivyobaki ili kwamba kisipotee chochote.”
\v 13 Basi wakakusanya na kujaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri- vipande vilivyosazwa na wale waliokula.
\p
\v 14 Kisha watu walipoona ishara hii aliyoifanya walisema, “Kweli huyu ndiye yule nabii ajaye ulimwenguni.”
\v 15 Yesu alipotambua kuwa walikuwa wanataka kumkamata ili wamfanye kuwa mfalme wao kwa nguvu, alijitenga, na akaenda mlimani yeye peke yake.
\p
\v 16 Ilipokuwa jioni, wanafunzi wake walishuka kwenda ziwani.
\v 17 Wakapanda kwenye mtumbwi na walikuwa wakivuka kuelekea Kapernaumu. (Giza lilikuwa limeingia na Yesu alikuwa bado hajaja kwao).
\v 18 Wakati huo upepo mkali ulikuwa ukivuma, na bahari ilikuwa ikiendelea kuchafuka.
\v 19 Tena wanafunzi wake walipokuwa wamepiga makasia kama ishirini na matano au thelathini, wakamwona Yesu akitembea juu ya bahari kuukaribia mtumbwi, na wakaogopa.
\v 22 Siku iliyofuata, mkutano uliokuwa umesimama upande wa bahari waliona kuwa hakuna mtumbwi mwingine isipokuwa ule ambao Yesu na wanafunzi wake walikuwa hawajaupanda lakini wanafunzi wake walikuwa wameenda zao wenyewe.
\v 24 Wakati makutano walipotambua kuwa sio Yesu wala wanafunzi wake walikuwa kule, wao wenyewe walipanda ndani ya mitumbwi wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu.
\p
\v 25 Baada ya kumpata upande mwingine wa ziwa wakamuuliza, “Rabi ulikuja lini huku?”
\v 26 Yesu akawajibu, akawambia, “Amini, amini, mnanitafuta mimi, sio kwa sababu mliziona ishara, bali kwa sababu mlikula mikate na kushiba.
\v 27 Acheni kukifanyia kazi chakula chenye kuharibika, bali mkifanyie kazi chakula kidumucho hata milele kile ambacho mwana wa Adamu atawapa, kwa kuwa Mungu Baba ameweka muhuri juu yake.”
\p
\v 28 Kisha wakamwambia, “Ni nini tunapaswa kufanya ili kuzifanya kazi za Mungu?”
\v 29 Yesu akajibu, “Hii ndiyo kazi ya Mungu: kwamba mmwamini yeye aliyemtuma.”
\v 30 Basi wakamwambia, “Ni ishara zipi utakazofanya, kwamba tunaweza kuziona na kukuamini? Utafanya nini?
\v 31 Baba zetu walikula manna jangwani, kama ilivyo andikwa, “Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale.”
\p
\v 32 Kisha Yesu akawajibu, “Amini, amini, sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye awapaye mkate wa kweli kutoka mbinguni.
\v 33 Kwa kuwa mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupatia uzima ulimwengu.
\p
\v 34 Basi wakamwambia, “Bwana tupatie huu mkate wakati wote.”
\v 35 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima, yeye ajaye kwangu hatapata njaa na yeye aniaminiye hatahisi kiu kamwe.”
\v 36 Ingawa niliwaambia kwamba, mmeniona, na bado hamuamini.
\v 37 Wote ambao Baba anaonipa watakuja kwangu, na yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
\v 38 Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni, sio kwa ajili ya kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
\v 39 Na haya ndiyo mapenzi yake aliyenituma, kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali nitawafufua siku ya mwisho.
\v 49 Mababa zenu walikula manna jangwani, na wakafa.
\v 50 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, ili kwamba mtu aule sehemu yake ili asife.
\v 51 Mimi ni mkate uishio ambao umeshuka kutoka mbinguni. Kama mtu yeyote akila sehemu ya mkate huu, ataishi milele. Mkate nitakao utoa ni mwili wangu kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”
\p
\v 52 Wayahudi wakakasirika wenyewe kwa wenyewe na wakaanza kubishana wakisema, “Mtu huyu anawezaje kutupa mwili wake tuule?”
\v 53 Kisha Yesu akawaambia, “Amini, amini, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamta kuwa na uzima ndani yenu.
\v 54 Yeyote aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.
\v 55 Kwa kuwa mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
\v 71 Sasa alikuwa akiongea kuhusu Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, kwa kuwa alikuwa ni yeye akiwa mmoja wa wale kumi na wawili, ambaye ndiye angemsaliti Yesu.
\v 1 Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu hakupenda kuingia Yudea maana Wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua.
\v 10 Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.
\v 11 Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, “Yuko wapi?”
\v 12 Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “Hapana, huwapotosha makutano.”
\v 14 Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
\v 15 Wayahudi wakawa wakishangaa na kusema, “Kwa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe.”
\v 16 Yesu akawajibu na kuwaambia, “Mafundisho yangu siyo yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
\v 17 Iwapo yeyote atapenda kufanya mapenzi yake yeye, atajua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu, au kama ninazungumza kutoka kwangu mwenyewe.
\v 18 Kila anayezungumza yatokayo kwake mwenywe hutafuta utukufu wake, bali kila atafutaye utukufu wake yeye aliyemtuma, mtu huyo ni wa kweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.
\v 21 Yesu akajibu na akawaambia, “Nimetenda kazi moja, nanyi nyote mmeshangazwa kwa sababu yake.
\v 22 Musa aliwapa tohara (siyo kwamba inatoka kwa Musa, bali ile inatoka kwa mababa), na katika Sabato mnamtahiri mtu.
\v 23 Iwapo mtu atapokea tohara katika siku ya Sabato ili kwamba sheria ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa katika Sabato?
\v 24 Msihukumu kulingana na mwonekano, bali hukumuni kwa hak
\p
\v 25 Baadhi yao kutoka Yerusalemu wakasema, “Siye huyu wanayemtafuta kumwua?
\v 26 Na tazama, anaongea wazi wazi, na hawasemi chochote juu yake. Haiwezi ikawa kwamba viongozi wanajua kweli kuwa huyu ni Kristo, inaweza kuwa?
\v 27 Tunajua huyu mtu anatokea wapi. Kristo atakapokuja, hata hivyo, hakuna atakayejua wapi anakotoka.”
\p
\v 28 Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, “Ninyi nyote mnanijua mimi na mnajua nitokako. Sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye aliyenituma ni wa kweli, na hamumjui yeye.
\v 29 Ninamjua yeye kwa sababu nimetoka kwake na alinituma.”
\p
\v 30 Walikuwa wanajaribu kumkamata, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono wake juu yake kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
\v 31 Hata hivyo, wengi katika makutano walimwamini. Walisema, “Kristo atakapokuja, atafanya ishara nyingi kuliko alizofanya mtu huyu?”
\v 35 Kwa hiyo Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi kwamba tusiweze kumuona? Ataenda kwa waliotawanyika kati ya Wayunani na kuwafundisha Wayunani?
\v 36 Ni neno gani hili alilolisema, ‘Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako hamtamweza kuja’?”
\p
\v 37 Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, “Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe.
\v 38 Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima.”
\v 9 \f + \ft Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7:53 - 8:11 hapo juu. \f* Waliposikia hayo, waliondoka mmoja mmoja, kuanzia aliye mzee. Mwishowe Yesu aliachwa peke yake, pamoja na mwanamke aliyekuwa katikati yao.
\v 10 Yesu alisimama na kumwambia, “Mwanamke, waliokushitaki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?”
\v 11 Akasema, “Hakuna hata mmoja Bwana.” Yesu akasema, “Hata mimi sikuhukumu. Enenda. Kuanzia sasa na kuendelea usitende dhambi tena.”
