# Kutoka kwao litatoka jiwe kuu la pembeni "Jiwe la pembeni litatoka kwao." Kiongozi mhimu anazungumzwa kama vile jiwe kuu la msingi wa jengo. # kutoka kwao kitatoka kigingi cha hema "kigingi cha hema kitatoka kwao." Viongozi wakuu wanazungumzwa kama vile vigingi vikubwa vinavyolishikilia hema mahali pake. # kutoka kwao utatoka upinde wa vita "upinde wa vita utatoka kwao." Viongozi wa kijeshi wanasemwa kama walikuwa upinde uliotumiwa vitani. # Watakuwa kama mashujaa "Watakuwa wenye nguvu vitani" # wawakanyagao adui zao katika matope ya mitaani vitani "wawashindao adui zao kwa ukamilifu" # nao watawaabisha wapanda farasi "nao watawashinda adui zao wapiganao nao katika farasi"