# yaliyo mabaya machoni pa Bwana "machoni pa Bwana" inawakilisha kitu ambacho Bwana anakifikiria au kuwaza juu ya jambo fulani. # akawatia mikononi mwa Wafilisti "mkono" inamaanisha nguvu ya kushinda vitani. "aliruhusu Wafilisti wawashinde" # Miaka arobaini "miaka 40" # Sora Hili lilikuwa jina la mji katika Israeli. Ilikuwa katika mji wa Yuda karibu na mpaka wa Dani. # Wadani Watu wa kabila la Dani. # Manoa Hili ni jina la mwanaume.