\p
\v 12 Tena Yesu akazungumza na watu akisema, “Mimi ni nuru ya ulimwengu; yeyote anifuataye hatatembea gizani bali atakuwa na nuru ya uzima.”
\v 14 Yesu alijibu akawaambia, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli. Ninajua mahali nilikotoka na kule ninakoenda, lakini ninyi hamjui mahali ninapotoka au kule ninakoenda.
\v 20 Alisema maneno haya akiwa karibu na hazina alipokuwa akifundisha hekaluni, na hakuna hata mmoja aliyemkamata kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
\v 23 Yesu akawaambia, “Mnatoka chini; mimi natoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu.
\v 24 Kwa hiyo, niliwaambieni kuwa mtakufa katika dhambi zenu. Vinginevyo muamini kuwa MIMI NDIYE, mtakufa katika dhambi zenu.”
\p
\v 25 Kwa hiyo wakamwambia, “Wewe ni nani?” Yesu akawaambia, “Yale niliyowaambia tangu mwanzo.
\v 26 Ninayo mambo mengi ya kuzungumza na kuhukumu juu yenu. Hata hivyo, yeye aliyenituma ni wa kweli; na mambo niliyoyasikia kutoka kwake, mambo haya nayasema kwa ulimwengu.”
\v 28 Yesu akasema, “Mtakapomwinua juu Mwana wa Mtu, ndipo mtakapojua kuwa MIMI NDIYE, na kwamba sifanyi lolote kwa nafsi yangu. Kama Baba alivyonifundisha, ninazungumza mambo haya.
\v 29 Yeye aliyenituma yuko pamoja nami, na yeye hajaniacha peke yangu, kwani kila mara nafanya yale yanayompendeza.”
\v 30 Wakati Yesu akisema mambo haya, wengi wakamwamini.
\p
\v 31 Yesu akasema kwa wale Wayahudi waliomwamini, “Ikiwa mtakaa katika neno langu, ndipo mtakuwa wanafunzi wangu kweli,
\v 32 nanyi mtaijua kweli, na kweli itawaweka huru.”
\v 33 Walimjibu, “Sisi ni uzao wa Ibrahimu na kamwe hatujawahi kuwa chini ya utumwa wa yeyote; utasemaje, “Tutawekwa huru?”
\v 34 Yesu aliwajibu, “Amini, amini, nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
\v 35 Mtumwa hakai nyumbani wakati wote; mwana hudumu siku zote.
\v 36 Kwa hiyo, ikiwa Mwana atawaweka huru, mtakuwa huru kweli.”
\v 37 Ninajua kwamba ninyi ni uzao wa Ibrahimu; mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.
\v 38 Ninasema mambo ambayo nimeyaona pamoja na Baba yangu, na ninyi vile vile mnafanya mambo ambayo mliyasikia kutoka kwa baba yenu.”
\p
\v 39 Walijibu na kumwambia, “Baba yetu ni Ibrahimu.” Yesu akawaambia, “Kama mngelikuwa watoto wa Ibrahimu, mngefanya kazi za Ibrahimu.
\v 40 Hata sasa mnatafuta kuniua, mtu aliyewaambia ukweli kwamba nilisikia kutoka kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivi.
\v 41 Mnafanya kazi za baba yenu.” Wakamwambia, “Hatukuzaliwa katika uzinzi, tunaye Baba mmoja, Mungu.”
\v 42 Yesu akawaambia, “Ikiwa Mungu ni Baba yenu, mngenipenda mimi, kwa maana nimetoka kwa Mungu; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye alinituma.
\v 43 Kwa nini hamyaelewi maneno yangu? Kwa sababu hamuwezi kuvumilia kuyasikia maneno yangu.
\v 44 Ninyi ni wa baba yenu, shetani, na mnataka kuzitenda tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo na hawezi kusimama katika kweli kwa sababu kweli haimo ndani yake. Anapoongea uongo, anaongea kutoka kwenye asili yake kwa sababu ni mwongo na baba wa uongo.
\v 52 Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kuwa una pepo. Ibrahimu na nabii walikufa; lakini unasema, ‘Ikiwa mtu atalishika neno langu, hataonja mauti.’
\v 53 Wewe si mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu aliyekufa, sivyo? Manabii pia walikufa. Wewe wajifanya kuwa nani?”
\v 54 Yesu akajibu, “Ikiwa nitajitukuza mwenyewe, utukufu wangu ni bure; ni Baba yangu anayenitukuza - yule mnayemsema kuwa ni Mungu wenu.
\v 55 Ninyi hamjamjua yeye, lakini mimi namjua yeye. Ikiwa nitasema, ‘Simjui,’ nitakuwa kama nyinyi, muongo. Hata hivyo, ninamjua na maneno yake nimeyashika.
\v 56 Baba yenu Abrahamu alishangilia alivyoiona siku yangu; aliiona na alifurahi.
\p
\v 57 Wayahudi wakamwambia, “Haujafikisha umri wa miaka hamsini bado, nawe umemuona Ibrahimu?”
\v 58 Yesu akawaambia, “Amini, amini, nawaambia, kabla Ibrahimu hajazaliwa, MIMI NIKO.”
\v 59 Ndipo walichukua mawe wapate kumpiga, lakini Yesu alijificha na akatoka nje ya hekalu.
\v 1 Hata Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu kipofu tangu kuzaliwa kwake.
\v 2 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Rabi, nani aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?”
\v 3 Yesu akawajibu, “Siyo huyu mtu wala wazazi wake waliotenda dhambi, bali kazi za Mungu zipate kufunuliwa kupitia kwake.
\v 4 Tunapaswa kufanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana. Usiku waja wakati ambapo hakuna atakayeweza kufanya kazi.
\v 5 Wakati niwapo ulimwenguni, mimi ndimi nuru ya ulimwengu.”
\p
\v 6 Baada ya Yesu kusema maneno haya, alitema mate kwenye ardhi, alifanya tope, na akampaka yule mtu lile tope machoni.
\v 7 Akamwambia, nenda kaoge katika kisima cha Siloam (Inayotafsiriwa kama ‘aliyetumwa’).” Kwa hiyo huyo mtu alienda, akanawa, na akarudi, anaona.
\v 8 Majirani wa yule mtu na wale waliomuona mwanzo kama mwombaji wakawa wanasema, Je! Huyu siye yule mtu aliyekuwa akikaa na kuomba?” Wengine walisema, “Ni yeye.”
\v 9 Na wengine walisema, “Hapana, bali anafanana naye.” Lakini alikuwa akisema, “Ni mimi.”
\v 11 Alijibu, “Mtu aitwaye Yesu alifanya tope na kupaka macho yangu na kuniambia, ‘Nenda Siloam ukanawe.’ Kwa hiyo nilienda, na nikanawa, na nikapata kuona tena.”
\v 12 Wakamwambia, “Yuko wapi?” Alijibu, “Sijui.”
\p
\v 13 Wakampeleka yule mtu aliyewahi kuwa kipofu kwa Mafarisayo.
\v 14 Nayo ilikuwa siku ya Sabato wakati Yesu alipotengeneza tope na kuyafumbua macho yake.
\v 15 Ndipo tena Mafarisayo wakamwuliza alipataje kuona. Aliwaambia, “Aliweka tope katika macho yangu, nikanawa, na sasa naweza kuona.”
\v 16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Mtu huyu hajatoka kwa Mungu kwa sababu haishiki Sabato.” Wengine walisema, “Inawezekanaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?” Kwa hiyo kukawa na mgawanyiko kati yao.
\v 17 Ndipo wakamwuliza yule kipofu tena, “Unasemaje juu yake kwa sababu aliyafungua macho yako?” Kipofu akasema, “Ni nabii.”
