# "nikasikia" anayezungumza ni Yohana. # nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni Neno "sauti" inaonesha mtu anayezungumza. "Nikasikia mtu akinena kwa sauti toka mbinguni" # sasa wokovu umekuja, nguvu Mungu kuwaokoa watu kwa nguvu zake inazungumziwa kana kwamba wokovu wake na nguvu zake ni vitu vinavyoweza kuja. "Sasa Mungu amewaokoa watu wake kwa nguvu zake" # umekuja "kuanza kuwepo kabisa" au "kutokea" au "kuwa kweli." Sio kwamba vitu hivi havikuwepo kabala, lakini sasa Mungu anavidhihirisha kwa sababu wakati wake kutokea "umekuja." # ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake Utawala wa Mungu na mamlaka ya Kristo yanazungumziwa kama vile vinakuja. "Mungu atawala kama mfalme, na Kristo wake anamamlaka yote" # mshitaki wa ndugu zetu ametupwa chini Huyu ni joka aliyetupwa chini katika 12:10 # ndugu zetu Waumini wenzao wanazungumziwa kana kwamba walikuwa ni ndugu. "waumini wenzetu" # mchana na usiku Hizi sehemu mbili za siku zinatumika pamoja kumaanisha "wakati wote" au "bila kukoma"