sw_tn/psa/066/010.md

25 lines
860 B
Markdown

# Umetuleta kwenye wavu
Mwandishi anazungumzia adhabu ya Mungu kana kwamba Mungu aliwashika watu wake katika wavu.
# wavu
mtego kwa ajili ya ndege au mnyama
# umeweka mzigo mkubwa viunoni mwetu
Mwandishi anazungumzia kile ambacho watu wamestahamili kama kulazimika kubeba mizigo mizito migongoni mwao.
# Umewafanya watu kuendesha juu ya vichwa vyetu
Hii ni picha ya kushindwa vibaya vitani. "Ni kana kwamba adui zetu wametushinda vitani na wameendesha vibandawazi vyetu juu ya miili yetu iliyoanguka"
# tulipita katika moto na maji
Mungu aliwajaribu kwa maafa ya asili kama moto na mafuriko. "tuliteseka kama watu wanavyoteseka kutokana na moto na mafuriko"
# sehemu yenye nafasi
Mwandishi anazungumzia baraka walizonazo sasa watu wa Israeli kana kwamba wameletwa katika nafasi kubwa ya wazi ambapo wako salama. "nafasi ya wazi ambapo tuko salama"