\v 19 Waliwauliza wazazi, “Je, huyu ni mtoto wenu mnayesema alizaliwa kipofu? Amewezaje sasa kuona?”
\v 20 Hivyo wazazi wake wakamjibu, “Tunajua kuwa huyu ni mtoto wetu na kwamba alizaliwa kipofu.
\v 21 Jinsi gani sasa anaona, hatujui, na yeye aliyemfumbua macho yake, hatumjui. Mwulizeni yeye. Ni mtu mzima. Anaweza kujieleza mwenyewe.”
\v 22 Wazazi wake walisema mambo haya, kwa sababu waliwaogopa Wayahudi. Kwa maana Wayahudi walikuwa wamekubaliana tayari kuwa, ikiwa yeyote atakiri kuwa Yesu ni Kristo, atatengwa na sinagogi.
\v 23 Kwa sababu hii, wazazi wake walisema, “Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.”
\p
\v 24 Kwa hiyo kwa mara ya pili, walimwita yule mtu aliyewahi kuwa kipofu na kumwambia, “Mpe Mungu utukufu. Tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi.”
\v 25 Ndipo yule mtu alijibu, “Awe ni mwenye dhambi, mimi sijui. Kitu kimoja ninachokijua: nilikuwa kipofu, na sasa ninaona.”
\v 1 Amini, amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
\v 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.
\v 17 Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena.
\v 18 Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba.”
\p
\v 19 Mgawanyiko tena ukatokea kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
\v 20 Wengi wao wakasema, “Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?”
\v 21 Wengine wakasema, “Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?”
\p
\v 22 Ndipo ikaja sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu.
\v 23 Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.
\v 24 Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, “Mpaka lini utatuweka katika mashaka? Kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.
\v 25 Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.
\v 28 Ninawapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu.
\v 29 Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja awezaye kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.
\v 30 Mimi na Baba tu mmoja.”
\p
\v 31 Wakabeba mawe ili wampige tena.
\v 32 Yesu akawajibu, “Nimeshawaonesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba. Kwa kazi zipi kati ya hizo mnataka kunipiga mawe?”
\v 33 Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa kazi yoyote iliyo nzuri, lakini kwa kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu.”
\v 34 Yesu akawajibu, “Haikuandikwa katika sheria yenu, ‘Nilisema, ninyi ni miungu?’
\v 35 Ikiwa aliwaita miungu, kwa wale ambao Neno la Mungu liliwajilia (na Maandiko hayawezi kuvunjwa),
\v 36 mnasema juu ya yule ambaye Baba alimtoa na kumtuma katika ulimwengu, ‘Unakufuru,’ kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu’?
\v 37 “Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini.
\v 38 Hata hivyo, ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, ziaminini kazi ili kwamba muweze kujua na kufahamu kwamba Baba yuko ndani yangu na mimi niko ndani ya Baba.”
\v 40 Yesu akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo Yohana alikuwa akibatiza kwanza, na akakaa huko.
\v 41 Watu wengi wakaja kwa Yesu huku wakisema, “Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini mambo yote aliyoyasema Yohana juu ya huyu mtu ni ya kweli.”
\v 1 Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Alitokea Bethania, kijiji cha Mariamu na dada yake Martha.
\v 2 Alikuwa ni Mariamu yule yule aliyempaka Bwana marhamu na kumfuta miguu yake kwa nywele zake, ambaye ndugu yake Lazaro alikuwa ni mgonjwa.
\v 3 Ndipo dada hawa walituma ujumbe kwa Yesu na kusema, “Bwana, angalia yule umpendaye ni mgonjwa.”
\v 4 Yesu aliposikia alisema, “Ugonjwa huu si wa mauti, lakini, badala yake ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu ili kwamba Mwana wa Mungu apate kutukuzwa katika huo ugonjwa.”
\v 5 Ikawa Yesu alimpenda Martha na dada yake na Lazaro.
\v 6 Aliposikia kuwa Lazaro ni mgonjwa, Yesu alikaa siku mbili zaidi mahali alipokuwa.
\p
\v 7 Ndipo baada ya hili aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni Yudea tena.”
\v 8 Wanafunzi wakamwambia, “Rabi, Wayahudi walikuwa wakijaribu kukupiga mawe, na wewe unataka kurudi huko tena?”
\v 9 Yesu akawajibu, “Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu anapotembea mchana hawezi kujikwaa, kwa sababu anaona kwa mwanga wa ulimwengu huu.
\v 10 Hata hivyo, ikiwa atatembea usiku, atajikwaa kwa sababu nuru haiko ndani yake.”
\p
\v 11 Yesu akasema mambo haya, na baada ya mambo haya, akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini ninakwenda ili kwamba nipate kumuamsha kutoka usingizini.”
\v 12 Ndipo wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala, ataamka.
\v 13 Wakati huu Yesu alikuwa akizungumza habari za kifo cha Lazaro, lakini wao walidhani anazungumza juu ya kulala usingizi.
\v 14 Ndipo Yesu akazungumza nao wazi wazi, “Lazaro amekufa.
\v 15 Nina furaha kwa ajili yenu, kwamba sikuwepo kule ili kwamba mpate kuamini. Twendeni kwake.”
\v 16 Basi Tomaso, aliyeitwa Pacha, aliwaambia wanafunzi wenzake, “Nasi twendeni pia tukafe pamoja na Yesu.”
\p
\v 17 Wakati Yesu alipokuja, alikuta kwamba Lazaro tayari amekwishakuwa kaburini siku nne.
\v 18 Nayo Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu kama kilomita mbili hivi.
\v 19 Wengi kati ya Wayahudi wakaja kwa Martha na Mariamu kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.
\v 30 Naye Yesu alikuwa hajaja bado ndani ya kijiji, bali alikuwa bado mahali alipokutana na Martha.
\v 31 Ndipo Wayahudi waliokuwa na Mariamu katika nyumba na wale waliokuwa wakimfariji, walipomuona akiinuka haraka na kutoka nje, walimfuata; walidhani kuwa anaenda kaburini ili akalie huko.
\p
\v 32 Wakati Mariamu, alipofika pale Yesu alipokuwa alimuona na, akaanguka chini ya miguu yake na kumwambia, “Bwana, kama ungelikuwa hapa, ndugu yangu asingelikufa.”
\v 33 Yesu alipomuona analia, na Wayahudi waliokuja pamoja naye walikuwa wakilia pia, aliomboleza katika roho na kufadhaika;
\v 37 Lakini wengine kati yao wakasema, “Siyo huyu, mtu aliyeyafumbua macho ya yule aliyekuwa kipofu, hakuweza kumfanya huyu mtu asife?”
\p
\v 38 Ndipo Yesu, huku akiomboleza nafsini mwake tena, alienda kwenye kaburi. Sasa lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.
\v 39 Yesu akasema, “Liondoweni jiwe.” Martha, dada yake na Lazaro, yeye aliyekufa, akamwambia Yesu, “Bwana, kwa muda huu, mwili utakuwa umeoza, kwa sababu amekwishakuwa maiti kwa siku nne.”
\v 40 Yesu akamwambia, “Mimi sikuwaambia ya kwamba, kama ukiamini, utauona utukufu wa Mungu?”
\p
\v 41 Basi wakaliondoa jiwe. Yesu akainua macho yake juu na kusema, “Baba, nakushukuru kwa kuwa unanisikiliza.
\v 42 Nilijua kwamba unanisikia mara zote, lakini ni kwa sababu ya kusanyiko ambalo limesimama kunizunguka kwamba nimesema haya, ili kwamba wapate kuamini kuwa wewe umenituma.”
\v 43 Baada ya kusema haya, alilia kwa sauti kubwa, “Lazaro, toka nje!”
\v 44 Mfu alitoka nje amefungwa mikono na miguu kwa sanda za kuzikia, na uso wake ulifungwa na kitambaa.” Yesu akawaambia, “Mfungueni mkamwache aende.”
