# Maelezo ya Jumala: Haya ni maneno ya Yahwe kwa watu wa Israeli # mwisho uko juu yako "uhai wako umeisha" au "mwisho wa mda wako umefika" # kutokana na njia zako "kulingana na mambo unayoyafanya" au "kwa sababu ya mambo maovu ufanyayo" # nitaleta machukizo yako yote juu yako "nitaufanya uzoefu wako matokeo ya tabia yako ya machikizo" au "nitakuadhibu kwa kufanya haya mambo ninayoyachukia sana" # machukizo Hii inarejelea kwa tabia ambayo Mungu aichukiayo. # Kwa kuwa macho yangu hayatakuhurumia "Kwa kuwa sitakutazama kwa huruma" # nitaleta njia zako juu yako "nitakufanya mzoefu wa matokeo ya tabia yako mbaya" au "nitakuadhibu kwa mambo mabaya uyafanyayo." # machukizo yako yatakuwa katikati yako "matokeo ya tabia yako ya chuki yatakuzunguka" au 2) "sanamu zako zitakuwa pamoja nawe na hazitakuwa na uwezo."