# Sentensi Unganishi Paulo anawashauri waamini kuwa katika hali ya umoja na unyenyekevu na kuwakumbusha mfano wa Kristo. # Ikiwa "Ninaamini ni kweli" # ikiwa kuna kutia moyo katika Kristo "kwamba Kristo amewatia moyo" # ikiwa kuna faraja kutoka katika pendo lake "ikiwa pendo lake limekupa faraja" # ikiwa kuna ushirika wa Roho "ikiwa una ushirika pamoja na Roho" # ikiwa kuna rehema na huruma "ikiwa mmezoea matendo mengi ya Mungu ya huruma na rehema" # fanya furaha yangu Paulo hapa anazungumzia furaha kana kwamba kilikuwa kimiminika kinajazwa kwenye kibebeo. "Kumenisababisha kusifu mno"