\p
\v 45 Ndipo Wayahudi wengi waliokuja kwa Mariamu na kuona Yesu alichofanya, walimwamini;
\v 54 Yesu hakutembea tena wazi wazi kati ya Wayahudi, bali aliondoka hapo na kwenda nchi iliyo karibu na jangwa katika mji uitwao Efraimu. Hapo alikaa na wanafunzi.
\v 57 Wakati huu wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwamba ikiwa mmoja atajua Yesu alipo, anapaswa kutoa taarifa ili kwamba wapate kumkamata.
\v 3 Kisha Mariamu akachukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake; nyumba yote ilijaa harufu ya manukato.
\v 6 Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini, bali kwa sababu alikuwa mwizi: yeye ndiye aliyeshika mfuko wa fedha na alikuwa anachukua baadhi ya vilivyowekwa humo kwa ajili yake mwenyewe.
\v 7 Yesu alisema, “Mwache aweke alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu.
\v 8 Maskini mtakuwa nao siku zote; lakini hamtakuwa nami siku zote.”
\p
\v 9 Basi umati mkubwa wa Wayahudi walipata kujua ya kuwa Yesu yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili ya Yesu tu, ila wamwone na Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka katika wafu.
\v 10 Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri ili wamue Lazaro;
\v 12 Na siku iliyofuata umati mkubwa walikuja kwenye sikukuu. Waliposikia ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu,
\v 13 walichukua matawi ya miti ya mitende na kutoka nje kwenda kumlaki na wakapiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli.”
\v 14 Yesu alimpata mwana-punda akampanda; kama vile ilivyoandikwa,
\v 16 Wanafunzi wake hawakuyaelewa mambo haya hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kuwa mambo haya aliandikiwa yeye na ya kwamba wametenda mambo haya kwake.
\v 34 Mkutano wakamjibu, “Sisi tumesikia katika sheria ya kwamba Kristo atadumu hata milele. Nawe wasemaje, ‘Mwana Adamu lazima ainuliwe juu?’ Huyu Mwana wa Mtu ni nani?”
\v 35 Basi Yesu akawaambia, “Nuru ingalipo pamoja nanyi muda kidogo. Tembeeni maadamu mnayo nuru, ili kwamba giza lisije likawaweza. Yeye aendeaye gizani hajui aendako.
\v 36 Mngali mnayo nuru, iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Yesu aliyasema haya na kisha akaenda zake akajificha wasimwone.
\v 37 Ingawa Yesu alifanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, bado hawakumwamini
\v 38 ili litimie neno la nabii Isaya, alilosema: “Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”
\v 39 Ndio sababu wao hawakuamini, maana Isaya alisema tena,
\v 40 “Amewapofusha macho, na ameifanya migumu mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao na wakafahamu kwa mioyo yao, na wakaongoka nami nikawaponya.”
\p
\v 41 Isaya alisema maneno hayo kwa kuwa aliuona utukufu wa Yesu na akanena habari zake.
\p
\v 42 Walakini, hata wakuu wengi walimwamini Yesu; lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakukiri ili wasije wakafurushwa kutoka kwa sinagogi.
\v 1 Sasa kabla ya sikukuu ya pasaka, kwa sababu Yesu alifahamu kuwa saa yake imefika ambayo atatoka katika dunia hii kwenda kwa baba, akiwa amewapenda watu wake ambao walikuwa duniani, aliwapenda mpaka mwisho.
\v 2 Ikawa tayari Ibilisi alikuwa amewaka katika moyo wa Yuda Isikariote, mwana wa simoni, kumsaliti Yesu.
\v 3 Yesu alifahamu kuwa baba ameweka vitu vyote katika mikono yake na kwamba ametoka kwa Mungu na alikuwa anakwenda tena kwa Mungu.
\v 4 Aliamka chakulani na akatandika chini vazi lake la nje. Kisha alichukua taulo na akajifunga mwenyewe.
\v 6 Akaja kwa Simoni Petro, na Petro akamwambia, “Bwana, unataka kuniosha miguu yangu?”
\v 7 Yesu akajibu na kumwambia, “Nifanyalo hulijui sasa, lakini utaelewa baadaye.”
\v 8 Petro akamwambia, “Hutaniosha miguu yangu kamwe.” Yesu akamjibu, “Ikiwa sitakuosha, hutakuwa na sehemu pamoja nami.”
\v 9 Simoni Petro akamwambia, “Bwana, usinioshe miguu yangu tuu, bali pia na mikono na kichwa changu.”
\v 10 Yesu akamwambia, “Yeyote ambaye amekwisha kuoga haitaji kuoga isipokuwa miguu yake, na amekuwa safi mwili wake wote; ninyi mmekuwa safi, lakini si nyote.”
\v 11 Kwa kuwa Yesu alijua yule atakaye msaliti; hii ndiyo sababu alisema, si nyote mmekuwa safi.”
\p
\v 12 Wakati Yesu alipokuwa amewaosha miguu yao na akiisha chukua vazi lake na kukaa tena, aliwaambia, “Je mnaelewa kile ambacho nimewafanyia?
\v 13 Mnaniita mimi “Mwalimu” na “Bwana,” hii mnasema kweli, maana ndivyo nilivyo.
\v 14 Ikiwa mimi Bwana na mwalimu, nimewaosha miguu yenu, ninyi pia imewapasa kuwaosha wenzenu miguu.
\v 16 Amini, Amini, nawambia, mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala yule ambaye ametumwa si mkuu kuliko yule aliye mtuma.
\v 17 Ikiwa unafahamu mambo haya, umebarikiwa ukiyatenda.
\v 18 Sisemi kuhusu ninyi nyote, kwa kuwa nawajua wale ambao nimewachagua - bali nasema haya ili kwamba maandiko yaweze kutimilizwa: ‘Yeye alaye mkate wangu ameniinulia kisigino chake.’
\p
\v 19 Ninawambia hili sasa kabla halijatokea ili kwamba litakapotokea, muweze kuamini kuwa mimi NDIYE.
\v 20 “Amini, amini, nawambia, anipokeaye mimi humpokea ambaye nina mtuma, na yule anipokeaye mimi humpokea yule aliye nituma mimi.”
\p
\v 21 Wakati Yesu aliposema haya, alisumbuka rohoni, alishuhudia na kusema, “Amini, amini, nawambia kwamba mmoja wenu atanisaliti.”
\v 23 Kulikuwa katika meza, mmoja wa wanafunzi wake ameegama kifuani mwa Yesu yule ambaye Yesu alimpenda.
\v 24 Simoni Petro alimuuliza mwanafunzi huyu na kusema, “Twambie ni yupi ambaye kwake anazungumza.”
\v 25 Mwanafunzi yule aliye egama kifuani mwa Yesu na akamwambia, “Bwana, ni nani?”
\v 26 Kisha Yesu alijibu, “Ni kwake yule nitakaye chovya kipande cha mkate na kumpatia.” Hivyo alipo kuwa amechovya mkate, alimpatia Yuda mwana wa Simon Iskariote.
\v 27 Na baada ya mkate, Shetani alimuingia. Kisha Yesu akamwambia, “Kile ambacho unataka kukifanya ukifanye haraka.”
\v 28 Sasa hakuna mtu katika meza alijua sababu ya Yesu kusema jambo hili kwake.
\v 29 Baadhi yao walidhani kwamba, kwa sababu Yuda alishika mfuko wa fedha, Yesu alimwambia, “Nunua vitu tunavyohitaji kwa ajili ya sikukuu,” au kwamba anapaswa kutoa kitu kwa masikini.
\v 30 Baada ya Yuda kupokea mkate, alitoka nje haraka; na ilikuwa usiku.
