# Kauli Unganishi: Malaika wa mwisho wa wale saba anaanza kupuliza tarumbeta yake. # malaika wa saba Huyu ni malaika wa mwisho kati ya wale saba. "malaika wa mwisho" au "malaika namba saba" # sauti kubwa zilinena mbinguni na kusema Usemi "sauti kubwa" huwakilisha wananenaji wanaozungumza kwa sauti kubwa. "Wasemaji mbinguni wakanena kwa sauti kubwa na kusema" # Ufalme wa dunia Hapa inamaanisha mamlaka ya kutawala ulimwengu. "Mamlaka ya kutawala dunia" # dunia Hii inamaanisha kila mtu duniani. "kila mtu duniani" # ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake Neno "ufalme" hapa linamaanisha mamlaka ya Bwana wetu na Kristo wake waliyonayo kutawala. # Ufalme wa dunia umeshakuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake "Bwana wetu na Kristo wake sasa ni watawala wa dunia"