\p
\v 31 Wakati Yuda alipokuwa ameondoka, Yesu alisema, “Sasa mwana wa Adam ametukuzwa, na Mungu ametukuzwa katika yeye.
\v 32 Mungu atamtukuza katika yeye mwenyewe, na atamtukuza mara moja.
\p
\v 33 Watoto wadogo, niko pamoja nanyi kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama nilivyowambia Wayahudi, ‘Niendako, hamuwezi kuja.’ Sasa nawambia ninyi, pia.
\v 34 Ninawapa amri mpya, kwamba mpendane; kama mimi nilivyo wapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi pia imewapasa kupendana ninyi kwa ninyi.
\v 35 Kwa ajili ya hili watu watatambua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu, ikiwa mna upendo kwa kila mmoja na mwingine.”
\p
\v 36 Simoni Petro alimwambia, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akajibu, “Mahali ninapokwenda kwa sasa hutaweza kunifuata, lakini utanifuata baadaye.”
\v 37 Petro akamwambia, “Bwana, kwa nini nisikufuate hata sasa? Mimi nitayatoa maisha yangu kwa ajili yako.”
\v 38 Yesu akajibu, “Je utayatoa maisha yako kwa ajili yangu? Amini amini nakwambia, jogoo hatawika kabla hujanikana mara tatu.”
\v 1 “Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko. Unamwamini Mungu niamini pia na mimi.
\v 2 Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi; kama isingekuwa hivyo, ningekuwa nimekuambia, kwa vile ninakwenda kukuandalia mahali kwa ajili yako.
\v 6 Yesu alimwambia, “Mimi ndiye njia, kweli, na uzima; hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.
\v 7 Kama mngeli nijua mimi, mngalikuwa mnamjua na Baba yangu pia; kuanzia sasa na kuendelea mnamjua na mmeshamuona yeye.”
\p
\v 8 Filipo alimwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba, na hivyo itakuwa imetutosha.”
\v 9 Yesu akamwambia, “Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Filipo? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; Jinsi gani unasema, ‘Tuonyeshe Baba?’
\v 10 Hamuamini kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa kusudi langu mwenyewe; badala yake, ni Baba anayeishi ndani yangu anayetenda kazi yake.
\v 12 Amini, amini, nawaambia, yeye aniaminiye, mimi kazi zile nizifanyazo, atazifanya kazi hizi pia; na atafanya hata kazi kubwa kwasababu ninakwenda kwa Baba.
\v 13 Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana.
\v 14 Nanyi mkiomba kitu chochote katika jina langu, hilo nitafanya.
\p
\v 15 Kama mkinipenda, mtazishika amri zangu.
\v 16 Na nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine ili kwamba aweze kuwa pamoja nanyi milele,
\v 17 Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea yeye kwa sababu haumuoni, au kumjuwa yeye. Hata hivyo ninyi, mnamjua yeye, kwani anakaa pamoja nayi na atakuwa ndani yenu.
\v 18 Sitawaacha kama yatima, nitarudi kwenu.
\v 19 Kwa muda kidogo, ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mwaniona. Kwa sababu ninaishi, nanyi mtaishi pia.
\v 21 Yeyote azishikaye amri zangu na kuzitenda, ndiye ambaye anipenda mimi; na ambaye anipenda mimi atapendwa na Baba yangu, na nitampenda na nitajionyesha mimi mwenyewe kwake.”
\p
\v 22 Yuda (siyo Iskariote) akamwambia Yesu, “Bwana, Je! Ni nini kinatokea kwamba utajionyesha mwenyewe kwetu na siyo kwa ulimwengu?
\v 23 Yesu alijibu akamwambia, “Kama yeyote akinipenda, atalishika neno langu. Baba yangu atampenda, na tutakuja kwake na tutafanya makao yetu pamoja naye.
\v 25 Nimeyasema mambo haya kwenu, wakati bado ninaishi miongoni mwenu.
\v 26 Hata hivyo, Mfariji, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha mambo yote na atawafanya mkumbuke yote ambayo niliyasema kwenu.
\v 27 Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyo yenu wala msiwe na woga.
\p
\v 28 Mlisikia vile nilivyowaambia, ‘Ninaenda zangu, na nitarudi kwenu.’ Kama mngelinipenda mimi, mngekuwa na furaha kwa sababu ninakwenda kwa Baba, kwa kuwa Baba ni mkuu kuliko mimi.
\v 29 Sasa nimekwisha kuwaambia kabla haijatokea ili kwamba, wakati ikitokea, mweze kuamini.
\v 30 Sitaongea nanyi maneno mengi, kwa kuwa mkuu wa dunia hii anakuja. Yeye hana nguvu juu yangu,
\v 31 lakini ili kwamba ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba, nafanya ambacho Baba ananiagiza mimi, kama vile alivyonipa amri. Inukeni, na tutoke mahali hapa.
\v 1 Mimi ni mzabibu wa kweli, na baba yangu ndiye mkulima.
\v 2 Kila tawi ndani yangu ambalo halizai tunda, huliondoa na husafisha kila tawi ambalo huzaa ili kwamba liweze kuzaa matunda zaidi.
\v 3 Ninyi tayari mmekuwa safi kwa sababu ya ujumbe ambao nimekwisha waambia.
\v 4 Mkae ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake lisipo kuwa katika mzabibu, vivyo hivyo nayi, msipo kaa ndani yangu.
\p
\v 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Yeyote anayedumuye ndani yangu na mimi ndani yake, yeye huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote.
\v 6 Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, hutupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea.
\v 14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo.
\v 15 Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa kuwa nimewajulisheni mambo yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba.
\v 16 Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mzae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hili liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni.
\v 18 Kama ulimwengu utawachukia, mjuwe kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.
\v 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda kama wa kwao. Lakini kwa sababau ninyi sio wa ulimwengu na kwa sababu niliwachagua kutoka katika ulimwengu, ni kwa ajili hii ulimwengu huwachukia.
\v 20 Kumbukeni neno ambalo niliwaambia, ‘Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake.’ Ikiwa walinitesa mimi, watawateseni ninyi pia; Kama walishika neno langu, watalishika la kwenu pia.
\v 21 Watawatenda mambo haya yote kwa ajili ya jina langu kwa sababu hawamjui yule aliyenituma.
\v 22 Kama nisingekuja na kuwaambia, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
\v 23 Anichukiaye mimi humchukia Baba pia.
\v 24 Ikiwa sijafanya kazi miongoni mwao ambayo hapana mmoja aliyeifanya, wangelikuwa hawana dhambi; lakini sasa wamefanya yote mawili wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu.
\v 25 Hili linatokea ili kwamba neno litimie ambalo limeandikwa katika sheria yao: ‘Wananichukia mimi bila sababu.’
\p
\v 26 Wakati mfariji amekuja, ambaye nitamtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyu ndiye, Roho wa kweli, ambaye anatokea kwa Baba, atanishuhudia.
\v 3 Watawatendea mambo haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala mimi.
\v 4 Nimewaambia mambo haya ili kwamba wakati wa haya kutokea ukifika, mtakumbuka jinsi nilivyowaambia. Sikuwaambia kuhusu mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
\p
\v 5 Sasa naenda kwa yule aliyenituma; lakini hakuna kati yenu anayeniuliza, “Unaenda wapi?”
\v 6 Kwa sababu nimesema maneno haya kwenu, huzuni imejaa mioyoni mwenu.
\v 7 Hata hivyo, nawaambia ukweli: ni vyema kwenu nikiondoka; kwa maana nisipoondoka, mfariji hatakuja kwenu; lakini nikienda ntamtuma kwenu.
\v 8 Atakapokuja, mfariji atauthibitishia ulimwengu dhambi, utauwa na hukumu.
\v 9 Kuhusiana na dhambi, kwa sababu hawakuniamini,
\v 10 kuhusiana na utauwa, kwa maana naenda kwa baba,
\v 11 na kuhusiana na hukumu kwa sababu mkuu wa dunia hii ashahukumiwa.
\p
\v 12 Ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamtayaelewa sasa.
\v 13 Lakini, yeye, Roho wa kweli, akija, atawaongoza katika kweli yote; kwa kuwa hataongea kwa ajili yake mwenyewe; lakini yoyote atakayoyasikia, atayasema mambo hayo; na atawajulisha juu ya mambo yatakayokuja.
\v 15 Vitu vyote alivyonavyo Baba ni vyangu; kwa hiyo, nimesema kwamba Roho atachukua mambo yangu na atayadhihirisha kwenu.
\p
\v 16 Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi tena, mtaniona.”
\v 17 Baadhi ya wanafunzi wake wakaambiana, “Ni nini anachotuambia, “Muda mfupi, na hamtaniona tena,’ na, kisha, mda mfupi mtaniona,’ na, ‘Kwa sababu naenda kwa Baba?”
\v 18 Kwa hiyo wakasema, “Ni kitu gani anachosema, ‘Bado mda mfupi?’ Hatujui asemavyo.”
\p
\v 19 Yesu aliona kuwa walitamani kumuuliza, naye akawaambia, “Mnajiuliza wenyewe kuhusu hili, nilivyosema, ‘Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi mtaniona?’
\v 20 Amini, amini, nawaambia, mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utashangilia, mtakuwa na huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.
\v 21 Mwanamke anakuwa na huzuni wakati anapokuwa na uchungu kwa sababu wakati wa kujifungua umefika; lakini anapojifungua mtoto, hakumbuki tena maumivu kwa sababu ya furaha yake kwamba mtoto amezaliwa duniani.
\v 25 Nimezungumza na ninyi kwa lugha isiyoeleweka, lakini saa inakuja ambapo sitazungumza kwa lugha isiyoeleweka lakini badala yake nitawaambia waziwazi kuhusu Baba.
\v 26 Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitaomba kwa Baba kwa ajili yenu;
\v 27 Kwa kuwa Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na kwa sababu mmeniamini kuwa nimetoka kwa Baba.
\v 28 Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni; tena, naondoka ulimwenguni na ninaenda kwa Baba.”
\p
\v 29 Wanafunzi wake wakamwambia, “Unaona, sasa unaongea wazi wazi na hautumii mafumbo.
\v 30 Sasa, tunajua kwamba unajua mambo yote, na hauhitaji mtu yoyote akuulize maswali. Kwa sababu hii tunaamini kuwa unatoka kwa Mungu.
\p
\v 31 Yesu akawajibu, “Sasa mmeamini?”
\v 32 Tazama, saa inakuja, ndiyo na hakika imefika, ambapo mtatawanyika kila mmoja na kwao mtaniacha mwenyewe. Lakini siko peke yangu kwa sababu Baba yupo nami.
\v 1 Yesu aliyasema mambo haya; kisha akainua macho yake kuelelea mbinguni na akasema, “Baba, saa imewadia; mtukuze mwanao ili na mwana naye akutukuze wewe -
\v 6 Nililifunua jina lako kwa watu ulionipa hapa duniani. Walikuwa watu wako; lakini ulinikabidhi mimi. Nao wamelishika neno lako.
\v 7 Sasa wanajua kuwa kila kitu ulichonipa mimi kinatoka kwako,
\v 8 kwa kuwa nimewapa maneno yale yote uliyonipatia mimi. Waliyapokea na kweli wakajua ya kuwa mimi nimetoka kwako, na wakaamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
\v 9 Ninawaombea wao. Siuombei ulimwaengu bali wale ulionipa kwa kuwa wao ni wako.
\v 10 Vitu vyote ambavyo ni vyangu ni vyako, na vile ulivyonavyo wewe ni vyangu; nami ninatukuzwa katika hivyo.
\v 11 Mimi simo tena ulimwenguni, bali wao wamo ulimwenguni, nami sasa naja kwako. Baba Mtakatifu, watunze kwa jina lako lile ulilonipa mimi ili wao nao wawe kitu kimoja, kama vile mimi na wewe tu kitu kimoja.
\v 12 Nilipokuwa nao, niliwalinda kwa jina ulilonipa; Niliwalinda, na hakuna hata mmoja wao aliyepotea isipokuwa mwana wa upotevu, ili kwamba maandiko yatimie.
\p
\v 13 Sasa ninakuja kwako; lakini ninasema haya ulimwenguni ili kwamba furaha yangu ikamilishwe ndani yao wenyewe.
\v 14 Nimewapa neno lako; dunia imewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwengu
\v 15 Siwaombei kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu.
\v 16 Wao si wa dunia kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwenguni.
\v 17 Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika kweli; neno lako ndiyo kweli.
\v 18 Jinsi ulivyonituma ulimwenguni, nami nimewatuma ulimwenguni.
\v 20 Si hawa tu ninaowaombea, bali na wale watakaoamini kupitia neno lao
\v 21 ili kwamba wao nao wawe kitu kimoja, kama vila wewe Baba, ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Nawaombea ili kwamba wao pia waweze kuwa ndani yetu ili ulimwengu uweze kuamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
\v 22 Utukufu ule ulionipa mimi - nimewapa wao, ili kwamba waweze kuwa kitu kimoja, kama vile sisi tulivyo kitu kimoja -
\v 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili waweze kukamilishwa katika umoja; ili ulimwengu ujue kuwa hakika wewe ndiye uliyenituma, na kuwapenda, kama vile wewe ulivyonipenda, mimi.
\v 24 Baba, kile ulichonipa mimi - natamani kwamba wao pia waweze kuwa pamoja nami mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu, ule ulionipa: kwa kuwa wewe ulinipenda mimi kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.
\p
\v 25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua wewe, lakini mimi nakujua wewe; na hawa wanajua kwamba ulinituma.
\v 26 Nililifanya jina lako lijulikane kwao, na nitalifanya lijulikane ili kwamba lile pendo ambalo kwalo ulinipenda mimi liweze kuwa ndani yao, na mimi niweze kuwa ndani yao.”
\v 1 Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea upande wa pili wa kijito cha Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambayo yeye na wanafunzi wake wakaingia ndani yake.
\p
\v 2 Sasa yule Yuda, aliyetaka kumsaliti, naye alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akikutana na wanafunzi wake mara kwa mara.
\v 3 Naye Yudasi, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.
\v 4 Naye Yesu, haku akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake, alijitokeza mbele na akawauliza, “Ni nani mnayemtafuta?”
\v 5 Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareth.” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Naye Yudasi aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja na wale askari.
\v 6 Kwa hiyo alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi kinyume na kuanguka chini.
\v 7 Halafu akawauliza tena, “Ni nani mnayemtafuta? Nao wakamjibu tena “Yesu mnazareth.”
\v 8 Yesu akawajibu, “Nimekwisha kuwaambia kuwa Mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa wengine waende.”
\v 9 Haya yalikuwa hivyo ili lile neno litimilike; pale aliposema; “Katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja.”
\p
\v 10 Ndipo Simon Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani mkuu. Na jina lake mtumishi yule lilikuwa Malko.
\v 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?”
\p
\v 12 Basi lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi, walimkamata Yesu na kumfunga.
\v 13 Nao wakamwongoza kwanza mpaka kwa Anasi, kwani yeye alikuwa mkwe wa Kayafa, ambaye ndiye aliyekuwa Kuhani mkuu kwa mwaka huo.
\v 15 Simon Petro alimfuata Yesu, na vivyo hivyo mwanafunzi mwingine. Na yule mwanafunzi alikuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, naye akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani mkuu;
\v 16 lakini Petro alikuwa amesimama nje ya mlango. Basi yule mwanafunzi aliyekuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, alitoka nje akaenda kuongea na yule mlinda mlango na kumwingiza Petro ndani.
\v 17 Basi yule kijakazi aliyekuwa akilinda mlango, alimwambia Petro, “Je wewe si mmoja wa wafuasi wa huyu mtu?” Naye akasema, “Mimi siye.”
\v 18 Na wale watumishi na wakuu walikuwa wamesimama mahali pale; wamekoka moto wa makaa kwa maana, kulikuwa na baridi, na hivyo walikuwa wakiota moto ili kupata joto. Naye Petro alikuwa nao, akiota moto akiwa amesimama.
\p
\v 19 Kuhani mkuu alimhoji Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.
\v 20 Yesu akamjbu, “Nimeuambia waziwazi ulimwengu. Mimi nilifundisha wakati wote kwenye masinagogi na hekaluni mahali ambapo wayahudi hukusanyika. Nami sikusema lolote katika siri.
\v 22 Yesu alipokwisha sema hivyo, mmoja wa maofisa aliyekuwa amesimama akampiga kofi na kisha akasema, “Je, hivyo ndivyo inavyokupasa kumjibu kuhani mkuu?”
\v 23 Naye Yesu akamjibu, “Kama nimesema jambo lolote baya basi uwe shahidi kwa ajili ya uovu, na kama nimemjibu vyema kwa nini kunipiga?
\v 25 Sasa Simoni Petro alikuwa amesimama akijipasha joto mwenyewe. Halafu wale watu wakamwambia. “Je, wewe pia si mmoja wa wanaafunzi wake?” Akakana akisema “Mimi siye.”
\v 26 Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ambaye alikuwa ndugu wa yule mwanaume ambaye Petro alimkata sikio, alisema, “Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?”
\v 28 Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika bali waweze kuila pasaka.
\v 29 Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. “Ni shitaka gani mnalolileta kuhusu huyu mtu?”
\v 30 Wakamjibu na kumwambia, “Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.”
\v 31 Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria zenu.” Nao Wayahudi wakamwambia, “Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote.”
\v 33 Basi Pilato akaingia tena Praitorio akumwita Yesu; akamwambia, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?”
\v 34 Yesu akamjibu, “Je, wewe waniuliza swali hili kwa sababu wataka kujua au kwa sababu wengine wamekutuma ili uniulize mimi?”
\v 35 Naye Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, au sivyo?” Taifa lako na kuhani mkuu ndio waliokuleta kwangu; wewe umefanya nini?
\v 36 Yesu akajibu; “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa na sehemu katika ulimwengu huu watumwa wangu wangenipigania ili nisitolewe kwa Wayahudi. Kwa kweli ufalme wangu hautoki hapa.” Basi
\v 37 Pilato akamwambia, “Je, wewe basi u mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe ndivyo unanvyosema kuwa mimi ni mfalme, kwa sababu hii mimi nilizaliwa na kwa sababu hii mimi nimekuja ulimwenguni ili niwe shahidi wa ile kweli. Yeyote aliye wa hiyo kweli huisikiliza sauti yangu.
\v 38 Pilato akamwambia, “Kweli ni nini?” Naye alipokwisha sema haya akaenda kwa Wayahudi na kuwaambia “Sioni kosa lolote katika mtu huyu.
\v 39 Walakini, ninyi mna utamaduni unaonifanya nimfunfungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Je mnataka nimfungulie mfalme wa Wayahudi.”
\v 1 Basi Pilato alimchukua Yesu na kuamuru apigwe mijeredi.
\v 2 Wale maaskari wakasokota miiba na kutengeneza taji. Wakaiweka juu ya kichwa cha Yesu na kumvalisha vazi la rangi ya zambarau.
\v 3 Wakamjia na kusema, “Wewe mfalme wa Wayahudi!” na kisha kumpiga kwa mikono yao.
\p
\v 4 Kisha Pilato alitoka nje na kuwaambia watu, “Tazama nawaleteeni huyu mtu kwenu ili mjue kwamba mimi sikuona hatia yoyote ndani yake.”
\v 5 Kwa hiyo Yesu akatoka nje; alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau. Ndipo Pilato akawaambia, “Tazameni mtu huyu hapa!”
\p
\v 6 Kwa hiyo wakati kuhani mkuu na wakuu walipomwona Yesu, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe, msulubishe.” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa kuwa mimi sioni hatia ndani yake.”
\v 7 Wayahudi wakamjibu Pilato, “Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu.”
\p
\v 8 Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa,
\v 9 akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, “Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu.
\v 10 Kisha Pilato akamwambia, “Je, wewe huongei na mimi? Je, wewe hujui kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua na mamlakaya kukusulubisha?”
\q
\v 11 Yesu akamjibu, “Usingekuwa na nguvu dhidi yangu kama usingepewa toka juu. Kwa hiyo, mtu aliyenitoa kwako ana dhambi kubwa.”
\p
\v 12 Kutokana na jibu hili, Pilato akataka kumwacha huru, lakini Wayahudi wakapiga kelele wakisema, “Kama utamwacha huru basi wewe si rafiki wa Kaisari: Kila ajifanyaye kuwa mfalme hunena kinyume cha Kaisari.”
\v 13 Pilato alipoyasikia maneno haya, akamleta Yesu nje kisha akakaa kwenye kiti cha hukumu mahali pale panapojulikana kama sakafu, lakini kwa Kiebrania, Gabatha.
\v 14 Ilikuwa siku ya maandalizi ya Pasaka panapo muda wa saa ya sita. Pilato akawaambia Wayahudi, “Tazameni mfalme wenu huyu hapa!”
\p
\v 15 Wakapiga kelele, “Mwondoshe, mwondoshe, msulubishe!” Pilato akawaambia, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?” Naye Kuhani mkuu akajibu, “Sisi hatuna mfalme isipokuwa Kaisari.”
\p
\v 16 Ndipo Pilato alipomtoa Yesu kwao ili asulubiwe.
\p
\v 17 Nao wakamchukua Yesu, naye akatoka, hali ameubeba msalaba wake mwenyewe mpaka kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa, kwa Kihebrania huitwa Golgotha.
\v 20 Wengi wa Wayahudi waliisoma alama hiyo kwani mahali pale aliposulibishwa Yesu palikuwa karibu na mji. Alama hiyo iliadikwa kwa Kiebrania, kwa Kirumi na kwa Kiyunani.
\v 23 Baada ya askari kumsulubisha Yesu, walichukua mavazi yake na kuyagawa katika mafungu manne, kila askari fungu moja, vivyo hivyo na kanzo. Sasa ile kanzu haikuwa imeshonwa bali ilkuwa imefumwa yote tokea juu.
\v 24 Kisha wakasemezana wao kwa wao, “Tusiipasue, bali tupigeni kura ili kuona itakuwa ya nani.” Hili lilitokea ili lile andiko litimizwe, lile lisemalo waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura.”
\p
\v 25 Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.
\v 26 Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!”
\q
\v 27 Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.
\p
\v 28 Baada ya hilo, huku Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, “Naona kiu.”
\v 29 Chombo kilichokuwa kimejaa siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake.
\v 30 Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, “Imekwisha.” Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.
\p
\v 31 Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale waliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe.
\v 32 Ndipo askari walipokuja na kuvunja miguu ya mtu wa kwanza na wa pili aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.
\v 36 Mambo haya yalikuwa ili lile neno lililonenwa lipate kutimia, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.”
\v 37 Tena andiko lingine husema, “Watamtazama yeye waliyemchoma”
\p
\v 38 Baada ya mambo haya Yusufu wa Arimathaya, kwa vile alikuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri kwa kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato kwamba auchukue mwili wa Yesu. Naye Pilato akampa ruhusa. Kwa hiyo Yusufu akaja kuuondoa mwili wa Yesu.
\v 40 Kwa hiyo waukauchukua mwili wa Yesu wakaufanga kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi wakati wa kuzika.
\v 41 Mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani; ndani ya ile bustani kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakuna mtu alikuwa amawahi kuzikwa humo.
\v 1 Mapema siku ya kwanza ya juma, kungali bado giza, Mariamu Magdalena alikuja kaburini; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
\v 2 Kwa hiyo akakimbia mbio kwenda kwa Simon Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, kisha akawaambia, “Wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza.”
\p
\v 3 Kisha Petro na yule mwanafunzi mwingine wakatoka, kuelekea kaburini.
\v 4 Wote walipiga mbio kwa pamoja; yule mwanafunzi mwingine alikimbia kwa kasi zaidi ya Petro na kufika kaburini wa kwanza.
\v 11 Hata hivyo, Mariamu alikuwa amesimama kaburini akilia, alivyokuwa akiendelea kulia aliinama kisha akatazama kaburini.
\v 12 Akaona malaika wawili waliovalia mavazi meupe wamekaa mmoja kichwani na mwingine miguuni mahali ambapo Yesu alikuwa amelala.
\p
\v 13 Nao wakamwambia, “Mwanamke, kwa nini unalia?” Naye akawaambia, “Ni kwa sababu wamemchukua Bwana wangu, nami sijui walikomweka.”
\v 14 Alipokwisha sema hayo, aligeuka na kumwona Yesu akiwa amesimama. Lakini hakutambua kama huyo alikuwa Yesu.
\q
\v 15 Naye Yesu akamwambia, “Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?” Naye huku akidhani kuwa ni mtunza bustani akamwambia, “Bwana, kama ni wewe uliyemchukua, niambie ulikomweka, nami nitamchukua.”
\p
\v 16 Yesu akamwambia, “Mariamu.” Naye akageuka mwenyewe na kumwambia kwa Kiaramu, “Raboni,” yaani hii ni kusema, “Mwalimu.”
\q
\v 17 Yesu akamwambia, “Usiniguse, kwani bado sijapaa kwenda kwa baba; bali uende kwa ndugu zangu ukawaambie kuwa nitapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye pia ni Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”
\q
\v 18 Mariamu Magdalena akaja kuwaambia wanafunzi, “Nimemwona Bwana,” na kwamba amemwambia mambo haya.
\p
\v 19 Na ilipokuwa jioni, siku hiyo, siku ya kwanza ya juma, na milango ikiwa imefungwa mahali wanafunzi walipokuwapo kwa kuwahofia Wayahudi, Yesu alikuja na kusimama katikati yao na kuwaambia, “Amani iwe kwenu.”
\v 23 Yeyote mmsameheye dhambi, amesamehewa; na wale mtakaowafungia watafungiwa.”
\p
\v 24 Thomaso, mmoja wa wale kumi na wawili, aliyeitwa Didimas, hakuwa na wanafunzi wenzake Yesu alipokuja.
\v 25 Wale wanafunzi wengine waka mwambia baadaye, “Tumemwona Bwana.” Naye akawaambia, “Kama sitaona alama za misumari katika mikono yake, na kuweka vidole vyangu kwenye hizo alama, na pia kuweka mkono wangu kwenye ubavu wake sitaamini.”
\p
\v 26 Baada ya siku nane wanafunzi walikuwa chumbani tena, naye Thomaso alikuwa pamoja nao. Wakati milango ilipokuwa imefungwa Yesu alisimama katikati yao. Na akasema, “Amani na iwe nanyi.”
\q
\v 27 Kisha akamwambia Thomaso, leta kidole chako na uone mikono yangu; leta hapa mikono yako na uweke kwenye ubavu wangu; wala usiwe asiyeamini bali aaminiye.”
\q
\v 28 Naye Thomaso akajibu na kumwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu.”
\q
\v 29 Yesu akamwambia, Kwa kuwa umeniona, umeamini. Wamebarikiwa wao wanaoamini, pasipokuona.”
\p
\v 30 Kisha Yesu alifanya ishara nyingi mbele ya wanafunzi, ambazo hazijawahi kuandikwa katika kitabu hiki;
\v 1 Baada ya mambo hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi katika bahari ya Tiberia; hivi ndivyo alivyojidhihirisha mwenyewe:
\v 2 Simon Petro alikuwa pamoja na Thomaso aitwaye Didimas, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili wa Yesu.
\v 3 Simon Petro akawaambia, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Sisi, pia tutaenda nawe.” Wakaenda wakaingia kwenye mashua, lakini usiku huo wote hawakupata chochote.
\p
\v 4 Na asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufukweni, nao wanafunzi hawakutambua kuwa alikuwa Yesu.
\q
\v 5 Kisha Yesu akawaambia, “Vijana, mna chochote cha kula?” Nao wakamjibu, “Hapana.”
\q
\v 6 Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kuume wa mashua, nanyi mtapata kiasi.” Kwa hiyo wakashusha wavu nao hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki.
\v 7 Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, “Ni Bwana.” Naye Simon Petro aliposikia kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa vizuri), kisha akajitupa baharini.
\v 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwenye mashua (kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni), nao walikuwa wakivuta zile nyavu zilizokuwa zimejaa samaki.
\v 11 Basi Simon Petro akapanda na kuukokota ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa, kiasi cha samaki 153; japo walikuwa wengi, ule wavu haukuchanika.
\v 12 Yesu akawaambia, “Njooni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanfunzi aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua kuwa alikuwa ni Bwana.
\v 13 Yesu akaja, akachukua ule mkate, kisha akawapa, akafanya vivyo hivyo na kwa wale samaki.
\v 15 Baada ya kuwa wamefungua kinywa, Yesu akamwambia Simon Petro, “Simon mwana wa Yohana je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana; “Wewe wajua kuwa mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wanakondoo wangu.”
\p
\v 16 Akamwambia mara ya pili, “Simon mwana wa Yona, je, wanipenda?” Petro akamwambia, “Ndiyo, Bwana; wewe wajua kuwa nakupenda. “Yesu akamwambia, “Chunga kondoo wangu.”
\p
\v 17 Akamwambia tena mara ya tatu, “Simon, mwana wa Yohana, Je wanipenda?” Naye Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, “Je Wewe wanipenda?” Naye akamwambia, “Bwana, unajua yote; unajua kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
\p
\v 18 Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda.”
\v 19 Yesu alisema haya ili kuonesha ni aina gani ya kifo ambacho Petro angemtukuza Mungu. Baada ya kuwa amesema haya, akamwambia Petro, “Nifuate.”
\p
\v 20 Petro aligeuka na kumwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akawafuata- Huyu ndiye aliyekuwa amajiegemeza kwenye kifua cha Yesu wakati wa chakula cha jioni na kumwuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”
\v 21 Petro alimwona na kisha akamwuliza Yesu, “Bwana, Huyu mtu atafanya nini?”
\p
\v 22 Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, hilo linakuhusu nini?” Nifuate.”
\v 23 Kwa hiyo habari hii ikaenea miongoni mwa wale ndugu, kwamba mwanafunzi huyo hatakufa. Lakini Yesu hakumwambia Petro kuwa, mwanafunzi huyo hafi, “Kama nataka yeye abaki mpaka nitakapokuja yakuhusu nini?”
\p
\v 24 Huyu ndiye mwanafunzi atoaye ushuhuda wa mambo haya, na ndiye aliye andika mambo haya, na tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
\v 25 Kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu aliyafanya. Kama kila moja lingeandikwa, nadhani kwamba ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.